Ufisadi wa Kifo Vipimo vya UKIMWI

Nionavyo Mimi Kwa Wale Ambao Wameshagonga Ni Kuwaacha Bila Ya Kuwapa Dawa Za Kurefusha Maisha Ili Wafe Mapema Waache Kuambukiza Wengine Maana Ukiwasikia Wenyewe Wanavyojisifia Ati Ni Lazima Waondoke Na Wengi.kwa Hiyo Bomu Tunajitengenezea Wenyewe. Maana Angalia Hata Wakishameza Zile Dawa Wanavyonawiri Na Wengine Wamediriki Kuniambia Ati Nguvu Zao Za Kungonoka Zimekuwa Mara Dufu Baada Ya Kumeza Dawa Za Kurefusha Maisha. Sasa Hamuoni Ni Hatari Hii? Hakuna Wakati Mgumu Kwa Waafrica Ktk Dunia Hii Kama Sasa, Lakini Cha Ajabiu Wenyewe Hawajali Ni Lazima Wajue Janga Hili Ni Kubwa Kuliko Vita Zote Kuu Tatu Zilizopita Za Dunia.
 
Niliku Nafanya Maongezi Na Rafiki Yangu Mmoja Mtaliano Maongezi Ya Kawaida Tu, Basi Nikajikuta Nagusia Suala La Ukimwi Tanzania Na Namna Gani Ya Kukabiliana Nalo Basi Yule Bwana Alinionea Huruma Sana Na Akaniambia Kuanzia Sasa Hesabu Miaka Kumi Mbele Na Siyo Tanzania Pekee Bali Na Karibu Nusu Ya Waafrica Wote Wanaoishi Africa Watakuwa Wameteketea Kwa Ugonjwa Huu Mbaya Kabisa Kutokea Tangu Kuumbwa Kwa Dunia. Nilipomuuliza Ni Kwanini Akaniambia Waafrica Huwa Hawajithamini Na Haswa Wale Waliooa Na Walio Olewa Akazidi Kusema Africa Ni Rahisi Kabisa Kufanya Ngono Na Mke Au Mume Wa Mtu Kuliko Mahala Pengine Popote Duniani Na Hata Hao Wanaojiita Maboyfriend Na Na Girlfriend Asilimia Nyingi Ni Wanafiki Wa Wanagawa Uroda Kwa Yeyote Mwenye Kuhitaji Akasema Asilimia 95 Ya Waafrica Hawajiheshimu Wala Kujithamini Ktk Suala La Ngono
Sorry to ask... Did you buy his CRAP?
How did this Italian guy come to such a conclusion? I think stereotyping is what made him say so...just because Africa is underdeveloped, poor etc then anything can be said cos it all goes with that!!!!
Kama kweli wanandoa wa kiafrika tu ndio hawajithamini kwa nini basi nchi zinazodaiwa kuendelea wanafanya biashara ya ngono hadi kufikia kuipa uhalali ili waweze kuikata kodi?? Je hao wanaouza miili ktk hayo madanguro wanawauzia waafrika au watu wa dunia nzima???
Kila kinachotokea Afrika sasa hivi in one way or another kwenye nchi zilizoendelea kilishawahi kufanyika na huenda kimepewa kipaumbele na kufikia hatua ya kukifanya hicho kitu kionekane ni Civilised in one way or another!
Waafrika at least kwa uelewa wangu wapo ambao wanaziheshimu sana ndoa na mahusiano yao ya kimapenzi ila pia kama kawaida ya binadamu tunatofautiana wapo ambao heshima ya ndoa hawana! Ila kisiwe kigezo cha kuwafanya watu wa nje kuongelea Waafrika na sisi tukabaki tunawasikiliza utadhani wanatuletea miujiza ya msaada!!!

IT CAN BE DONE....PLAY YOUR PART..! MIMI NA WEWE TUANZE KUBADILIKA.........! WASWAHILI HUSEMA MOJA NDIO MWANZO WA HESABU......SASA TUMEFIKA MBILI....(isiishie kuwa maneno matupu bali kwa vitendo) TUHAKIKISHE TUNATOKOMEZA UKIMWI KAMA KINA KAWAW,T.KOMBO NA WENGINEO WALIVYOTOKOMEZA UKOLONI....!

Mkuu this i agree with u 100% lets get it going!!!!
 
Sorry to ask... Did you buy his CRAP?
How did this Italian guy come to such a conclusion? I think stereotyping is what made him say so...just because Africa is underdeveloped, poor etc then anything can be said cos it all goes with that!!!!
Kama kweli wanandoa wa kiafrika tu ndio hawajithamini kwa nini basi nchi zinazodaiwa kuendelea wanafanya biashara ya ngono hadi kufikia kuipa uhalali ili waweze kuikata kodi?? Je hao wanaouza miili ktk hayo madanguro wanawauzia waafrika au watu wa dunia nzima???
Kila kinachotokea Afrika sasa hivi in one way or another kwenye nchi zilizoendelea kilishawahi kufanyika na huenda kimepewa kipaumbele na kufikia hatua ya kukifanya hicho kitu kionekane ni Civilised in one way or another!
Waafrika at least kwa uelewa wangu wapo ambao wanaziheshimu sana ndoa na mahusiano yao ya kimapenzi ila pia kama kawaida ya binadamu tunatofautiana wapo ambao heshima ya ndoa hawana! Ila kisiwe kigezo cha kuwafanya watu wa nje kuongelea Waafrika na sisi tukabaki tunawasikiliza utadhani wanatuletea miujiza ya msaada!!!



Mkuu this i agree with u 100% lets get it going!!!!

msaada gani tena unataka wakati washakutumia dawa ya kukupunguzia makali yake? na pesa ya kununua chakula washakutumia au unajifanya leo humjui bushi ni nani?
 
msaada gani tena unataka wakati washakutumia dawa ya kukupunguzia makali yake? na pesa ya kununua chakula washakutumia au unajifanya leo humjui bushi ni nani?

......Waafrika ndivyo tulivyo...!

Tuendelee kusubiri Mtaliano atupe assesment yake na jinsi ya kuepuka kuipoteza nguvu kazi ya nchi!!!

kwi kwi kwi... kumbe nao ni wadau katika mambo ya ndani ya Afrika.......
 
