Uchaguzi: Wenyeviti serikali za vijiji CHADEMA 8 CCM 3

"Ni upepo tu huo utapita, CCM ina mtaji wa wanachama milioni 6"!!!!!!! Fikra za kimagamba ni fikra zilizokufa.
 
Nakwambia mimi jana alikuja balozi wa CCM anaalika watu waende kwenye uchaguzi wa balozi. Alidai amealika kikao hicho mara tatu lakini watu hawahudhurii. Wameandaa pia form za kujaza kila mpiga kura nadhani wanafanya sensa ya wanachama wao. Kilichonishangaza ni kwamba hawataji kuwa ni uchaguzi wa CCM ila wanasema tu ni uchaguzi wa mjumbe wa shina letu. Nilijaribu kumdadisi kuwa je hawa ni wajumbe wa CCM au serikali? Akasema na yeye hajui, ndipo nilipoamua kumwambia ukweli kuwa uchaguzi wa CCM unawahusu wanaCCM na siyo kila mtu maana uchaguzi wa serikali za mitaa ni 2014. Alitoka amenyong'onyea akidai hata yeye ameshachoka anataka wengine wachaguliwe. Inaonyesha zoezi la uchaguzi wa ccm kwenye ngazi ya mashina haliendi kabisa sehemu nyingi sijui watafanyaje maana huko ndiko wanakojivunia kuwa wanarecord ya wanachama wao waaaminfu. Hawataamini macho yao watakapopata repoti za uchaguzi wa mwaka huu na pengine hautafanyika kabisa. Nilimwambia nitaenda kwenye kikao kile ili tuwaelimishe tofauti hizi ili watu waamue kama wanashiriki au la. Pia nilimwambia tutachagua mjumbe wakutuwakilisha eneo letu si kwa kigezo cha chama fulani ila atakuwa coordinator wa shughuli za eneo letu ila hatakuwa wachama fulani. Watu wengi hawana uelewa wa tofauti ya balaozi wa ccm na serikali ya mtaa au kitongoji, bado wako kwenye chama kimoja.

Hapa ndo nimegundua kuwa hata wale wananchama 6m wa ccm si kweli maana wanawatumia hawa mabalozi kufanya hiyo sensa ambayo wao either kwa kutokujua hujitambulisha kama watumishi wa serikali hivyo inakuwa rahisi kuwachukulia watu wote kwenye eneo lake ni wa CCM hata kama hawana hata kadi ya CCM.

Chadema wanatakiwa kutoa elimu juu ya jambo hili wanapofanya mikutano ya hadhara maana huwa linawa cost sana inapofika wakati wa uchaguzi maana akina mama wanawaogopa hawa mabalozi wakidhani ni watumishi wa serikali hivyo wakisema kitu akina mama huwa wanatii na hapo ndiyo huwa mwanzo wakukusanywa kwenye vikundi na kupewa chumvi na fulana za magamba. Na kwa vile mama zetu hutpima moyo kufanya maamuzi, hujikuta wanashindwa kuisaliti CCM siku ya kupiga kura kwa sababu ya chumvi tu. Akina mama wakielimishwa kuwakatalia hawa mabalozi itakuwa mwisho wa CCM huko vijijin!
 
"Kulikuwa na vituko vya hapa na pale na katika tukio lililovuta hisia za wengi ni lile la aliyekuwa mgombea wa CCM kijiji cha Minkoto, Lupil Siengo, kuhamia Chadema muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo aliyekuwa mpinzani wake, Alphonce Kanungo wa Chadema kuibuka kidedea"
 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vingi, CHADEMA wamepita bila kupingwa katika baadhi ya vitongoji. Furaha zaidi, mgombea mmoja wa ngazi ya Mwenyekiti wa Kijiji kwa tiketi ya CCM amejiunga na CHADEMA mara moja baada ya matokeo kutangazwa.
 
Huu ni upepo tu unapita
attachment.php
 
hakika ni ni maombi na dua za watz mungu amesikia na hakika wajiandae kupumzika milele mwaka 2015 na wale wote waliofilisi rasmali zetu tuwa hoji na kama wana hatia warudishe mali zetu na wafungwe, kamwe tuctengwe na dhana za udini, ukabila au ukanda watz adui wetu ni wala rushwa na wahujumu uchumi na maendeleo yenye tija kwa kila mtanzania anaeishi hapa,
Vijana tumekula kiapo kuondoa huu mfumo dhalimu.
Viva CDM, wanafiki wote tuwatimue wacje waka tuwekeya kiwingu kama kule Kenya wakati wa mabadiliko mwaka 2003-2007.
wakubwa nawasilisha.
 
M4C hatari, viva chadema and its a good move towards 2015.

kidogo kidogo mwisho watazoea kuwa wapinzani. Mungu ibariki tz,Mungu wabariki waliochaguliwa wawatendee mema wananchi. Mungu walaani mafisadi wote wa nchi hii
 
Kipigo kinaendelea..

Magamba yamejifungia yanajadili pumba na kuota vitambi!!
 
Back
Top Bottom