Udhaifu wa Idara na Wizara za serikali ya Tanzania

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Karibu idara na wizara zote za serikali mawasiliano ni dhaifu sana.

Idara na wizara hawajui TEKNOHAMA na kama wanajua hawaitumii na wala hawajui mafanikio yake.

Pia Idara Nyingi na Wizara hawajui kuhusu mawasiliano ya Umma, yaani hawajui ni habari zipi siri au habari zipi watu wanastahili kujua.

Bado wafanyakazi wengi wa serikali wana Ukiritimba uliochanganyika na uoga. Hapa kuna tatizo kubwa sana, sijui wazee wamejazana huko kwenye idara na wizara na wanajifanya kuwa wana uzoefu. Kama Kijana wa Chuo Kikuu akiajiriwa, hawezi kufanya kazi vizuri, kwa weledi maana hawa wazee wamekalia mafile au wana ukiritimba. 'Too much conservative'

Tanzania inatumia gharama kubwa kutangaza nchi kwa ajili ya wawekezaji halafu utendaji serikalini ni mbovu sana.

Angalia Kenya, South Africa, USA, UK, Netherlands - unaweza kuwaandikia email na unapata majibu ndani ya 48 Hours. Na kama hawana jibu wanakuelekeza wapi utapata majibu muafaka.

Idara na Wizara nyingi za Serikali ya Tanzania zina website ila zipo in active kama magofu. Kama ukiandika barua kwa email zilizopo pale kwenye website, basi email ita bounce au hata ikienda hutapata majibu hata baada ya miezi. Au unakuta ipo email address moja tu ya ps au dg.

Au ukiandika barua kwa postal bank kama kawa majibu hutapata, hata ile jibu la kusema barua yako tumepokea hakuna.

Ukienda Wizarani, nayo inakuwa ngumu. UKitaka kufanya kitu chochote hakikisha una nyoosha mkono (10%) kama kawa.

Hivyo basi Tanzania haitakaa ipate wawekezaji kwa sababu hakuna mawasiliano. Hata wale wanaofanikiwa kuja hawana maadili, tayari wametoa 10% ndo wapate msaada wa kuwekeza.

Bado IMF na World Bank Wanasema kuwa Tanzania hakuna mazingira mazuri ya uwekezaji.

Pia nalaani tabia ya Serikali ya Tanzania na Viongozi wa siasa hasa chama kinachotawala kwa kupendelea wawekezaji wa nje. Nchi ikitegemea wawekezaji wa nje kwa asilimia kubwa sana, uchumi hautakuwa na shillingi itazidi kudorora.

Vitu kama Ardhi sio vya kuchezea, Mwekezaji wa nje anakuja na anapewa maelfu ya maekari halafu watanzania wanaachwa patupu. Au hii tabia ya serikali kunyang'anya wananchi na kuwapa wawekezaji ni mbaya mno. Nguvu kazi ya Tanzania haitumiki hvyo uchumi utakuwaje?

Tanzania ina wasomi wachache zaidi katika Africa mashariki, ila hata hao wasomi wachache hawana ajira. Shame!!!

serikali imelala sana, shillingi inadorora, madeni ya nje na ndani mengi mno.

Sijui la kusema tena, imetosha bye bye
 
Back
Top Bottom