Niliku Nafanya Maongezi Na Rafiki Yangu Mmoja Mtaliano Maongezi Ya Kawaida Tu, Basi Nikajikuta Nagusia Suala La Ukimwi Tanzania Na Namna Gani Ya Kukabiliana Nalo Basi Yule Bwana Alinionea Huruma Sana Na Akaniambia Kuanzia Sasa Hesabu Miaka Kumi Mbele Na Siyo Tanzania Pekee Bali Na Karibu Nusu Ya Waafrica Wote Wanaoishi Africa Watakuwa Wameteketea Kwa Ugonjwa Huu Mbaya Kabisa Kutokea Tangu Kuumbwa Kwa Dunia. Nilipomuuliza Ni Kwanini Akaniambia Waafrica Huwa Hawajithamini Na Haswa Wale Waliooa Na Walio Olewa Akazidi Kusema Africa Ni Rahisi Kabisa Kufanya Ngono Na Mke Au Mume Wa Mtu Kuliko Mahala Pengine Popote Duniani Na Hata Hao Wanaojiita Maboyfriend Na Na Girlfriend Asilimia Nyingi Ni Wanafiki Wa Wanagawa Uroda Kwa Yeyote Mwenye Kuhitaji Akasema Asilimia 95 Ya Waafrica Hawajiheshimu Wala Kujithamini Ktk Suala La Ngono

He conclude that we will be finished from which basis/research?, i personal looked at him as he is too much idealistic than realistic even though kun elements za ukweli kiasi!
We should note that kwamba vita dhidi ya UKIMWI ni broad more than hata vile wengi tunavyodhani, adui yetu UKIMWI anapata BACK UP sana from the west sisi hilo hatujui!, AVAILABILTY of ARV's doesnt mean ACCESSIBILTY of them, still the way forward is so trickly and tedious for Africa as far as Sub Saharan Africa its concerned!
 
Niliku Nafanya Maongezi Na Rafiki Yangu Mmoja Mtaliano Maongezi Ya Kawaida Tu, Basi Nikajikuta Nagusia Suala La Ukimwi Tanzania Na Namna Gani Ya Kukabiliana Nalo Basi Yule Bwana Alinionea Huruma Sana Na Akaniambia Kuanzia Sasa Hesabu Miaka Kumi Mbele Na Siyo Tanzania Pekee Bali Na Karibu Nusu Ya Waafrica Wote Wanaoishi Africa Watakuwa Wameteketea Kwa Ugonjwa Huu Mbaya Kabisa Kutokea Tangu Kuumbwa Kwa Dunia. Nilipomuuliza Ni Kwanini Akaniambia Waafrica Huwa Hawajithamini Na Haswa Wale Waliooa Na Walio Olewa Akazidi Kusema Africa Ni Rahisi Kabisa Kufanya Ngono Na Mke Au Mume Wa Mtu Kuliko Mahala Pengine Popote Duniani Na Hata Hao Wanaojiita Maboyfriend Na Na Girlfriend Asilimia Nyingi Ni Wanafiki Wa Wanagawa Uroda Kwa Yeyote Mwenye Kuhitaji Akasema Asilimia 95 Ya Waafrica Hawajiheshimu Wala Kujithamini Ktk Suala La Ngono

Hizo habari zinaweza kuwa za kweli au la.

Wazungu wamezoea sana kutu demonise Waafrika na kujisahau. Sitaki kulinganisha matendo yao na ya kwetu, la hasha. Ila ninachotaka kusema ni kuwa wazungu wanajiona kuwa wana morals zaidi kuliko waafrika.

Mfano mmoja:

Miaka ya nyuma kiasi, tukiwa huku Ulaya, tulitembelewa na mama wa rika la makamu hivi kutoka Mwanza, ambaye alialikwa na rafiki zake Wammisionari ambao nao walishafanya kazi huko Mwanza. Sasa yule mama Mtanzania akawa anatueleza kuwa wale wammisionari walikuwa wanasema kuwa Waafrika hatuna morals kwa vile tunapenda sana ngono. Mfano halisi ni kuwa binti wa mama huyo alizalia nyumbani (hakuolewa). Sisi tukamuambia kuwa huo ni upuuzi mtupu...wazungu kwa maoni yetu wanaongoza kwa vitenda vya ngono ovyo.

Nenda kwenye ma night club, ngono nje nje. Naye akatueleza kuwa binti ya wale wammisionari analala na boyfriend wake pale nyumbani kwa wazazi wake! Kwa sababu sisi tulikuwa tunafahamiana na wale Wammisionari, na tunajua nyumbani kwao, tukamweleza yule mama kuwa tukimrudisha kwa wenyeji wake tutamuonyesha kitu.

Tulipofika tulimuonyesha yule mama dula la ngono (Sex Shop) na matabgazo yake yote, ambalo lipo katika ground floor ya apartment waliokuwa wakiisha wale Wammisionari!!
 
kwa ukweli sisi wafrika tunapoambiwa ukweli na tukawa hatukufurahiwa nao huwa na hasira baada ya kuitizama hiyo hoja wenzetu hao wazungu wao huangalia ukweli upo wapi na wakashirikiana kutafuta ufumbuzi kwa sisi wafrika hatupo hivyo na hili husababishwa na viongozi tunaowachanguwa na hapa nitatowa mfano kama huo aliotowa mtowa maoni hapo juu kuhusiana yule bibi wa mwanza aliyekwenda kuwatembelea huko ulaya na yakaongelewa yaliyo ongelea kuhusu wafrika .

kuna wakati nikiwa nchi ya ulaya kulikuwa nakijana mmoja MTANZANIA ambae kwa bahati walipendana na mshicha wa kizungu ikafikia wakati akataka kumuowa lakini swali lilipofika kwa baba mzazi halikuwa jepesi Alimwita kija yule wa KITANZANIA na kumuliza wewe utaweza kuishi nae vipi mwanangu mkiwa huko kwenu TZ ikiwa nchi yenu mika yote ni kuomba omba hata bajeti ya nchi hawezi kuwa bila pesa zetuza walipa kodi hapa kwetu na kusaidiwa nchi yenu sasa wewe utaishi nae vipi ??

Maneno kama hayo kwangu mimi binafsi ni matusi na dharau ya mwisho lakini kwa viongozi wetu ni sifa inayowapelekea kuwa waombaji zaidi hapa nataka kueleza jinsi gani wafrika tumekuwa tunadharauliwa kila pande za dunia na ndio mpaka sasa wazungu wengi wanaimani hiyo kuwa wengi tutaondoka kwa ukimwi isipokuwa wanazungumza miongoni mwao
 
SEE ATTCHEMENTS


PCCB, DCI should comb Ministry of Health and flush out criminal elements

FINNIGAN WA SIMBEYE
DAR ES SALAAM


ONCE again in a space of less than six months, the corruption jinx at the Ministry of Health and Social Welfare has raised its ugly head again. This time around the controversy surrounds a three-man probe team report which was presented to the media by the Minister, Professor David Homeli Mwakyusa.

The controversial report which has taken the probe team over a year to complete against a scheduled time of three and a half months, was aimed at finding out why German made Cyflow CD4 counter and South Korean made SD Bioline HIV rapid test kit were being barred from being used in the country despite the fact that the medical equipment had been locally evaluated and approved.

Prof. Mwakyusa stirred a controversial media debate when he said that Cyflow was actually banned for use in the country following poor evaluation results at the then Muhimbili University College for Health Sciences (now Muhimbili University for Health and Allied Sciences (MUHAS) in 2004.

Prof. Mwakyusa, one of the country’s most coveted medical doctors, went on to assert in a statement that Cyflow has even failed to impress the World Health Organization (WHO) which doesn’t recommend use of the machine because of technical deficiencies. The minister further contended that the equipment is never used in any developed country!

German manufacturers of Cyflow, Partec Essential Healthcare reacted angrily to Prof. Mwakyusa’s statement and the company has since produced enough evidence to prove its case that the machine is popularly used in developed and developing world, including WHO sponsored projects and that its evaluation at MUCHS was sabotaged.

For over a decade now, a network of criminal personalities at MoHSW and its affiliates which include Medical Stores Department, MUHAS and National Aids Control Programme, among others, have forged a satanic relationship with Dar es Salaam-based businessman, Bharat Rajani of Biocare Health Products Limited who supplied Becton Dickinson made FacsCount CD4 Counter and Capillus while shutting out all other competitors as if Tanzania is a centralized command economy.

Prof. Mwakyusa who seemed to have been misinformed thoroughly by his two peers in the profession, Professor Philip Hiza and Raphael Lema who had all along quarreled with the rapporteur of the probe team report, Dr Juma Madati, whose commitment to deliver on the project can be proven by his taking of a two months unpaid leave in 2006, went on to defend his ministry’s continued purchasing of Capillus HIV rapid test kit which was formally phased out after a decade of domination, last year.

He said Capillus is scientifically effective and the country has a reliable cold chain to ferry the Irish made kit which has never undergone compulsory evaluation as required by regulations governing importation of foreign technologies into the country, upcountry where the kit is actually designed to be used as hospitals and health centres are not available.

Former Permanent Secretary at MoHSW, Hilda Gondwe, issued a statement in November 2006, which categorically stated that Capillus was not effective for use in the country because of its strict cold chain requirement. Gondwe was later removed from the ministry probably because she stepped on high profile public office holders’ interests because just recently Medical Stores Department ordered a huge consignment of Capillus valued at over 4bn/-.

There is a serious problem of accountability and professional ethics among senior technical officials at this sensitive ministry where former Permanent Secretary Mariam Mwaffisi was so frustrated that she said in public that some correspondence addressed to her was actually hijacked and replied without her knowledge.

This suspect network of highly qualified Tanzania medical doctors, pharmacists and other related professions which is lubricated by donor money paid to Rajan’s company which also almost monopolizes all medical supplies to the MoHSW, must be probed by law enforcing agencies, Prevention and Combating of Corruption Bureau and Directorate of Criminal Investigations.

This criminal cartel is as dangerous as that which was recently dismantled by President Jakaya Mrisho Kikwete at the Bank of Tanzania by the sacking of former governor Daudi Ballali. The problem at MoHSW and its affiliates, is not Prof. Mwakyusa or Wilson Mukama the current PS and indeed not Dr. Deo Mtasiwa, the chief medical officer, but key technical personnel who have overstayed at the ministry and established an empire of evil supported by some donors whose interest is to show on books that they gave Tanzania $4m in support of HIV and AIDS activities but the reality is that their companies are dumping obsolete technologies in our country.
 

Attachments

  • LastMailTiMinister28.6.07.doc
    53.5 KB · Views: 174
I would like to congratulate you Dr Madati for being honest to your people.
What I dont understand is that if indeed the Minister accepted and acknowledged your commitment which led you to produce a good well researched report why then he went on and gave unfounding announcement to the public? does he himself knew from the beggining a hidden agenda with the other 2 probe team fela?

IT IS GOOD THAT YOU HAVE DECIDED TO ACT WISELY AND BRING THIS MATTER TO THE ATTENTION OF THE PUBLIC.WE ARE NOW EAGERLY WAITING FOR REACTION.

Before we come to our well known conclusion: UFISADI
 
Damn!

after reading all correspondences.....naona kuna kitu bado tutakuwa tunakimiss..........i.e., the other side of Profs...........i mean somethin ain't right or straight here..........

...Kinachosikitisha zaidi ni pale kuona wasomi kama hawa wanapoonyesha upuuzi wa kutokuwa organised from facts findings mpaka presentations.....MIJITU MIZIMA INASHINDWA KUJIONGOZA!!!!!.......SHAME ON YOU ALL!!

TATIZO INAONEKANA BADO LIPO.....na solution haijapatikana na hiyo probe team wamekula pesa.

USHAURI KWA WAZIRI.
1. Watu uliowateua wameshindwa kazi....Mkome Nyani Giladi..........wape notice warudishe pesa zote (wakatwe toka ktk mishahara yao).

2.Unda probe team nyingine

3. Hii ni issue Sensitive Wananchi tunahitaji maelezo ya kina..........nini kinaendelea
 
Damn!

after reading all correspondences.....naona kuna kitu bado tutakuwa tunakimiss..........i.e., the other side of Profs...........i mean somethin ain't right or straight here..........

...Kinachosikitisha zaidi ni pale kuona wasomi kama hawa wanapoonyesha upuuzi wa kutokuwa organised from facts findings mpaka presentations.....MIJITU MIZIMA INASHINDWA KUJIONGOZA!!!!!.......SHAME ON YOU ALL!!

