Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Maalim SEIF yupo IGUNGA
JE Yupo ki serikali au kichama? Kama ni kichama je Magari aliyotumia, Posho zake na za wapambe wake nani anawalipa?
Je haoni yale aliyokuwa anayalalamikia wakati akiwa mpinzani sasa yupo serikalini anayatenda?
 
Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,
Ukweli ni kuwa CUF haina historia na haijawahi kukifanyie vurugu chama kingine cha upinzani, CUF ni chama makini na tutaendelea kuwa hivyo, jana Igunga tumekuwa na misafara miwili, wafuasi wetu wengi walijigawa katika msafara wa Maalim Seif na kuhudhuria kikao cha ndani na at the same time wafuasi wetu wengine wengi walijigawa kumsindikiza mgombea wetu LEOPOLD MAHONA. Katika mazingira hayo automatically CHADEMA wangekuwa wengi katika urudishaji fomu kwani hiyo tu ndio ilikuwa shughuli yao jana huku sie CUF tukiwa na shughuli mbili tofauti kwa wakati mmoja na zote zilihitaji wafuasi na viongozi.

Msafara wa mgombea wetu ulienda kwa amani na hapakuwa na matatizo yoyote, masuala ya kuingiliana hayakuwa mantiki kubwa kwani kupeleka fomu hakukuwa na ratiba rasmi na kila chama kilijipangia, CUF tulipofika barabara kuu tukakutana na CHADEMA na tulipishana kwa busara kwani tumekutana barabarani kila mtu akitokea ofisini kwake and then tulipoenda mbele zaidi tulikutana na CHADEMA kwa mara ya pili na kila upande ulitumia busara ndio maana hatukupigana.

Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).

Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.
Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).

Baada ya matukio hayo tulilalamika rasmi kwa Kamanda Oparesheni Maalum(SIRO) na Kamanda wa FFU(Anacletus) ambapo baada ya kuwapa taarifa walituita viongozi wa CUF na CHADEMA kujadili chanzo cha vurugu hizo na kila upande ulitoa malalamiko yake.

Nataka kusisitiza kuwa sie CUF tumekwenda Igunga kumnadi mgombea wetu na kulisaka jimbo kwa njia za kidemokrasia, kamwe hatutamia silaha wala mabavu wala vitisho kuiska amani na demokrasia.

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu - Bara,
Chama Cha Wananchi CUF,
Igunga - Tabora,
07/09/2011.
Ndugu Mtatiro unazungumzia CUF ipi CUF-Bara au CUF-Zanzibar maana tulishawahi kusikia mnaweka vinyesi kwenye visima vya maji, kama hiyo sio fujo ni nini.
 
Im sure jf is the home of intellectuals. Please ague intellectually. Hoja si Maalim Seif kupokewa kwa shangwe ila katoa na kasema nini Igunga kilichopokewa kwa shangwe?

Halafu Maalim alikutana na wanachama wake wa Igunga na wala si wananchi wa Igunga. Tafadhal zingatia maana ya maneno uyasemayo.
 
Akichangia katika kikao hicho mjumbe mmoja Athumani Mambo, alisema kuwa CCM kumchagua Wassira kuwa mmoja wa wapiga kampeni katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ni jambo la msingi sana kwani Wassira anao uwezo mkubwa wa kushawishi wananchi.

Nafikiri alitaka kumaanisha "uwezo mkubwa wa kudanganya" au?? Maana wananchi wana macho ya kuona wao wenyewe!! Ushawishi wa nini??
 
Asante kwa taarifa mliopo igunga tunawategemea nyinyi mtupe taarifa kamili na zaukweli bila upendeleo.chadema kuweni macho kwani hao cuf wametumwa kuvuruga chadema kwa sababu kama kushinda hawana jeuri hiyo.

My conclusion! ni kweli CDM hali ni tete. Hii kulialia inaashiria maji yamewashika shingoni. Huwezi kuwa na majority halafu ukawa unalia kwa kasi hii. Hivi hiyo pipoz pawa Igunga hai- apply?.
 
Nimeweka taarifa ya mkakati Igunga na jinsi JF,WAHARIRI NA WAANDFISHI WALIVYONUNULIWA ILA NAONA HAIPOSTIWI JE?Moderetor nao wamefikia bei?
 
Mwandishi Jacob Daffi wa mwanahalisi amedai kunasa waraka wa ccm unaelezea kwamba ccm imepanga kutumia sh milioni 35 kuhonga waandishi wa magazeti na television ili kupika habari nzuri kuhusu chama hicho.

Lengo ni kuhakikisha habari nzuri tu ndizo zinaandikwa kuhusu kampeni za Igunga.

Kwa mujibu wa waraka huo magazeti yatakayotumika kwa mkakati huo ni mwananchi,majira,nipashe,jambo leo,habari leo na mtanzania.

Television zitakazohusika ni itv,tbc one na chanel ten.Pia baadhi ya mitandao ya kijamii itahusishwa katika mpango huu mchafu.

Imedaiwa mpango huu wote umeandaliwa na idara ya nape nnauye.Habari kamili imeandikwa uk wa 6 wa mwanahalisi.
 
mkuu tena udini umefikaje humu. Hebu changia mada husika acha udini humu. ukitaka huo udini yatakutokea puani.

Mkuu hata mimi nimeiangalia kwa makini hiyo picha na nilichoona ni hijab kibao, yeah! inabidi tu tuamini kuwa huo ulikuwa ni mkutano wa siasa hata kama mwongeaji haonyeshwi. "War is deceit"
 
Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,
Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).

Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.
Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).
Mtatiro hizo mbinu zenu zitawamaliza na mkiendelea hivyo mtaambulia kura mia tatu kama mlivyopata Busanda, kwa kushirikiana na CCM na polisi mmeambiwa kuanzisha fujo ionekane CDM inafanya fujo, kitendo cha kupeleka gari lenu la matangazo marambili mbele ya msafara wa CDM ni kielelezo tosha cha utovu wa nidhamu, halafu eti mnakuwa wa kwanza kukimbilia polisi mbinu za kitoto hizo.

Hizo mbinu za viwembe na visu si za CDM ni mbinu za CUF toka enzi za IGP Mahita mmezirithi toka Zanzibar mnafikiri na bara zita apply. Kama ushahidi wakukutwa na visu ni kadi na bendera za chama chao kwa hiyo ushahidi uliotolewa na Mahita kuwa CUF wamekutwa na majambia na visu tena vikiwa na rangi ya bendera yenu tuuamini? be greater man.
 
Akiongea na TBC taifa msimamizi wa uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga amesema vyama vya chadema na ccm vimechukua form za pingamizi,ameeleza kwamba hajajua watakuwa wanapinga wagombea wa chama gani kwani bado hawajarudisha form hizo na mwisho wa kurudisha ni sa' 12 jioni leo hii.

Tusubiri tuone, wasiwasi wangu isije ikawa zile tetesi za mgombea wa chadema kuwekewa pingamizi zina ukweli!
 
Nape na Mwigulu wamefikia wapi mpaka wanapeleka kijeba wa watu!!!!!!!! Du! magamba kwisha habari yao!!
 
wasisahau kumpa neti maana hili baba kwa kulala halijambo .huyo hajaenda kuokoa jahazi ila kaenda kulala kama kawaida yake?
 
HUENDA HABARI ZINA UKWELI ccm WANATUMIA SHORT CUT KUSHINDA. hII NI DALILI YA KUPOTEZA LEGITIMACY!
 
Mitandao ya kijamii nayo wainunue? -- sina uhakika kwa hilo ila kwa JF hata waje na 100billion tutasema ukweli daima fitna kwetu mwiko.
 
Hivyo vyombo vya habari vikae vizuri na visome alama za nyakati. Wamiliki wa vyombo vy habari Rwanda, wengine walisimamishwa hapo Arusha kwa mahakama ya kimataifa ICC, nawapa tahadhari tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom