Uchunguzi dhidi ya Blandina Nyoni na Jairo umekamilika - Hosea Edward

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema ipo katika hatua za mwisho za uchunguzi wa tuhuma dhidi ya aliyekuwa Katika Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, na Katibu aliyekuwa Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.

Mkurugenzi Mkuu wake, Dk. Edward Hoseah, akizungumza na paparazzi jana, alisema ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Jairo na Nyoni, utajulikana siku chache zijazo kutokana na taasisi hiyo kuwa katika hatua za mwisho za uchunguzi.

"Tupo katika final touch (hatua ya mwisho), tutakapokuwa tayari tutawafahamisha, kila kitu kimeshakamilika, bado vitu vidogovidogo tu, " alisema Dk. Hoseah.

Alisema taasisi yake inawajibika kufanya uchunguzi wa kina pasipo kukurupuka, na endapo itampeleka mtuhumiwa mahakamani kuwe na ushahidi uliokamilika.

Miezi kadhaa iliyopita, Takukuru ilikamilisha uchunguzi dhidi ya Jairo na Nyoni na kupeleka majalada yao kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Fereshi, hatua zaidi za kisheria.

Hata hivyo, Dk.Fereshi wakati anapitia ripoti hiyo ya Takukuru, alibaini kuwa kulikuwa na mapungufu ya kiuchunguzi na hivyo kuyarejesha tena Takukuru ifanyiwe marekebisho.

Jairo anachunguzwa kwa tuhuma za kuchangisha mamilioni ya Shilingi kutoka katika taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Nishati na Madini ajili ya kuwashawishi wabunge waipitishe wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/12.

Tuhuma dhidi ya Jairo ziliibuliwa kwa mara ya kwanza Bunge na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo.
Kufuatia tuhuma hizo ambazo zilizua mjadala mkali bungeni, Spika Anne Makinda, aliunda kamati ndogo teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Tunduru Kaskazini (CCM), Ramo Makani.

Makani akisoma ripoti ya kamati yake bungeni, Novemba 20, mwaka jana, akisema uchunguzi ulibaini kwamba, Jairo aliomba fedha kiasi cha Sh. milioni 180 kutoka taasisi nne.

Alizitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililoombwa Sh. milioni 40, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura) Sh. milioni 40, Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) Sh. milioni 50 na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Sh. milioni 50.

Hata hivyo, alisema kiasi kilichochangwa ni Sh. milioni 140 tu kutoka Tanesco, Rea na TPDC wakati Ewura waligharimia chakula cha mchana wa siku tatu pamoja na tafrija iliyokuwa imepangwa kufanyika baada ya kupitishwa kwa bajeti, ambayo iliwagharimu Sh. milioni 9.7.

Makani alisema uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mbali na fedha hizo, kulikuwa na kiasi kingine cha Sh. milioni 428.8 kilichotoka katika Idara mbili za wizara hiyo, ambazo ni Uhasibu Sh. milioni 150.7 na Idara ya Sera na Mipango iliyotoa Sh. milioni 278 kwa ajili ya kusaidia upitishaji wa bajeti.

Alisema fedha zote hizo ikiwa Sh. milioni 568.8, ziliingizwa kwenye akaunti ya taasisi ya GST iliyopo mjini Dodoma, lakini akasema kati ya hizo, Sh. milioni 150.7 zilikuwa kwa ajili ya gharama za vikao na semina na kiasi kilichokuwa mahususi kwa ajili ya uwasilishaji wa bajeti bungeni kilikuwa Sh. milioni 418.8.

Makani alisema maelezo waliyopewa na wizara husika, walifikia uamuzi wa kuomba fedha hizo kutokana na fungu ambalo hutumika kwa ajili ya shughuli za bajeti kubakiwa na Sh. milioni 35 tu kati ya Sh. milioni 207 zilizokuwa zikihitajika.

Hata hivyo, alisema wizara haikuzingatia kanuni husika za fedha katika kuomba fedha hizo, na kwamba aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, alipohojiwa na kamati hiyo, alisema utaratibu uliotumiwa kwamba si halali.

Alisema kamati pia ilibaini kwamba kulikuwa na vitendo vya kughushi na udanganyifu katika hesabu za gharama za uendeshaji wa semina ya wabunge ya Juni 26, mwaka jana, ambayo iliendeshwa na Wizara ya Nishati na Madini.

Makani alisema ili kufanikisha semina hiyo, Jairo aliziandikia tena taasisi nne; ambazo ni Rea, Ewura, TPDC na Tanesco kutoa Sh. milioni 22 kila moja na fedha zote zilikusanywa na kufikia kiasi cha Sh. milioni 88, fedha ambazo zililipwa kwa mhasibu wa wizara, Hawa Ramadhani.

Alisema kwa mujibu wa barua hiyo, Jairo aliainisha kwamba, bajeti ya semina hiyo ni gharama za ukumbi Sh. milioni 39 na posho kwa wabunge Sh. milioni 46 , hivyo kufanya mahitaji kuwa Sh.milioni 85 tofauti na kiasi cha Sh. milioni 88 kilichochangishwa.

Makani alisema maelekezo yaliyotolewa na Ofisi ya Bunge kuhusu malipo hayo ni viongozi wa Bunge kulipwa Sh. 250,000, wabunge Sh. 110,000, wakuu wa idara Sh. 80,000, maofisa Sh. 50,000 na watoa huduma nyingine Sh. 20,000.

Kufuatia hali hiyo, Kamati hiyo ilipendekeza kuwajibishwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Hata hivyo, ni Jairo pekee aliyewajibishwa kwa kusimamishwa kazi na baadaye kuondolewa katika wadhifa wake. Luhanjo alistaafu utumishi wa umma bila kuchukuliwa hatua zozote wakati Utouh anaendelea na wadhifa wake.

Kwa uapnde wake, Nyoni, anachunguzwa kutokana na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake akiwa mtumishi wa umma. Kutokana na tuhuma hizo saba ambazo ziliainishwa wakati wa mgomno wa madaktari ulioanza Januari mwaka huu, hali hiyo ilimlazimu Waziri Mkuu, Mizengo Panda, kutangaza kumsimamisha kazi ili uchunguzi uweze kufanyika.

Nyoni alisimamishwa kazi sambamba na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa, ambaye walituhumiwa pamoja


REJEA BAADHI YA TUHUMA ZA NYONI BLANDINA

Yafuatayo ni baadhiya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapakazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-

1. Amekuwa akijilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa KudhibitiUkimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissionerkupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisamanunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo,manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo chaManunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.

3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu(Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzajimwingine kinyume na kanuni za manunuzi.

4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni yaKaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangualipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.

5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbiakwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwakuwa tayari ana ‘Conflict of Interest'

6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa nikumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi nauongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na DonathaKoko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara

7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo(dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwadereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki pikiya miguu mitatu (Bajaj)

8. Amenunua vingamuzi vya magari (Vehicle Security and Fuel control system)vibovu kwa ajili ya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibuza manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenyemakao yake huko Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchinizikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wakewakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yakevikiwa na madeni lukuki.

9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for MedicalResearch (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizizilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010

10. Mwishoni mwa mwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi3,083,400,000 mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Projectbila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo pia zilihojiwana CAG.

11. Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wa dunia mzunguko wa 11 (GlobalFund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP)kwa kushindwa kutumia fedha zote zilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko yanyuma. Kwa kifupi ni kwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significantunspent balances.

12. Amekuwa akizuia uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda),Chief Internal Auditor (Bi Anna Joseph Mhere) na Director of Adminstration andPersonnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katika utendaji waWizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant mara mbili, Chief InternalAuditor mara moja na Director of Administration and Personnnel mara moja.Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wa wakurugenzi hawa kwa sababu ni watuwaoga na wamekuwa wakikubali chochote anachosema hata kama kinavunja kanunu nataratibu za serikali mfano katika maeneo ya Manunuzi.

Kwa nini Chief Accountant (Hellen Saria Mwakipunda) na Chief Internal Auditor(Anna Joseph Mhere) wanamuogopa kama Mungu Blandina Nyoni? Ni hivi: HellenMwakipunda, alikua Junior staff kwa Nyoni, kipindi hicho Nyoni ni Mhasibu mkuuwa Serikali. Blandina Nyoni ndiye aliye mpandisha cheo Mwakipunda na kuwa ChiefAccountant, kipindi hicho hata CPA hakuwa nayo. Anna Mhere alipata u-CIA akiwana Advance Diploma in Accountancy - ADA tu. Ili swala lilikuwa linawashangazawatu wengi sana. Sasa kwa inferiority complex walizokuwa nazo hawa wakina mama,ni lazima wamuabudu Blandina Nyoni.

13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu wa Kitecho cha Ugavi Mzee Funga kwendaHospitali ya Mirembe Dodoma kwa kukataa kununua Uniforms, suti na Maua kutokakwa Mariedo kwa sababu alihoji ni kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawanaMkataba na hawajashindanishwa na wauzaji wengine.

14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu waserikali hadi Wizara ya Maliasili na Utalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama nadereva huyo huyo kutoka Maliasili hadi Wizara ya Afya kinyume na taratibu nakanuni za Utumishi wa umma ambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote waserikali kuhama na dereva au / na secretary

15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkya kutokana na Naibu huyo kugomakupangiwa dereva ambaye ni Informer wake. Hadi leo hii hamsalimii hatawakikutana kwenye kordo. Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.

16. Alikuwa na uhusiano mbaya na Naibu Waziri wake aliyeondoka Bi Aisha Kigodakwa sababu ambazo hazijulikani. Kama ilivyo kwa Lucy Nkya nae pia walikuwahawasalimiani.

17. Akiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, aligombana na Waziri wake Bi ShamsaMwangunga na wakawa hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo

18. Alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali alikuwa anateua ndugu zake na watuanaofahamiana nao na kuwapa vyeo vya u Chief Accountants na Chief Internalauditors bila kuwa na sifa kamili ya kupewa vyeo hivyo. Mfano kuhold CPA (T) naMasters.

19. Amesababisha kushuka kwa morali ya utumishi kwa Wafanyakazi wa Wizara yaAfya na Ustawi wa Jamii. Hivi sasa ndiyo Wizara inayoongoza kwa kuwa nawatumishi wengi walioamua kwenda likizo ya masomo ili kuepuka manyanyaso yake.

20. Ameanzisha utaratibu ndani ya Wizara ya Afya wa kupokea Excheque kutokahazina na anazihold bila kufanya distribution kwenye idara zake. Kutokana nautaratibu wake huu anafanya malipo kwa kutegemea mahitaji yanavyojitokeza.Utaratibu huu ni kinyume na kanuni za hazina za matumizi ya fedha za umma.

21. Ikitokea kazi za Construction na maintanance anacomand tenda ipewe kwaMzenzi Contractors Ltd. Alishinikisha Mzenzi ajenge ofisi za Wizara zilizopoDodoma na akafanikiwa, baadae alishinikiza Mzenzi ajenge jengo banda laMaonyesho la Wizara kwa ajili ya Nane nane lilipo Dodoma na akafanikiwa naalishinikiza Mzenzi apewe tenda ya kufanya small maintanance wizarani kwenyeofisi yake, Ofisi ya Waziri na Naibu Waziri kwa ajili ya kuweka tiles nakuboresha vyoo na akafanikiwa.

22. Katika section ya Matibabu ya nje amejenga Network na Hospitali za Indiaambazo zinapelekewa wagonjwa kuibill wizara inflated invoice prices.

23. Amechukua mashine za kusafishia figo akishirikiana na Dk Linda Ezekielpamoja na reagent na filter wakazipeleka Msasani kwenye Hospitali yao ambayoBlandina Nyoni ana shares.

24. Amejenga banda la maonyesho ya sikukuu ya nane nane kwa kutumia fedha zaNIMR kwa Shilingi 1.5 billion. Lakini banda lenyewe lililopo pale Nane naneDodoma ukiliangalia tu kwa haraka haraka kwa macho thamani yake haizidi hatamillion 400.

25. Ameingiza robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka KoreaKusini.

26. Ameingiza kinyemela bila kufuata taratibu za Manunuzi kampuni ya kufanyausafi ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

27. Ameshinikiza kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited kupewa tenda nambaME/007/2009-10/HQ/G/191 kwa ajili ya Printing and Placing of Billboards withTB/TBHIV bila kufuata taratibu za manunuzi. Kwa maelezo zaidi juu hii tendasoma maelezo kutoka 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada hii orodha

28. Blandina Nyoni akishirikiana na Dr Deo Mtasiwa wamecheza mchezo mchafukatika tenda ya ununuzi wa Bajaj kama ilivyoratibiwa na Wizara ya Miundombinukupitia tenda namba ME/015/2009 - 2010/S/06. Katika tenda hiyo bajaj mojailinunuliwa kwa US$ 8,400. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutokakwa 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada ya orodha hii.

29. Ametengua uteuzi wa Dr Mtimba kama Mkurugenzi Msaidizi na kumuhamishia DamuSalama Tabora na badala yake amemkaimisha Dr Budeba kwa miaka miwili mfululizobila kumthibitisha kushika nafasi hiyo kinyume na taratibu za utumishi.Anafanya hivyo kwa sababu Dr Mtima hana urafiki naye.

30. Ametengua uteuzi wa Dr Sawe ambaye angeenda India kuwapokea Wagonjwa nabadala yake kamteua Dr Goroka ambaye kiudugu ni mtu na Mama yake. Hivi sasakampeleka Dr Ngoka ambaye ni family friend wake pia.

31. Ametengua uteuzi wa Dr Sawa anayesimamia uandikishaji / usajili waHospitali binafsi na kumpatia Mtoto wa Balozi Lusinde ambaye ni rafiki yake nawalisoma nae High School Kilakala mmoja akiwa Form V mwingine akiwa Form VI

32. Ametengua uteuzi wa Dr Muhame ambaye alikuwa Msajili wa tiba asilia nakumpatia Dr Naomi ambaye ni Mama Mdogo wake. Yaani yeye na Blandina ni mtu namtoto wa binamu.

33. Yeye ndiye chanzo cha masahibu yaliyowakabili Watanzania kwa kukosa hudumaya afya kwa zaidi ya Wiki mbili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kitendochake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwa kuwahamishia Mikoanipale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali.


Kampuniya Jambo Concepts Tanzania Limited, P. O. Box 3209, Dar es Salaam ilianzakuingia Wizarani baada ya Nyoni kuwa KM. Kuna tenda nambaME/007/2009-10/HQ/G/191 kwa ajili ya "Printing and Placing of Billboards withTB/TBHIV". Zabuni hii ilitangazwa kwenye vyombo vya habari na kufunguliwaTarehe 18/11/2010. Katika ufunguzi, ni kampuni mbili tu ndo zilijitokeza, JamboConcepts Tanzania Limited ikiwa ni mojawapo (nisingependa kutaja kampuninyingine). Kwenye ufunguzi kampuni ya Jambo Concepts haikuwasilisha nyarakanyingi husika ambazo utumika wakati wa tathmini. Lakini baada ya ufunguzi,Nyoni alimuita mkuu wa kitengo cha ununuzi na Ugavi, akamueleza anataka JamboConcepts ishinde, kilichofanyika ni kwamba mwakilishi wa jambo concepts (MzeeKibanike), aliitwa na kuelezwa ni nyaraka gani anatakiwa alete. Kweli alileta,na kushinda zabuni hii kupitia barua ya ushindi yenye kumbukumbu na. CAB209/549/02E/51 ya Tarehe 2/12/2010. Baada ya hapo, Jambo concepts akawa hana helaya kufanyia kazi, ikabidi Nyoni na Hellen Mwakipunda waizinishe advance paymentkwa kampuni hii ya 50% for free with no any guarantee.

Blandina Nyoni ame centralize manunuzi yote, sasa kwenye mambo ya printing ofdocuments or anything, ametoa agazo kwamba zikafanywe na Health Education Unit– HEU, kitengo chini ya Wizara. Sasa kinachofanyika ni hivi; HEU hawana anyfacility ya kuweza kufanya printing, sasa wakishapata order ya printing,wanaipatia kampuni ya Jambo Concepts (ambayo na yenyewe ni middle man) afuJambo concepts wanaenda kwenye makampuni ya printing. CAG au TAKUKURUkaichunguzeni HEU, ni vipi wanaweza kupokea kazi za printing ili hali wenyewehawana printing facility?

Ununuzi wa bajaj:
Hii zabuni ilikua namba ME/007/2009-10/HQ/G/149 – "Supply of Side CarAmbulance". Sasa ukweli wake huko hivi; Zabuni hii, ilikua inafadhiliwa na HSDPII, chini ya usimamizi wa World Bank. Wizara ilitangaza zabuni hii na pia WorldBank ilitangaza pia, ufunguzi ulikua Tarehe 24/3/2010, tathmini ikafanyika,bodi ya zabuni ikampitisha mshindi kwa wastani wa bajaji 1 kwa USD 7,850.Ripoti ya tathmini ikapelekwa World Bank kwa mapitio kwa mujibu wa taratibu.Baada ya kupelekwa huko CMO, Dr. Deo Mtasiwa akagundua kuwa kampuni yakealiyotaka kushinda aijapendekezwa (alikua anataka ishinde Ranger Production Co.S.A (PTY) Limited, South Africa), akawasiliana na Msimamizi wa Sector ya afyapale World Bank, akamueleza kuwa anataka Rangers Production ipewe hiyo zabuni,huyo jamaa wa World Bank akakata, akamueleza ni kinyume cha utaratibu. Dr. DeoMtasiwa akaona haitoshi, akamueleza kuwa, anaomba hizo pesa ziende Wizara yaMiundombinu, ili kule afanye anavyojua yeye ili kampuni ya Rangers ishinde.Huyo jamaa wa World Bank, akamueleza kuwa hayo mambo ya Kiswahili kule hakuna, pesaikishatengwa kwa utaratibu flani haiwezi kutumika vinginevyo, cha kufanyaatafute pesa kwingine. Kweli, Dr. Deo Mtasiwa akamwambia jamaa wa World Bank,aifute hiyo tenda, itafanywa na Wizara ya Miundombinu. Sasa, alichokifanya nikuamisha pesa, akazipeleka MSD, afu MSD ndio wakawalipa Wizara ya Miundombinu,Wizara ya Miundombinu ikaagiza hizo bajaji kwa niaba ya Wizara ya Afya. KuleWizara ya Miundombinu hii tena inasomeka no. ME/015/2009 – 2010/S/06 na ununuzihuo ulikua ni kwa gharama ya USD 8,400 kwa pikipiki.

Kilichomuamisha Mzee Funga (Kaimu Afisa Ugavi Mkuu). Blandina Nyoni, alichongadili la kufanya matengenezo ya jingo la wizara. Sasa, yeye akapendekeza kuwahiyo kazi yote (zaidi ya 300M) ipewe kampuni ya Mzenzi Contractor kwa utaratibuwa "Single Source". Sasa mzee Funga, akakata na akamjulisha hivyo kwenyemadokezo, swala hili lilimuuzi sana Blandina Nyoni. Na ndio maana leo, MzeeFunga yuko kule Mirembe Hospital kama Afisa Ugavi.

