Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
LATIFA,
Kila siku nakuambia jifunze matumizi ya herufu kubwa na ndogo, angalia sasa kumbe na wewe Kilaza, Teh teh teh teh

ignorance is a big setback to civilization .... i am out to ignore an idiot

Source: Mtanzania 9/9/11.

Kweli kama viongozi wetu ndio hawa, nchi hii sasa inaenda kubaya kabisa.

Wana JF: Nilidhani angeenda na kauli za kuwapoza wana Igunga kwa kipigo kikali cha maisha magumu na mlo mmoja, mfumuko wa bei na kilimo duni, yeye anasema kafurahi sana kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Dar hadi Igunga bila kuona vumbi.

Kimsingi, namuunga mkono na furaha yake kwa kuwa labda kwao lami ndio maendeleo. Ona haya ya Igunga;

1. Kilimo cha pamba hoi.
2. Huduma za afya mtihani
3. Shule ni kusadikikaa
4. Access to clean drinking water ni ndoto ya mwendawazimu
5. Huduma za kibenki mashahidi nyie.
6. Stendi safi ya mabasi imebaki kwenye ilani
7. Vikundi vya kinamama na vijana vya maendeleo hoi
8. Miundombinu kichekesho, shahidi yeye mwenyewe na Mwigulu,
9. ....
Sasa kwa yeye kusema anaona raha lami imepita Igunga, basi hiyo lami ndio itatatua matatizo hayo na mengine mengi? Lami itashusha bei ya sukari? Lami itashusha bei ya mkate? Vipi hiyo lami itagawa dawa kutibu magonjwa? Lami itawapa wana Igunga maji safi ya kunywa?

Mi nadhani Mkapa angeenda kuwaomba wanaigunga msamaha kwa kusahaulika na zaidi sana kuwaangukia ili wamchague mgombea wao badala ya kusema lami safi sana.

Wazee wa kazi, Nawasilisha.
Baada CCM ya kuangukia pua hapo igunga Mkapa atagoma kuongea na waandishi wa habari kuhusiana na hilo kama kawaida yake.

Watanzania wa kawaida na hasa wanaigunga wanakumbuka hoja mbili kila wanaposikia uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, kwanza tunafikiria juhudi za kujitakasa za Chama Cha Mapinduzi na pili tunakumbuka maneno ya kada maarufu wa chama cha mapinduzi ndugu na mpendwa wetu Rostamu Azizi aliyesema kuwa chama hiki kimebaki kuwa chama cha siasa uchwara kwa maana ya mjumuiko wa watu ambao kazi yao kubwa ni kuwachafua wengine.

Siku zote tumesikia ama kwa uwazi au kwa kificho juu ya tuhuma za mapacha watatu, mmoja amejitoa na wengine wawili bado. Swali na kitendawili ambacho lazima Mkapa akitegue leo au kesho wakati akizingua kampeni za CCM Igunga ni je Ufisadi CCM maana yake ilikuwa ni Rostamu pekee, je hoja ya Rostamu ya siasa uchwara, CCM inasemaje? vinginevyo hawataaminika na wanaigunga na watahesabika kama wameenda Igunga kufanya mchezo wa kuigiza.

Mkapa hata kama ni kada wa CCM chama hiki hakikumtendea haki na mimi kama mtanzania ambaye kodi yangu inamtunza Mkapa nasema kumuinua Rais mstaafu akafanye kampeni za ubunge ni kumdhalilisha, yeye saizi yake ni kumnadi Mgombea Urais. Hivi ikitokea CCM imeshindwa Igunga watasemaje? Mkapa atajisikiaje? najua wamemchukua kwa sababu ni mzoefu wa kushindwa rejea Temeke na Mrema. Mnapomdhoofisha lulu yenu nani atazunguka 2015 kumnadi mgombea wenu.

Mkapa asiye safi rohoni na machoni kwa Watanzania ushiriki wake Igunga nini tafsiri yake kwa Watanzania "Chama hiki hakina mtu safi anayeweza kumnadi mgombea wa CCM" Kwa nini si Salimu, Kwanini si Waryoba, Kwa nini si Anna Abdalah, Kwa nini si Nchimbi, Kwa nini si Sita? HAYA BWANA NAWAACHIA WENYEWE. Sijisikii amani Rais mstaafu kuingia mgogoro wa kupigana madongo ya kisiasa na vijana wa miaka 20 na hawatamuacha kabisa.

Ama kwangu mimi naona CCM imepanga kumumaliza Mkapa ili asiwe na mvuto au sauti katika mchakato wa kutafuta mgombea wao mwaka 2015. Kwa sababu kila akiinua shingo watamwambia na wewe yako tuliyasikia Igunga. Kama akishindwa watamwambia kaa pembeni wewe huwezi kumnadi mgombea wetu kwa hiyo usituchagulie

Usani wa CCM kwenye siasa ni kwamba wanataka wote wachafuke ili asiwepo wa kumnyooshea kidole mwenzake

VIVA uwazi na Ukweli

Ni kodi zetu sote CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, CCM , CHAUSA na kadhalika hivyo chama kimoja kujikweza na barabara fulani ni makosa.

ni kweli ccm ina nguvu, sababu wanatumia fedha za umma kufanyia kampeni. wenye vyeo fulani huko lg mpaka kampeni zikiisha watakuwa wana magari, pikipiki, n.k. wale low profile wataambulia kofia, flana na khanga za kuingia nazo hata kwenye nyumba za ibada!

Watanzania wa kawaida na hasa wanaigunga wanakumbuka hoja mbili kila wanaposikia uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, kwanza tunafikiria juhudi za kujitakasa za Chama Cha Mapinduzi na pili tunakumbuka maneno ya kada maarufu wa chama cha mapinduzi ndugu na mpendwa wetu Rostamu Azizi aliyesema kuwa chama hiki kimebaki kuwa chama cha siasa uchwara kwa maana ya mjumuiko wa watu ambao kazi yao kubwa ni kuwachafua wengine.

Siku zote tumesikia ama kwa uwazi au kwa kificho juu ya tuhuma za mapacha watatu, mmoja amejitoa na wengine wawili bado. Swali na kitendawili ambacho lazima Mkapa akitegue leo au kesho wakati akizingua kampeni za CCM Igunga ni je Ufisadi CCM maana yake ilikuwa ni Rostamu pekee, je hoja ya Rostamu ya siasa uchwara, CCM inasemaje? vinginevyo hawataaminika na wanaigunga na watahesabika kama wameenda Igunga kufanya mchezo wa kuigiza.

Mkapa hata kama ni kada wa CCM chama hiki hakikumtendea haki na mimi kama mtanzania ambaye kodi yangu inamtunza Mkapa nasema kumuinua Rais mstaafu akafanye kampeni za ubunge ni kumdhalilisha, yeye saizi yake ni kumnadi Mgombea Urais. Hivi ikitokea CCM imeshindwa Igunga watasemaje? Mkapa atajisikiaje? najua wamemchukua kwa sababu ni mzoefu wa kushindwa rejea Temeke na Mrema. Mnapomdhoofisha lulu yenu nani atazunguka 2015 kumnadi mgombea wenu.

Mkapa asiye safi rohoni na machoni kwa Watanzania ushiriki wake Igunga nini tafsiri yake kwa Watanzania "Chama hiki hakina mtu safi anayeweza kumnadi mgombea wa CCM" Kwa nini si Salimu, Kwanini si Waryoba, Kwa nini si Anna Abdalah, Kwa nini si Nchimbi, Kwa nini si Sita? HAYA BWANA NAWAACHIA WENYEWE. Sijisikii amani Rais mstaafu kuingia mgogoro wa kupigana madongo ya kisiasa na vijana wa miaka 20 na hawatamuacha kabisa.

Ama kwangu mimi naona CCM imepanga kumumaliza Mkapa ili asiwe na mvuto au sauti katika mchakato wa kutafuta mgombea wao mwaka 2015. Kwa sababu kila akiinua shingo watamwambia na wewe yako tuliyasikia Igunga. Kama akishindwa watamwambia kaa pembeni wewe huwezi kumnadi mgombea wetu kwa hiyo usituchagulie

Usani wa CCM kwenye siasa ni kwamba wanataka wote wachafuke ili asiwepo wa kumnyooshea kidole mwenzake

VIVA uwazi na Ukweli

Viongozi wa chadema wanatafuta kushika dola ya hii nchi Mkapa anatafuta nini sasa hivi?

