Ufugaji wa Kuku aina ya Kuchi na masoko yake ndani na nje ya Tanzania

Ina maana nikitaka kula kuku aina ya kuchi na wali mimi na familia yangu itatugharimu kwa zaidi ya 220,000 kwa mlo mmoja (kuku mzuri kuchi akigharimu TZS 200,000)?
 
Lets get serious, wapi naweza pata mbegu nzuri ya kuku aina ya kuchi? Naomba ani PM tafadhali.
 
Kuku wa Laki mbili?
siyo laki mbili ni elf arobaini ya Tanzania. watch hiyo clip. kuku aina ya kuchi huuzwa shilingi elf mbili (2000) za kenya ambazo ni sawa na elf arobaini (40,000) za Tanzania. (shilingi moja ya kenya ni sawa na shilingi ishirini za Tanzania)
 
Hawa kuku wana kipi cha ziada cha tofauti na kuku wengine? Kwa minajili ya Nyama, mayai nk??
 
Wadau nahitaji kuwafahamu kwa undani hawa kuku aina ya kuchi maaana wanauzwa ghali sana.nahitaji kufahamu jinsi ya kuwafuga na soko lake Likoje?
 
Hawana tofauti sana na kuku wa kienyeji ila unashauriwa uwafuge sehemu yenye uzio au bandani ili wasitoke kuchanganyika na kuku wengine hasa wa jirani.
Kuchi hutaga mayai yasiyozidi 12. Na ni nadra sana kutotoa yote. Katika hayo 12 akitotoa 7 au 8 shukuru mungu.

Kuna kuchi wa aina tofauti.
1. Mwamba
2. Selani
3. Pilipili
4. Ngamia
nakadhalika.
Thamani ya kuchi hutegemea aina.

Kuna kuchi halisi/original na kuchi kama jamii ya kuchi.

Soko lake ni kama unavyoona biashara ya Forever Living. Yaani biashara ya mtandao. Nikiwa na maana kuwa wateja wa kuchi ni wale wanaowajua kuchi na thamani yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom