Nimemsikia makamu Mwenyekiti wa CCM ndugu Philip Mangula juzi akiwa ktk ziara zake sambamba na katibu mkuu wa CCM ndugu Bashiru wakijigamba kwamba,uchaguzi ujao wa 2020 hakuna mbunge wala Diwani kutoka vyama vya upinzani watapenya,kwamba hawawezi kushinda hata jimbo na kata yoyote.
Kauli hii imekuwa ikisisitizwa sana na viongozi hawa akiwamo hata Polepole hasa pale wanapokuwa wanawapokea wabunge au madiwani wanaohama vyama vya upinzani,na kwa mantiki hiyo inaonekana ni moja ya silaha wanayoitumia kuwarubuni na kufikia bei hata kuhama.
Nimetafakari kwa muda sana kuhusu kauli hiyo ya hakuna mbunge wala diwani wa upinzani atakaepenya...nawaza je CCM hii inapendwa sana? Je CCM hii imetekeleza vema ilani yake? Je CCM hii inawajali wanyonge? Je CCM hii inawavutia watu kwa sababu ya Itikadi yake?.
Maswali hayo yakanifanya nirejee kitabu cha Makwaia wa Kuhenga,kiitwacho CCM NA MSTAKABALI WA NCHI YETU.
Nimekutana na kauli ya Mzee Mangula ya mwaka 2007 ktk uchaguzi wa chama,ilinukuliwa na mwandishi nami nainukuu,
"Tusipoangalia udiwani na Ubunge utakuwa unapigwa mnada au kufanyiwa tenda na hivyo uongozi kununuliwa na wenye fedha"
Hili tumeliona,sasa CCM inawanunua wapinzani kwa kuwahonga vyeo na pesa kujaribu kuhalalisha kupendwa kwao,tena mtoa kauli hiyo ndio anasimamia mauzo na tenda.
Lakini kitabu hicho,mwandishi amemnukuu Dr Bashiru,wakati akihojiana nae,nami namnukuu.
Chama cha siasa sio mkusanyiko wa majini dume yenye tamaa...Majini ambayo yametanguliza tamaa kufa na kupona,tamaa ya kutengeneza pesa au kupata vyeo kwa gharama yoyote"
Sasa Leo Bashiru huyo huyo ndio anayatafuta majini dume,amekuwa dalali wa majini dume yanayosaka madaraka au pesa ayajaze kwenye Chama chake kionekane kinakubalika pamoja na mwenyekiti wake ndugu John Magufuli.
Mwandishi pia ukurasa wa 21 amenukuu barua ya Mzee Butiku kwenda kwa mwenyekiti wa CCM wakati huo Mzee Mkapa...
Anasema,
CCM haitaweza kuepuka kuvunjika kutoka na dhambi ya kukiuka maadili,ahadi na kiapo chake chenyewe.CCM ambayo inaliacha Bunge lake kutunga sheria ya kuhalalisha rushwa na kuiita takrima......haiwezi kuepuka hukumu ya dhambi ya kuruhusu kupitishwa na kutumia sheria ambayo ina udhalimu ndani yake.
Leo CCM wanahonga pesa na vyeo kununua wabunge na madiwani ili kuaminisha watu CCM inapendwa sana,kuaminisha mwenyekiti wao Magufuli anapendwa sana.
Kwa mtiririko huo wameanza kuaminisha umma,wabunge na madiwani,na wale wanaotaka kugombea uchaguzi ujao kupitia vyama vya upinzani kwamba hakuna atakaepenya,hakuna atakaechaguliwa,kauli hii inarudiwa sana, ili iwaingie wananchi NA waiamini....
Najiuliza kwa kipi? Hivi Leo CCM ni Chama cha Itikadi gani? Ni ujamaa au ubepari?yaani Chama kimebaki tu kama genge LA wapiga fedha za umma.Nisaidieni CCM kinafuata itikadi gani?
Wamefeli kutekeleza ilani wenyewe,wanatumia ujinga wa wananchi kuwalaghai,walichosema kuhusu Mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ibara 152(e) kupunguza bei ya gesi na majiko ili kuokoa misitu nalo wameshindwa.
Walisema wataendeleza mamlaka za serikali za mtaa nako wamefeli,maana badala ya kuhamasisha Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato ili zijiendeshe vema,wakazipora vyanzo vya mapato,walisema watazifanyia mapitio sheria ili kuharakisha ugatuaji wa madaraka nako wamefeli.
Ibara 145(a) kuhusu utawala bora,demokrasia na uwajibikaji hili kili mtu anajua wameshindwa vibaya.
Ibara ya 145(g) ya ilani yao walisema watakamilisha mchakato wa katiba mpya,matokeo yake Mwenyekiti wao na Raid Magufuli alikataa kwamba haikuwa kipaumbele chake.
Hali ya uchumi na maisha ya watu yalivyo kila MTU anasoma namba.
Sasa huo mkazo wa kusema wagombea wa upinzani hawatachaguliwa utajwa sana based on what???
Nilichokigundua ni kwamba...
Jeshini kina kitu kinaitwa TARGET DAMAGE CRITERIA.
Kuna criteria NNE
1: Annihilation, upigaji target kwa kina hii ni wa kuingamiza target isiweze tena kuhama,kuondoka(Maneuver) hapa kinachokuwa huwa ni target ya platoon(Platoon strong points) au eneo lililohifadhiwa mizinga na vifaa vyake.
2emolition: Uboamoaji/Kuharibu.
Upigaji wa target kwa kina hii kinachokuwa komekusudiwa ni kubomoa majengo,madaraja,au njia na kusababisha kutokutumika tena.
3:Neutralization: Ni upigaji wa target na kufanya isiweze ku-maneuver kwa muda.
4:Harassment: Upigaji huu wa target hukusudiwa kuleta usumbufu kwa target iliyokusudiwa,hii ndio hutumika kwa ajili ya kushusha morali wa wapiganaji, maana ni pigo LA kisaikolojia,hutumika kwa ajili ya demoralization kwa adui.
Katika mapambano moja ya jambo muhimu sana ni Morali wa wapiganaji, kwa hiyo kauli ya CCM kupitia kwa makamu mwenyekiti Mzee Mangula na katibu wao Bashiru wanajaribu kutumia hii Target Damage Criteria namba 4 ya Harassment fire ili kuweka psychological pressure kwa wabunge walioko upinzani,madiwani na wanaotaka kugombea uchaguzi ujao ili wawe demoralised (washuke morali) kisha wajisalimishe CCM.
Ukweli ni kwamba CCM wameshashindwa,tena kadri siku zinavyosonga ndio wanachukiwa sana na RAIA,Upinzani unazidi kuimarika hususan CHADEMA... Na Kuna baadhi ya uimara huo umejengwa na CCM.
Wasitetereke kwa wachache wanao hangaika na vyama kuvitumia kama daraja la kupata madarka au pesa.
Tuendelee kudai Tume huru, wenye kuathiriwa na harassment fire waende,RAIA tupate Tume huru ndio watajua CCM inapendwa au La
Sent using Jamii Forums mobile app