Ufisadi wa Kutisha EPZA

Ogwari

Member
Apr 14, 2011
26
15
Zito Kabwe amemtoa nje Waziri Chami aliyeongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Mauzo nje (EPZ), Dk. Adelhelm Meru, na watendaji wa mamlaka hiyo kwa madai ya ufisadi wa sh bilioni 41 katika mradi wa Benjamin Mkapa ulioko Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Dk. Chami na watendaji hao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya mjumbe wa Kamati ya POAC kuhitaji ufafanuzi wa matumizi ya fedha katika mradi huo kwa kutofautiana na ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya (CCM), alisema kutokana na hali hiyo kamati inahitaji kupata maelezo ya kina kwani inaonyesha kuna matumizi yaliyofanywa na kuzidi gharama za ujenzi wa mradi huo ambazo ni sh bilioni 14 kama ilivyopangwa na serikali.
Kwa mujibu wa taarifa za CAG, kuna matumizi ya zaidi ya sh bilioni 41.

“Tunahitaji ufafanuzi juu ya mradi huu sasa; inanyesha hata kuna malipo yalifanyika katika ununuzi wa vifaa hakunyesha stakabadhi za malipo, sasa hali hii inajenga shaka, kwa kuwa mwenyekiti wa baraza ambaye pia ni Waziri wa Viwanda unaweza kutupatia majibu ya kina kuhusu hili,” alisema Bulaya.

Hata hivyo majibu hayo yalipingwa na mwenyekiti wa kamati hiyo alimtaka Waziri Chami na watendaji wake kutoka EPZ kuondoka kikaoni na mara watakapopata nyaraka hizo waje tena mbele ya kamati hiyo na kutoa maelezo yao ya kina.
“Lengo letu ni kujenga… kwa hili katika mradi huu wa Benjamin Mkapa, kuna kitu ambacho hakileti tafsiri nzuri kwenu hivyo tunawataka muondoke na pindi mtakapopata nyaraka hizo muhimu ndipo mje mbele ya kamati.
…Lakini sasa inaoyesha kuna malipo yalikuwa yakifanywa bila hata kufuata utaratibu hadi kufikia sh bilioni 41; tunapata shaka na matumizi ya fedha za serikali kuchezewa na wajanja wachache,” alisema Zitto.

Kutokana na maamuzi hayo wajumbe wa kamati hiyo waliunga mkono hatua hiyo hali iliyomlazimu Waziri Chami na timu yake kunyanyuka na kutoka nje ya ukumbi huo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya EPZ, inaonyesha kuwa toka mradi huo ulipoanzishwa watendaji hao wa EPZ wamekuwa wakilalamikiwa kutokana na kufuja fedha za umma ikiwemo kujilipa mishahara mikubwa na hata kufanya matumizi ya ununuzi wa vifaa kinyume cha sheria.

Kamati pia imeomba ufafanuzi kuhusu matumizi makubwa ya fedha yaliyofanya na Mkurugenzi mkuu wa EPZA Adelhmer Mero Katika maandalizi ya warsha ya maonyesho ya EPZA Yaliyofanyika mwezi uliopita i
 
Ogwari Nyarwath, Hii nchi inatisha kila kona ni mchezo wa ufisadi I bet hatutakaa tuendelee milele zote kama chama hiki cha magamba kitaendelea hadi 2015. This is really bad for this generation!, who will save this country out of looting for future generation? It is you, I, they, them, we. Let us act now. :pound:
 
Hii Nchi ni Nchi ya ajabu sana Dr Meru ni fisadi mkubwa ,Miaka ya 2000,s Akiwa mkurugenzi mkuu wa VETA alifukuzwa kazi na Mkapa,nilishangaa sana alipoteuliwa na Mbayuwayu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA. Zito hongera sana next time akija na forgery zake peleka file zake TAKUKURU achunguzwe tumechoshwa na ufisadi ,ana tatizo lingine la ufuska jamaa anapenda vibaya alivyokuwa Manager wa VETA kanda ya kaskazini Moshi alikuwa na uhusiano usio wa kawaida na secretary wake ilifika wakati kila tender alikuwa anampa laaziz wake,Akahamishwa VETA Makao makuu akaendelea na Mtindo huu this time ikawa worse kila tender akawa anampa mama mmoja pale ni mke wa mtu ambaye pia alikuwa ni Laaziz wake ikafika hatua huyo mama akapewa talaka,.

Alipohamishiwa wizara ya viwanda na Biashara jamaa akaendelea na huu upuuzi,Worse still last month akafanya ufisadi mwingine ku- Outsorce maandalizi ya warsha ya EPZA Iliyofanyika mlimani City kwa laaziz wake,
 
kha! Hili dubwana meru hatari sana. Yani ukimwona kwenye tv kama mtu vile. Halafu hamuoni ni kama kamchezo hivi kwamba ben alimtimua veta. Sasa anasimamia mradi ulioasisiwa na ben! Mbaya zaidi anaendeleza ufisadi. Jk noma!
 
Mi nadhani suluhisho ni katiba mpya, na tukiipata katiba mpya tuanze kuwafilisi wote wanaoiibia nchi kiujanja ujanja.
 
Mi nadhani suluhisho ni katiba mpya, na tukiipata katiba mpya tuanze kuwafilisi wote wanaoiibia nchi kiujanja ujanja.

Suala la katibu mpya halina mjada ni lazima tuwe na katiba mpya, Hii issue ya Dr Mero ipo straight forward haitaji kusubiri katiba mpya sheria za rushwa zilizopo zinatosheleza kumfikisha mahakamani
 
Hii Nchi ni Nchi ya ajabu sana Dr Meru ni fisadi mkubwa ,Miaka ya 2000,s Akiwa mkurugenzi mkuu wa VETA alifukuzwa kazi na Mkapa,nilishangaa sana alipoteuliwa na Mbayuwayu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA. Zito hongera sana next time akija na forgery zake peleka file zake TAKUKURU achunguzwe tumechoshwa na ufisadi ,ana tatizo lingine la ufuska jamaa anapenda vibaya alivyokuwa Manager wa VETA kanda ya kaskazini Moshi alikuwa na uhusiano usio wa kawaida na secretary wake ilifika wakati kila tender alikuwa anampa laaziz wake,Akahamishwa VETA Makao makuu akaendelea na Mtindo huu this time ikawa worse kila tender akawa anampa mama mmoja pale ni mke wa mtu ambaye pia alikuwa ni Laaziz wake ikafika hatua huyo mama akapewa talaka,.

Alipohamishiwa wizara ya viwanda na Biashara jamaa akaendelea na huu upuuzi,Worse still last month akafanya ufisadi mwingine ku- Outsorce maandalizi ya warsha ya EPZA Iliyofanyika mlimani City kwa laaziz wake,

Labda uliungama dhambi zake kwa mbayuwayu akasamehewa kwa jina la Gamba. Lakini inaonekana amerudia sasa sijui ataungama kwa jina gani? :smow:
 
Suala la katibu mpya halina mjada ni lazima tuwe na katiba mpya, Hii issue ya Dr Mero ipo straight forward haitaji kusubiri katiba mpya sheria za rushwa zilizopo zinatosheleza kumfikisha mahakamani

Sio serikali hii,hivyo vita vya rushwa vinapiganwa kwa warsha na kongamano...
 
Ogwari Nyarwath, Hii nchi inatisha kila kona ni mchezo wa ufisadi I bet hatutakaa tuendelee milele zote kama chama hiki cha magamba kitaendelea hadi 2015. This is really bad for this generation!, who will save this country out of looting for future generation? It is you, I, they, them, we. Let us act now. :pound:
kwenye red you wrote kinyesi.
 
Hao EPZ wameenda kuvunja Hazina na kujilipa hayo mabilioni? Nadhani Serikali inatakiwa kufanya "Monitoring & Evaluation" ya miradi yote mikubwa kila baada ya hatua fulani kabla ya kutoa pesa zaidi kwenye mradi husika. Multinational NGOs nyingi zimefanikiwa kwa kuwa na program ya "Monitoring & Evaluation" kwa kila mradi wanaoufadhili.
 
Vincent
Nakubaliana na wewe kabisa ni lazima Monitoring & Evaluation ya miradi yote mikubwa ifanywe,Na ianze na Ofisi za WAMA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom