Uchaguzi Jimbo la Kalenga: Vitus Lewa mwana wa Kalenga umma unakuhitaji!

Habari WanaJF,

Bila shaka Wanachi wa Kalenga wanasubiri kwa hamu List ya Wagombea kupitia vyama mbalimbali,ktk uchaguzi mdogo wa ubunge utakaofanyika mapema mwezi Machi.

Ama kwa upande wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) bila shaka kuna makamanda tayari wameshatangaza nia ya kugombea ubunge,miongoni mwao ni Mwl.Vitus Lawa.
Huyu ni kamanda ambaye ameongoza harakati hasa kanda ya kaskazini(hivyo namfahamu vilivyo)
Pengine Jina VITUS LAWA likawa geni wa baadhi yetu,basi kama ni hivyo;
VITUS LAWA ni Mwalimu aliehitimu shahada yake pale Mwenge Univesity. Kwa kuwa alipangwa kikazi maeneo ya Lushoto hivyo harakati alizifanyia kanda ya kaskazini.
Bw.Vitus Alianza harakati za kisiasa mwaka 2010 akisimama kama mshauri mwezeshaji Kwa wagombea wa Udiwani na Ubunge wilaya ya Lushoto kupitia Chadema.Alihusika pia kwenye uanzishaji Na ufunguzi wa ofisi mbalimbali za chama ikiwemo kuandaa mikutano ya Chama.
Kwa kifupi,huwezi kutaja maendeleo ya Chadema Lushoto bila kumtaja Mwl.Vitus Lawa
kwani kwa sasa ni bado ni mshauri Chadema Lushoto na akiwa kama mlezi wa chama Kata ya Ngwelo.

Ama kwa upande wa Wilaya ya Simanjiro alisimama kama wakala wa chama kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki uliomuingiza kamanda Joshua Nassari bungeni.
Pia amekua mjumbe wa sera,utafiti na Irani ya Chama kanda ya kaskazini.

Nyota njema huonekana Asubuhi, Kwa wale Mlio soma Chuo kikuu cha Mwenge kati ya mwaka 2010-2013 mtakubaliana ma mimi kwamba Bw.Vitus Lawa amekua mshauri wa baraza la wazee,akisimamia ushawishi wa Chama kwenye serikali ya wanafunzi na Ngazi nyingi
kwa Upande wa Kalenga alianza harakati tangu mwaka jana hivyo bila shaka baadhi wanatambua mchango wake.

Ni Mwaka jana alipotangaza nia yake kwa maandishi akiomba Wanachama wenzake kumpa ridhaa ya kuwa Mrithi wa nafasi ilochwa wazi na Dkt.Mgimwa aliefariki.
Sisi watu wa kanda ya kaskazini kwa kweli tunaamini Chama kitampa ridhaa na hivyo kumpa nafasi ya kukomboa wana KALENGA

Kila la kheri Bw.Lawa.

Hivi nyinyi makamanda wa Chadomo mbona kila mtu msemaji..........pili Mgimwa kafariki Januari 2014 wewe kwa nini unasema mlikubaliana mwaka jana......hili ndio tatizo la chama kutokuedeshwa kitaasisi
 
Kuweka kumbukumbu sawa Kamanda Vitus Innocent Lawa (Mtoto wa Walimu) ameshiriki kwa kiasi kikubwa kujenga jimbo la Kalenga kupitia programu ya "CHADEMA NI MSINGI".Pamoja kuwa mwalimu anatumia muda anaopata kushiriki katika ujenzi wa chama.

Kamanda Vitus Innocent Lawa ni mzizi imara ukilinganisha na wagombea wengine kwa kuwa na mtaji mkubwa wa kisasa kutokana na historia yake na wazazi wake.Ni kamanda aliyekulia kwenye familia ya walimu,Wazazi wake wamefundisha shule mbalimbali za jimbo la Kalenga, ametokeo kwenye ukoo wenye historia kubwa kwa wananchi wa Kalenga. Naamini atapeperusha vizuri bendera ya CHADEMA.

Nashukuru kwa ufafanuzi!!

Kwa hapo anakianzio kizuri... Ahakikishe walimu wote wa kalenga anawafikia ikibidi mmoja baada ya mwingine... na kijijini walimu ni muhimu sana!!1
 
Back
Top Bottom