Uber Dar es salaam

Ipo na inafanya kazi.
Kuna siku nilipanda hapo mjini, ile kushuka dereva akajisahau akaanza kunidai nauli.
Ndo nikaanza kumuelekeza jinsi atakavyolipwa, akaelewa nikamuacha nikasepa.

Safi sana mkuu.
 
Base fare: 100 KSh
Cost per min:: 4 KSh
Cost per km: 60.27 KSh
Service fee: 0 KSh
Cancellation fee: 200 KSh
 
Kwani lazima utoe povu sasa, au yeye kuchangia kimekuwasha nini?
Juma nature aliimba "ustaarabu, jambo bora tena la heshima, nashangaa sijui kwanini watu wengi hawajui maana ya ustaarabu, najiulza toka walivyozaliwa, walikuwa hawana ustaarabu."

Ndio hayo.. Kataja kwa kenya, wewe inaweza kukusaidia japo kukisia bei itakuwaje kwa tz, mbovu lina mtoka, ili mradi apate mabishano ya utaifa tu.
 
Hivi huku kwetu nje kidogo ya jiji, hii huduma inaweza kutufikia.
Mfano ; Niko mabwepande ucku nahitaji hii huduma naweza ipata?
 
Masalkheri mabibi na mabwana,

Mwezi ulopita kampuni ya Uber ilizindua huduma zake Dar Es Salaam.

Tokea wafanye uzinduzi huo sijasikia chochote kingine zaidi kuhusu huduma hiyo [na kusema ukweli sijafuatilia kwa ukaribu].

Sasa basi, ningependa kujua maoni ya watu yakoje kuhusiana na hiyo huduma. Ningependa kujua mazuri yake, mapungufu yake, changamoto zilizopo, jinsi mapokezi yake kwa ujumla yalivyo, na kadhalika.

Kama kuna watu ambao tayari wameshaitumia hiyo huduma basi ningependa ushirikiano wao katika kuchangia maoni yao. Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wenu mtiifu,

Alhaji Nyani Ngabu bin Kibadiru.
Kwani application yao inafananaje maana sijaiona google store.....zimekuja nyingi na hata haieleweki ni ipi!
 
Kwani application yao inafananaje maana sijaiona google store.....zimekuja nyingi na hata haieleweki ni ipi!

Rider app iko hivi....

aid1304771-728px-Use-Uber-Step-9-Version-3.jpg.webp
 
Ipo na inafanya kazi.
Kuna siku nilipanda hapo mjini, ile kushuka dereva akajisahau akaanza kunidai nauli.
Ndo nikaanza kumuelekeza jinsi atakavyolipwa, akaelewa nikamuacha nikasepa.
ungemuachia tip... vijana washazoea makaratasi sasa hizo e-money na wao lazima washangae kidogo
 
Lete bei kwa kibongo unatuletea kwa kikenya hizo price ili iweje mkuu
Msaada hapo
 
Back
Top Bottom