thisisboman1
Member
- Feb 11, 2019
- 5
- 11
Nmeanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara.
VIJANA WENZANGU, Niwatoe hofu na kuwatia moyo ufugaji wa kuku wa kienyeji utakupa matokeo makubwa kupanda kiuchumi, kwa kuzingatia ufugaji wenye tija.
Mimi nafuga mradi unajiendesha nimezingatia eneo la uwekezaji na namna Bora ya kuepusha magonjwa kwenye mifugo nazingatia chanjo, usafi, ukaribu na kuwasoma vilivyo kuku hii imenisaidia malezi mazuri kiujumla na biashara kuleta faida.
NIMEWEZAJE KUMUDU HILI?
1. Tetea hutaga mayai, Huwa nahakikisha lazima Kila mwaka uzalishaji uongezeke, nilianza na kuuza trei moja Kila siku (MAYAI KIENYEJI) 500x30=15000 pili nilihakikisha Kila mwezi natotolesha vifaranga 50 kupitia tetea 5 tu kwa maana sikuwa na uwezo wa kununua INCUBATOR
2.Ukiachana na faida ya mayai kwa trei pia Huwa napiga hesabu ya tetea ambao Wamepunguza uwezo wa kutaga naingiza sokoni hapo ni baada ya kunizalishia mayai kwa miezi kati ya 6-8 hapa nachanganya na majogoo yaliyoanza kuwika makadilio wa miezi 6 kumbuka kwenye kutotolesha napata kuku mchanganyiko jogoo na tetea ndiyo maana lazima nipate majogoo pia ya kuuza hapa pia ni faida
3. NIKAZIE HAPA KWANGU MIMI KUKU WA KIENYEJI NI FAIDA TU, Hii ni kwasababu wanajitafutia chakula nawapa pumba kidogo kwa mwezi Tsh 9000 na eneo ninalofugia lipo mbali na makazi ya watu nikiwa na maana kwamba na takribani ekari na nusu, pia pembeni yangu walio nizunguka hawaendelezi Maeneo yao HIVYO ni fursa kupitia kuku ambao pia hunisaidia kuingiza pesa na kununua Maeneo mengine ya jirani hapa napata faida ya kuongeza eneo na kujiimarisha kiuzalishaji.
HIVYO NDIVYO NILIVYOANZA NAKUTIA MOYO NA WEWE, PITIA PICHA HAPO CHINI ZINAZOONYESHA NILIVYOANZA.
KWENYE PICHA UTAKUTANA NA BANDA LA KUKU LA MIFUKO (VIROBA) NDIYO NILILOANZIA KUFUGIA UTALIONA VIZURI NA NDANI PIA NIMEJENGA MWENYEWE KWA MITI, MIFUKO, KAMBA NA MISUMARI KIDOGO.