Ufisadi ndani ya Mlimani City Project

ila kuhusu effective use of the land kama anavyosema bwana mundu..ni kweli..pale kuna kosa..originally yale majengo yalikuwa yawe ni gorofa angalau moja hata watakaokumbuka ile michoro ya kwanza kabisa ilikuwa inaonyesha hivyo na hata engineer aliyefanya EIA (environment impact assesment) namjua kuna siku alisema hivyo...sasa kinachotokea i dont know...

kuhusu zile nyumba za mama Ana Mkapa pale kuna bomu na utapeli mkubwa sana, mama ana alilazimika kuzifanya ziwe za yatika baada ya ishu kufumuka..kwa plan ile hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuamini kwamba zile nyumba zilikuwa za watoto yatima...yule mama hana roho nzuri kiasi hiko..
ukiangalia vizuri hata plan ya finishing aliibadilisha badae..kaangalie madilisha...ilikuwa yawe ya vioo lakini mwisho ikapigwa nyavu ya kawaida tu...labda nae tutaangalia huko baadae itakuwaje na ana mkataba gani na serikali kuhusu ile ardhi but it is a completely a waste...


SIKU ZOTE NCHI ITALIWA NA WAJANJA...

Its obvious you know more than you are revealing je kuna ubaya gani kama client aliamua kubadili mawazo? consultant si anafuata tuu au ?
 
Hivi hawa na NORCONSULT kitu kimoja? if so then mmoja wao alikuwa na kashfa ya rushwa na serikali imepewa ripoti na jamaa wa WORLD BANK lakini madudu yaliomo humo ndani hiyo ripoti haiwezi kuwekwa public...kisa? wakubwa wametajwa

Sio kitu kimoja. ni kampuni mbili tofauti, NORCONSULT ni washauri wa ujenzi na NOREMCO ni wajenzi (contractors) ila zote ni kampuni za Norway.
 
Hold on! Hivi hebu ni waulize, hata kama huyo jamaa asingepewa miaka 50 au hilo eneo nani tanzania angeweza jenga hilo eneo the way it is with this UFISADI? Nani angeweza kuja na project ya namna hiyo. The lesser evil. Mi sion shida.
 
Hivi hawa na NORCONSULT kitu kimoja? if so then mmoja wao alikuwa na kashfa ya rushwa na serikali imepewa ripoti na jamaa wa WORLD BANK lakini madudu yaliomo humo ndani hiyo ripoti haiwezi kuwekwa public...kisa? wakubwa wametajwa

I am not sure ni mradi gani, lakini nina hakika kuwa NOREMCO hawali rushwa wala kujihusisha nayo, hii imeiweka kwenye wakati mgumu sana hasa kupata miradi ya barabara! walishinda tender ya BOT lakini walitakiwa watoe kitu kidogo wakagoma! badala yake wakapewa hao group five. Noremco dereva akikamatwa na trafiki akatoa rushwa hana kazi!
 
Jamani wadanganyika wenzangu kwa info nilizozipata kutoka kwa wachunguzi wa mambo kuhusu mkataba wa mwarabu wa Mlimani City na Chuo Kikuuu...

Habari zinasema yule mwarabu kapewa kile kiwanja ajenge na afanyie biashara kwa muda wa miaka 50 bila kulipia kodi yoyote........ halafu baada ya muda huo ndo majengo na kila kitu vinakuwa chini ya chuo... Ebu tuangalie hii kitu jinsi ilivyokaa..

Ni nani atakaye faidi katika huu mkataba?

1. Je mwekezaji ametumia sh. ngapi kuwekeza??
2. Je baada ya miaka 50 atakuwa amerudisha hela yake?
3. Je design life ya majengo ni miaka mingapi? na mkataba unasemaje kuhusu hilo?
4. Je mandhari ya pale yatakuwaje baada ya miaka 50?? na how economy of city will be stimulated?
5. je unafikiri mataba wa miaka mingapi huko sahihi?
6. Je unatishika na namba ya miaka au ufisadi?? mwekezaji angesema atawapa baada ya miaka 3 ungefurahi hata kama kuna ufisadi ndani yake?
 
Ni bahati mbaya sana tumewaruhusu watu kuleta mada ingali hawajafanya utafiti wowote ule! Ninaona hata shida kuchangia maana utaanzia wapi! Mradi wa Mlimani City ni mchakato wa siku nyingi ulianzia 1994, na kuna land use plan ilifanywa na Ardhi University wakati ule na baadae wakatengeneza Strategic Plan. Matokeo ya jitihada hizi ilikuwa NSSF alitamani na yeye kuwekeza lakini masharti yakawa magumu. NSSF alitakiwa atoe premium ya Tshs 1.5bn wakati ule kwa ajili ya ardhi ya kujenga hostel. Alivyoona ni ghali, aka-offa kutumia kiwanja alichokuwa tyari katika mkakati wa kununua kutoka Breweries na hiyo ikawa ni mwanzo wa Mabibo Hostel.

Hawa wa Botswana wametoa premium na wanalipa jamani, miradi hii ilikuwa chini ya the then Income Generation Unit, isingewezekana ikawa kiholela hivyo. Masharti yapo, kama mnaopita pale mtaona sasa wanajenga vitu vinavyofanana na mahitaji ya Chuo Kikuu, siwezi nikakumbuka chapu chapu kichwani lakini kuna Conferences, maofisi na maabara na amusement park ambayo itasaidia pia kwa wale wanaojihusisha na maisha ya wanyama (zoology).

Samahani kama nimeandika kwa hasira wakuu, maana kweli bila utafiti huruhusiwi kusema.
 
Ole Naiko na nani? Mshana sijui ni nani. Mnawaonea tu. Muulizeni Dr Chungu ambaye alikuwa Director of Planning wa UDSM wakati wakinegotiate mradi huu na huyo mhindi wa Botswana.

The little I know, pamoja na kulipwa kodi kwa sasa UDSM ina shares za 25 per cent. Baada ya muda shareholding itakuwa inaongezeka. Sasa sijui kama hiyo ni bad deal. Kwa sababu hiyo 25 per cent ni contribution yake kwa njia ya ardhi yake. Halafu wanalipwa percent fulani ya kodi pamoja na certain percentage kwa kile kinacholipwa na wapangaji wengine. Sasa Mungu akupe nini.

Hivi nyie waswahili mnataka 100 peecent bila hata kuingiza kitu? Hvi mkoje nyie? Mimi I think Dr Chunga na wenzie didi a good job. Kudos to them
 
Ole Naiko na nani? Mshana sijui ni nani. Mnawaonea tu. Muulizeni Dr Chungu ambaye alikuwa Director of Planning wa UDSM wakati wakinegotiate mradi huu na huyo mhindi wa Botswana. The littke I know pamoja na kulipwa kodi kwa sasa UDSM ina shares za 25 per cent. Baada ya muda shareholding itakuwa inaongezeka. Sasa sijui kama hiyo ni bad deal. Kwa sababu hiyo 25 per cent ni contribution yake kwa njia ya ardhi yake. Halfau wanalipwa percent fulani ya kodi pamoja na certain percentage kwa kile kinacholipwa na wapangaji wengine. Sasa Mungu akupe nini. Hivi nyie waswahili mnataka 100 peecent bila hata kuingiza kitu? Hvi mkoje nyie? Mimi I think Dr Chunga na wenzie didi a good job. Kudos to them



Thibitisha hizo taarifa zako!!!!
 
Back
Top Bottom