Uchambuzi wangu kuhusu kupendwa kwa Magufuli mitandaoni na mitaani baada ya kufa na Ripoti ya CAG

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,168
33,420
Magufuli pamoja na mazuri yote yanayosemwa kama yapo, lakini ndio kiongozi pekee Tanzania aliedhibiti sana vyombo vya habari kuliko Raisi yoyote yule. Kama Kuna watu hawalioni hili kuna tatizo.

Baada ya kuanzisha Bunge Live, ni Utawala wa Magufuli pekee ndio ulioondoa Bunge kuoneshwa Live.

Ni Utawala wa Magufuli pekee ndio CAG aliondolewa kwa utaratibu ambao sio rasmi kutokana na Ripoti yake kutaja baadhi ya madudu ya Serikali na Bunge.

Kwa mfano kutokufahamika kwa matumizi ya 1.5 trillion na matumizi makubwa fedha za uma ya Spika akitibiwa India.

Ni wakati wa Magufuli pekee ndio ulipiga Marufuku Shughuli za vyama vya Siasa.

Ni wakati wa Utawala wa Magufuli zaidi ndio wapinzani waliteswa sana, kupigwa, kupigwa risasi, kufungwa, kufilisiwa, kutekwa, kubabikiwa kesi, kurubuniwa, na kila aina ya manyanyaso.

Ni wakati wa Magufuli pekee ndio uhuru wa kutoa maoni uliminywa.

Sasa baadhi ya vitu nilivyovitaja hapo juu hivyo ndivyo nyenzo za Uwazi,Utawala Bora,Demokeasia na Uhuru wa kutoa maoni.

Ukiwa na hivyo wewe kiongozi kama unataka kupambana na rushwa na ufisadi hizo ndizo nyenzo zako.

Vyombo huru vya habari
Mdhibiti na mkaguzi Mkuu
Bunge huru. Kuwa huru ninpamoja na kuoneshwa live.
Uhuru was vyama vya Siasa kufanya Shughuli zao.
Uhuru wa watu kutoa maoni, hapa ni pamoja na Mitandao ya kijamii.
N.k.

Mitandao ya kijamii,
Hapa kwenye Mitandao ya kijamii Kuna watu watu hupenda hutumia majina yao halisi kutoa maoni au dukuduku zao,na Kuna watu hupenda kuficha majina yao halisi kutoa maoni au dukududku zao.

Pia katika Mitandao ya kijamii ipo iliyopata misukosuko wakati wa Utawala wa Magufuli tofauti na utawala wa Raisialietangulia kabla ya Magufuli.

Mitandao ya kijamii iliyopata misukosuko ikiwa Ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa watendaji au wamiliki wake ni pamoja na JamiiForums.

Lakini ipo iliyoungwa au kuzimwa kwa muda ikiwa Ni pamoja na Twitter.

Kuna Mitandao inadiwa ina watumiaji wengi hapa Tanzania lakini haikupata misukosuko Kama hi miwili mfano Face Book na Instagram kwa uchache.

Na kwa bahati nzuri hii ni Mitandao ambayo watumiaji wake wengi hutumia majina halisi,t ofauti na mtandao kwa mfano JamiiForums ambao watu hawatumii majina yao halisi.

Sasa najiuliza huko Facebook kwa mfano ndiko watumiaji wengi, io wote hawajaridhika na Ripoti ya CAG iliyotoka juzi na baada ya kuwa Magufuli ametutoka.

Sababu zinazowafanya wasiridhike ndio zimenipelekea kutoa maoni haya.

Je, huyu CAG wa Sasa ambae alichaguliwa na Magufuli baada Ya Prof Assad kadanganya kuhusu mapungufu yaliyofanyika awamu ya tano? Je, kwa manufaa ya Nani adanganye?

Je, hawakuona tabia za Magufuli za kuzuia watu kuhoji?
Kama wabunge wa Upinzani
Vyombo vya habari
CAG Mussa Assad
JF na Twitter
N.k

Hawakuhoji kwa Nini nyenzo hizi za Uwazi na utwala Bora leo ndio zimekua adui mkubwa wa Magufuli?

Je atawezaje yeye peke yake na CCM yake kupambana na Ufisadi na Rushwa bila nyezo hizo?

Maoni ya Face Book na Instagram.
Wakati wa Magufuli ilikua Ni huru na rahisi kumsifu na kutukana wapinzani wake wa ndani ya CCM na nje ya CCM ukaandika Jina lako na namba ya simu ukaweka.

Wakati huohuo wakosoaji walipo jaribu kujifanya majasiri kukosoa na kuweka majina yao walitekwa na kupotezwa.

Kwa Hali hiyo ndipo uwaja wa maoni ukabaki kwa wasifiaji na wapongezaji na waungaji mkono.wakajitoa kabisa na wachache waliobaki wakabaki kutumia majina bandia na wengine wakaunga juhudi kwa kuanza kusifia kwa wale walioamua kubaki na majina yao halisi.
Hii maana yake Nini,maana yake watu waliiogopa kutoa maoni tofauti au mbadala.

Hivyo Mitandao ikabaki na wachangiaaji wakabaki wasifiaji kwa wingi na wakosoaji wakajitenga kwa hofu na bado licha ya Magufuli kututoka lakini watu bado wana hofu kwa sababu aliekufa Ni Magufuli lakini Wasiojulikana bado wapo.

Kupendwa kwa Magufuli.
Na kuua Upinzani.

Wakati Magufuli akiwa hai tuliambiwa anapendwa Sana na kaua upinzani kabisa ,wapinzani hawata pata kitu,uchaguzi mkuu utakua Ni rahisi Sana.

Ilitakiwa Magufuli aioneshe dunia kuwa yeye kweli anapendwa na mabeberu wasimsumbue kwa

Kufanya uchaguzi wa Serikali za mitaa kuwa huru na haki.

Kuweka tume huru na ya haki inayokubaliwa na wadau wote.

Kuendesha uchaguzi Mkuu uliopita kwa uwazi,uhuru,ushirikishwaji na haki.Matokeo yake yangempa kibali kwa Mungu na wanadamu.

Kabla ya Uchaguzi watu waliamini Upinzani umekufa.

Cha ajabu,
Mikutano ya kampeni ya Lisu ilifanya maajabu.
Kila siku ilikua inajaza watu na wenye hamasa kubwa,je walikua wanatoka wapi Kama Magufuli aliua Upinzani?

Hakukua na bendi,
Hakukua na wasanii maarufu,
Hakua na mabango,
Mikutano yake ya mwanzo haikua ikitangazwa na ilihujumiwa, je ule umati ulikua unatoka wapi?

Naamini hao watu wa Lisu bado wapo.

Msiba
Kwa kawaida sio vizuri kufurahia mtu akifa.
Kwa kawaida watu huenda misibani hata misiba ya maadui zetu.

Ni wachache Sana wanaoweza kuandika au kufurahi hadharani pale maadui zao wanapopatwa na matatizo au hata kufa,lakini mioyoni mwao hufurahi ama hushangilia kimyakimya.

Hayati Magufuli kapatwa na matatizo mawili la kwanza kafariki, na la pili Utawala wake umebainika kuwa na shida kidogo kwa mujibu wa CAG.

Je, Magufuli hajafa?
Je, CAG muongo?

Je, kuna watu hawaamini Kama kafa kweli?
Je, kuna watu hawaamini Kama serikali yake imekutwa na Ufisadi?
Sasa tufanyeje?

Tuite Wakaguzi huru wa Mahesabu ili kupata ukweli halisi? Ili awamu ya Tano ibakie kuwa Safi?

Kwa Nini CAG atoe taarifa ya uongo?

Kwa manufaa ya Nani?

Huu Ni uchambuzi wangu,Ni maoni yangu,Mimi sio Mwandishi wa habari nisamehewe kwa makosa ya kiuandishi.
 
Uchunguzi huru ndio kabisa unaweza kuwaweka katika hali mbaya zaidi kwani hata ile dhana: "Zimwi likujualo halikuli ukakishwa" haitokuwepo.
 
Back
Top Bottom