Uchaguzi usipoleta maana hiyo ni uharibifu wa muda!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Demokrasia tunayoifuata ni kuchagua kiongozi umtakaye katika mazingira yatakayoonesha kwamba ameshinda au kushindwa kihalali. Yaani haki ya mpigakura ionekane peupe, na kuheshimiwa na wadau wote.

Hilo ni muhimu kwani siku mpigakura nitakapogundua kwamba nipige au nisipige kura yangu yote ni sawa!
Kwa hakika sitapoteza muda, kusimama kutwa, katika ninalofahamu kuwa nani atashinda, liwake jua, inyeshe mvua.

Kwamba inahitaji ujasiri wa kiwenda wazimu, kwa mtu mzima kujifanya eti ninachagua kiongozi, ilihali nikijua ninatwanga maji kwenye kinu, mshahara kuloa shati.

Kwamba unanihamasisha nipige kura, huku wewe unalazimisha isivyo haki kumuweka rais, mbunge au diwani umtakaye katika mahali palipokusudiwa.

Kimsingi hiyo haitakuwa ni haki.

Yaani mimi nitakaponifikisha hapo sina la kufanya zaidi, isipokuwa nitaacha kujishughurisha na mambo ya uchaguzi.

Ni bora nipoteze haki yangu ya kuchagua au kuchaguliwa, kuliko kufanyiwa na watu kanyaboya.

Ndiposa tuliona kama taifa tuwe na katiba mpya, itakayokuja na tume huru ya uchaguzi.

Ndugu zangu viwili hivi ndivyo vitachochea hamasa ya kutumia haki hiyo ya kuchagua ama kuchaguliwa na wengine.

Wakati tukiendelea na.danadana za katiba mpya tusisahau usemi usemao kuwa; Mamlaka ni kama kushikiria kindege, ambapo ukikibana sana kinakufa! Na ukilegeza mno kinaruka!

Kumbe kinachotakiwa hapo ni ku-balance.

910c0421d5d0583e0fab21e447045f63.jpg
 
View attachment 2766362
 
Attachments

  • Screenshot_20230408-204546.png
    Screenshot_20230408-204546.png
    151.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom