Ubabaishaji wa kampuni ya usafirishaji abiria mabasi ya Dar Lux toka Mwanza-Dar

Habari wakuu,
Kwanza nawatakieni heri ya sikukuu ya Pasaka. Nia na dhumuni la kuandika Uzi huu ni kutokana na kero za kiusafiri hasa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine zaidi ile ya masafa marefu kama Dar to KG, Mwanza to Dar n.k

Dar Lux wamekuwa mbwa sana kwenye utoaji wa huduma zao. Yaani Alhamis tuliondoka mwanza saa nne kuelekea Dar mwisho wa siku kutokana na kuchelewa kuondoka wanaanza kupapatika njiani kwa mwendo wa juu zaidi na hata hivyo tukalala Gairo. Tukafika Dar es salaam saa saba mchana siku ya ijumaa.

Hapohapo jamaa wakasema eti wakifika wanapakia abiria wengine kurudi nao mwanza. Ina maana watu walotakiwa kusafiri saa 12 asubuhi wakatumiwa SMS usiku kama sisi kwamba kuna dharura hivyo wataomba waondoke muda mwingine japo naamini waliwadanganya hawakuwaambia wataondoka saa nane au Tisa mchana,kama sisi walivotuambia tutaondoka saa mbili na nusu badala yake tukaondoka saa nne. NILIKUWA NAWAAMINI SANA HAO JAMAA SASA HIVI NI WABABAISHAJI BALAA JAPO GARI ZAO UKIPANDA KWA KIASI FLANI UNAKUWA COMFORTABLE.

Kingine ninachotaka kujua ni kwa namna gani naweza pata msaada wa kisheria ninapopatwa na na kwa yeyote atayepatwa na kadhia kama hii!? Inaudhi mnoooo!!! Halafu kwenye nauli wanaringa balaa bila 50 elfu hujapanda gari zao na wanajisikia sana hafu mwisho wa siku wanaleta mauzauza hayo
Kampuni pekee ambayo ina asilimia kubwa kdg ya uaminifu kwa sasa ni SHABIBY BUS SERVICE tu ombeni Mungu waanzishe ruti ya mwanza hamtapata kero hizo asee
 
Dar lux kwa kweli wanahudumaa mbayaaa saana na hawajali mteja kabsa na ninatabiria vibya hii kampuni haitakuwepo baada ya miaka miwili. Ilkuwa niwafungulie kesi mwaka jana sema sikuwepo hapa nchini kitendo walichonifanyia ni kitendo cha kihuni sana. Naungana na mleta mada Dar lux isiwe kipaunbele. Tafuteni magari mengne ya kawaida.
 
Pole, mmiliki wake kuna tetesi ni tapeli/jambazi/mwizi kama wale jamaa wa easy finance, kadhulumu watu wengi sana kwa kukukopesha mil unaweka bondi ya house then anapotea, then siku ya siku anaibuka umechelewesha mkopo, au unakuta nyumba yako keshaichukulia mkopo na hizo hela ndiyo utakatishaji, kakaa sana ndani kipindi hiki cha haki kwa haki, wakati mwingine basi zinakosa mafuta hivyo pole sana, mi nilishaacha kuzipanda
Hiyo tabia alikua anayo mama wa mshikaji wangu yeye alikua anakopesha watu
Sasa ikikopa labda elfu 50 mkakubaliana ulipe 60 kwa muda wa wiki mbili na ukipitisha inaongeza 10 kila wiki sasa anachokifanya ikifika siku ya kutoa hela kama hujapeleka anakuacha then hata mkikutana akukumbushi wala nini na hata ukimwambia mambo mabaya anasema usiwe na shaka.

Balaa linakuja akishaona hesabu zake zimetimia anaenda polisi anawapanga then anakujia unajikuta unalipa hata laki 2,,,tabia hii iliendelea kwa muda mpaka ilipokomaa alipomzingua mke wa mjeda
 
Jamaa nasikia yuko chimbo anawaza atoke vipi..last time alisafirisha baadhi ya madereva mpaka China kiwandani kuona mabasi yanavyotengenezwa na kupata mafunzo kidogo..soon anadondosha vyuma vya maana..
 
Huyu Ally's star wa sasa si yule wa zamani. Wa sasa ni mdogo wake na yule aliyemiliki Ally Sports Bus.
Allys Sport Bus jamaa umenikumbusha mbali, nimeyatumia sana yale Mabasi Mwanza saa 1 jioni mkitoka Dar 12 asubh, kama mnaenda Dar na zile foleni za Kibamba-Kimara saa 1:45 jioni mpo Ubungo, Kosa lake baadaye alinunua mabasi ya nisan diesel yakawa yanapiga route za Shy, Tbr, Dom kutokea Mwanza nadhani yale yalimpiga hasara.
 
Pale unapopaona ni dukani au transit center ya magari wanayoagiza.

Huyo jamaa/mmiliki anaonekana ni magumashi flani hivi kwa ukwepaji kodi, (kwa nini nasema hivo?) bado kuna tafiti inafanyika kupitia urafiki wake na kampuni ya Higer, maana anaagiza mabasi na yanakuja kwa rangi na jina la dar lux yakifika hapa Bongoland anayapiga bei.

Ndiyo maana unaona kuna mabasi mengine pale yana namba ila hayaingii barabarani.

it's technical to avoiding some revenue.
Magari yakifika si TRA inasajiri sasa akiyauza kuna kosa? Avha roho ya kimaskini unataka jamaa afilisike we itakusaidia nn? Kwa taarifa yako hata kukwepa kodi ni sifa Trump ni Rais wa linchi likubwa, alikwepa kodi na anajisifia kuwa yeye ni smart kuliko serikali.
Tuache roho za kutaka wenye pesa wazalilike jamaa amewekeza kutoa huduma.
 
Dar lux kwa kweli wanahudumaa mbayaaa saana na hawajali mteja kabsa na ninatabiria vibya hii kampuni haitakuwepo baada ya miaka miwili. Ilkuwa niwafungulie kesi mwaka jana sema sikuwepo hapa nchini kitendo walichonifanyia ni kitendo cha kihuni sana. Naungana na mleta mada Dar lux isiwe kipaunbele. Tafuteni magari mengne ya kawaida.
Ni wivu tu
 
Back
Top Bottom