2.Unda probe team nyingine

3. Hii ni issue Sensitive Wananchi tunahitaji maelezo ya kina..........nini kinaendelea

Nakubaliana na wewe.Hii ni aibu kwa wasomi hawa na wametia doa kwa wasomi wengine.Papo hapo nachelea kulaumu kwa ujumlajumla kwa sababu naamini miongoni mwao yupo/wapo waliojitoa kufanya kazi kwa uaminifu ndo maana wakashindwa kuwa na msimamo wa pamoja ambao umesababisha hadi sisi akina yahe tukajua kinachojili.

Kitu kingine kinachosikitisha ni utaratibu wa kulipia matumizi ya kamati,inaonekana mtu binafsi anapewa fungu anaweka kwenye akaunti yake kisha anaamua atumie ngapi na abakishe ngapi ingawa mie sio mfanyakazi nina wasiwsi na hizi taratibu za malipo na kama zilifanya kazi kama zilivyoombwa.

'PROBE' INAWEZEKANA MATUMIZI YA HIZI PROBE TEAM YAKAZIDI BAJETI YA BAADHI YA WIZARA
 
nadhani hapa kuna hoja nzito, ngoja wengine tupitie hiyo attachment.

HEeeeeellooo!
Chemistry iko mbali sana na English?
Halafu, huyu alikuwa 'administrator,' (Chief Chemist) kwa muda mrefu vile, hata taratibu za uandishi wa barua rasmi hakuuzoea?
Na zaidi, si kasoma shule za kikoloni huyu - mbona mambo ni kama yale yale yetu sisi tuliosomea chini ya mwembe?

Anyway, sishangai kamati ile teule kushindwa kazi; kama mambo yenyewe ndio yalikuwa haya.

Hawa warudishe hela, kazi iliwashinda.
 
Prof. Mwakyusa anaswa tena na mtego wa mafisadi

na mwandishi wetu

KWA mara nyingine tena, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kukubali kunaswa na mtego wa mafisadi na kutangaza ripoti ya uongo kuhusu kipimo cha Capillus na mashine ya kupima chembechembe za damu (CD 4) inayojulikana kama Cyflow.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Profesa Mwakyusa aliwaambia waandishi wa habari kuwa kamati aliyounda zaidi ya mwaka mmoja uliopita kuchunguza kashfa ya vipimo vya kupimia ukimwi (HIV rapid Test Kit) na mashine ya kupimia chembechembe za damu, aina ya CD 4, ilibaini kuwa kipimo cha Capillus kinafaa kutumika hapa nchini na kuongeza kwamba mashine ya Cyflow haina ubora wa kutosha.

Alisema mashine hiyo inayotengenezwa nchini Ujerumani, haina uwezo wa kupima chembeche za CD4 zikiwa chini ya 200.

Taarifa hiyo ya Dk. Mwakyusa, inayotokana na ripoti mbili tofauti za kamati moja aliyoiunda na zote mbili zikipingana, moja ikisema kuwa uchunguzi uliofanywa Muhimbili uligubikwa na rushwa, na nyingine ikisema hakukuwa na rushwa kabisa.


Kamati yake iliyokuwa na watu watatu tu, ilitoa ripoti mbili tofauti zinazopingana; moja ikisema tathmini ya mashine ya Cyflow iliyofanywa na Hospitali ya Muhimbili Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Mwakyusa hakugusia kabisa suala la ripoti hizo mbili, wala kupingana kwake. Na hakuonyesha kabisa kwamba kulikuwa na ripoti mbili tofauti mezani kwake.

Katika mkutano huo, Mwakyusa aliitumia ripoti iliyoficha ufisadi bila kuzingatia kwamba ni yeye mwenyewe aliyewabadilisha vituo vya kazi, watu wote waliohusika katika kashfa hiyo na kuviahidi vyombo vya habari kuwa suala hilo angelikabidhi mikononi mwa PCCB.

Taarifa ambayo inapingana kabisa na utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka mabara yote duniani. Utafiti huo kutoka vyuo vikuu kadhaa vinavyoheshimika duniani kote, unaonyesha kuwa Cyflow, ni moja kati ya mashine bora duniani za kupima chembechembe za damu mwilini. Ni chuo Kikuu cha Muhimbili peke yake duniani kilichofanya tathmini na kuonyesha kuwa mashine hiyo ina udhaifu.

Mmoja kati ya wanasayansi waliompa changamoto Profesa Mwakyusa ni Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Magonjwa (National Institute for Medical Research) Dr. John Changalucha ambaye amesema yeye ameitumia mashine hiyo kwa muda wa miaka miwili sasa na inampa matokeo mazuri kabisa kama alivyotarajia.

Akizungumza na Rai kwa njia ya simu, Dk. Changalucha alisema tangu mwishoni mwa mwaka 2005, amekuwa akiitumia mashine hiyo aina ya Cyflow na inawasaidia sana katika utafiti wa TB na inafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

“Ni mashine ndogo na rahisi kuitumia. Inafanya kazi tofauti na udogo wake,”alisema Dk. Changalucha.

Alisema pamoja na yeye kuitumia mashine hiyo, amekuwa akisoma kutoka kwa wanasayansi wenzake duniani taarifa mbali mbali za ufanisi wa mashine hiyo na hizo ndiyo zinamwongoza kama mwanasayansi.

Dk. Changalucha alitoa changamoto kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuiweka hadharani ripoti ya tathmini iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Muhimbili ili wanasayansi wengine waweze kujua wenzao wa Muhimbili walivyofanya.

“Hivyo ndivyo wanasayansi tunavyofanya. Tunaongozwa na documentations. Tunaposema Cyflow inafaa, tumewasoma wengine. Tunaposema FactsCount inafaa ni baada ya kuwasoma wengine. Hatusikilizi vipande vinavyotolewa kwenye press conference. Tunaitaka ripoti nzima tuisome wenyewe kisayansi. Hiyo ndiyo sayansi,” alisema Dk. Changalucha.

Maelezo ya Dk. Changalucha yanafanana na maelezo ya mabingwa wengine kutoka taasisi kadhaa duniani ambazo zimethibitisha ubora wa mashine hiyo.

Ingawa Profesa Mwakyusa katika mkutano wake na vyombo vya habari alisema mashine hiyo inatumiwa na nchi za Kiafrika tu, na akashangaa ni kwa nini, Rai inaweza kuthibitisha kuwa Profesa Mwakyusa ni mwongo kwani uchunguzi wetu umebaini kuwa inatumiwa katika mabara yote duniani.

Tofauti na maelezo ya Profesa Mwakyusa kwamba mashine hiyo inatumiwa katika nchi za Afrika tu, Rai imegundua kuwa baadhi ya taasisi muhimu zinazotumia mashine hiyo nje ya Afrika ni pamoja na Harvard School for Public Health, Boston, Marekani,

Taasisi ya Human Virology, Chuo Kikuu cha Baltimore, Maryland, Marekani,

Taasisi ya Microbiology, na magonjwa ya kitropiki, Antwerp, Ubelgiji, Taasisi ya Croix-Rouge Française, Paris, Ufaransa,

Maabara ya Kinga ya mwili katika Hospitali ya Pitiè Salpetriere, Paris, Ufaransa.

Nyingine ni Taasisi ya kinga ya mwili, Idara ya Biomedical Sciences, Chuo Kikuu cha Modena na Reggio Emilia, Italia,

Hospitali ya Spallanzani, Rome, Italia,

Taasisi ya Imunolojia katika hospitali ya Pascale, Naples, Italia, Taasisi ya Immunology, katika kliniki ya Robert-Rössle- Berlin Ujerumani, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Bad Oeynhausen, Ujerumani, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Lübeck, Ujerumani, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Münster, Ujerumani, Wizara ya Afya, huko California, Marekani


Kwa upande wa Afrika, zipo nchi nyingi zinazotumia mashine hiyo ikiwa ni pamoja na Senegal, Cameroon, Ghana, Malawi, Sudan, Rwanda, Kenya, Uganda, Zimbabwe na Bukina Faso.

Huko Nigeria, mashine hiyo inatumiwa na mpango wa misaada wa Rais wa Marekani (PEPFAR).

Kwa upande wa Tanzania, taasisi za kidini zisizoguswa na masuala ya ufisadi zinatumia mashine hiyo ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Kanisa Katoliki, Consolata ya Ikonda, Makete ambayo kiongozi wa Hospitali hiyo Padre Sandro, anasema ilikuwa imeshahudumia wagonjwa 2,000 kwa wastani wa wagonjwa 50 kwa siku.

Hospitali nyingine zinazotumia mashine hii kwa upande wa Tanzania, ni ile ya Tanwat Njombe ambayo kwa mujibu wa muuguzi, Bety Liduke, mwaka jana tu, 2007 ilihudumia watu 1,800. Hospitali nyingine zinazofahamika kutumia mashine hizo ni pamoja na Hospitali ya Brock Bond Njombe, na Peramiho ya Songea.

Wakati Profesa Mwakyusa akisema Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitoa kasoro mashine ya Cyflow, kampuni ya Partec inayotengeneza mashine hiyo inasema siyo WHO bali ni watu mmoja tu katika Idara ya Essential Health Technology (EHT) anayewahujumu kwa faida ya kampuni ya Kimarekani. Kampuni hiyo, imeamua kuliandikia WHO ikilitaka limfanyie uchunguzi ofisa wake, ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Essential Health Technologies mjini Bursseles, Dr. Vercauteren Dk. Gaby Vercauteren.

Katika barua yao ya mashtaka iliyopelekwa kwenye chombo cha kisheria cha WHO na nakala kutumwa kwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo, kampuni ya Partec, anataka daktari huyo achunguzwe kwa jinsi alivyohusika katika tathmini ya Muhimbili na anavyoendelea kuipaka matope mashine hiyo.

Kampuni hiyo, pia inataka WHO ichunguze mazingira ya kuajiriwa katika Idara hiyo, Daktari wa Kitanzania, Willy Urassa ambaye wakati wa kuifanyia tathmini mashine hiyo alikuwa akifanya kazi Muhimbili na wanamtuhumu kuhusika katika hujuma hiyo.


Rai imethibitisha kutokana na mawasiano ya barua pepe kwamba Dk. Urassa sasa ni miongoni mwa watendaji katika kitengo cha (EHT) Switzerland. Hatukuweza kupata mawasiliano yake kupitia email yake urassaw@who.int ambayo hadi wakati tukienda mitamboni, alikuwa hajajibu.

Habari zaidi tulizozipata tukienda mitamboni, zinaeleza kwamba Dk. Vercauteren ndiye aliyemwita kazini Dk. Willy Urassa. Sasa Dk. Urassa sasa amehamia Switzerland katika Idara anayoiongoza Dk. Vercaurteren.

Katika ripoti iliyobainisha dalili za rushwa, imeonyesha wazi uhusiano uliokuwapo kati ya Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya na Dk. Vercauteren. Katikati ya tathmini, Dk. Ndugulile alimpelekea Dk. Vercauteren ujumbe wa email ya Desemba 23 mwaka 2005 akimwambia mambo ya siri yaliyoonekana kwenye tathmini ambayo yeye alikuwa hahusiki nayo. Ni Dk. Ndugulile mwenyewe aliyepeleka email hizo kwenye kamati ya Profesa Mwakyusa lakini akiwasihi wasimtaje.

Kitu kinachowashangaza wengi ni kwamba wakati mashine ya Cyflow ililazimika kupitia katika chekeche mara tano katika kipindi cha miezi 12, mashine iliyopewa baraka haijawahi kutathminiwa nchini licha ya sheria kutaka kufanya hivyo. Kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Maabara za Afya za Umma mwakla 1997, na tangazo la serikali namba 226 kifungu kidogo cha 2.5.2 (1)—(v) linalotoa masharti ya matumizi ya kifaa chochote cha tiba, ni lazima kifaa chochote kipate tathmini moja ndani ya nchi, na moja nje ya nchi. Zaidi ya mashine 40 za Facts Count zinazotumika hapa nchini, hakuna hata moja iliyofanyiwa tathmini hapa nchini.

Ripoti hiyo ya awali ambayo Profesa Mwakyusa hataki kuiongelea, inaonyesha kuwa kulikuwepo na mbinu nyingi zilizoandaliwa kuichafua mashine ya Cyflow wakati wa kuifanyia tathmini, jambo ambalo lilisababisha ionekane haina ufanisi wa kutosha. Moja ya mbinu ilikuwa ni kuchelewesha vifaa vyake toka bandarini ambayo ripoti mpya inasema vilicheleweshwa na kampuni inayoitengeneza.

Baada ya matokeo ya tathmini hiyo kutolewa, Oktoba 6, 2005, Dk. Roland Gohde, Rais wa kampuni inayotengeneza mashine hizo na ambaye pia ndiye Mtendaji Mkuu na mtoto wa mwasisi wa mashine hiyo, Profesa Wolfgang Gohde, alilalamikia matokeo hayo akisema: "Uchunguzi wa MUHAS ulichukua kipindi kirefu cha miezi 14 bila sababu na hivyo kusababisha vitendanishi kuisha muda wa uhai wake (expiry) na hivyo kutoa majibu yasiyo sahihi.

Aliongeza: "Ripoti ya MUHAS kwamba mashine ya Cyflow ni dhaifu katika kupima idadi ya CD 4 pungufu ya 200 si sahihi na haiendani na ripoti za wanasayansi wengine maarufu duniani kwa lengo la kuzinufaisha mashine zilizokuwepo za Facs Counter kutoka Marekani."

Baada ya kupigwa marufuku Cyflow, sasa Tanzania imebakiwa na mashine aina ya Facs Counter ambaye kila kipimo kimoja kinagharimu dola 40 za Kimarekani. Gharama ya kipimo cha Cyflow ni dola 2 tu.

Ili nchi kuweza kufikia ufanisi katika upimaji na udhibiti wa virusi vya ukimwi, kunahitajika angalau aina nne za mashine zikiwapo rapid test, CD4 tests, viral load na chemistry analyzers.


Kwa Tanzania, ni mtu mmoja tu Bharat Rajan wa Biocare Health Products ambaye huwa anashinda mara zote tenda zote za kuingiza vifaa hivi. Kampuni hii imekuwa na ukiritiba huu tangu mwaka 1966 na mtu akitaka kuagiza mashine za kupima CD4, ni lazima apeleke proforma invoice kwa Rajan ambaye ndiye anaruhusu mashine hiyo kuletwa ndani kwa masharti kwamba ni lazima iwe Facts Count. Wakati fulani, aliyekuwa Waziri wa Afya, Anna Abdalah aliwahi kuonya maisha ya Watanzania kuwekwa mikononi mwa mtu mmoja.

Source: Gazeti la Raihttp://www.newhabari.com/rai/habari.php?id=507&section=habari
 
SOMA RAI !

03.04.2008

Sasa Wizara ya Afya yatetea takataka zake

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]na mwandishi wetu

KATIKA kipindi kisichozidi wiki tatu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imetoa taarifa mbili, zenye maelezo yanayojipinga yenyewe kwa yenyewe kuhusu ununuzi wa vitendanishi aina ya Capillus na kutuhumiwa kueleza uongo dhidi ya ubora wa mashine ya kupimia chembechembe za CD4 aina ya Cyflow.

Mkanganyiko huo umejitokeza baada ya wizara hiyo kutoa taarifa zinazopingana kuhusu msimamo wake juu ya matumizi ya vitendanishi vya Capillus na matokeo ya tathimini ya mashine ya Cyflow.

Na katika kilichoonekana kama kutaka kujisafisha, wizara hiyo imetumia mamilioni ya shilingi kununua kurasa za magazeti ili kutoa taarifa ya kuweka sawa mambo. Hata hivyo, taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Wilson Mkama, ina mambo yanaoonekana kupingana na taarifa iliyotolewa na waziri wake, Profesa David Mwakyusa

Taarifa aliyotoa Profesa Mwakyusa wiki mbili zilizopita, ilieleza kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitaarifu wizara yake kwamba mashine hiyo haifai. Hata hivyo, katika tangazo la wizara la wiki hii, wizara inasema WHO haijawahi kuwaambia kuhusu mashine hiyo kwa sababu haijawahi kuifanyia tathmini. Tangazo lilisema kuwa WHO liliwashauri kuwa wafuate vigezo vya nchini ili kutumia au kutoitumia mashine hiyo.

Habari ambazo Rai imezipata kutoka Shirika la Afya Duniani, zinaeleza kuwa chini ya utaratibu wa shirika hilo, ili teknolojia mpya ya kitabibu iweze kutumika katika nchi yoyote, ni lazima iwe imefanyiwa tathimini tatu; kati ya hizo, tathmini moja iwe imefanyika katika nchi husika na mbili katika taasisi nyingine za kimataifa. Hata hivyo, Rai inayo taarifa kwamba mashine aina ya FactsCount iliyochaguliwa, haijawahi kufanyiwa tathmini hapa nchini.

Mbali ya maelekezo ya WHO, pia sheria za Tanzania zinataka hivyo. Kitu kinachowashangaza wengi ni kwamba wakati mashine ya Cyflow ililazimika kupitia katika chekeche mara tano katika kipindi cha miezi 12, mashine iliyopewa baraka (Facs Counter) haijawahi kutathminiwa nchini licha ya sheria kutaka kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Maabara za Afya za Umma mwaka 1997, na tangazo la serikali namba 226 kifungu kidogo cha 2.5.2 (1)—(v) linalotoa masharti ya matumizi ya kifaa chochote cha tiba, ni lazima kifaa chochote kipate tathmini moja ndani ya nchi, na moja nje ya nchi. Zaidi ya mashine 40 za Facts Count zinazotumika hapa nchini, hakuna hata moja iliyofanyiwa tathmini hapa nchini.

Shirika hilo la Afya duniani, limethibitisha kwamba tayari limekwishanunua mashine 100 aina ya iliyokatazwa Tanzania na kuzisambaza nchi mbali mbali duniani. Hivi sasa, India inaziondoa mashine zote za FactsCount na kuzibadilisha na Cyflow. Thailand ina mashine zipatazo 132 na zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa nchini humo. Katika taarifa yake wiki mbili zilizopita, Waziri wa Afya, alisema kwamba Cyflow, zinatumika katika nchi za Afrika tu.

Kwa upande wa vitendanishi aina ya Capillus,Wizara hiyo inakiri kwamba mwaka 2004, baada ya Serikali kuamua kupeleka huduma za upimaji wa VVU hadi vijijini iliamua kutafuta vitendanishi mbadala ambavyo havihitaji uhifadhi wa baridi, na kutangaza rasmi azma ya kuachana na Capillus mwaka 2006. Wakati akitoa taarifa yake wiki mbili zilizopita, Waziri wa Afya alisema wizara yake itaendelea kuzitumia Capillus kwa sababu imeandaa miundo mbinu ya kutosha. Hata hivyo, tangazo la Jumatano wiki hii katika magazeti mbali mbali, wizara hiyo hiyo imesema kuwa inaviondoa vitendanishi hivyo kwa sababu haina uwezo wa kuvitunza katika jotoridi la nyuzi kati ya mbili hadi nane kwa muda wote.

Katika ununuzi wa vitendanishi hivyo, Wizara ya Afya imeendelea kutoa kisingizio kwamba bado watumishi wake wapo katika mchakato wa mafunzo kuhusu matumizi ya vitendanishi vingine.

Vitendanishi hivyo ambavyo viliingizwa na wizara katika utaratibu mpya wa upimaji wa Virusi vya Ukimwi (New Algorithm) ni Unigold, SD Bioline na Determine. Pia wizara hiyo inaeleza kuwa ingawa mafunzo hayo yalipangwa kufanyika mwaka jana, Wizara hiyo, ilirefusha muda wa utoaji wa mafunzo hayo kwa kisingizio kwamba baada ya kutangazwa kwa kampeni ya kitaifa ya upimaji VVU utaratibu wa utoaji mafunzo pia ulivurugika. Kwa mujibu wa wizara, maelezo hayo ndiyo yaliyotoa mwanya wa kuendelea kutumia vitendanishi hivyo nchini.

Taarifa ya Wizara ya Afya inaeleza kuwa Julai 12 mwaka jana, Bohari Kuu ya dawa nchini (MSD) iliagizwa kununua Kits 21,896 za vitendanishi vya Capillus zenye thamani ya takriban Sh. bilioni nne kwa kufuata taratibu za sheria za ununuzi. Hata hivyo maelezo hayo yamezua mkanganyiko mwingine kwani wizara iliagiza vitendanishi hivyo vinunuliwe wakati vilishaondolewa katika 'Nationa Algorithm'.

Kwa maelezo mengine ni kwamba vitendanishi hivyo vilinunuliwa huku vikiwa havijasajiliwa na Bodi ya Maabara za Umma (PHLB), jambo ambalo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria ya ununuzi wa vifaa vya afya.

Mkanganyiko mwingine unaojitokeza ni pale Wizara ya Afya ilipoamua kununua idadi kubwa ya vitendanishi hivyo na kuviingiza nchini kwa awamu saba kwa kisingizio kwamba ilifanyika hivyo ili kulinda ubora na uhai wa vitendanishi hivyo kwa sababu ya hifadhi yake. Pamoja na kwamba jambo hilo ni ukiukwaji wa taratibu za sheria za ununuzi, Rai imekuwa ikipigia kelele suala hili la uwezo wa nchi kutunza vitendanishi hivi ambavyo vinahitaji kutunzwa kwenye nyuzi joto mbili hadi nane kwa wakati wote kwa mujibu wa maelekezo ya Shirika la Afya Duniani aliyotumiwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo mwanzoni mwa kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU.

Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya wameliambia Rai kuwa lengo la kununua vitendanishi hivyo na kuviingiza nchini kwa awamu kulitokana na hali halisi ya hapa nchini kwamba hapakuwapo na vifaa vya kutosha vya kutunza vitendanishi hivyo, jambo ambalo limeendelea kuwa tatizo kubwa hadi leo.

Maofisa hao wamesema kwa kuwa hali ya utunzaji wa vitendanishi hivyo ilikuwa ikijulikana tangu awali, hapakuwapo haja ya kusaini mkataba wa kununua Kits nyingi kwa mkupuo kisha ziletwe nchini kwa awamu saba. Baadhi ya vyanzo vyetu vya habari vilieleza kuwa mkataba huo ulikuwa na lengo la kutumia kisingizio cha kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU kununua idadi kubwa ya vitendanishi hivyo.

Uchunguzi uliofanywa na Rai kwa siku kadhaa umebaini kuwa vitendanishi hivyo vimekuwa vikiagizwa

nchini na kuhifadhiwa kwa muda katika maghala ya MSD kisha kusambazwa mikoani bila kuzingatia

masharti ya kuvihifadhi katika nyuzi joto kati ya mbili hadi nane.

Taarifa ya sasa ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayoeleza kwamba baada ya vitendanishi (capillus) vinavyotarajiwa kuingizwa nchini mwezi huu, Serikali haitanunua vitendanishi vingine vya aina hiyo, inapingana na taarifa iliyotolewa na wizara hiyo hiyo wiki chache zilizopita iliyokuwa ikielezaa kuwa kipimo cha Capillus ni bora. Hivyo vitaendelea kutumika nchini. Taarifa hiyo iliongeza kwamba wizara hiyo ina vifaa vya kutosha vya kutunza vitendanishi hivyo.
[/FONT]

tumepata e-mail leo:

"...We must realise that there is a serious problem but this is as far as the people are ignorant. The political leadership is usually misled. Once the information is public,even the president will be forced to perform his constitutional duties.

We had similar situations in Kenya which need a whistle blower.

Yesterday, the meeting between the some four selected journalists ended up not being a press conference!!
The minister wanted to find a way of cover up since the matter is very serious there. He wants to bribe the journalist to 'go slow'. He even wanted to find out the source of original report.You can see he is fully involved in the corrupt deal.

Its important to note that a similar scandal was reported by ThisDay recently but on Financial scandal at the central bank of Tanzania..."

"...Concerning Mr Rajani of Biocare,I understand the man lost his wife a few months ago. The funeral was attended by almost the whole Cabinet including the prime minister. This shows that the man has used his money in many ways than one. We must therefore scare away his seasonal political friends by exposing the matter..."
 
Kinachoendelea hapa ni hadithi za kusadikika. Wale wanaodai ni wasafi ndio wachafu kuliko.
Kinachoendelea hapa ni kuwa kuna wanasiasa wenye maslahi na vifaa husika. Wanawachafua watendaji wa Wizara ya Afya ili waweze kutimiza azma yao ya kuingiza vifaa vyao vya maabara.
Lengo lao ni kupata gawio katika fedha za UKIMWI. Bahati mbaya baadhi ya waandishi wamekuwa wakitumiwa kuishambulia Wizara ya Afya bila kupata upande wa pili wa "saga" hii.
 
Mimi binafsi nafikiri tatizo hili la Ukimwi Afrika, miongono mwa sababu nyinginezo,moja wao ikiwa upungufu wa elimu ya kutosha, na hulka za waafrika.

Hadi miaka ya katikati ya tisini,elimu ya ukimwi na magonjwa ya ngono yalikuwa hayaja wafikia wengi,Tanzania,napia nchi za ulaya na marekani msisitizo ulikuwa si mkubwa kwavile maambukizi hayakuwa mabaya. Watu walikuwa wanafikiri mtu mwenye ukimwi utamjua kwa kumuangalia usoni au atakuwa amekonda, hivyo watu walikuwa wanangonoka tu bila hofu, ndio maana miaka hii wale carrier ndio wanaugua, sasa jumlisha ni watu wangapi alisha waambukiza kipindi hicho ambacho alikuwa hajui ana virusi.

Kuhusu tabia za kufanya ngono,jamani tukubalini tu,wazungu ngono wanafanya,tena sana tuu lakini wenzetu kwa kujikinga wanajua na wanaweka mbele sana.Kama wanatoka nje ya ndoa wazungu huwa na tabia ya kujikinga,sisi waafrika pamoja na kujua kuhusu kondomu hulka hiyo hatuna!!!!!na zile traditions zetu kwamba wanaume hata kwenye ndoa ana uhuru wa kuzaa nje analeta mtoto nyumbani mke hana usemi,kwa vile anahofia talaka na wazee wanamshauri aendelee!!!hizi tabia zimeua sana.

Kingine ulimbukeni wa baadhi ya waafrika wengi,akifanikiwa akapata cheo,au pesa nyingi basi maisha ni kulala na wanawake bila kondomu madai ndio utamu zaidi.

Wanawake wakiafrika wameathirika sana kwavile hali ya umasikini ya bara la afrika mwanamke anakosa njia nyingi ya kujikwamua maisha zaidi ya kumtegemea mwanaume, either ajiuze au avumilie ndoa kwa mwanaume ambaye anafanya ngono nje.

Hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo zime/zinaifanya afrika kati ya mabara yote kuathirika mno,na unless tuna badilika tutabaki tu kuwalaumu wazungu wanatusingizia.

Mimi binafsi nimepoteza ndugu na marafiki wengi sana kwa ukimwi,wengi wakiambukizwa wakiwa ndoani.

Hii tabia ya kuficha maradhi ni mbaya mno,watu hawasemi,kama mtu alikuwa na virusi vikamsababishia cancer au tb au stroke au uti wa mgongo,basi isemwe tuu marehemu aliathirika na virusi vya ukimwi vilivyo msababishia ugonjwa.... ulio muua. Ina saidia hata wale aliowaambukiza ambao bado wapo wajiwahi matibabu mapema na ili wasiendelee kuambukiza wengine.

Mungu ainusuru Afrika na watu wake.
 
Nionavyo Mimi Kwa Wale Ambao Wameshagonga Ni Kuwaacha Bila Ya Kuwapa Dawa Za Kurefusha Maisha Ili Wafe Mapema Waache Kuambukiza Wengine Maana Ukiwasikia Wenyewe Wanavyojisifia Ati Ni Lazima Waondoke Na Wengi.kwa Hiyo Bomu Tunajitengenezea Wenyewe. Maana Angalia Hata Wakishameza Zile Dawa Wanavyonawiri Na Wengine Wamediriki Kuniambia Ati Nguvu Zao Za Kungonoka Zimekuwa Mara Dufu Baada Ya Kumeza Dawa Za Kurefusha Maisha. Sasa Hamuoni Ni Hatari Hii? Hakuna Wakati Mgumu Kwa Waafrica Ktk Dunia Hii Kama Sasa, Lakini Cha Ajabiu Wenyewe Hawajali Ni Lazima Wajue Janga Hili Ni Kubwa Kuliko Vita Zote Kuu Tatu Zilizopita Za Dunia.
Are you for real????? How can you ever suggest something like this???
 
Niliku Nafanya Maongezi Na Rafiki Yangu Mmoja Mtaliano Maongezi Ya Kawaida Tu, Basi Nikajikuta Nagusia Suala La Ukimwi Tanzania Na Namna Gani Ya Kukabiliana Nalo Basi Yule Bwana Alinionea Huruma Sana Na Akaniambia Kuanzia Sasa Hesabu Miaka Kumi Mbele Na Siyo Tanzania Pekee Bali Na Karibu Nusu Ya Waafrica Wote Wanaoishi Africa Watakuwa Wameteketea Kwa Ugonjwa Huu Mbaya Kabisa Kutokea Tangu Kuumbwa Kwa Dunia. Nilipomuuliza Ni Kwanini Akaniambia Waafrica Huwa Hawajithamini Na Haswa Wale Waliooa Na Walio Olewa Akazidi Kusema Africa Ni Rahisi Kabisa Kufanya Ngono Na Mke Au Mume Wa Mtu Kuliko Mahala Pengine Popote Duniani Na Hata Hao Wanaojiita Maboyfriend Na Na Girlfriend Asilimia Nyingi Ni Wanafiki Wa Wanagawa Uroda Kwa Yeyote Mwenye Kuhitaji Akasema Asilimia 95 Ya Waafrica Hawajiheshimu Wala Kujithamini Ktk Suala La Ngono

The notation that "Waafrika Hawathamini miili yao na ndoa zao" is not a fact. Kinachokosekana kwa Waafrika kwa ujumla ni elimu ya kutosha juu ukimwi, kumbuka jamii za Kiafrika wazazi hawapo Comfortable to talking about sex with their childrens. Ninaishi Marekani kwa muda wa miaka kumi, kama kuna jamii inayopeda kugawa uroda ovyo ni watu wa dunia ya kwanza, kama kuna watu wasio thamin ndoa zao ni watu wa dunia ya kwanza. Remember divorce rate in the first world is 50%.
 
Kwa ngono onyo waZungu wanaongoza labda kwao haukuenezwa sana kama ilivyo Afrika. Je ni kweli ukimwi umetengenezwa maabara na ni Biological weapon ya Marekani kudhoofisha baadhi ya mataifa hasa Africa for their future benefits?Hebu mwenye historia ya ukimwi atumwagie kidogo ili wale wasioelewa sawasawa kama mimi tupate kuelewa na kujilinda zaidi. Wanataka kupunguza manpower ya Africa maana ni hatari kwao baadae hasa wengi wakipata elimu ya kutosha na kupambana nao ktk nyanja mbalimbali.
 
Back
Top Bottom