Uchambuzi: Katiba Mpya

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Yapata miaka 7 tangu 2015 Mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya ulipokwama baada ya wawakilishi wa makundi mbalimbali katika bunge la katiba kushindwa kuafikiana kupitisha katiba pendekezwa.

Mkwamo huu ulichukua sura mpya baada ya Uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo hayati John Magufuli aliyechaguliwa kuwa Rais kisha kutamka wazi kuwa jambo la katiba mpya halikuwa kipaumbele katika utawala wake uliokoma machi 17, 2021 alipokata pumzi.
Baada ya kifo cha Magufuli aliyekuwa makamu wake Samia Suluhu Hassan akachukua kiti cha Urais ambacho mpaka leo anakikalia kwa mujibu wa katiba ya jamhuri.

Baada ya kuapishwa Rais Samia alikiri kuwa jambo la katiba mpya ni muhimu ingawaje linapaswa Kusubiri kidogo hali ya uchumi na changamoto mbalimbali ndani ya nchi zitatuliwe.

Miezi kadhaa mbele Samia akiongoza kamati kuu ya chama tawala cha Mapinduzi CCM, ambacho yeye ni mwenyekiti, kamati ililidhia na kuunga mkono mchakato wa mabadiliko ya kikatiba.

Kwa mtazamo wa CCM mchakato unapaswa kuendelea ulipokomea 2015 baada ya kuvurugika.
Ingawaje wadau mbalimbali na vyama vingine vya siasa wanahimiza mchakato uanze upya kwa kuangalia maoni ya Wananchi yaliyokusanywa na tume ya mabadiliko chini ya Jaji msaafu Joseph Warioba.

Je nini kinakwamisha kikatiba mpya kupatikana kwa haraka licha ya kila upande kukubali umuhimu wake?

Sababu ya kwanza ni mtazamo na muitikio wa chama tawala kilichopo madarakani chini ya Rais Samia.

CCM haiamini moja kwa moja katika mabadiliko ya katiba nzima bali inaona bora yafanyike mabadiliko ya vipengele vichache vinavyolalamikiwa ndani ya katiba ya 1977.

Katika kusimamia msimamo huo Rais Samia aliteua kikosi kazi chenye wajumbe kadhaa ili kukusanya maoni kwa wadau namna gani yafanyike mabadiliko ndani ya katiba.
katika ripoti ya awali kikosi hicho kiliwahi kutamka wazi kuwa wadau wamependekeza mabadiliko ya katiba yafanyike baada ya Uchaguzi mkuu wa 2025 jambo ambalo lilipingwa vikali na wadau waliodaiwa kutoa maoni pamoja na wananchi.

Kikosi kazi kiliingia tena kazini ambapo muda wowote kinatarajia kukabidhi ripoti mbele ya Rais.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi na vyama vya siasa kuwa kikosi kazi kinapoteza muda kwakua maoni yalishakusanywa na tume ya warioba.

Sababu ya pili ni wananchi kutegemea vyama vya siasa na wanasiasa ili kufanikisha madai ya katiba mpya jambo ambalo ni gumu kwa namna fulani.
Kutokana na sababu mbalimbali wanasiasa wanaweza kuchelewesha madai ya katiba mpya kutokana na kuwa na harakati zisizo na mwendelezo kutokana na kuendekeza maslahi yao binafsi na ya vyama vyao.
Mfano ikitokea Mwanasiasa anae tegemewa kuongoza kampeni ya madai ya katiba mpya akateuliwa kuwa kiongozi katika wadhifa fulani Serikalini ni wazi kuwa atapunguza nguvu katika harakati.

Pia Mwanasiasa anaweza kukabiliwa na vishawishi kama kupewa rushwa ya fedha ili asiwe kipaumbele katika madai ya katiba mpya.

Wananchi kuendelea kuwasubiri wanasiasa wajenge njia ya madai ya katiba mpya ni kujichelewesha kwa maana ni rahisi kuwaziba midomo wanasiasa lakini haiwezekani kuwaziba midomo wananchi zaidi ya milioni 50 wakiamua kudai katiba mpya kwa vitendo.

Uwepo wa wananchi na Viongozi wasio na msimamo wa mawazo pia kunachangia kuchelewa kwa mchakato wa katiba mpya.
Kuna Viongozi ambao hawana msimamo wa kimawazo licha ya kutambua umuhimu wa suala la katiba mpya bado ni watumwa wa fikra za wakuu wao katika vyeo hawasimami na mawazo ya Wananchi ambao ndio Chanzo cha uwepo wa serikali.

Hofu ya chama kilichopo madarakani kupoteza madaraka inaweza kuchangia kuchelewa kwa mchakato wa katiba mpya.
Kama CCM inaamini mchakato wa katiba mpya unaweza kuoindoa madarakani basi ni wazi kuwa inaweza kuwa sababu ya kuchelewa kwa mchakato.

Kukosekana kwa umoja baina ya makundi mbalimbali ya vyama vya siasa, wananchi na serikali juu ya mchakato wa katiba mpya kwakua kila kundi linavutia upande wake bila kuangalia maslahi mapana ya taifa kwa maendeleo ya kizazi kilichopo na kijacho.

Sababu nyingine ni ukosefu wa elimu ya msingi juu ya katiba na masuala mbalimbali kuhusu mifumo ya utawala, demokrasia na haki za binadamu ambapo wananchi hawawezi kuchukua hatua na kutekeleza wajibu wao.

Follow Peter Mwaihola
 
Mkuu tutamaliza bucha zote ..., ila mzizi wa fitina ni huu hapa:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu
 
Safi sana peter Mwaibora
 
Back
Top Bottom