Uchambuzi wa The Citizen kuhusu majadiliano ya Acacia

Waandishi wa habari huwa wanajifanya wana akili sana. Angalia huyu jamaa alichokiandika.
Amejitahidi mno kuwaaminisha watu kuwa serikali imeingia kwenye mazungumzo na barrick bila kuwa na roadmaps, bila kuwa na targets na bila kuwa na watu wenye experiece kwenye mazungumzo. Blah blah blah. Anayeongoza majadiliano kwa upande wa barrick ni negotiation kingpin... Blah blah upuuzi. Watu wasitafute kujiinua kisiasa kutokana na outcome ya mazungumzo. Blah blah.

Jibu ni rahisi sana. Mwandishi nae hana tofauti na sisi. Hajui ni watu gani waliomo kwenye kamati ya majadiliano kwa upande wa tanzania. Na hili limekuwa pigo kubwa kwa watu wenge mlengo wa kupenda kupindisha mambo.

Sisi tuko gizani. Naye yuko gizani vilevile. Aendelee kuwa mpole...
 
277 Containers still holding by the government zipo pale bandarini kama hawaridhiki na kamati wakachukue na wao sample wajiridhishe. Acha blaablaa subiri report baada ya majadiliano.
Mkuu unafikiri wameridhika? Wangeridhika kusengekuwepo na majadiliano, wangelipa tu na biashara iendelee. Hiyo hatua ya wao kuchukua sample inaweza kuwa sehemu ya majadiliano.
 
this is just makala ya uchambuzi ya mtu aonavyo tunapaswa tutofautiane kwa hoja siyo matusi wala maneno ya kwenye khanga. sasa sijui kwa nini mtazamo wa mtu ukiwa tofauti na baadhi ya matendo ya serikali wanaonekana siyo wazalendo
 
Mkuu, hilo pendekezo lako ni baya kwa sababu litaishia kuivua nguo serikali na wasomi wetu. Kwani kila mtu mwenye akili timamu anafahamu fika kwamba zile data za prof Muruma zilikuwa ni za kupika! Kama wewe hulijui hilo, una bahati mbaya. Nakuhakikishia kwamba kati ya mambo ambayo serikali haitakuwa tayari kuona yanafanyika ni kufanya sampling upya ya hayo makontena.
Daah....maprofesa wamepika data wakiwa chini ya kiapo ! Halafu unasema una akili timamu ! Hao watu waliokuwa wanajaribu ku lobby/intervene walikuwa wana interest gani kama kamati zote zilikuwa zinapika uongo !? Hata walipogundua documents details zina differ, huo pia ni uongo wa kupika ? Acheni kuandika upumbavu kwenye mambo serious ! K
 
Kumponda kiongozi wa timu yako na kusifia wa upande mwingine ndio impartiality?!
Kwanini usiponde au kusifia baada ya outcome!


Kusema ukweli ni kuponda?

Wewe ulichotakiwa kusema ni kupinga kwa ushahidi alichokiandika Mgaya kuwa si sawa badala ya kuleta maneno ya khanga.

You will never grow! if you cant take ownership of your actions and learn from your mistakes.

Hizi tamaduni zilizojengwa na sera za CCM zimewaathiri sana watanzania, siyo kila kiongozi ni mtukufu lazima ujue hilo.

Hivyo akikosea anaambiwa na Mgaya maeleza kiufasaha sana ila kwa sababu zako binafsi umeamua kuchukua upande usio sahihi
 
Ati Mbowe anaita press conference anataka apewe report asome !? Ili iweje ? Apigie mistari na kukazia wino !? Ati invoice ya tax evasion demand dhidi ya acacia ni kubwa ! Sijui utaalamu wa kukokotoa kodi aliupata wapi while yeye anajulikana ni Dj !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wakati wanaimgia hiyo mikataba bado wao walijiona wana akili sana na kwakuwa wao hawataki mawazo ya wengine haya bac wacha tuchapwe tu kama kawaida yetu
Mawazo mengine ni Lissu alisema tutapelekwa MIGA !
 
Yaani watu mnahangaika saaaana na kutaka kujua nini kinaendelea kwenye timu ya majadiliano utadhani mliiunda nyie! Magu kabana angle zote,hii siyo serikali ya kishilawadu ambapo siri za serikali mnazipata kila siku. Huyo mwanasheria aliyeandika hii makala ni mwanafunzi wa Kabudi so sikio halizidi kichwa! Ninachokijua ni kwamba kuna watanzania ni wachawi kuliko hata shetani! Yaani wanatamani sisi tupoteze ili tu Magu afeli! Sijui hii ngozi nyeusi ililaaniwa na nan??? Eeee Mungu tusaidie sisi waafrika tujitambue,tuondolee roho ya husuda na tupe roho ya upendo,tujipende,tupendane,tulipende bara letu la Afrika na tuzipende nchi zetu.
Si mkuu alitwambia wazungu walikubali kulipa sasa majadiliano ya nini?.
 
Mkuu unafikiri wameridhika? Wangeridhika kusengekuwepo na majadiliano, wangelipa tu na biashara iendelee. Hiyo hatua ya wao kuchukua sample inaweza kuwa sehemu ya majadiliano.
Kutoridhika kwao wewe kunakusumbua nini !?
 
Back
Top Bottom