'Ubunge' wa Heche Tarime waingia doa

kwa heche sawa lakini kwa zitto ni dhambi kubwa

Mkuu, mbona sioni tatizo la zitto kutangaza nia? Au kutangaza nia ni kutangaza mgogoro! Ninachofahamu ni kwamba wengi watatangaza nia, ila mchakato na taratibu za chama utafuatwa na kama akipitishwa, atapeperusha bendera ya chama! Thats all. Kwangu mimi sioni tatizo!
 
Kilaza kamuuuilize Mbowe kwanini alikemea kutangaza nia za kugombea urais na ubunge siku walipokuwa wanafanya usanii wa kusafisha fedha yao chafu..?

Mkuu, Mbowe mwenyewe alitangaza kugombea ubunge wa Hai miaka miwili kabla ya uchaguzi. Alichokisema ni kwamba haongozi genge la watu wenye tamaa ya madaraka. Na sidhani kama kutangaza nia ni tamaa. Nasikitika kwa kuniita kilaza. Sijui tatizo Mkuu!
 
Mkuu, Mbowe mwenyewe alitangaza kugombea ubunge wa Hai miaka miwili kabla ya uchaguzi. Alichokisema ni kwamba haongozi genge la watu wenye tamaa ya madaraka. Na sidhani kama kutangaza nia ni tamaa. Nasikitika kwa kuniita kilaza. Sijui tatizo Mkuu!

Nisamehe mkuu kwa kukuita kilaza japo sikubaliani na wewe. Kunradhi.
 
Vipi kuhusu kamanda mwita mwikabe ambaye aligombea mwaka 2010,nadhani angeachiwa arudie tena

Nae anaruhusiwa kugombea tena ndani ya chama, akipitishwa atakiwakilisha tena chama chake. Kutangaza nia kwa Heche hakumzuii kugombea tena!
 
Ijumaa, Agosti 17, 2012 07:21 Na Mwandishi Wetu, Tarime

SIKU chache tu baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa (BAVICHA), John Heche kutangaza nia ya kugombea ubunge jimboni Tarime katika uchaguzi mkuu 2015, nia hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi wa jimbo hilo.

Baadhi wameunga mkono hatua hiyo, huku wengine wakipinga, wakidai huu si muda muafaka kwa kiongozi huyo kutangaza nia hiyo, kwa sababu anaweza kukigawa chama.

Baadhi ya wananchi hao, ambao wamejitambulisha kuwa ni wanachama wa Chadema, waliliambia MTANZANIA kuwa, Heche ndiyo chimbuko la makundi ambayo yalisababisha Chadema kupoteza jimbo hilo mwaka 2010.

Walidai kuwa, badala yake kiongozi huyo wa BAVICHA, angetumia nafasi aliyo nayo ya kitaifa kuwatumikia wakazi wa jimbo hilo katika kutatu kero mbalimbali, badala ya kufikiria ubunge kwanza.

“Bado miaka mitatu kufikia uchaguzi mkuu 2015, haikupaswa kwa mwanachama yeyote kuvuka na kuanza kufikiria kushinda uchaguzi akiwa peke yake bila msaada na kuungwa mkono na zaidi ya theluthi mbili ya wananchama wote jimboni.

“Sasa leo tunaweza kuhamisha mawazo yetu katika kupambana na umasikini tukaanza kufikiria ubunge,” alisema Samwel Chacha.

Naye mkazi mmoja wa mji mdogo wa Sirari, Julius Makima, alisema Heche ndiye pekee anayeweza kutetea maslahi ya jimbo hilo na wilaya nzima, kwa kuwa alishathibitisha hilo wakati akiwa diwani wa Kata ya Tarime Mjini kupitia Chadema, katika uchaguzi uliopita.

Alisema kwa muda mrefu, mwenyekiti huyo wa BAVICHA ameonyesha ukomavu wa kisiasa ambapo mara kadhaa ameonyesha uwezo wa kuunganisha koo zote za kabila la Wakurya na kusaidia kuepusha mapigano ya mara kwa mara ya koo hizo.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sokoni katika mji mdogo wa Sirari, mapema wiki hii, Heche aliweka bayana msimamo wake huo wa kugombea ubunge Jimbo la Tarime katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, endapo chama chake kitampitisha.


Hiii ni Nov unaleta story ya Agosti 17

Mbona kichwa cha habari kimeegemea sehemu moja kuna mwinge alisema heche ndo uwezo wa kutetea wana Tarime ya isisomeke kuwa Heche ndo mwenye uwezo wa kuwatetea wana Tarime?
 
Outdated info! Bila shaka hii habar imeletwa humu na juliana shonza, mtela na genge lake.
Aghaaaa.......
 
Back
Top Bottom