Ubaguzi na hali duni ya maisha kwa jamii ya watu weusi

Mike_

Senior Member
Jan 9, 2021
190
243
Habarini wakuu.

Leo nilikuwa naangalia makala ya Africa News Channel YouTube ilikuwa inaelezea ubaguzi na hali duni ya maisha wanayokumbana nayo ya jamii ya Wairaq weusi. Nikagundua kuwa katika nchi nyingi watu wenye asili ya Africa huwa ndio wanaokuwa masikini kuliko makundi mengine.

Nikafikiria documentary nyingine ya jamii ya Wasidi ya India, nikagundua hali yao ni duni vilevile na wanatengwa na Wahindi wengine.

Marekani ambayo ni diverse society, race maskini kuliko zote ni race ya watu weusi.

Zamani nilidhani watu maskini weusi wapo Africa tu, ila baada ya kuexperience maisha ya watu wa Haiti, nikabadili mtazamo.

Swali nisaidieni majibu: Kwa nini kila sehemu duniani watu weusi ndio huwa maskini kuliko race zingine na huwa wanabaguliwa kuliko makundi mengine?

Na sababu haswa ya hali hii ni nini?
 
mtu mweusi akiachwa huru afanye mambo yake bila vigingi ataitawala dunia.
 
11 January 2024

Papua New Guinea

POLISI WAGOMA, VIBAKA WAINGIA MITAANI KUPORA MALI


View: https://m.youtube.com/watch?v=OQUEKR5XubY

Mhanga wa uporaji atoa ushuhuda jinsi makundi ya watu walivyoiingia mitaani kupora ... baada ya Polisi kuwa katika mgomo ...

1704986876162.png

Ripoti kamili na Christopher Cottrell
Akiripoti kutoka mji mkuu Port Moresby, nchini Papua New Guinea

Januari 11, 2024
7:27 a.m. ET
Waziri mkuu wa Papua New Guinea siku ya Alhamisi alitangaza hali ya hatari ya wiki mbili katika mji mkuu, Port Moresby, na kumsimamisha kazi mkuu wa polisi wa taifa hilo la kisiwa cha Pasifiki baada ya maandamano ya ghasia kuuacha mji huo ukiwa na makombora.

Machafuko hayo yalianza siku ya Jumatano baada ya polisi, maafisa wa ulinzi na watumishi wengine wa umma kuonekana kuacha kazi zao kupinga kile walichokisema kuwa ni kukatwa mishahara bila kutarajiwa.

Serikali ililaumu hitilafu hiyo kwa iliyotokea ktk mfumo wa kompyuta kusababisha makato pia tozo na hivyo kuahidi kurekebisha tatizo hilo, lakini hali uporaji mjini Port Moresby ilianza haraka... na kuistua serikali

Source : The New York Times
 
11 January 2024
Papua New Guinea

MACHAFUKO, UVUNJIFU WA USALAMA YATOKANA NA UMASIKINI

Wachambuzi wanalaumu sera mbovu za serikali, ughali wa maisha, ukosefu wa ajira na tofauti ya walionacho kulinanisha na wasio nacho kuwa kimepelekea watu masikini hata wale wenye ajira za mshahara duni kuingia mtaani kufanya uporaji

1704987990114.png

Jamaa akijitwisha mali iliyoporwa
 
Nimeikuta hii tunabaguliwa hata kwenye madhehebu yetu
 

Attachments

  • Kila_Siku_Hatujifunzi_Sisi_🙌🏿_Bado_TunajifanyaKimbelembele_😄_Baizawei_Bora_Tujich..._See_more.mp4
    538 KB
Back
Top Bottom