Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Naunga mkono hoja kwasababu tanzania ilipofikia sasa tumefanya siasa kama mchezo wa mpira kila mtu anataka timu yake ishinde hata kama aina ubora na kusahau kuweka maslai ya taifa mbele,mikwangu naona ni bora tuondoe itikadi zetu na tuchague kiongozi bora na si bora kiongozi ili mradi wananchi waweze kupata maendeleo.

Wale viwavi wa cdm leo hawana cha kusema hasa baada ya kamanda Rostam kushiriki uzinduzi wa kampeni chini ya uongozi wa Raisi mstaafu mzee Benjamini William Mkapa

Mkapa,Rostam ni wezi hivi wanasema nini wakipanda jukwaani?Mwombeni na Mramba aje kuwasaidia

Kama kujaza watu ndiyo kushinda uchaguzi basi acha tusubiri na tuone!

Hivi ndugu yangu Mwita, wewe umeajiriwa humu kwa kazi moja ya kubisha tuuuuuuuu au? hebu tupe uwiano wa hizo picha basi then ulete zako kuthibitisha kuwa anachosema PLATO ni uongo.
Watu wengine sijui mna hurka gani!

wale viwavi wa cdm leo hawana cha kusema hasa baada ya kamanda rostam kushiriki uzinduzi wa kampeni chini ya uongozi wa raisi mstaafu mzee benjamini william mkapa
du. Kamanda wa nini? Kagoda agricurture? Aa dowans?

Wale viwavi wa cdm leo hawana cha kusema hasa baada ya kamanda Rostam kushiriki uzinduzi wa kampeni chini ya uongozi wa Raisi mstaafu mzee Benjamini William Mkapa
Huo wa RA siyo ukamanda, bali upungufu wa akili. Kama ana akili timamu hawezi kukaa jukwaa moja na akina NAPE aliowashutumu kwa siasa uchwara zilizochangia yeye kuachia ngazi. Huu ni wendawazimu kabisaa!

Wale viwavi wa cdm leo hawana cha kusema hasa baada ya kamanda Rostam kushiriki uzinduzi wa kampeni chini ya uongozi wa Raisi mstaafu mzee Benjamini William Mkapa

Wakuu,

Wengi tumeshangaa Rais mtaafu kupanda tena jukwaani, kwa kawaida tulikuwa tumezoea kuliona Tingatinga la CCM (Samweli Malecela) kuwa front na kukata kata magogo, mizizi, miamba na miti ili kuchonga barabara.

Cha ajabu namwona Mkapa naye anapiga front Igunga, ndiyo najiuliza VIPI HILI NDIYO TINGATINGA JIPYA LA CCM ? kama kweli hili limetengenezwa toka China, Japan au Ujerumani? Je litahimili misukosuko ya miamba ardhini na kusonga mbele?

Binafsi watu tunamuheshimu sana huyu Rais wetu katufanyia mengi sasa kupanda jukwaani ni ishara kuwa sasa anataka mashambulizi yote ya kiasiasa yaanze kuelekezwa kwake? Je bado anaweza purukushani za kisiasa za majukwaani? Je atavumilia makombora toka kwa vijana wa CHADEMA? hatakasirika?

Tunamkaribisha sana igunga ila asije akatuambia sisi vijana tunamkosea adabu maana kaingia mwenyewe ulingoni kwa mara nyingine tena.

MY TAKE: CCM acheni wazee wapumike, kulikuwa hakuna haja yoyote ya kumsumbua mzee wa watu, kashawatumikia wananchi miaka 10 akiwa rais na mingine mingi tu. Huu ni muda wake wa kupumzika. Kama Mmewakosea wananchi na mna uhakika hawatawapeni kura angalieni mlipojikwaa lakini si kuwasumbua wazee wetu. Mtamponza mzee wa watu.

Hivi mnafikiri haya maneno ya kinafiki yanalisaidia taifa?

Kama kuna chama cha siasa kilichofilisika kimaadili na ki-utashi basi ni CCM. Uwepo wa Rostam Azizi kwenye hii kampeni defies logic kabisa kabisa! Swali la kujiuliza kwa nini kuna uchaguzi mdogo leo hii Igunga? Aliyechaguliwa mwaka jana amekufa? kama hajafa nini kilimpata? na inakuwaje mtu mliyemkataa (according to ccm na wimbo wao wa mgamba) leo hii mnakubali?

Mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi Rais Kikwete alienda Igunga na kumnadi Rostam Azizi huku akisema ni mtu safi, miezi 10 baadae hao hao wakubwa wakasema Rostam hafai, leo hii wanarudi tena (ccm ile ile) kusema Dr. Kafumu anafaa! Kama walikosea kwa Rostam Azizi na kusema anafaa, leo hii wamepata wapi akili za kujuwa Dr Kafumu anafaa?

Halafu bila hata haya wala soni Mkapa na Mukama wanajidai kuwa Igunga ya 94 si hii leo! Wanadai kuna maendeleo! Kwani Igunga ya 94 haikuwa ya CCM? Nchi hii haijataliwa na chama kingine chochote zaidi ya ccm na mama yake (TANU). Sasa wanataka kusema IGUNGA ya 94 ilkuwa mbaya sana kwa sababu wakati huo ilikuwa (IGUNGA) chini ya FRELIMO? Wanaongea nini hasa hawa viongozi? Na hayo maendeleo wanayosema ni yepi hasa? Maji yanapatikana muda wote? Umeme wa uhakika? Wanafunzi wanafaulu zaidi kuliko sehemu nyingine Tanzania hii? au wana huduma bora za afya? Maendeleo gani?

Huo wa RA siyo ukamanda, bali upungufu wa akili. Kama ana akili timamu hawezi kukaa jukwaa moja na akina NAPE aliowashutumu kwa siasa uchwara zilizochangia yeye kuachia ngazi. Huu ni wendawazimu kabisaa!

The reverse should also be true: Kama Mukama, Nape, Mkapa etc ni wasafi sijui kwanini wanakubali kuambatana/kushirikiana na huyu Rostam. Rostam alitakiwa afichwe kabisa nyuma ya pazia asahaulike kwenye hiki chama. Unless wanataka kukubali kuwa yeye ni mkubwa kuliko chama. Je wanataka ku-symbolize nini hasa? Je huyu DPP kama kweli anania yakumshtaki Rostam na Manji akiona hili tukio anapata picha ipi hasa? Tusisahau action speaks louder than words!!

Wale viwavi wa cdm leo hawana cha kusema hasa baada ya kamanda Rostam kushiriki uzinduzi wa kampeni chini ya uongozi wa Raisi mstaafu mzee Benjamini William Mkapa

Makupa,Kujiuzulu kwa Rostam kunasababisha mamilioni ya fedha yatumiki kwny uchaguzi,wanafunzi hawana walimu,madawati wala vitabu,wajawazito matatizo kibao,je ahadi za leo za mkapa ccm hajawahi kuzitoa tena?miaka yote wao si ndio wameongoza hilo jimbo?hawakuyaona?Kujiuzulu kwa RA ndio siasa uchwara zim
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=171212&p=2474616

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom