Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,309
- 19,179
Wana JF, nilishangaa sana siku nilipoenda nchi fulani jirani nilipotaka kubadilisha fedha, nilibadilishiwa kwa kiwango kile kile bila kujali nilikuwa nabadili noti za $1, $5, $10, $20, $50 au $100. NIkakumbuka hapa kwetu Tanzania ukienda Bureau de Change unapewa kiwango tofauti kulingana kwa noti za $1, $5, $10, $20. Angalia hapo chini, noti a $1, $5, $10 na $20 unabadilishiwa kwa Tshs 1700, lakini noti za $50 na $100 unabadilishiwa kwa Tshs 2370! Jambo la ajabu ni kwamba wao wanapokuuzia dola wanauza kwa bei ile ile bila kutofautisha wanakupa noti ipi. Hapo chini utaona noti zote za $1, $5, $10, $20, $50 au $100 zinauzwa kwa Tshs 2400. Huu ni wizi!
Sasa ninachojiuliza ni kama hii ni kanuni iliyotolewa na BOT kwamba fedha za Marekani hapa nchi zinakuwa na thamani tofauti kulingana na noti. Na, hawa watu wa Bureau de Change wanapofanya transacton na BOT, nao huwa wanapewa thamani tofauti ya kubadilisha kwa noti tofauti za USA?
Kumbuka kwamba, kama noti za Marekani zinapaswa kuwa na thamani ile ile bila kujali ni noti ya kiasi gani, basi Watanzania tumekuwa tukiibiwa na hawa wabadilisha fedha kwa muda mrefu sana, na wizi huu kubarikiwa na BOT. NI mabilioni tumeibiwa. Na kwa nini tofauti hii iwe kwa Tanzania tu? Kama Bureau de Change wamefanya hili kwa kukiuka sheria, nashauri BOT wawapige faini kulingana na walianza lini biashara, na fedha za faini ziende kununua madawati au kujenga madarasa.