Uchekibobu hadi misibani? ndio kuiga gani huku

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nimeona hii picha ya msiba wa Juliet Mrina (pendo) na nimeona mwendelezo wa kile kinachoitwa kizazi kipya, kufika msibani kiganwe gangwe wakiamini labda ndivyo "wakubwa" wanavyofanya inapofika misiba. Siku hizi hata kanga, suti na nguo za heshima vijana hawataki kuvaa tena kwani "wanaomboleza kisasa" (whatever that means).

<!--ThumbEnd-->

Ndio "ukisasa" wenyewe huu, na ni nani huyo tunayemuiga?
 
MMJJ, Naona unamuonea huyu jamaa. Kwani kuna kibaya kipi alichovaa? Tena nionavyo mimi kafanya na heshima kufanya vazi lake kuwa jeusi, dalili ya yeye mwenyewe kuomboleza.
 
Hata mimi nimemuona huyo Prof. Jay leo mchana pale Muhimbili kanisani wakati wa kumuaga Julieth. Labda ndio uniqueness as they say, tho imekuwa negatively
 
Jaribu kutazama hata misiba ya Kitaifa siku hizi ni mwendo wa ukisasa kwend mbele mkuu na babu yangu Mwanakijiji
 
Binafsi sioni ubaya wowote na vazi la jamaa. It's not that outlandish...I've seen worse. Afadhali alivyovaa hivi kuliko angevaa ile iitwayo kata kund.u. (pants on the ground..lol)

Ila naona kama kashika bandana nyekundu...sasa sijui hiyo ya nini? Au ni kuonesha kwamba yeye ni "blood"...

Ingependeza zaidi kama angevaa suruali kuliko hiyo pensi nyanya na pia angevaa t-shirt isiyo na chata hapo mbele au angevaa shati kabisa. But overall his attire ain't that bad....
 
Waseminari wanataka kutuletea principles zao za useminari sasa, mpaka kutuamulia twende msibani vipi. Huyo Jay angeweza kwenda much worse than that na wala nisingeshangaa.

Mbona tunapoteza muda mwingi katika superficialies? Kati ya kilicho nje na kilicho ndani kipi muhimu?

Wewe unataka kila mtu avae suti na tai? Wengine wako kazini full time wanauza image hao, ndiyo kazi yao, sasa unawakataza wasivae according to kazi zao utawaweka wewe mjini?

Mtatufanya tukose raha misibani kisa tu tume rock "Dolce & Gabbana"

Maana hii modern day Roman Inquisition ya waseminari wetu ndipo inapoelekea.

Mimi nilifikiri waseminari ni watu wa kuchambua intellect zaidi ya hizi superficialities.
 
Daa, hii Tshirt yenye FUVU sijui ilikuwa ikimaanisha nini?

Kumwambia marehemu "soon you will look like this?" au maana nyingine?

Hii inanikumusha juzijuzi hapa Sikonge, mazishi ya Mama Muuza gongo, walikuja jamaa wako Nzwiiii na wengine wakiwa na tumizinga (chupa za soda zikiwa na Gongo) kwenye mifuko ya suruali. Jeneza lilipelekwa kwa mwendo kasi kwani jamaa hawana muda mrefu wa kupoteza na mazishi.
 
Wewe unataka kila mtu avae suti na tai? Wengine wako kazini full time wanauza image hao, ndiyo kazi yao, sasa unawakataza wasivae according to kazi zao utawaweka wewe mjini?

Kiranga...kuna mambo ya proper attire, setting, na decorum. Wewe ungeona sawa kama mdada angekupigia ki sketi kifupi na stilleto na ki top kinachoonesha cleavage hapo kwenye huo msiba?
 
Waseminari wanataka kutuletea principles zao za useminari sasa, mpaka kutuamulia twende msibani vipi. Huyo Jay angeweza kwenda much worse than that na wala nisingeshangaa.

unaamini vitu kirahisi sana na kujenga hoja kutokana navyo..LOL Miye nimeuliza tu kama ndio maombolezo ya kisasa, sehemu ya biashara na kujitangaza hey more power to them.
 
Usisahau kwamba siamini, bali najua.

Hata kama wewe mwenyewe hujui, hizo ni effects za useminari, amini usiamini. Ukiwa mseminari na kupitia tanuru la waseminari, ukiwiva ni vigumu sana ku allow liberality, unakuwa ushakunywa maji mengi sana ya useminari.
 
hahaha hilo ni kweli kwa waliopitia seminari kama kina Membe na wenzao. I can't tell inakuwaje..
 
Kwa hili naona Wacongo wametupita.

Kama ni kuzibuka, wenzetu wamezibuka tangu siku nyingi sana. Ila inapokuja kwenye misiba, hata hao akina Fally Ipupa nao wanavaa kiheshima sana ingawa siku za kawaida wanavaa mtepesho.

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=7pzN4GzHctA&feature=PlayList&p=7C26A12B6C12D6DC&playnext=1&playnext_from=PL&index=1"]YouTube- Madilu System - 9:02 Min Funeral Short Version (Lingala)[/ame]
 
Kiranga...kuna mambo ya proper attire, setting, na decorum. Wewe ungeona sawa kama mdada angekupigia ki sketi kifupi na stilleto na ki top kinachoonesha cleavage hapo kwenye huo msiba?

Proper attire kwa nani? Hiyo proper attire kwa an English gentleman's standard inaweza isiwe practical bongo, au proper attire ya aborigine wa Papua New Guinea inaweza isiwe appropriate Cipriani Wall St.

Kama ulivyosema mwenyewe, kibongo fleva inawezekana hapo ndipo katinga proper yao, kasamehe kata *****, katinga black, hilo fuvu ni symbolism ya kifo, halafu kaweka heshima kalifunika fuvu kiasi, halafu kitambaa alichotumia chekundu kinabeba gravity ya situation, kwamba damu imeacha kutembea, mchezaji kapewa kadi nyekundu katoka nje ya mchezo. Yeye kama msanii utaona anaenda na symbolism.

Hilo pensi linaendana na joto la Dar.

Akikwambia hivyo utasemaje?
 
kwa mujibu wa Kiranga ni kile kilicho ndani kinachomatter.. it doesn't matter mazingira au mtu anavyoonekana.. kwani kufanya hivyo ni kuleta maadili ya kiseminari.
 
Proper attire kwa nani? Hiyo proper attire kwa an English gentleman's standard inaweza isiwe practical bongo, au proper attire ya aborigine wa Papua New Guinea inaweza isiwe appropriate Cipriani Wall St.

Kama ulivyosema mwenyewe, kibongo fleva inawezekana hapo ndipo katinga proper yao, kasamehe kata *****, katinga black, hilo fuvu ni symbolism ya kifo, halafu kaweka heshima kalifunika fuvu kiasi, halafu kitambaa alichotumia chekundu kinabeba gravity ya situation, kwamba damu imeacha kutembea, mchezaji kapewa kadi nyekundu katoka nje ya mchezo. Yeye kama msanii utaona anaenda na symbolism.

Hilo pensi linaendana na joto la Dar.

Akikwambia hivyo utasemaje?

kwa kweli itabidi tukubaliane naye tu na nadhani hiyo ndiyo reasoning yenyewe.
 
Proper attire kwa nani? Hiyo proper attire kwa an English gentleman's standard inaweza isiwe practical bongo, au proper attire ya aborigine wa Papua New Guinea inaweza isiwe appropriate Cipriani Wall St.

Proper attire kwa Watanzania....mainstream Tanzania.

Kama ulivyosema mwenyewe, kibongo fleva inawezekana hapo ndipo katinga proper yao, kasamehe kata *****, katinga black, hilo fuvu ni symbolism ya kifo, halafu kaweka heshima kalifunika fuvu kiasi, halafu kitambaa alichotumia chekundu kinabeba gravity ya situation, kwamba damu imeacha kutembea, mchezaji kapewa kadi nyekundu katoka nje ya mchezo. Yeye kama msanii utaona anaenda na symbolism.

Vipi kuhusu setting na decorum? Kama angekuwa anaenda kwenye sehemu za mastarehe sidhani kwamba ingekuwa issue (ingawa bado sioni kama alivyo vaa ni vibaya sana kulingana na sehemu na mazingira). Nimekuuliza swali kama ingekuwa mdada (let's say ni mcheza dansi) aliyevaa ki hoochie mama kwenye msiba bado ungeona sawa tu? Nyonyo karibu zote ziko nje..akiinama unaona goodies zake...na viatu kakuvalia heels za inchi sita...Kiranga...kweli ungeona sawa au basi tu unataka kuleta ligi huku ukijua kabisa kuna baadhi ya mambo yako in poor taste kulingana na occassion na mengineyo?

Hilo pensi linaendana na joto la Dar.

Akikwambia hivyo utasemaje?

Nitasema acha visingizio vilivyo lame....hautayeyuka miguu ukivaa suruali....
 
Back
Top Bottom