Ununuzi wa Fuel Tracking and Control System:
Blandina Nyoni aliliona hili dili, akaanza na propaganda kwamba maderevawanaiba mafuta, au mafuta hayatumiki vizuri etc. Sasa akaja na aidia ya kufungahivi vifaa kwenye magari. Lakini wakamuuliza, je hiyo gharama ya upotevu wamafuta ni kiasi gani? Hizo log book wanazojaza madereva zina kazi gani?Blandina Nyoni akasonga mbele, akaitafuta kampuni yake ya mfukoni inaitwaGalooli Limited, Tel Aviv, Israel, akataka ipewe tenda hii kwa single sourcekama kawaida yake. Wajumbe wa Bodi ya Zabuni walikataa ununuzi huu, sababu kubwailikuwa, inapasa upembuzi yakinifu ufanyike kabla ya kuendeleza mchakato waununuzi. Blandina Nyoni akapewa ujumbe kuwa Bodi ya zabuni imekataa.Alichofanya yeye, akamwambia mkuu wa kitengo cha ununuzi na Ugavi aandae"Circular Resolution" ambayo itampasa kila mjumbe aweke saini, kama amekubaliau amekataa, ili Blandina Nyoni aweze kuwajuwa wabaya wake, ngoma ilivyokuanzito wajumbe wa Bodi walipitisha Ununuzi huu na Galooli ilijulishwa kuwaimeshinda kwa thamani ya USD 180,555, barua ilikua namari CAB 209/549/02E/35 yaTarehe 18/10/2010. Hiyo ilikua ni gharama ya vifaa tu, baadae hiyo kampuniikaongezewa mkataba wa "Installation Services" ambao una gharama kama hiyo. Leohii, hivyo vifaa havifanyi kazi, kumbe vilikua vibovu, stori ikawa imeishiahapo. Sasa, PPRA fanyeni uchunguzi, je ununuzi huu ulikua kwenye mpango, aubaada ya ununuzi mlijulishwa? Pia CAG chunguzeni hizo pesa zilitoka kifungukipi? TAKUKURU,TISS na nyie nendeni!

Kuhusu kampuni ya McKinsey and Co:
Hii kampuni ililetwa na Dr. Deo Mtasiwa kwa ajili ya kusimamia miradi ya wizarainayofadhiliwa na Global Funds, kisingizio kikubwa kilikuwa kwamba wizarahaijui namna ya kusimamia miradi ya Global Funds. Style ya kampuni hii ni kamaNet Group Solution ya Tanesco. Kama kawaida kampuni hii iliingia pale wizaranikwa utaratibu wa single source. Wakafanya kazi kwa miezi kama 4 tu, wakatoainvoice yao ya miezi 4 ipatayo USD 1.2 Million. Ishu ikawa tutailipaje bilakuwa na mkataba? Dr. Deo Mtasiwa akamuamuru mkuu wa kitengo cha manunuzi naUgavi aandae mkataba. Nafikiri mkuu wa ununuzi na Ugavi alikua amechoka namambo ya hawa mapacha wawili. Baada ya kuandaa mkataba, akawajulisha PPRA. PPRAwakaandika barua kali sana, iliyokuwa inauliza mambo zaidi ya 15. Dr DeoMtasiwa na Blandina Nyoni wakaona mambo yamekua mazito, sasa ikabidi waombe"appointment" ya kwenda kuonana na CEO Dr. Mlinga. Barua yenye kumbukumbu nambaAB.209/437/02/111 ya 7/11/2011 ikaandikwa kuomba huo mkutano uwe Tarehe9/11/2011 siku ya Ijumaa. Blandina Nyoni, Dr Deo Mtasiwa pamoja na wakurugenziwote walienda PPRA, baada ya kikao hicho ishu ikaisha, na ikabaki history.TAKUKURU, TISS sasa ni wakati wenu wa kwenda kujua nini kilijiri kwenye huomkutano.

Wizi unaofanyika kwenye fedha za Global Funds. Kwa kawaida kila mwaka, wizarainaandika proposal za maombi ya fedha huko Global Funds. Kinachofanyika hapa,wizara inapendekeza moja kwa moja kwenye proposal, kuwa kazi Fulani, kwa mfanoPromotional and Communication itafanya PSI, na pia wanaweka gharama husika.Maana yake ni nini, kwa kufanya hivyo, proposal ikishapita hizo kampuni zinakuadirect contracted, pasipo aina yoyote ya ushindani. Kwa taarifa tu, kampunimoja inauwezo wa kupewa USD zaidi ya 5 Million, na kampuni zinakuwa zaidi ya 4.Utaratibu huu umefanyika kwa muda mrefu, zaidi ya miaka 7. Kampuni ambazozimekuwa zikipewa hizi tenda kwa miaka yote inayozidi 7 ni PSI, KPMG, MEDA,Ifakara Health Institute na World Vision. Kwa style hii, Blandina na DrMtasiwa, baadae wanakatiwa mshiko wao na mambo yanakwenda mbele

Wizi uliofanyika kwenye ununuzi wa vyandarua. Global Funds ilitoa kiasikinachozidi USD 150 million kwa ajili ya ununuzi wa vyandarua kwa nchi nzima.Kilichofanyika ni hichi. Blandina akachangamkia dili kwa kupendekeza kazi yoteya usimamizi wa ununuzi ufanywe na kampuni binafsi. Akaichagua kampuni ya MEDA,ambayo Faith Patrick, MD wa hapo ni rafiki yake. Alifanya hivyo kwa kisingiziokwamba kitengo cha ununuzi cha wizara hakina "capacity" ya ununuzi, chakushangaza hapa mbona kitengo hicho kinafanya manunuzi mengine yote? Kwa hiyoMEDA ikawa "procurement agent". Kwa kuwa MEDA haikuwa na uwezo wa kuendesha nakusimamia taratibu za manununuzi, ikambidi Blandina aunde task force palewizarani kwa ajili ya kuwasaidia MEDA mambo yanapokuwa magumu. Kwa hiyo, MEDAkampuni binafisi ikapewa jukumu la kusimamia vyandarua vya taifa. Kwenye hilidili MEDA ililipwa zaidi ya USD 8 Millioni kama procurement agency fee. Kuhususwala la usambazaji wa vyandarua, hii biashara ilikua ya kubabaisha tu, na kayanyingi hazijapata hivyo vyandarua.

Uchangishaji wa TZS 50 Millioni kwa ajili ya sherehe za miaka 50:
Ule utaratibu ambao Bwana Jairo aliutumia kuchangisha fedha kwa ajili yakupitisha bajeti, Blandina Nyoni aliutumia. Aliagiza kila Idara, taasisi namiradi ya wizara kuchangia kiasi cha TZS 50 millioni kwa ajili ya kufanikishashughuli za miaka 50. "Wausika" nendeni kule kwenye mradi wa malaria au kifuakikuu na ukoma mtapata majibu.

Kwa nini Chief Accountant (Hellen Mwakipunda) na Chief Internal Auditor (AnnaMuhere) wanamuogopa kama Mungu Blandina Nyoni! Hellen Mwakipunda, alikua juniorstaff kwa Nyoni, kipindi hicho Nyoni ni Mhasibu mkuu wa Serikali. BlandinaNyoni ndiye aliye mpandisha cheo mwakipunda na kuwa Chief Accountant, kipindihicho hata CPA hakuwa nayo. Anna Mhere alipata u-CIA akiwa na Advance Diplomain Accountancy - ADA tu, ili swala lilikuwa linawashangaza watu wengi sana.Sasa kwa inferiority complex walizokuwa nazo hawa wakina mama, lazimawanamuabudu Blandina.

Kuhusu Elias Mkumbo na Donata Koko kuwa Infoma:
Hii ishu ni kweli na ni watu ambao kila mtu pale wizarani analifahamu. Ilifikiawakati mkumbo akawa anatengwa na madereva wenzake, pia Donata Koko ilifikawakati Blandina akawa anamtumia utafikiri yeye ndio mkuu wa ununuzi na Ugavi.Kwa taarifa za uhakika, infoma mwingine ni dada mmoja ambaye ni secretary. Huyu dada alikuwa nae tokea akiwa wizara ya maliasili
 
  • Thanks
Reactions: FJM
rais kikwete ananikataza kuwafikisha mahakamani vigogo-dr.hosea
chenge hausiki kwenye kashfa ya rada-hosea
nyoni na jairo hawakupokutoa wala kupokea rushwa-hosea
blah blah blah...embecile
 
kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, P. O. Box 3209, Dar es Salaam ilianzakuingia Wizarani baada ya Nyoni kuwa KM. Kuna tenda nambaME/007/2009-10/HQ/G/191 kwa ajili ya "Printing and Placing of Billboards withTB/TBHIV". Zabuni hii ilitangazwa kwenye vyombo vya habari na kufunguliwaTarehe 18/11/2010. Katika ufunguzi, ni kampuni mbili tu ndo zilijitokeza, JamboConcepts Tanzania Limited ikiwa ni mojawapo (nisingependa kutaja kampuninyingine). Kwenye ufunguzi kampuni ya Jambo Concepts haikuwasilisha nyarakanyingi husika ambazo utumika wakati wa tathmini. Lakini baada ya ufunguzi,Nyoni alimuita mkuu wa kitengo cha ununuzi na Ugavi, akamueleza anataka JamboConcepts ishinde, kilichofanyika ni kwamba mwakilishi wa jambo concepts (MzeeKibanike), aliitwa na kuelezwa ni nyaraka gani anatakiwa alete. Kweli alileta,na kushinda zabuni hii kupitia barua ya ushindi yenye kumbukumbu na. CAB209/549/02E/51 ya Tarehe 2/12/2010. Baada ya hapo, Jambo concepts akawa hana helaya kufanyia kazi, ikabidi Nyoni na Hellen Mwakipunda waizinishe advance paymentkwa kampuni hii ya 50% for free with no any guarantee.
Hii ni Kampuni ya Riziwan Kikwete ,mtoto wa Sultan, ndio pia wanachapisha gazeti la udaku la Jambo leo, hivyo hapa Nyoni alikuwa anatekeleza either Maagizo kutoka kwa Sultan Mkuu au Mdogo.
 
Ndg wana jamvi, hivi Jairo aliye kuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini yuko wapi kwa sasa? Kuna tetesi kuwa ameonekana anaendeshwa kwenye STK moja hapa Dar. Mwenye taarifa a-up-date bandugu
 
yuko hapa hapa Bongo anakula bata mpaka kuku wanaona wivu, ataanza kuonekana kwenye public eyes kuanzia 2015 akiwa kwenye karandinga la kijani akielekea Segerea, yeye na wenzake kina Ngeleja na wengineo baada ya M4C kufanya kweli na Chadema kukamata usukani.
 
Yule ni best wa JK atamlinda hadi muda wake wa kuchukua mafao ufike sio yeye tu na Mama Blandina Nyoni pia!wanakula mishahara ya bure na huduma zote wanapatiwa kama makatibu wakuu....
 
Ukisikia Tanzania yenye amani ndiyo hii au mwenzetu unataka kuleta vita; wewe utakuwa umetumwa na wapinzani.
 
Hana lolote atakua anakula udaga na michembe huko kwao hii serkali ukiindoka kwene system unafulia kiac flan!
 
Nchi hii kuna Amani tele sana
wezi wanadunda km nini

2015 Mungu ataiangalia Nchi kwa huruma na Wapinzani watakwenda Magogoni ili nasi tupate ile inaitwa

Nchi ya Ahadi yenye Asali na Maziwa
iliyotajwa kwenye Biblia.

Tumenunua maji yetu kwa hela
Tumekuwa Wakimbizi Nchini
mwetu,Jairo kwa kweli aendelekula Bata mpaka Kuku aone wivu

M4C ndiyo itakayo ondoa haya yote.
 
Ndg wana jamvi, hivi Jairo aliye kuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini yuko wapi kwa sasa? Kuna tetesi kuwa ameonekana anaendeshwa kwenye STK moja hapa Dar. Mwenye taarifa a-up-date bandugu



sio tetesi, mi mwenyewe nimeshamshuhudia kwa macho yangu na nilihoji uhalali wa hii kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom