Ufufukaji wa uchumi wa China kunufaisha uchumi wa dunia unaokabiliwa na changamoto

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111431924583.jpg
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) hivi karibuni lilitoa ripoti, likipunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa nchi kubwa kiuchumi duniani, isipokuwa China, ambayo uchumi wake unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.2 kwa mwaka huu. Kabla ya hapo, Benki ya Dunia pia ilitoa makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa China. Rais wa Benki hiyo David Malpass amesema uchumi wa dunia utakuwa dhaifu mwaka huu, lakini uchumi wa China utakuwa wa "kipekee."

Ripoti ya IMF sio tu ilipunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu hadi asilimia 2.8, bali pia ilitumia maneno mazito kama vile “changamoto kubwa”, “utatanishi” na “hatari” kuelezea hali ya uchumi wa dunia. Ripoti hiyo inakadiria kuwa mwaka huu, ukuaji wa mapato ya nchi nyingi utapungua, na kiwango cha ukosefu wa ajira kitaongezeka, wakati huohuo ukuaji wa uchumi kwa takriban asilimia 90 ya nchi zilizoendelea utapungua. Ripoti hiyo pia ilitaja sababu kuu ambazo ni pamoja na msukusuko wa mambo ya kifedha katika nchi za magharibi, mfumuko wa bei, mgogoro unaoendelea nchini Ukraine, na athari ya janga la COVID-19.

Kutokana na hali ngumu duniani, uchumi wa China umeendelea kuonyesha mwelekeo wa kufufua. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China, pato la taifa la China katika robo ya kwanza ya mwaka huu lilikuwa dola trilioni 4.16 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 4.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki, na kuzidi makadirio yaa awali ambayo ni asilimia 4.0.

Ukuaji mzuri wa uchumi wa China unatokana na msingi wake thabiti. Mwaka jana, pato la taifa la China lilifikia dola trilioni 18 za kimarekani, na kuendelea kushika nafasi ya pili duniani. Pato la taifa kwa mtu lilifikia dola 12,741 za kimarekani, thamani ya biashara ya bidhaa ilizidi dola trilioni 6.2 za kimarekani. Licha ya hayo, China ina soko kubwa mno kutokana na idadi yake ya watu ambao ni zaidi ya bilioni 1.4, na kundi la watu wenye kipato cha kati zaidi ya milioni 400. Aidha, nia thabiti ya kufungua mlango pia ni sababu muhimu ya ukuaji wa uchumi wake.

Ukuaji mzuri wa uchumi wa China umeleta matumaini kwa uchumi wa dunia. Mkurugenzi mkuu wa IMF Georgieva Lake hivi karibuni alisema, China inatarajiwa kuchangia takriban theluthi moja ya ukuaji wa uchumi wa dunia mwaka huu, na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi nyingine. Mshauri wa masuala ya uchumi ambaye pia nia mkurugenzi wa idara ya utafiti ya shirika hilo Pierre-Olivier Gulancha amesema China itakuwa injini kuu ya ukuaji wa uchumi duniani.

Wachambuzi wameeleza kuwa, jumuiya ya kimataifa ina matumaini makubwa juu ya manufaa yatakayoletwa na uchumi wa China kwa uchumi wa dunia. Kwanza ni kutokana na ukubwa wa uchumi wa China. Hivi sasa uchumi cha China tayari umechukua asilimia 18 ya uchumi wa dunia, na ukuaji wake mzuri bila shaka utatoa mchango kwa ukuaji wa uchumi wa dunia. Kwa upande mwingine, China imesisitiza kufungua mlango zaidi, kwa kupitia mifumo mbalimbali ya ushirikiano kati yake na pande nyingi ikiwemo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu.

Kwa kuwa na lengo la kupata maendeleo ya pamoja na nchi nyingine duniani, ukuaji wa China hakika utanufaisha uchumi wa dunia.
 
Hata sikumoja usije ukaamini document au vichapisho vinavyotolewa na CCP

SERIKALI ya China inayoongozwa na chama cha CCP haina na haijawai kuwa na uwazi kwenye mambo yake na wachina wanalijua hili.

