SoC04 Uanzishwaji wa Mashamba ya kimkakati ya Umma kutatua changamoto ya Udumavu nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
63
43
Hali ya udumavu nnchini
Changamoto ya udumavu nchini imekua ni suala mtambuka kwa muda sasa. Kwa kiasi kikubwa waathiriwa wakiwa ni watoto, kitakwimu udumavu wa lishe umepungua toka 31% ya 2018 hadi 30% kwa 2022,( Ripoti ya Viashiria vya Afya ya Uzazi na mtoto na malaria,2022).

Katika ripoti hii mikoa kumi yenye udumavu mkubwa imeanishwa kama ifuatavyo; Iringa 56.9%, Njombe 50.4%, Rukwa 49.8%, Geita 38.6%, Ruvuma 35.6%, Kagera 34.3%, Simiyu 33.2%, Tabora 33.1%, Katavi 32.2%, Manyara 32%, Songwe 31.9% na Mbeya 31.5%.
Picha: Watoto wenye utapiamlo
IMG_20240524_123047.jpg

Chanzo: MwanaHalisi

Hivyo kufuatia hali hii serikali na wadau wa maendeleo hawana budi kuja na mpango wa uanzishaji wa programu ya lishe chini ya mashamba ya umma, mashamba haya yataendeshwa kwa kuzingatia yafuatayo.

Tathimini ya hali ilivyo ki-halmashauri, wilaya na mkoa. Utambuzi ufanyike kutambua hali ilivyo mijini na vijijini, mashuleni, kwenye vitua vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu na watoto toka kaya maskini.
Tathmini kutambua maeneo rafiki uanzishwaji wa mashamba.

Jopo la wataalamu wa ardhi, kilimo na mifugo, mipango, wachumi na wataalamu wa mazingira. Hawa watatambua maeneo, kupima udongo, kutathimini athari za kimazingira na mengineyo yahusuyo mradi.

Fedha za kuendeshea mashamba.
Halmashauri husika zitatumia vyanzo vya mapato mbalimbali ikiwemo; mfuko wa maendeleo wa halmashauri, wadau wa maendeleo na serikali kuu.

Uendeshwaji wa mashamba
Mfumo mmoja wapo kati ya ifuatayo utatumika kuendesha mashamba.
• Halmashauri kuzalisha moja kwa moja.
• Halmashauri kutegemeana
Hapa halmashauri A na B zitajikita kuzalisha mazao ya kilimo na halmashauri C itazalisha mazao ya mifugo. Wachumi na wataalamu wa mipango watengeneze mfumo maalumu wa mabadirishano ya bidhaa baina ya halmashauri katika wilaya ama mikoa kutegemeana na umbali na gharama zinginezo.

Wahudumu wa mashamba

• Vijana katika halmashauri wachukuliwe na kupewa mafunzo na hatimaye ajira katika miradi. Hawa wataatamiwa na maafisa kilimo/mifugo katika halmashauri husika.

• Wafungwa wa vifungo vya nnje na wanaoelekea kumaliza vifungo kufanya kazi kwa muda maalumu chini ya uangalizi wa Jeshi la Magereza.

• Wanafunzi
Hawa watafanya kazi mashambani kama sehemu ya mafunzo ya stadi za maisha katika vipindi vyao vya likizo. Hapa yaangaliwe madara yasiyo ya mtihani mfano darasa la 3 na 5.

Miundombinu shambani

• Ujenzi wa ghala za kuhifadhia nafaka na mazao ya mifugo(mayai/maziwa)kusimamiwa na halmashauri.

• Vyombo vya usafiri( malori)

•Viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kusindika malighafi toka shamba vikisimamiwa na maafisa lishe.
•Majiko ya kisasa mashuleni na kwenye vituo vya kulelea watoto.

• Kuanzisha mfumo mzuri wa mawasiliano baina ya; ofisi ya kilimo/mifugo halmashauri, wadau wa maendeleo na wasimamizi wa mashamba na maghala chini ya uangalizi wa ofisi ya mkurugenzi halmashauri.

Usambazaji wa vyakula na tathimini ya maendeleo ya mashamba.

• Programu ya mtoto na Lishe katika kliniki za watoto.
Programu hizi zitawalenga watoto walio na udumavu, chakula lishe na elimu vitakua vikitolewa katika kliniki hizi kwa wazazi na walezi kwa kufuata mipango na taratibu za maafisa lishe.

•Programu ya mtoto na Lishe katika kaya maskini.
Utambuzi wa kaya maskini, usajili watoto na elimu ya lishe.
Uratibu wa ugawaji wa chakula na ufatiliaji wa maendeleo ya zoezi haya yote yatafanywa chini ya uratibu wa halmashauri, viongozi wa serikali za mitaa na maafisa lishe.

• Mashuleni na kwenye vituo vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu.
Magari ya halmashauri na wadau wengine wa maendeleo yatatumika kusambaza vyakula katika maeneo hayo kulingana na mahitaji.

Picha: Mtoto mwenye afya akipatiwa chakula na mama yake.
IMG_20240524_123132.jpg

Chanzo: www.ennonline.net

Usimamizi wa mazao ya ziada
Kwa mazao ya ziada, viwanda vidogo vidogo pembezoni mwa mashamba vitatumika kusindika na kufungasha mazao na kuuzwa kwa bei rafiki katika maeneo yatakayoamuliwa mfano masoko, vituo vya kliniki ama katika maduka ya hospitali za umma. Fedha zitakazopatikana zitatumika kuendeshea shughuli ndogo ndogo za kila siku shambani.

Usimamizi na tathimini ya maendeleo ya mashamba.

• Usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara, hivi vitafanywa na kitengo cha ukaguzi cha ndani ya halmashauri. Wataangalia hali ya udumavu, maendeleo ya mashamba na mengineyo.

• Kwa upande wa tathimini ya mradi yafuatayo yafatafanyika.

- Ukusanyaji wa taarifa ya mahitaji yaliyopo na mafanikio yaliyopatikana katika programu kulinganiaha na malengo pangwa ya mradi.

- Uandaaji wa ripoti za mara kwa mara toka shuleni, kliniki, katika kaya maskini na katika vituo vya watoto. Mtiririko wa taarifa ufanywe kila mwezi kwenda kwenye mfuko wa chakula wa halmashauri.
Faida za uanzishwaji wa mashamba ya kimkakati katika halmashauri.
Kumaliza changamoto ya udumavu wa lishe nnchini kwa watoto.
•Kuongeza ufanisi wa watoto mashuleni, chakula bora na afya ni vitu vinavyoenda sambamba. Uwepo wa chakula mashuleni utapandiaha morali ya watototo kupenda shule na kufaulu vizuri.
•Kulinda afya ya watoto.
•Kupunguza gharama za matibabu kwa familia na kwa serikali.
•Ajira kwa vijana watakao pata nafasi latika mashamba ya halmashauri.
•Elimu ya stadi ya kilimo kwa wanafunzi wa shule watakaokua wakifanya kazi kwa muda maalumu katika mashamba.
•Chanzo cha mapato ya ndani kwa halmashauri husika.
Hitimisho
Maendeleo sehemu yoyote yanaanza na Afya. Watanzania wana msemo maarufu wa "Mtu ni Afya" na "Mwili haujengwi kwa tofari", utimamu wa afya ndio mwanzo wa maendeleo ya jamii. Shime kwa serikali na wadau wengine kuona fahari kwa kuanza kujali afya za watoto na jamii. Mashamba ya umma yatakayo kua yakitoa vyakula hayana budi kuanzishwa katika halmashauri zetu.​
 
Nzuri sana hii, ama kweli Tanzania tuitakayo inakuja kwa kishindo👊. Mawazo kama haya unaweza jenga picha nchi imeamka kwa kiwango gani. Nzuri.
Jopo la wataalamu wa ardhi, kilimo na mifugo, mipango, wachumi na wataalamu wa mazingira. Hawa watatambua maeneo, kupima udongo, kutathimini athari za kimazingira na mengineyo yahusuyo mradi.
Kila eneo lizalishe kulingana na uimara wake (strength) na kisha;

Halmashauri kutegemeana

Hapa halmashauri A na B zitajikita kuzalisha mazao ya kilimo na halmashauri C itazalisha mazao ya mifugo. Wachumi na wataalamu wa mipango watengeneze mfumo maalumu wa mabadirishano ya bidhaa baina ya halmashauri katika wilaya ama mikoa kutegemeana na umbali na gharama zinginezo.
Litapokea bidhaa lisiyozalisha kulingana na uhitaji wake. Ni swala tu la tafiti na takwimu. Nchi itaenda kisasa sana asee.
Ukusanyaji wa taarifa ya mahitaji yaliyopo na mafanikio yaliyopatikana katika programu kulinganiaha na malengo pangwa ya mradi.

- Uandaaji wa ripoti za mara kwa mara toka shuleni, kliniki, katika kaya maskini na katika vituo vya watoto. Mtiririko wa taarifa ufanywe kila mwezi kwenda kwenye mfuko wa chakula wa halmashauri.
'Data driven aproach' yaani kama mpenzi wa utafiti nikishuhudia mtu anasisitiza matumizi ya data na takwimu...... naona kabisa tunaelekea mahala
 
Nzuri sana hii, ama kweli Tanzania tuitakayo inakuja kwa kishindo👊. Mawazo kama haya unaweza jenga picha nchi imeamka kwa kiwango gani. Nzuri.

Kila eneo lizalishe kulingana na uimara wake (strength) na kisha;


Litapokea bidhaa lisiyozalisha kulingana na uhitaji wake. Ni swala tu la tafiti na takwimu. Nchi itaenda kisasa sana asee.

'Data driven aproach' yaani kama mpenzi wa utafiti nikishuhudia mtu anasisitiza matumizi ya data na takwimu...... naona kabisa tunaelekea mahala
Shukrani, matumizi ya data ni msingi wa uandaaji wa mpango wa maendeleo.
 
Back
Top Bottom