Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 16,243
- 25,069
Nafasi ya Simba kwenda Robo Fainali imeanza kuwa ngumu
“Nafasi ya Simba kwenda robo fainali imeanza kuwa ngumu zaidi. Simba wameambulia pointi mbili katika mechi zao mbili za mwanzo. Na sasa wana safari ya kukabiliana na Wydad pale Morocco. Mechi mbili zijazo watacheza na hawa jamaa wa Afrika Kaskazini wakianzia na pambano la ugenini ambalo litakuwa la machozi jasho na damu kwa wenyeji.
"Wydad wamepoteza mechi mbili. Moja nyumbani dhidi ya Jwaneng nyingine wamepoteza dhidi ya ASEC Mimosas. Pambano hili dhidi ya Simba watalitumia kwa kujaribu kuwafuta machozi mashabiki wao. Hawatataka kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, au mechi ya tatu mfululizo katika kundi. Simba wana kazi.
"Kama Simba wataweza kufanya vema katika mechi mbili zijazo dhidi ya Wydad, huku ASEC na Jwaneng wakipunguzana wenyewe kwa wenyewe inaweza kuwasaidia. Tatizo ni kwa Simba ipi? Hii ya Onana? Benchikha ana kazi kubwa ya kufanya. Tusubiri tuone.” Mchambuzi Edo Kumwembe.
Hatma ya Yanga bado, Yanga watashinda mechi ijayo.