Imetoa taarifa kwamba Kuna ukuaji wa uchumi wa more than 4 percent walakini 1 in 5 adult hawana ajira ,

Hakuna asiyejua kwa sasa China ipo kwenye wakati mgumu sana kibiashara, makampuni mengi ya west yanajiondoa China kutokana na sera mbovu za CCP na ukiukwaji wa haki za binadamu.

USA wamerekodi increase of 900% high of Chinese illegal migrants kwenye southern border. Kuna wimbi kubwa la wachina zaidi ya milion 1.3 wamekimbilia Vietnam na hawana mpango wa kurudi china

Wachina wengi sana saivi wanakimbilia Vietnam Philippines nchi za southern china na west.

Ikiwa uchumi ni mzuri, kwanini wananchi waikimbie nchi yao...??

Makampuni mengi ya west kwa sasa yanaachana na China saivi yanahamia India, Vietnam, Germany

Mfano mdogo tu FOXCONN the major iPhone manufacturer wa China ambae ni mzalishaji wa more than 50% wa iPhone Duniani kote amepunguza 60% ya wafanyakazi na kwasasa anataka kufungua branch Vietnam.

Kwanini kama uchumi wa China ni mzuri makampuni yanahaha kuhama mainland China..??

Shughuli za usafirishaji bandari nyingi za China zimeshuka kwa asilimia kubwa, watu wanaachishwa kazi na wengine kutakuwa kufanya kwa siku moja na kupunzika siku mbili au tatu,

China Kuna hali mbaya kiuchumi but CCP wanajaribu kupika data ili ionekane kuko poa.

China inauhitaji ulimwengu kuliko ulimwengu unavyoiitajji China.
 
Ni kama enzi za Jiwe, unaficha takwimu ili kuvuta uwekezaji.
 
Na hawajawahi kukiri kwamba ulikufa, ni kwamba uko china, local government zina madeni makubwa kinoma, hadi wanashindwa kulipa baadhi ya madai ya watu,

Kuna wimbi kubwa unemployment na matatizo makubwa ya real estate majumba yamejengwa lakini hayakaliki ni kwamba watu hawawezi kuafford gharama zake.

Lakini hili jambo hautolisikia kwa mawakala kama HAWA wa CCP
Maelezo yenu yanakinzana na ripoti za imf na wb
 
Ripoti hizo zinatolewa kutokana na taarifa zinazopelekwa na selikari husika.
Sasa jiulize iwapo CCP iliyapiga ban makampuni ya kimataifa ya finance na auditing kama Deloitte, Ernst & Young (EY), KPMG, and PricewaterhouseCoopers (PwC) yasifanye kazi main land China unategemea utapata ukweli wowote hapo?
Kwa hiyo unanijuza kuwa sipasw kuziamin ripoti za IMF na WB zinazohusu uchina isipokuwa nikuamin ww hapo grit thinka wa jf
 
Ripoti ta ukuaji wa uchumi wa China inayosema uchumi wake unakuwa kwa asilimia 4.5% imetolewa na baraza au taasisi ya statistics ya China na sio IMF, IFM Imetoa report ya uchumi ya ki Dunia kwa ujumla.

Fanya tafiti na usome vizuri kwanza, sio kila anachokuandikia jamaa unakibeba kama kilivyo
Nimeitoa ktk wavuti ya IMF
Screenshot_20230422-082513.jpg
 
A
Ww embu soma vizuri iyo ni projection jamaa dah unanichosha

Projection sio tafiti halisi, CCP imeset malengo ya kukuza uchumi wao kwa asilimia 5 mwaka huu na ndicho hicho IMF wamekiripoti

Soma iyo paragraph ya chini inayoanza na accordingly as we not from China... it means tafiti hazijafanywa na wao. Tumia akili....
Achana na huyo mjinga ,hajui hata real estate bubble iliyopo China Kwa sasa , kama unafuatilia mambo mwaka jana kuna kampuni kubwa la masuala ya real estate china worth more than 400billons (Evergrande) USD lilikuwa kwenye ukata wa kufirisika na hata sasa kuna tatizo sana kwenye hiyo sector na ndio inayobeba Gdp asilimia 60 ya china ,na wanasema hiyo real estate inaenda kucollpase muda si mrefu huku China yenyewe ikiwa kwenye debt crisis na mdororo wa uchumi ,ikicollapse real estate tu ni uchumi wa china site kwishney , ukiachilia covid lockdowns zinazoendelea china toka mwaka 2020 hadi sasa hivi kuna makampuni hayafanyi uzalishaji kama ilivyo takiwa na ,protests za covid lockdowns ni nyingi mno China Ila huwezi ona hawa wachina weusi wa bongo wanaongelea hilo .

Exodus ya. Wachina kukimbilia nchi nyingine hasa United States ,Canada na Europe ni kubwa sana kwa sasa ,mwenye akili atajua how bad Chinese economy is right now ,CCP ni manipulators WA data na hawapendi ziwe exposed hata siku moja ,nchi inayosanction mitandao ya kijamii tu kama facebook nk hiyo ni nchi au concentration camp ? .
Wachina wenyewe wanajua jinsi serikali yao ilivyo bingwa wa kucover up na kupiga propaganda
 
Hiyo ni tafsiri yako,
Hivi unajua deni la local government za China ni kiasi gani? Nikikwambia ni more than GDP ya Japan yaan deni ni kubwa kuliko GDP ya nchi nyingine utaelewa ninachozungumza,
Fatilia "Baidu" kama unajua kichina ndo utaelewa
Wewe unaandika usichokijua taarifa za China unazipatia Baidu kweli?
 
IMF Kaongea sangapi mbona mnajichanganya nyie? IMF Ametoa prediction na sio tafiti, tafiti zimefanywa na China na ripoti ya ukuaji wa uchumi wa robo mwka wa China imetlewa na taasisi ya statistics ya China ambao hawana uwazi na ukweli...
Note kipindi cha korona walivyokuwa wanapika data ndo utaelewa
Tunajua hizo ni GDP growth forecast kutoka IMF. Kwa hiyo za China ni za uongo na za nchi nyingine za kweli si ndo unatuaminisha hivyo?
 
Unaweza ukawa haujui unachokiongelea...

Embu nitajie kwanza vitu vi3 vikuu vinavyosimamia na kuwakilisha GDB ya nchi hasa mfano China?

Ukishindwa hili swali usinisumbue
IMF wameshatoa GDP growth forecast zao wewe kama haukubaliani nazo wewe ndio mwenye matatizo.

JP Morgan nao walitoa GDP growth forecast kuhusu China hazikupishana na za IMF

Sina muda wa kuandika hizo mambo kwa sababu unaendeshwa na mihemuko na chuki dhidi ya China
 
Na hawajawahi kukiri kwamba ulikufa, ni kwamba uko china, local government zina madeni makubwa kinoma, hadi wanashindwa kulipa baadhi ya madai ya watu,

Kuna wimbi kubwa unemployment na matatizo makubwa ya real estate majumba yamejengwa lakini hayakaliki ni kwamba watu hawawezi kuafford gharama zake.

Lakini hili jambo hautolisikia kwa mawakala kama HAWA wa CCP
Serikali za kisocialist ni miyeyusho sana, ndio maana kila anayeinuka kwenda kinyume na mamlaka anazibwa mdomo haraka sana Ili kufunika madudu kama haya!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Projection sio ukuaji halisi we jamaa dah, projection ni mwelekeo unaotegemewa na sio namba halisi.

Na naomba utambue sio chuki ni uhalisia na hoja, chuki unaitafsiri ww

Ni sawa sawa na kipindi Magufuli alipogoma kutoa takwimu za waathirika wa COVID halafu siku atoe namba then kupitia zile namba mataasisi ya nje yafanye projection zake
Unanifundisha maana ya neno projection tena?

Na kwenye first quarter (Q1) ya mwaka huu wa 2023 uchumi wa China umekua kwa 4.5% kuliko ilivyotarajiwa (projection)

Komaa na hiyo Baidu kupata data za uchumi wa China mkuu
 
Back
Top Bottom