Ufisadi wa kutisha BoT (Hazina) kuu ya Serikali

Ni Mimi Msiogope

JF-Expert Member
May 28, 2012
352
200
Watanzania wengi waliosoma vyuo vikuu vya Serikali huku wakifadhiliwa na Serikali kwa Asilimia tofauti 'Boom', Wamekuwa wakikatwa kwenye Mishahara yao kila mwezi pia kwa viwango tofauti. Taarifa za awali zinasema kuwa hazijulikani zipo kwenye Account gani hadi sasa na chanzo cha taarifa hii kimesema kuwa kuna Account zaidi ya 102 ambazo zimekuwa zikiingiziwa fedha kutoka 'Fungu' hilo. Hata hivyo nimejaribu kucheki kwenye vitabu vya Bajeti miaka yote sijaona kasma hii. Nimeamua kulipeleka bungeni.

Kama huna taarifa sahihi Stay tuned Bungeni ikipatikana nafasi Swali litaulizwa kwa Waziri husika.
 
Mbona mimi nilisha maliza kukatwa na mhasibu alikuwa napeleka Loan Board moja kwa moja? hizo ni zipi tena?
 
Mbona mimi nilisha maliza kukatwa na mhasibu alikuwa napeleka Loan Board moja kwa moja? hizo ni zipi tena?

Loan Board inatengewa fedha kila mwaka kama idara nyingine.. Hata hivyo kwenye Vitabu Loan Board haionekani kokote kama inaingiza chochote Hazina/BoT
 
Ndiyo maana kuna watu ambao tunakaribia kumaliza deni na wengine walishamaliza, ila kumbukumbu za bodi ya mikopo zinaonyesha hatuzaanza hata kulipa. Naona hii ndiyo free style ya LIWALO na LIWE:
 
Ndiyo maana kuna watu ambao tunakaribia kumaliza deni na wengine walishamaliza, ila kumbukumbu za bodi ya mikopo zinaonyesha hatuzaanza hata kulipa. Naona hii ndiyo free style ya LIWALO na LIWE:

Liwalo na Liwe!
Unajua Serikali inawachezea sana Watanzania.. Ukicheki kwenye mfumo wa fedha utagundua kuwa Serikali inaibiwa na watendaji wake kiasi kikubwa na sina hakika kama wanashtuka!.. Acha sisi wananchi tushtuke tuwaache na maneno yao ya LIWALO NA LIWE
 
Kuna wizi mkubwa sana BOT na Hazina ambao mpaka sasa haujaweza kuthibitiwa!! Njia waliotumia kutaka kuiba zile fedha za safari za Rais ni moja katika mbinu lukuki wanazotumia kuiibia serikali.
 
Kuna wizi mkubwa sana BOT na Hazina ambao mpaka sasa haujaweza kuthibitiwa!! Njia waliotumia kutaka kuiba zile fedha za safari za Rais ni moja katika mbinu lukuki wanazotumia kuiibia serikali.

Ikumbukwe hili ni la muda mrefu sana!.. Watu wameanza kukatwa zamani lakini inaishia mikononi mwa watu wachache..
 
Back
Top Bottom