Ufisadi mpaka michezoni

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
Mtibwa Sugar matatani
William Mjema
Daily News; Tuesday,January 06, 2009 @21:15

Timu ya Mtibwa Sugar iko katika hatari ya kupewa adhabu na Shirikisho la Soka Tanzania kutokana na klabu hiyo kutoa taarifa ya kulidanganya shirikisho hilo. Pia TFF imekataa ombi la klabu ya Moro United la kutaka mechi yake dhidi ya Azam FC iliyopangwa kufanyika Jumatatu ijayo iahirishwe kutokana na timu hiyo kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar inayoendelea.

Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema kuwa Januari 4 mwaka huu, Mtibwa iliiomba TFF kuahirisha mechi zake za Ligi Kuu kutokana na kuwa na wachezaji sita kwenye timu za taifa za Bara, Kilimanjaro Stars na ile ya Zanzibar, Karume Boys.

Mtibwa iliwataja wachezaji hao kuwa ni Shabani Nditi na Salum Swed alioko kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars na wale wa Karume Boys ambao ni Salum ussi, Abdulhalim Hamoud, Abdallah Juma na Soud Abdallah.

“Baada ya kupokea barua hiyo, TFF ilifuatilia kufahamu kama wachezaji walioko kwenye timu ya Zanzibar inayoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji na kubaini kuwa hakuna mchezaji hata mmoja kati ya waliotajwa kuwamo kwenye kikosi cha Zanzibar.

“Kutokana na mazingira hayo, Mtibwa wameandikiwa barua ya kutakiwa kutoa maelezo ni kwa nini klabu hiyo isiadhibiwe na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kutoa taarifa kwa uongozi zenye lengo la kupotosha vyombo vya maamuzi vya TFF,” alisema.

Akizungumzia ombi la Moro United, Kaijage alisema kuwa shirikisho lake limekataa ombi hilo kutokana na kutoombwa wala kuarifiwa kwa wakati mwafaka na Moro United juu ya ushiriki wake katika michuano hiyo. “TFF ilikwisha toa ratiba ya Ligi Kuu tangu Agosti 2008 kwa klabu zote ikiwamo Moro United na kupeleka tena marekebisho ya ratiba mwishoni mwa Desemba 2008.

“Ratiba inawadau wengi wakiwamo waamuzi, makamisaa, klabu, wasimamizi wa vituo na wamiliki wa viwanja ambao wote wanahitaji kupewa taarifa mapema. “ Moro United iliamua kushiriki mashindano hayo kwa hiyari yake. Hivyo taratibu za michezo ya Ligi Kuu zinaendelea kama zilivyopangwa na ratiba itaendelea kusomeka kama ilivyotangazwa.” Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu umepangwa kuanza Jumamosi.
Source: HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Mtibwa Sugar matatani
 
Back
Top Bottom