Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,920
- 15,611
Jeshi la anga la Ukraine hapo kabla ya kuanza kwa vita liliripotiwa kuwa na mifumo mingi anuai ya ulinzi wa anga lake, ambayo ni:
Sababu ni kuwa sasa hivi anga la Ukraine lipo uchi (halina ulinzi) na hivyo ndege za Russia zinajimwaga zipendavyo na popote pale zashambulia. Kwa maneno mengine ni kuwa ndege za Russia hazipati upinzani kwenye anga la Ukraine. Mnamo March 9, Russia iliripoti kuwa, kwa kutumia makombora ya shabaha kali zaidi ilikuwa tayari imeishashambulia na kuangamiza pisi 137 za S-300, Buk-M1 na S-125, ambapo kwa mujibu wa Russia hiyo ni sawa na zaidi ya asilimia 90 ya nguvu za ulinzi wa anga (makombora ya masafa marefu na mafupi) wa keshi la Ukraine.
Pia Russia ilisema kuwa iliharibu vituo 81 vya rada za Ukraine, na hivyo Ukraine kupoteza uwezo wa kukontol mapambano ya angani ya ndege zake na pia mifumo yake ya ulinzi wa anga.
Maelezo hayo ya Russia yanasapotiwa na maombi ya mara kwa mara ya Zelensky juu ya Marekani na nchi mbalimbali za NATO kusaidia kuzuia mashambulizi ya anga ya Russia, ikiwemo kuomba pisi moja S-300, na ndegevita nyinginezo.
Cc: T14 Armata, Mwanamkiwi
==========
- Pisi 250 za S-300 air-defense systems ambazo ni aina za S-300P, S-300PS na S-300PT. Hizi zote zinaweza kurusha makombora (SAM) ya masafa marefu ktk kulilinda anga
- Takribani pisi 72 za Buk-M1 systems ambazo hutoa makombora (SAM) ya masafa mafupi
- Pisi kadhaa za S-125 Pechora systems ambazo hurusha makombora (SAM) ya masafa mafupi
- Pisi 37 za Mikoyan MiG-29
- Pisi 34 za Sukhoi Su-27
- Pisi 14 za Sukhoi Su-24M bombers
- Pisi 31 za Sukhoi Su-24 close air support aircraft
- Tusingesikia ripoti nyingi za kushambuliwa na kuangamizwa kwa ngome za kijeshi, maghala/bohari za silaha, kambi za kijeshi, viwanda vya kijeshi, karakana za kijeshi wala majengo mbalimbali ktk mikoa/miji yoote ikiwemo Kyiv.
- Tusingemuona na kumsikia Zelensky akimpigia magoti Biden ampe pisi moja ya S-300 (wakati Ukraine inazo pisi 250 za S-300)
- Tusingesikia Zelensky akiziomba nchi za magharibi zisaidie kuikinga Ukraine na mashambulizi ya angani ya kila kukicha ya ndegevita za Russia (kuseti No-fly zone).
- Tusingemsikia Zelensky akililia apewe msaada wa pisi moja ya air defense system toka Israel
- Pia pengine tusingemsikia Zelensky akiomba pisi chache za ndegvita za kisovieti za MiG-29 toka NATO/Poland (wakati tayari anazo ndege za aina hiyo pisi 37)