Mkapa naona anafanya hivyo kwa sababu anajua madhambi aliyoyafanya ndiyo maana hawezi kumbishia JK akimwambia wasadiane kujibu mapigo. Kimsingi Mkapa angekuwa msafi kamwe asingehangaika anavyofanya leo. Anajua kama Chadema wakichukua hii nchi hayuko salama kwa ufisadi wake alioufanya.

Anaongea mbele ya umma kwa kujiamini akijua kuwa wanannchi wa kawaida hasa vijijini hawajui ufisadi wake. Amesahau kuwa habari huwaingia watu taratibu na Chadema wanaendelea kupenyeza habariza zake taratibu. Mambo yatakapokuwa hadharani kamwe hatadhubutu kuongea na hii Jeuri anayaoinyesha leo.

Ngoja tusubiri tuone kama ataweza kuhimili mashambulizi!

Kaingizwa choo cha kike mzee wa watuu sijui kama atatoka salama

Yes.

Naamini wana Igunga wote watakubaliana na kauli mbiu hii na watafanya kama ilivyoelekeza kuwa: KASHINDYE ASHINDE NA KAFUMU AFUMULIWE .

Hii inaonyesha kuwa CDM kuna vichwa vinavyofikiri! Kauli mbiu hii imekaa,imetulia na ni poa kabisa. Siyo kauli mbiu za Wanamagamba ambazo hazina kichwa wala miguu. Fikiria kauli mbiu ya MIAKA 50 inavyosema;ina-bore na inachefua mioyo! Eti Tumethubutu,Tumeweza,Tunasonga mbele. Ukianza kua-analyse neno kwa neno kuhusu kauli mbiu hii kuna maswali kibao yanayojitokeza. Unaposema umethubutu;kufanya nini,Je,ni kuendeleza UMASKINI,UJINGA na MARADHI kwa miaka 50? Unaposema Tumeweza; kufanya nini?Je,ni kufanya UFISADI,RUSHWA, UUZAJI/UGENISHAJI WA RASLIMALI ZA TAIFA KWA WAGENI kwa miaka 50? Unasonga mbele,maana yake unasonga mbele na huo UMASKINI,UJINGA,MARADHI,UFISADI,RUSHWA,UUZAJI/UGENISHAJI WA RASLIMALI ZA TAIFA KWA WAGENI kwa miaka mingine mingi ijayo!!!!

Hii ni kauli mbiu ya hovyo kabisa wala haiendani na hali halisi ya nchi yetu Tanzania. Bila shaka aliyetunga kauli mbiu hii alitumia makalio kufikiri na si ubongo!

Siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge jimbo la Igunga mkoani Tabora, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tayari wamekorofisha kwa kutuhumiana.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika chama hicho na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi na maafisa wa ngazi ya juu kutoka Makao Makuu jijini Dar es Salaam na Igunga, zinasema ugomvi huo umekuwa ukifukuta polepole na huenda ukalipuka zaidi hapo baadae huku viongozi wa kitaifa wakidaiwa wanafanya mchezo wa "kufunika kombe mwanaharamu apite"

Kukorofishana kwa viongozi wake wa wilaya ya Igunga, na Makao Makuu, kunatokana na kukataliwa kwa sehemu kubwa ya mapendekezo yaliyotolewa na wenyeji huku wageni wakijitawalia mamlaka makubwa ya kuongoza shughuli nzima.

Ugomvi umefika mbali zaidi baada ya CDM Makao Makuu kuendelea kutomuunga mkono mgombea ubunge wa CDM Joseph Kashindye, kwa vile wao walikuwa wakimtaka Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Taifa, Erasto Tumbo, dakika za mwisho alilazimika kuliondoa jina lake.

Huna lolote ww kwani unatoa maelezo mengi lakn hakuna ushahidi kwa uyasemayo na mlengo wako unajulikana kua ww ni mnafiki

• Thanks
Reactions: LAT
Nimeangalia kura za maoni kwa jimbo la Igunga kwenye site ya mwanahalisi, ingawa kura hizi hupiwa na Watanzania wote lakini pia inawapa taswira hawa wanaojiita wamiliki wa nchi (CCM) jinsi waTZ walivyochoshwa na Uzemba na udhalimu wao.

TiJFZSy2aCAAAAAElFTkSuQmCC

Kwa matokeo zaidi bofya hapa: Gazeti la MwanaHalisi

Ni moja ya alama kuashiria ushindi wa CDM huko Igunga................lakini nadhani haipaswi kubweteka tuongeze nguvu zaidi na maarifa ili ushindi upatikane hapo october,2

Kwani ulitegemea matokeo gani ikiwa gazeti lenyewe lilioendesha kura linafadhiliwa na Magwanda kwa asilimia 80?

......................Yule jamaa anayeitwa Mwita25 hapa JF ameiona hii thread,maana nasikia katumwa na Nape na ni mpango wa CCM kuonga hata member wa mitandao mbalimbali ya kijamii..na kwa taarifa za haraka huyu kilaza Mwita25 nae kasha kamata mlungula wake...

*CUF sasa yakata rufaa NEC dhidi ya CCM, CHADEMA
*CHADEMA waanza kampeni kwa kuwavaa Mkapa, Kafumu
*Mkapa atamba akisema kazi ni moja tu ni kushinda

Na Waandishi Wetu, Igunga

CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimeendelea kuwakomalia wagombea wa CCM na CHADEMA kwa kukata rufaa dhidi yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa
madai kuwa ni watumishi halali wa umma hivyo hawastahili kuwania kiti hicho.

Rufaa ya CUF inakuja siku moja tu baada ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo Bw. Protace Magayane, kutupilia mbali pingamizi la awali la chama hicho dhidi ya wagombea ubunge wa CCM na CHADEMA.

Akiwasilisha rufaa hiyo jana saa 8.30 mchana, mgombea ubunge wa CUF Bw. Leopold Mahona, akifuatana na mwanasheria wake ambaye pia ni Ofisa wa Haki za Binadamu na Sheria wa chama hicho Bw. Hashim Mziray, alisema anamini haki itatendeka kwa kuondolewa kwa wagombea hao.

Alitaja sababu za rufaa hiyo kuwa ni Dkt. Peter Kafumu (CCM) ni mfanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na huku mgombea wa CHADEMA Bw.Joseph Kashindye, akiwa Mkaguzi wa Shule Wilaya ya Igunga.

"Tumewasilisha rufaa yetu kwa sababu msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Igunga, ameshindwa kuwaengua Dalaly wa CCM na Kashindye wa CHADEMA kwa sabau bado ni waajiriwa wa Serikali. Kutokana na Ibara ya 72 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wagombea hawa wanatakiwa kuenguliwa," alisema Bw.Mziray.

Ofisa Uchaguzi Jimbo la Igunga Bi. Martha Bayo alipokea rufaa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw. Magayane na kuahidi kuwa itashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo Bw. Protace Magayane ametupia mbali pingamizi la CUF kutaka wagombea Ubunge wa CCM na CHADEMA waenguliwe kwa madai kuwa ni watumishi wa serikali na bado hawajaandika barua ya kujiuzuru nyadhifa zao.

Akiwa katika Kijiji cha Igurubi ambapo alianzia kampeni zake jana, mgombea huyo alitaja barabara inayotoka kijijini hapo hadi mjini Igunga na daraja la mto Mbutu kuwa kipaumbele chake cha kwanza iwapo atachaguliwa na kuomba siku 400 tu baada ya uchaguzi kukamilisha ahadi hiyo iwapo atachaguliwa.

Alisema Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bw. Rostam Aziz, waliahidi kujenga barabara hiyo na daraja la mto Mbutu bila mafanikio.

Alisema ana uchungu mkubwa na daraja hilo la mto Mbutu kwa madai kuwa ndugu zake wawili pia walipoteza maisha wakati wakivuka mto huo hivyo ni lazima awakomboe wananchi hao na adha hiyo ya muda mrefu.

CHADEMA wazindua kampeni

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe, amezindua rasmi kampeni za chama hicho kwa kumnadi mgombea wake Bw. Joseph Kashindye huku akiweka wazi kuwa CCM imefikia hatua za mwisho kufa.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza jana Bw. Mbowe alisema umati huo ni ushahidi tosha kuwa huo ndio ukweli kwa kukubalika kwa chama chake na kwamba kitashinda kiti hicho.

Alisema mgombea huyo ni risasi nyingine bungeni hivyo kuwataka wananchi kumchagua ili akaongeze nguvu bungeni na kwamba umasikini ambalo sasa ni janga la taifa halikuletwa na Mungu bali CCM.

Alisema nchi hivi sasa inatawaliwa na wageni kutoka nje na kwamba taifa limegeuka kuwa ombaomba huku kila mmoja akilalamika na kwamba ni aibu kwa serikali kuomba vyandarua vya mbu nje.

Akitoa takwimu alidai, wakati Rais wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi, anaondoka madarakani serikali ilikuwa inakusanya bilioni 25 kwa mwezi na kwamba maisha ya mtanzania yalikuwa nafuu kuliko sasa.

Alisema mafuta ya taa kupandishwa bei ni aibu kwa serikali kushindwa kusimamia sheria na kuwataka wana Igunga kuichagua CHADEMA.

Naye Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod Slaa, alimshukia vikali Dkt. Kafumu na Rais mstaafu wa awamu ya Benjamin Mkapa, akidai wamekuwa wakisimamia ufisadi ndani ya serikali kwa nyakati tofauti.

Alisema Dkt. Kafumu alishindwa kujiuzulu kutoka Wizara ya Nishati na Madini akidai kuwa wizara hiyo imegubikwa na kashfa ya rushwa na yeye anafahamu.

Alidai Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa kwa akimtuhumu kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu kwa kuanzisha kampuni ambayo alidai ilimnufaisha yeye binafsi chini ya mwamvuli wa Ikulu. “Akija hapa mdaini pango kwa kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu wakati ile ni mali
ya wananchi,”alisema Dkt. Slaa.

Alisema kuwa Dkt. Kafumu amekuwa akidai kuwa anapigana na ufisadi lakini huku ni kuwadanganya wananchi kwa kuwa alipaswa ajiuzulu kutokana na tuhuma za rushwa zilizoikumba wizara yake hasa katika sekta ya madini.

Dkt. Slaa aliwataka wananchi hao ambao walikuwa wamefurika katika uwanja wa Sokoine kumchagua Bw. Joseph Kashindye ili aweze kulinda rasilimali za Wana Igunga katika Halmashauri ili kupunguza panya waliopo wanaozitafuna.

Kwa upande wake Bw. Kashindye alisema ameamua kuacha ualimu ili kufuata nyayo za Baba wa taifa Mwalimu Julias Nyerere,aliyeacha ualimu kuwasaidia watanzania na yeye ameamu kuacha ualimu ili kutetea maslahi ya wana Igunga Bungeni.

Alisema fedha zilizokuwa zikipalekwa jimboni umo ilikuwa zimekuwa zikitumika vibaya na kwamba yeye akichaguliwa atazifuatilia huku akitoa mfano kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Hesabu za Serikali (CAG) alibaini wizi wa sh. bilioni tatu mwaka huu.

Mkapa atua na kutangaza ushindi wa CCM

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Benjamin Mkapa, aliwasili mjini Igunga jana
jioni na kutangaza rasmi kwamba kazi yake ni moja nayo ni kuitangazia CCM ushindi kwa kuwa ina cha kujivunia.

Rais Mkapa ambaye alisafiri kwa njia ya barabara kwa kile alichoita kuwa ni kutaka kukagua maendeleo makubwa yaliyofikiwa hivi sasa ndiye atakayefungua kampeni za CCM za Jimbo la Igunga
jumamosi.

"Nimewasili Igunga, wana Igunga kazi ni moja, ni ushindi tu," alisema Rais Mkapa wakati akisalimiana na wananchi baada ya kupokelewa katika kijiji cha Makomero kilometa
nane kutoka mjini Igunga.

"Nashukuru sana kuona kwamba mara hii nimefika hapa Igunga kwa kupita barabara ya lami, mara ya mwisho nilipita kukiwa vumbi tu, jamani haya si
maendeleo? alihoji Rais Mkapa huku akishangiliwa na wananchi.

Mkapa aliwataka wananchi wa Igunga kujitokeza kwa wingi Oktoba 2 mwaka huu kupiga kura na kuhakikisha wanampigia mgombea wa CCM Dkt. Peter Kafumu na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wamechagua maendeleo. "La msingi ni hilo mengine nitawaambia tutakapokutana katika mikutano ya kampeni, yapo mengi sana," alisema.

Msafara wa Mkapa ulipokelewa na magari yaliyozungukwa na vijana waendesha pikipiki na baiskeli. Kabla ya kuzindua kampeni za CCM katika viwanja vya Kumbukumbu ya Samora mjini Igunga leo Mkapa atakuwa na shughuli mbalimbali za kampeni na baada ya uzinduzi wa kampeni hizo ataendeleo na mikutano kesho yake.
Imeandaliwa na Peter Mwenda, Benjamin Masese na Moses Mabula

http://majira-hall.blogspot.com/2011/09/kivumbi-chatimka-jimboni-igunga.html#http://majira-hall.blogspot.com/2011/09/kivumbi-chatimka-jimboni-igunga.html#

Kwani ulitegemea matokeo gani ikiwa gazeti lenyewe lilioendesha kura linafadhiliwa na Magwanda kwa asilimia 80?

Kwa hiyo Unamaanisha RAI inafadhiliwa na CUF kwa sababu matokeo yake yanaonyesha Cuf ?Je wewe unaamini matokeo ya mtandao yanawakilisha wasomi wa Nchi hii hasa vijana ambao ndio tegemeo la taifa, usijidanganye na wala usijipe moyo.

Wakuu,

Wengi tumeshangaa Rais mtaafu kupanda tena jukwaani, kwa kawaida tulikuwa tumezoea kuliona Tingatinga la CCM (Samweli Malecela) kuwa front na kukata kata magogo, mizizi, miamba na miti ili kuchonga barabara.

Cha ajabu namwona Mkapa naye anapiga front Igunga, ndiyo najiuliza VIPI HILI NDIYO TINGATINGA JIPYA LA CCM ? kama kweli hili limetengenezwa toka China, Japan au Ujerumani? Je litahimili misukosuko ya miamba ardhini na kusonga mbele?

Binafsi watu tunamuheshimu sana huyu Rais wetu katufanyia mengi sasa kupanda jukwaani ni ishara kuwa sasa anataka mashambulizi yote ya kiasiasa yaanze kuelekezwa kwake? Je bado anaweza purukushani za kisiasa za majukwaani? Je atavumilia makombora toka kwa vijana wa CHADEMA? hatakasirika?

Tunamkaribisha sana igunga ila asije akatuambia sisi vijana tunamkosea adabu maana kaingia mwenyewe ulingoni kwa mara nyingine tena.

MY TAKE: CCM acheni wazee wapumike, kulikuwa hakuna haja yoyote ya kumsumbua mzee wa watu, kashawatumikia wananchi miaka 10 akiwa rais na mingine mingi tu. Huu ni muda wake wa kupumzika. Kama Mmewakosea wananchi na mna uhakika hawatawapeni kura angalieni mlipojikwaa lakini si kuwasumbua wazee wetu. Mtamponza mzee wa watu.

Ni tingatinga la kichina hilo,ambalo kwa nje linavutia ila ukigagua vifaa vyake vyote ni upupu mtupu..............Mkapa ni kati ya watu walitupumbaza watanzani tukapoteza uwezo wetu wa kujenga hoja na kusema wazi uovu wa viongozi.....aliminya uhuru wa kuongea na ndio maana unaweza ukasema alikuwa ni kiongozi mzuri...lakini ya Kiwira,ANBEN,BENK M nk ni alama tosha kusema huyu ni kati ya matingatinga ya kichina yaliyotengenezwa kuhuzwa nchi za dunia ya tatu...very cheap,very delicate....

Mwanaweja;2459872 Alisema Wassira atakwenda Igunga kuongeza nguvu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge said:

mwacheni akapige zake usingizi. na itakuwa kila akisimamishwa ili kuongea na wananchi, watu wa igunga watakimbia mbio kali kwa kuogopa SURA YAKE INAYOFANANA NA FARU wa porini.

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom