Ufugaji wa kisasa wa Sungura: Ushauri wa masoko na faida za ufugaji

Mtafuteni Chasha awape story za hawa sungura, na kwa nini ni sawa na Kware? kwa kifupi Sungura na kware wanafanana kwa 98% na ni muda tu hatutawasikia tena. Cheki na huyo jamaa kule fb atawapa nini kilicho nyuma ya pazia ya hao sungura Chasha Poultry Farm labdaanaweza tokea make huku siku hizi haonekani kabisa
 
Wanaliwa? Ni watamu? Unawachinjaje maana mie naona kama wanatia huruma sana!

Wanaliwa ni watamu kama kuku!! Na ukipikiwa hutajua utadhani umeandaliwa kuku!!

Niliwafahamu SUA kitengo cha animal science wanawafuga basi kila nikitaka nyama nilikuwa naenda kununua.

Wanachinjwa kisha wanavuliwa ngozi.

Napenda sana kuwafuga, na hakika nitawafuga.

Nitaanza kuwakaribisha majirani kwa kuwala, wakionja watarudi kununua
 
Nimewakumbuka jamaa zangu akina A na U niliwalisha siku moja nyama ya sungura maana walikuwa hawajawahi ionja! Basi siku moja baada ya mjadala mzito kuhusu utamu wa nyama ya sungura, wao wakidai hawawezi kudanganywa lazima wataigundua tu! Na hawaamini kama sungura anaweza kuwa mtamu kama bata! Siku ya siku ilivyowadia nikiwa kazini nikachukua sungura mmoja aliyenona nikamchinja huko huko vijijini, nikaja home nikamwandaa vizuri wakati wenyewe wakiwa bado kazini! Mlo ulipoandaliwa wacha vijana wafakamie rabbit huku wakipiga miluzi ya kunipongeza kwa mlo ulioenda shule! Tangu siku hiyo wakawa wapenzi wa rabbit ni mwisho! Sungura watamu jamani, kama unakula nyama ya bata!!
 
Naomba msaada juu ya ufugaji wa sungura wa kisasa na upatikanaji wa soko lake



Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu

Mabanda
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.

Ufugaji wa ndani
  • Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
  • Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
  • Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
  • Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
  • Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki
Ufugaji wa nje
  • Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
  • Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
  • Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
  • Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng’oa yote)
Maji
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku

Chakula
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)

Usafi
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto

Meno
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12

Miguu
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana

Ubebaji
Usimbebe kwa kutumia masikio yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba

Dawa
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu

Maelezo zaidi unaweza tembelea:-
 
UFUGAJI BORA WA SUNGURA

UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu

MABANDA
Kna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.

UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha

2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa

3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri

4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi

5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki

UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk

2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika

3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali

4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)

MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku

CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)

USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto


MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12

MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana

UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba

DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo.
 
Aina za Sungura

Mfugaji anahitaji kutambua sungura ambao atatumia kama mbegu kwa kuzalisha wengine wa hali ya juu.
Ni vyema kutenga sungura wangali wadogo wakiwa miezi minne kwa wa kike na miezi sita kwa sungura wa kiume yaani kabla hawajaanza kuzaa.
Baada ya kupandisha kwa mara ya kwanza na wanapopata mimba sungura hao wa kike ni vyema kuwatenga na kuwaweka katika chumba chao maalum ili kuanzisha kizazi kingine.

Kuna aina mbali mbali wa sungura lakini wanagawanywa mara mbili kwa matumizi.

Moja ni kwa matumizi ya ngozi yake kwa kutengeza kofia, mifuko, na mishipi
Pili kuna aina ya sungura ambao hufugwa kwa kuzalisha nyama. Mfano wa aina ya sungura wa ngozi ni “Angora” ambaye manyoa yake ni marefu. Na kwa sungura wanaofugwa kwa nyama ni aina ya sungura ambao hukua haraka, uzito wa sungura wa nyama ni kutoka kilo mbili hadi kilo tano. mfano Califonia White na Newzealand White, Chinchila Flemish Giant, Flemish Fender.

Faida za kufuga sungura

Kulingana na wataalam, sungura ni mnyama rahisi wa kufuga hana gharama kubwa. Sungura akitunzwa vyema inavyostahili haugui kwa urahisi na pia lishe yake ni rahisi kupatikana.

Chakula cha sungura ni kama nyasi, mamboga kama vile sukuma wiki, spinarch, karoti, na pia unaweza kununua chakula halisi cha sungura kutoka maduka ya vifaa vya wanyama.

Wataalam wanashauri mfugaji akaushe chakula cha sungura ili asikojoe ovyo na pia kukinga magojwa ya tumbo.

Nyama ya sungura ni tamu na wale ambao wameila huilinganisha na nyama ya kuku. Kulinagana na wataalam ni nyama nyeupe ambayo haina mafuta ya cholestrol na hiyvo wataalam wa lishe bora huhimiza matumizi ya nyama ya sungura kwani ni bora kwa afya.

Ufugaji wa sungura ni kitengo kidogo cha ustawi wa mifugo kwa minajili ya kuongeza uzalishaji wa nyama ya sungura, na pia kwa mapato. Kama mnyama yeyote sungura anahitaji utunzaji mwema ili waweze kuzalisha kwa wingi.

Pia anahitaji kujengewa chumba maalum na kuangaliwa kila siku na kuhakikisha usafi wa vyumba hivi. Na kama watoto wa binadamu pia sungura wanahitaji kupewa chakula kisafi cha hali ya juu kilicho na madini ya protini na kalsham na pia kupewa maji masafi.
 
Nahitaji kuja ili nije kupata Elimu kidogo kuhusu ufugaji huu naomba mawasiliano
 
Nahitaji kufanya calculation ya banda zima lakisasa nianze ufugaji intensively
 
Tunauza sungura kwaajili ya nyama na kwaajili ya mbegu kwa wale wanaotaka kuanza kufuga.
Tunapatikana Kibaha kwa Mathias, kwa yeyote anayehitaji tuwasiliane kwa namba: 0717781981
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom