Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Chuki, inawezekana ulisoma Igurubi zamani, enzi ya chama kimoja, hali ilikuwa hivyo kweli, lakini hebu niambie kata ya jirani yako ya Kinungu diwani wake ni wa chama gani? Kama sio Mh Adrian wa CHADEMA! Sema Kama sio kweli kuwa katika kata hiyo inataka uwe na moyo wa ujasiri kuvaa magwanda ya kijani. Kielelezo kizuri cha wilaya ni Kata ya makao makuu ya wilaya ambayo ni kata ya Igunga, hebu sema kweli, pamoja na nguvu zote za kifedha alizokuwa nazo Rostam, alieshinda udiwani kata hiyo ya Igunga ni nani? Kama sie Mh Vincent wa CHADEMA ambae ni seremala tu anaeshi Banda la uani baada ya kuchomewa nyumba yake? Sie kata ya Mwamashimba mgombea udiwani wa CDM alikubalika sana lakini akachakachuliwa kwa fedha za Rostam, wananchi tukakosa haki ya kuamua. Msijidanganye pale Igurubi kwa vijidhahabu vya Mwagala, Dr Kafumu pale keshachakachua viwanja vyote pale kwa wakuja, wana Igurubi wanasubiri kumpa Salam zake kwenye sanduku la kura! Kama hatapitishwa kiaina. Au ni yale maji ya chumvi ya tanki ndo yanakupagawisha? Wenzio hawayanywi wanaenda kuchimba yale ya visima vifupi kule chini kwenye mto uliokauka! Nenda kaangalie Igurubi hivi leo ukaone njaa ilivyopiga, dada zetu wanavyojiuza kwa bei poa kwa wachimbaji ili wapate hela ya kula, dah, pole sana chuki!

Mkuu,
na kata ya Kining'inila imechukuliwa na chama gani?

Thread ni kama alerting note kwa CDM against any cookies towards dem winning and securing da constituency. Infact Mwl yule anakubalika sana miongoni mwa kada mbalimbali. ila kwa alichokieleza cjui DED kuibua tuhuma dhidi ya Mwl ili hatimaye awekewe pingamizi its like porojo flani,, anyway its an alert against any mchezo mchafu

Mie nimesoma Igurubi Secondary.Mkuu wetu wa shule anaitwa Mwl.Masele
Sisi ndie tunayeijua igunga,
NAWAKUMBUSHA.
ukienda maeneo ya Igurubi,Itunduru,Mwamashimba,Mwanzugi,Mwisi,Igunga na Nanga nimetaja kidogo...
huko kote ni CCM tupu! hawajawahi kuchagua chama cha upinzani tangu wajumbe wa vijiji hadi vitongoji.Huko wao ni Chama TAWALA tu.
kwa mantiki hii, wanaodhani kuwa Chama Cha Map.. kina wakati mgumu kushinda huko wafanye utafiti wa kutosha tusijikute tunaapa bure tukamkosea Muumba!
na hayo ndiyo maeneo ambayo yanamwaga kura nyingi CCM.(siwapambi natoa uhalisia)
ili vyama vingine vishinde huko kazi ya ziada ya kunadi sera inakiwa ifanyike, la sivyo mtajikuta mnaishia kwenye ushabiki siku ziende.
KAZI IPO IGUNGA, NAFASI YA CCM BADO NI KUBWA! YOWE SIO KURA FINALI TAREHE 02.OCT.

Hapo kwenye nyekundu pana walakini,unataka kuniambia sehemu hizo ni kama 'egoli' kwa maendeleo kwa kuwa wamekuwa wakifaidi sera nzuri za CCM,ningekuelewa ungeniambia maeneo hayo yamejaa mazuzu CDM wafanye kazi ya ziada kuwazibua ili waanze kufikiri na kutafakari wapigapo kura...

Mie nimesoma Igurubi Secondary.Mkuu wetu wa shule anaitwa Mwl.Masele
Sisi ndie tunayeijua igunga,
NAWAKUMBUSHA.
ukienda maeneo ya Igurubi,Itunduru,Mwamashimba,Mwanzugi,Mwisi,Igunga na Nanga nimetaja kidogo...
huko kote ni CCM tupu! hawajawahi kuchagua chama cha upinzani tangu wajumbe wa vijiji hadi vitongoji.Huko wao ni Chama TAWALA tu.
kwa mantiki hii, wanaodhani kuwa Chama Cha Map.. kina wakati mgumu kushinda huko wafanye utafiti wa kutosha tusijikute tunaapa bure tukamkosea Muumba!
na hayo ndiyo maeneo ambayo yanamwaga kura nyingi CCM.(siwapambi natoa uhalisia)
ili vyama vingine vishinde huko kazi ya ziada ya kunadi sera inakiwa ifanyike, la sivyo mtajikuta mnaishia kwenye ushabiki siku ziende.
KAZI IPO IGUNGA, NAFASI YA CCM BADO NI KUBWA! YOWE SIO KURA FINALI TAREHE 02.OCT.

Hapo kwenye red! Shule ya Kata hiyo na kuwaza kwako ni ki-Kata Kata vile!! Pole sana. Kama Igunga watu hawajaamka tutawashangaa!

mmmhmh!!! ama kweli 'mbaazi zikikosa maua husingizia Jua' chadema mmeshashindwa kabla hata ya mbio kuanza! jimbo lile ni la ccm kwa hiyo litarudi nyumbani kwake! viti tulivyowaazima mnashindwa kuvitunza; bado mnataka vingine? hebu kitunzeni kiti cha shibuda KWANZA ndipo TUTAFIKIRIA kama tunaweza kuwaongeza vingine mwaka 2015; lakini c hiki cha Igunga!

Naanza kwa kuomba radhi kama nitafanya some technical mistakes katika posting yangu kwa vile ndio naanza kujiunga na forum hii, japo nimekuwa msomaji wake kwa muda. Nimejiunga na kuandika haya kwa uchungu ninaoupata na kisha sina pa kuyapeleka niliyoyapata hapa Igunga kisha nikabaki salama.

Mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya ubunge hapa Igunga Mwl Kashindye alikuwa mtumishi wa serikali akianzia ngazi ya chini kabisa ya Mwalimu wa UPE vijijini, alijiendeleza kielimu hadi kuhitimu chuo kikuu na kufikia kuwa Mkaguzi wa Elimu, vijiji vyote vya Igunga na watu wake na matatizo Yao anayajua vizuri sana, shida za waalimu anazijua vilivyo.

CCM ilikuwa imeshaandaa waalimu kuwa wasimamizi wa vituo, ili kuhakikisha kuwa CCM inashinda kwa Hali yoyote ile iwayo, lakini sasa kwa kuwa mgombea wa CDM ni Mwalimu mwenzao, wakati mgombea wa CCM, Dr Kafumu ni Commissioner wa madini katika wizara ya nishati na madini, wizara inayoongoza kwa utata hapa nchini, na yeye mwenyewe akiwa ndie mtaalam wa kutoa mikataba ya madini nchini, imeonekana uwezekano wa yeye Dr Kafumu kushinda kihalali itakuwa ni vigumu, inabidi "Mbinu Mbadala" zitumike.

Awali CCM ilitaka kuwabadilisha waalimu hao wa Igunga wasikae vituoni ili waletwe wengine kutoka Singida, lakini ikaonekana hawa wa hapa wanaweza kufanya hasira na wakampigia mwenzao kampeni ya kufa mtu.

Wakiachwa waendelee uchakachuaji vituoni utakuwa mgumu. Kamati ya siasa ya wilaya ya Igunga, ikishirikisha viongozi wa kimkoa na Taifa, akiwemo Mhazini Mkuu Taifa Ndg Mwigulu, iliketi na kuamua kwa kauli moja kumuita Mkurugenzi (DED) Ndg Magayane kuwa awasiliane na wahusika wa Wizara ya elimu ili profile nzima ya Mwl Kashindye ipatikane ili ichunguzwe itafutiwe kasoro, na kama hazipo basi lazima ziwe fabricated ili zitumike kumuengua.

Izingatiwe kuwa DED Magayane ana tuhuma nzito ya ufisadi katika ujenzi wa barabara fupi ya lami iendayo kwenye Halmashauri ya wilaya, ilikuwa afukuzwe kazi kabla ya uchaguzi huu, lakini amerejeshwa kazini kwa masharti kuwa lazima CCM ishinde, jimbo likipotea na yeye apotee.

Vipengele vya kumuengua vimeshapatikana inasubiriwa siku ifike DED Magayane afanye vitu vyake, ni siri kubwa, lakini kwa kuwa miongoni mwao kuna wanaochukia dhuluma, basi vimeshavujishwa na tutavipeleka kunako husika ili kuvidiffuse.

Aidha, Mkuu wa polisi wilaya ya Igunga ambaye alikataa kuzuia operation Sangara ya CHADEMA ilipoanza wilayani Igunga, licha ya kupelekewa barua kutoka CCM ya kumtaka afanye hivyo, keshatimuliwa na ameletwa OCD mpya spesheli kuikabili CHADEMA.

Hata aliekuwa Manager wa NMB Igunga keshahamishwa kisa eti ni Mchagga na anashabikia CHADEMA kwa hiyo imehofiwa kuwa atafanya kampeni kwa vile ana influence kubwa kwa wateja wake ambao ni wengi sana hapa Igunga.

Ni kweli kuwa Mwigulu anamwaga fedha kifashisti kwa kila taasisi na makundi ya jamii, waziwazi, lakini mitego ikitegwa na TAKUKURU wakiarifiwa waje wamshike live, TAKUKURU haohao wanamjulisha kwa simu kuwa wanakuja, anawaambia wasubiri kwanza amalize kugawa, akishamaliza na kuondoka, ndio anawapigia waende wakavamie hewa.

Ndugu zangu wanaJF, ni mengi mno yatakayoikwamisha CHADEMA hapa Igunga, hata sijui niwasilishe lipi na niache lipi, maskini CHADEMA, pamoja na kupendwa na wengi sijui itashinda vipi dhidi ya dhulma hizi, au labda tupige sana kelele za mwiziii kwa pamoja mpaka ardhi itikisike!

Naishi kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamashimba, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga. Niulizeni swali lolote kuhusiana na hali ilivyo nitajibu nitakayoweza bila ya woga.

Naomba Kuwasilisha!

Huu ni mwisho wa mwisho wa CCM.
Napita tu jamani.

Karibu jamvini. Wewe zilete tu hapa jamvini, habari ikifika hapa ujue haipiti bila kufanyiwa kazi, ili mradi iwe ni ya kweli.

Ccm can do anything illegal na kinyume na human right ili tu kutimaza matakwa yao.naamini kabisa kwa asilimia 120% kuwa wamebuni mbinu zote chafu.kama tu chaguzi ndogo za udiwani wanafanya udhalimu ije iwe ubunge?.mathalani uchaguzi wa diwani kata ya susuni wilayani tarime ambalo diwani wake aliuwa usiku akielekea mjini tarmi kwenye ppori la Nyandoto,ccm wakaspeculate kuwa aliyegombe udiwani kwa cdm ambaye ni baba yake na mbunge wa viti maalum Esther Matiko kuwa ndio kanunua watu wamuue kwa madai eti mbunge alimtumia tshs 80ml.

Speculation hizi awali ziligonga mwamba ambapo wanakijiji waligoma kwani wanamjua mzee Nicolas Matiko.Cha ajabu viongozi wa ccm wilaya akiwemo bwana Zakaria ambaye ni katibu mwenezi na mhazina pamoja alikuja hadi dodoma kumconvice mbunge Esther ambaye ni bintiye kuwa amshawishi baba yake asigombee,kwa taarifa nilizonazo mbunge alimwambia kuwa baba yake anautashi wake mwenyewe agombee au asigombee na hiyo ilikuwa ni tarehe 14.8.2011, na mauaji yalitokea 14.7.2011,,cha ajabu baada ya mzee Nicolas kuombwa na wanakijiji agombee na kuridhia kuchukua fomu usiku wa tarehe 15.8.2011 askari wasiopungua 25 wa kanda maalum tarime na rorya walivamia nyumbani kwa mzee huyo usiku wa saa saba na nusu na kumchukua ambapo kesho yake bila kuchelewa walimwandikia mada.

Cha kusikitisha habari iliyopo viongozi wa kata ya susuni, wilaya na mbunge Nyangwine nasikia wanafurahi wakisema sasa kata itarudi kwao kwani threater wao wamweka jela.na inasadikika watamshikilia mpaka ti baada ya uchaguzi kupita kwani mzee huyu na marehemu ndo atleast walikuwa wanaweza shindana.

Nilitaka tu kuonyesha ni jinsi gani mchezo wowote mchafu waweza chezwa na ccm kwa kutumia vyombo vya dola.kwani polisi hao hao walipinga vikali speculatipn za waccm kata.lkn baada maji kuwafika shingoni waajiri wao wamewaamuru kumbabika kesi mzee wa watu.

Na mbaya zaidi nasikia kuna mtuhumiwa mmoja kakamatwa tangu tarehe 17.7.2011 na alikiri kumuua marehemu na anaseme mzee matiko ahusiki lakini mijaa bado imemkomalia mzee wa watu.

CCM goooooooo to the grave........ Ur days r numbered. Wanachadema na wanamapinduzi wote tupinge unyanyasaji na upwokaji huu wa demokrasia.

Kama diwani wa bumera marwa tengera hadi leo walimbambika mada kesi october mwaka jana wakizani watamshinda bado wananchi walimchagua tu.

Nakushukuru kwa kuunga mkono, nami kwa moyo huo huo naungana na wewe kuwa CHADEMA iwe makini sana na hila za CCM. Wakati mwingine si CCM bali wakatumiwa CUF kama jimbo fulani ktk uchaguzi mdogo kama huu, CUF ilimwekea pingamizi mgombea wa CHADEMA na jimbo hilo likaenda CCM. Kama sikosei ni kati ya Mwanza, Shinyanga, Tabora nakumbuka tu kuwa aliyeshinda ni mbunge m/ke. Kwa hiyo tahadhari ni kitu kizuri zaidi, kama CHADEMA mpaka sasa bado hamjajifunza hila za wenzenu mtajaza wenyewe.

Mtoa mada ametoa taarifa za kiintelejensia hata kama si sikweli zitatusaidia kuwa makini zaidi. Tukumbuke kuwa kuku mwoga ana vifaranga vingi. Take CARE. Hatutaki tukose jimbo hili kwa uzembe hata kidogo kwa hiyo kila mtu atimize wajibu wake.

Ndugu Mwita kazi unayo hapo Igunga angalia Mwl mwenzako asije akashiindwa kwa uzembe. Simamia kiukamilifu zoezi hili mpaka kieleweke.

Nenda direct kwamba CUF imeizid CDM nguvu igunga na sio kutoa visingizio ving kujitetea.Mbona mgombea wa CDM alishawahiwekea pingamizi mgombea wa CUF kagera?

huyu DED mbona anatia huruma!! upande mmoja anaogopa kufukuzwa kazi, upande wa pili wananchi wameahidi wataiwinda familia yake kwa mishale kila mwanafamilia kokote watakakokuwa ikiwa atafanya hujuma, wamedai watalenga na kuyaunganisha masaburi kwa mshale, mbona itakuwa balaa, salaaaaaale kama utani vile!!!!! wengine wamefikia hatua ya kusema watamnyang'anya jina lao la kisukuma huyu mhazini wa ccm (Mwigulu madelu ncheemba) naendelea kutafiti watamnyang'anyaje hilo jina, kwani walimpaje,

This is purely defensive mechanism na uongo uliokomaa. By da way, nadhani mgombea wa CDM anaogopa kivuli cha historia ya matendo yake. Kwani enzi zake alikula sana hela za wasukuma na wanyantuzu wa Igunga waliokuwa wakiachisha shule mabinti zao kwa lengo la kuwaozesha. Sasa kwa hofu ya kujulikana kwa maovu yake, ndo maana wanaleta hoja za visingizio.

Mie nimesoma Igurubi Secondary.Mkuu wetu wa shule anaitwa Mwl.Masele
Sisi ndie tunayeijua igunga,
NAWAKUMBUSHA.
ukienda maeneo ya Igurubi,Itunduru,Mwamashimba,Mwanzugi,Mwisi,Igunga na Nanga nimetaja kidogo...
huko kote ni CCM tupu! hawajawahi kuchagua chama cha upinzani tangu wajumbe wa vijiji hadi vitongoji.Huko wao ni Chama TAWALA tu.
kwa mantiki hii, wanaodhani kuwa Chama Cha Map.. kina wakati mgumu kushinda huko wafanye utafiti wa kutosha tusijikute tunaapa bure tukamkosea Muumba!
na hayo ndiyo maeneo ambayo yanamwaga kura nyingi CCM.(siwapambi natoa uhalisia)
ili vyama vingine vishinde huko kazi ya ziada ya kunadi sera inakiwa ifanyike, la sivyo mtajikuta mnaishia kwenye ushabiki siku ziende.
KAZI IPO IGUNGA, NAFASI YA CCM BADO NI KUBWA! YOWE SIO KURA FINALI TAREHE 02.OCT.
Igurubi ni sekondari ya Kata?

This is purely defensive mechanism na uongo uliokomaa. By da way, nadhani mgombea wa CDM anaogopa kivuli cha historia ya matendo yake. Kwani enzi zake alikula sana hela za wasukuma na wanyantuzu wa Igunga waliokuwa wakiachisha shule mabinti zao kwa lengo la kuwaozesha. Sasa kwa hofu ya kujulikana kwa maovu yake, ndo maana wanaleta hoja za visingizio.

Hii inawahusu wana chadema! Halafu wanyantuzu wamehamia Igunga tangu lini?

This is purely defensive mechanism na uongo uliokomaa. By da way, nadhani mgombea wa CDM anaogopa kivuli cha historia ya matendo yake. Kwani enzi zake alikula sana hela za wasukuma na wanyantuzu wa Igunga waliokuwa wakiachisha shule mabinti zao kwa lengo la kuwaozesha. Sasa kwa hofu ya kujulikana kwa maovu yake, ndo maana wanaleta hoja za visingizio.
ChiefmTz, kinachofanya useme hoja ni vya visingizio nini? Kwanini usione kuwa defensive mechanism ni ile ya kumuondoa OCD wa Igunga kwenda kummpumzisha Tabora kabla muda wake wa kustaafu?

Tena kafanyiwa hivyo baada ya kupuuza barua iliyotoka CCM ikimtaka adhibiti operation Sangara ya CHADEMA iliyoanza kwa kishindo kikubwa tar 24/7/2011 kwenye kiwanja kilicho mbele ya ofisi ya CCM wilaya? Kwanini usione kuwa ni defensive mechanism kumuhamisha manager wa NMB Igunga Branch kisa eti nichagga kwa hiyo atakampenia CDM, habari hizi sio siri bali ni public knowledge hapa Ig. Kwanini usione kuwa ni defense mechanism kitendo cha DED Magayane kuwa na mahusiano binafsi yasiyo matakatifu na Bi Neema ambae ndie Katibu wa Wilaya wa CCM Igunga? (wala sio siri kamwe, everybody here knows) Kamati ya bunge ya Mrema ilipofanya ukaguzi hapa ilimpata Magayane na hatia ya ufisadi katika ujenzi wa kipande cha lami cha kuelekea Halmashauri, iliamuriwa asimamishwe kazi, kila mtu hapa Igunga anajua hivyo, ghafla wiki iliyopita karejeshwa kwa masharti hayo, hiyo sio defence mechanism ya ruling system?

Ukitaka kujua habari hizi zinavyovuja ni kuwa ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa, a huge conflict of interest, kuna upande unataka kuhakikisha CCM inashindwa Igunga, na sie kina Julian Asange wadogo tunasubiri kuzidaka kama paka anavyosubiri kwenye tundu la kutokea panya.

Hebu imagine CCM ikipoteza jimbo la Igunga, kisha Chenge nae atangaze kujiuzulu ubunge na Lowasa akitabasamu akisubiri zamu! Thubutu! Wataenda kumramba miguu asijiuzulu kuepusha aibu nyingine, lakini CCM ikishinda Igunga, CCM itapata kiburi cha ajabu, magamba yaliobaki yatang'olewa kwa nguvu.

Anyway, taarifa ya vigezo vitakavyotumika kumuengua Mwl Kashindye tumezipeleka kwa makamanda wa CDM, kama tusiporidhika na hatua watakazochukua, basi kuanzia kesho nawaahidi wanajf kuwa nitafungua thread special itakayovitaja waziwazi vipengele vitakavyotumika kumuengua mgombea huyo, tuone kwa uzito wake kama kuna mtu atabisha, wenye kupenda haki wote nina hakika watapanic, bila kujali itikadi za vyama vyao!

Natusubiri hiyo kesho mtaona jinsi "WikiLeaks" ya Igunga inavyofanya kazi, potelea mbali na wakaninyonge, nimeshachoka, najua wanajf wengi watahudhuria mazishi yangu! MGUNGA WA IGUNGA HAUKOSI MIBA!

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom