Mkuu itoshe tu kusema unamawazo mgando na yakizamani sanaYanayoendelea kwa vijana wetu Wasomi na ambao sio Wasomi huwezi kutofautisha kitu Katika kundi hili. Hoja za matusi na kutukana ndio njia pekee ya hawa vijana, Wanaamini upande mmoja wa habari
Yawezekana ni makosa yetu wazazi kuwajaza watu ujinga na wao kuyaamini kama yalivyo bila kufikiria au kujiridhisha
Mambo yafuatayo yameonyesha aina ya watu na vijana tulionao hapa JF :
Mosi, Hoja za kuendeleza gesi na maamuzi ya kutafuta wanasheria wa nje kwa ushauri, Vijana wamejazwa upepo kuwa wao wanaweza kazi hii ya sheria za kimataifa kwa kusoma soma sheria za International law pale Udsm na Udom, Wamekaa wanakula popcorn hawaelewi kuwa serikali inalipa madeni mengi kwa kudharau sheria za kimataifa, Ushauri wa kipuuzi wa wanasheria wa ndani kuwa tunaweza serikali imeishia kulipa hasara na medeni
Pili, Hoja za Bandari ya Bagamoyo, Wengi wamejazwa upepo bandari haifai,Wachina wanatupiga. Ukiwauliza wewe unafahamu mkataba wake anajibu nilimsikia Rais na Waziri. Leo hii mtu anaweza sema tutaajiri vijana 100,000 serikalini na vijana wanapiga makofi, Ukiuliza ajira zitatoka wapi kwa pesa ipi hakuna majibu, Mtu haelewi hata maana ya kina cha bandari bali utasikia aaha kule Bagamoyo si kwa Mzee JK ndio maana wanajenga bandari, Ukimuuliza sasa ulitaka JK azaliwe Dodoma
Tatu, Hoja za Freeman Mbowe na kesi inayoendelea huko mahakamani, Utasikia Leo shahidi amegalagazwa vibaya sana, Tangu lini shahidi akagalagazwa? Shahidi anaeleza alichokiona Yeye na kukishuhudia, Maswali anayoulizwa nje ya yale aliyoyasema na kuyaandika hayamuhusu,Jaji anajenga msingi kwa alichokisema shahidi, Maswali ya kuwa una degree ngapi? Una wake wangapi? Unamfahamu Tundu Lisu? Uliona watu wakibeba petrol na magogo?. Haya yote inategemea kama shahidi aliyasema kama hakuyasema ni kupoteza muda kumuuliza, Maswali nje ya context ya alichokisema na kukiandika shahidi ndio vijana wanashabikia huku wakiwa na Tecno na itel za wachina wasiowataka kujenga bandari ya Bagamoyo
Hoja ya Ridhwani Kikwete kuwa naibu Waziri, Utasikia aaha yule Ridhwani hafai kabisa, Ukiuliza lini Ridhwani amewahi kuwa Waziri na akakosea hakuna Jibu lolote, Lipi baya alilofanya Ridhwani utasikia aahaa nchi sasa imerudishwa kwa wapigaji, amepiga pesa gani hakuna majibu, Kumbe wanaumia kwanini mtoto wa fulani kawa Waziri, Kwanini uumie mtoto wa Mo Dewji kuwa tajiri kama Baba yake ulitaka avae kandambili zilizoshonwa shonwa
Hoja za Spika Ndugai kujiudhuru na chama chake cha ccm, Utasikia Spika ameonewa na Rais ana nguvu zaidi. Je unafahamu taratibu za ndani za ccm kanuni na maadili ambayo chama kilimpendekeza Ndugai kuwa Spika, Utasikia sifahamu, Ndani ya ccm mtu anawajibika kwa chama chake kwanza halafu ndio anawajibika kwenye nafasi yako uliyopewa, Hata Rais Samia anawajibika kwenye chama kwanza halafu kama Rais, Chama ndio kimekupa nguvu na sio cheo, Ndugai alivunja maadili na kanuni za chama kilichompendekeza awe Spika kwa kushindwa kujizuia kutofautisha nafasi akiwa Bungeni na nje ya Bunge
Vijana ambao wanategemea akili za watu wengine wawafikirie kwa niaba yao, Hao ni vijana mfu
siku hizi jf kunazidi kujaa watu wa hovyohovyo yani mtu anakuwa na akili mgando kiasi ambacho unashanga kama huyu ni mtu alopita vidudu ama la.
Nianze tu na wale watu wa kupandikizana chuki dhidi ya mtu flani, kundi flani ama taasisi flan, Watanzania tuache hiyo mihemko ya kubeba chuki ndani ya mioyo yetu kisa flani kasema simpendi flani na nampenda flani unakuta mtanzania anachuki haswaa na tasisi flani ukimuuliza wamekufanyajee utasikia oooh sijui ilikuwa hivi mara vilee. kiufupi usimkumbatie adui wa mwenzako na kutembea nae,
Mtoa mada ka sijakuelewa kuhusu issue ya Bwagamoyo!
issue ya bwagamoyo binafsi sijawahi ielewa hata na sitokaa nielewe, sioni sababu ya kujenga bandari bwagamoyo wakati mtwara na tanga kuna bandari nzuri zenye kina kizuri tuu na hata kama tukizitengeneza hazita gharimu fedha nyingi kama kwenda kuchima huko bwagamoyo. Bandari ya Dar inagharama nyingi kutokana na utoaji wa mchanga wa mara kwa mara pili mji ushakuwa huu tunahitaji kukuza miji mingine.
binafsi napendekeza kama wanamalengo mazuri fedha za Bwagamoyo wazihamishie mtwara ambako kunabandari nzuri yenye kina kirefu kisichihitaji kuchimbwa tena pia itafanya mkoa wa mtwara kuinuka kiuchumi, ikumbukwe sina maslahi na Mtwara
kama kweli ile kauli aliyozungumza mkuu aliyetangulia ni kweli basi hatuna haja ya kuwa na mikataba ya namna hiyo,tatizo lilipo bandari ya Dar es salaam la Sand deposit ndio tatizo linaloikuta Mtwara na Tanga... Bandari zote hizo zina mlango wa kuingilia meli sio an OPEN SEA matokeo yake ni Sand deposit za mara kwa mara na kizuizi kwa Mega Ships + Super tankers..
Bagamoyo ilichaguliwa na wawekezaji wenyewe baada ya research yao kwa bandari zote hizo, Bagamoyo ikaonekana ina kina kizuri, Open sea, na hakuna sand deposit, lakini pia kuna eneo kubwa lipo tupu tayari kwa ujenzi....(issue hapo ibaki kwenye mikataba tu)
Uzi wa kijinga zaidi tangu mwaka uanze
Na wengi waliomo humu ni wajinga kupindukia ,ndio maana Prof Baregu alisema nchi hii vijana ndio wapumbavu ,uwezo wao wa kufikiri ni mdogo na ndio maana kutwa nzima kupinga tu
Tupe mkataba ambao ni wanserikali na uliwekwa wazi,tuanzie na mkataba wa SGR na JNHPWewe toa ushahidi kama hakuna upigaji!
Ndio maana tukataka mikataba iwe wazi
Demokrasia ni pamoja na kutofautiana kwa facts sio kupinga tu eti democrasia ,Uzi wa kipumbavu kabisa. Mawazo yake ndio anataka yawe mawazo ya watu wote. Watu tumetofautiana kwenye kila kitu na ndio demokrasia hiyo....
Ndio maana Tz mlijitoa kwenye nchi wa uendeshaji wa serikali Kwa uwazi (Open Government partnership,OGP) chini ya mwendazake!Tupe mkataba ambao ni wanserikali na uliwekwa wazi,tuanzie na mkataba wa SGR na JNHP
Shida kubwa ni mentalityDemokrasia ni pamoja na kutofautiana kwa facts sio kupinga tu eti democrasia ,
Utaskia Nchi imeuzwa,hata kwenye mikopo watu wanaelezwa kwamba Tzn ni himilivu Ili kuchochea maendeleo haraka lazima tukope tufanye kwa haraka tena tunakopa mikopo soft loan lakini daa ujinga umejaa kama pipa kichwani..Kwenye bandari hapo vijana wengi wa bongo ni giza nene.
Mkuu hongera kwa kujaza madukuduku yako na kuyaleta katika hali ya kubeza walio kinyume na matamanio yako.
N ahapa ni sawa na kusema kwa kejeli kuwa unakuta mtu ni msomi au sio msomi analalamika hali ya hewa ya joto kali, wakati hajui mabadiliko ya tabia nchi. Ni sawa na kusema mtu analalamika mimea kuweka dawa wakati hajawahi kulima! Ulichokifanya ni kuweka mambo mengi kwa pamoja yanayokukera katika mfumo wa kubeza, lakini sioni kama una jipya kwenye bandiko lako. Inshort huna suluhisho lolote kwa uliyoyasema zaidi ya kuyaweka katika hali ya ujuaji.