Uchambuzi wa Zitto kuhusu Barrick Gold unapotosha

Disputing tax assessment does not imply rejecting the tax burden. Correct? Ndiyo nilimaliza kwa kusema kuwa anaweza kuomba msamaha wa kodi hiyo.
Hata mimi sikulenga obligation to pay tax nililenga kiwango cha kodi kama siyo realistic
 
KIchuguu anadhani kuwa eti bado TRA/Serikali inaweza kuendelea kudai Dola Billion 190, ambazo kimsingi ndiyo jambo la muhimu zaidi katika ugomvi wetu na Acacia/Barrick.
Kama hilo halijapatiwa ufumbuzi au utatuzi then Drama nzima ya Osoro na Mruma ni kazi bure!
Maana Kama tuna uhakika walituibia Trillion 425, Tulitakiwa tuwapeleke mahakamani watulipe hela zetu hizo siyo kupokea pipi ya dola Milion 300 ambazo kama ukicompare na dola bilion 190 ni pipi!.
Utaachaje Ng'ombe mzima kwa kupewa njiwa?
Ninaelewa sana emotions zako mzee. In fact personally sina uhakika na ukweli wa hiyo $190B estimate iliyofanywa na serikali; iko inflated sana. Hizo ni hela nyingi sana kuliko thamani ya kampuni nzima ya Barrick Gold ambayo thamani yake ni $24b, zaidi ya kampuni ya Ford Motor Corporation ambayo thamani yake ni $40b, na vile vile zaidi ya kampuni LG Electronics ambayo thamani yake ni $6b.
 
Rasimu ya makubaliano baina ya Barrick Gold na Serikali ya Tanzania (GoT) imeambatanishwa katika press release iliyotolewa na Barrick kuhusu takeover ya Acacia kama Appendix 4. Nimeambatanisha rasimu hiyo hapa chini. Jambo la kwanza kabisa Mheshimiwa Zitto angetambua kuwahii ni initial draft, bado kuna mazungumzo zaidi hadi pande zote mbili zikubaliane. Tatizo lilikokuwepo ni kuwa Acacia haikuwa na uhusiano mzuri na serikali ndiyo maana wakashindwa kukubaliana, hivyo Barrick ikaingilia kati na kuaza mazungumzo na serikali ambayo ndiyo yaliyoleta rasimu hii. Appendix yenyewe inasema ni kuwa bado haijakamilika na kukubaliwa na serikali kama ionekanavyo mwazoni tu; kwa hiyo haya hayajawa makuibaliano rasmi.
View attachment 1159207

View attachment 1159271


Mheshimiwa anatoa madai matano kuonyesha kuwa makubaliano hayo ni changa moto, lakini ukiyaangalia madai hayo, yana nusu ukweli na nusu uwongo, na ndiyo maana ninajumuisha kuwa yanapotosha. Nitayapitia madai yote kuonyesha ukweli wake na upotoshaji wake.


Dai Namba 1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.


Ukweli wa dai hili ni kuwa malipo hayo yatafanyika kwa kipindi cha miaka saba, lakini uwongo wake ni kuwa malipo hayo hayana uhusiano wowote na disputes na madaiano ya kodi baina ya serikali na ACACIA; ni malipo yanayofanywa kumaliza dispute, yaani serikali isiendelee kuidai ACAIA zile Bilion na vile vile ACACIA nayo isiidai serikali pesa yoyote kama inayonyeshwa katika vifungu vifuatavyo vya makubaliano hayo. Makubaliano ya malipo hayo ya $300m yamo kwenye vifungu A.13, na vifungu A.14 vya rasimu hiyo kama ionekanavyo hapa chini.
View attachment 1159201

Halafu malipo hayo yatafanyikwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye kifungu A.16 kama ionekanavyo hapa chini.

View attachment 1159202

Kabla ya makubaliano hayo kufikiwa inabidi pande zote mbili zikubaliane kimaandishi kuwa hazidiani kama ilivyoelezwa kwenye kifungu A.10. Yaani Acacia itamke kuwa haiiidai serikali, na serikali pia itamke kuwa haiidai Acacia. Kwa maana nyingine ni kuwa Acacia ilipwe madeni yake yote inayoidai serikali, na vile vile serikali nayo ilipwe madeni yake yote inayoidai Acacia. Sasa nadhani hapa ndipo Mheshimwa Zitto amehitimisha kuwa Acacia inaidai serikali $240m, lakini akasahau kuwa serikali nayo inaidai Acacia $190b. Maelezo yaliyomo kwenye kifungu hicho cha A.10 ni haya hapa

View attachment 1159204
View attachment 1159205
View attachment 1159206
View attachment 1159208
View attachment 1159209


Sasa kama Mheshimiwa Zito angesoma vizuri kifungu cha A.11angeona kuwa kinasema hivi:


View attachment 1159210

Yaani Acacia inaweza kuondoa madai yake dhidi ya serikali na vile vile serikali inaweza kuondoa madai yake dhidi ya Acacia halafu ndipo wote wakaanza maisha mapya. Sasa hatua hiyo haijafikiwa ndiyo maana Mheshimiwa amepotosha.

Kwa hiyo kwa jumla hitmisho la Mheshimwa Zitto kuhusiana na hiyo $300m katika dai lake namba moja linapotosha sana.

Kwa vile post imeshakuwa ndefu sana, nitaachia hapa na baadaye kufungua post nyingine kujadili madai mengine yaliyotolewa na Mheshimiwa Mbunge Zitto kwa kutumia document hiyo ya Appendix 4.

Jibu langu kwenye dai lake la pili liko hapa https://www.jamiiforums.com/threads...-gold-unapotosha.1609126/page-2#post-32237690

Jibu langu kwenye dai lake la tatu liko hapa https://www.jamiiforums.com/threads...-gold-unapotosha.1609126/page-4#post-32238344

Jibu langu kwenye dai lake la nne liko hapa https://www.jamiiforums.com/threads...-gold-unapotosha.1609126/page-5#post-32239262

na mwisho jibu langu kwenye dai lake la tano liko hapa https://www.jamiiforums.com/threads...-gold-unapotosha.1609126/page-6#post-32240111

Umetoa ufafanuzi mzuri sana.
Zitto kazi yake kubwa SIKU ZOTE ni kupotosha watu.
 
GOT have damaged their country reputation in the mining industry and to the wealth of their country long term for political short gains .... unless this government is replaced with a more accommodating one to the industry.

It is a very difficult task to regain trust once you lose it ..
 
Makubaliano yapo kwenye linki hii hapa ambayo ndiyo pia Zito ametumia. Nimeambatanisha Appendix 4 ambayo ndiyo rasimu ya makubaliano yenyewe; ipo kwenye ukurasa wa 69 hadi 79. Angalia kama hizo clips znilizoweka hapo ziko edited, nionyeshe sehemu zilizokuwa edited.
Mkuu naona unahangaika sana na hizo porojo za ccm, ukweli ni kwamba hakuna cha maana saana kitachopatikana hapo, hiyo ni mapendekezo ya makubaliano na acacia walishasema awali kabisa kwamba maridhiano yoyote lazima yaidhinishwe na acacia, kwa hiyo usitegemee watakubali kirahisi kuachia hizo dola milion 240 kirahisi, niliyasema haya mapema, nakushauri ungekula ugali wako ukalala, haya mambo ya sanaa za tz achana nayo
 
Sio kwamba Zito anapotosha tu, Agenda inayoonekana kutawala JF ni kupinga Serikali kwa hali na mali. Kwanza watakufungia kwa kosa dogo lakini kama wewe upo upande wa kuikosoa serikali hata utukane vipi unapeta, ndio sababu sisi wengine tunasema kwamba JF imenunuliwa na Mbowe pamoja na Chadema. Hakuna mawazo huru ni yale ya wapotoshaji na kama Kichuguu alivyoonesha hapa haka ka Kabwe hakana lolote na kanafahamu 2020 hakana chake tena kamebaki kuwewesekaweweseka tu.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Sio kwamba Zito anapotosha tu, Agenda inayoonekana kutawala JF ni kupinga Serikali kwa hali na mali. Kwanza watakufungia kwa kosa dogo lakini kama wewe upo upande wa kuikosoa serikali hata utukane vipi unapeta, ndio sababu sisi wengine tunasema kwamba JF imenunuliwa na Mbowe pamoja na Chadema. Hakuna mawazo huru ni yale ya wapotoshaji na kama Kichuguu alivyoonesha hapa haka ka Kabwe hakana lolote na kanafahamu 2020 hakana chake tena kamebaki kuwewesekaweweseka tu.
Mkuu, bahati mbaya ni kwamba hamjazoea mambo haya ya uhuru wa mwanadamu kujieleza, nashangaa unapofikia hatua ya kusema JF imenunuliwa na Mbowe, !!, jifunzeni kuzoea haya mambo ya Uhuru kwani Dunia iliyostaarabika inavotaka, hapa sisi tunajinafasi, naamini mtapata tabu sana kuifikiria JF, Hili ni jamvi Huru kwetu wastarabu, nyinyi kaeni na li TBC- lenu
 
Mkuu, bahati mbaya ni kwamba hamjazoea mambo haya ya uhuru wa mwanadamu kujieleza, nashangaa unapofikia hatua ya kusema JF imenunuliwa na Mbowe, !!, jifunzeni kuzoea haya mambo ya Uhuru kwani Dunia iliyostaarabika inavotaka, hapa sisi tunajinafasi, naamini mtapata tabu sana kuifikiria JF, Hili ni jamvi Huru kwetu wastarabu, nyinyi kaeni na li TBC- lenu

Kwanza hujui hata JF alipoanzia, unakurupuka tu. Kuna watu humu wewe hufahamu, kama sio wao isingekuwepo.
 
Mkuu naona unahangaika sana na hizo porojo za ccm, ukweli ni kwamba hakuna cha maana saana kitachopatikana hapo, hiyo ni mapendekezo ya makubaliano na acacia walishasema awali kabisa kwamba maridhiano yoyote lazima yaidhinishwe na acacia, kwa hiyo usitegemee watakubali kirahisi kuachia hizo dola milion 240 kirahisi, niliyasema haya mapema, nakushauri ungekula ugali wako ukalala, haya mambo ya sanaa za tz achana nayo
Umetokea kilabu gani; inawezekana walikuchanganyia
 
Back
Top Bottom