Uagizaji wa magari kupitia tradecareview toka Japan

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,530
13,469
Wna JF
Kuna gari zuri nimeliona kwenye web ya tradecarview, nataka kuagiza.
Je kuna mtu keshaagiza gari kupitia hao jamaa? nina experience na Trade Haus Logistics (THL) tu.
Je ni waaminifu? wako reliable kwa maana ubora wanaousema ni kweli?
Naomba msaada kabla sijaingizwa mkenge, si unajua pesa zetu ni za kuunga unga na gundi!

Nashukuru
 
Kaunga

Tradecareview hawauzi magari wenyewe,wao wanaonyesha magari ya makampuni mbalimbali. hata biashara unapofanya unafanya na kmpuni husika iliyoweka tangazo la gari.

Mimi nimwahi kutafuta gari kupitia Tradecarview na nikaagiza kutoka kwenye kampuni yenye gari husika. Leta jina la kampuni inayouza hilo gari wanajamii watakusaidia kufanya uchunguzi. Tradecarview hawana tatizo lolote, japo unaweza ukaona gari kwenye mtandao wao na ukaingizwa mjini kwani kuna makampuni fake au halali lakini watu wake si waaminifu
 
Tradecareview sio Kampuni ya kuuza magari bali ni mtandao unatumiwa na makampuni kutangaza magari yanayouzwa. Mimi na Jamaa zangu wa karibu wawili tumeagiza na tumetumepata magari yetu. Hakikisha kuwa hautumi pesa kwenye Kampuni moja kwa moja, tumia PAY TRADE, gari utalipata. Kama utatuma pesa moja kwa moja kuna uwezekano wa kuingia kwenye mikono ya matapeli.
 
Yah umakini unatakiwa katika ilo waweza ingizwa mjini bure!
Ivi jamani mambo ya mionzi ya nuclear na haya magari ya toka japani inakuwaje?
 
Wana system ya Pay trade, kwamba unalipa kupitia wao! Wanakata 3% ya CIF +50$, hivyo hiyo kampuni ikiingia mitini wao (tradecarview) wanakurefund! Ndo nilitaka kujua kama kuna mtu ametrade kwa njia hiyo

Gari ninayoitaka inauzwa na Wild Goose japan!

nashukuru kwa msaada wako
 
Tradecareview sio Kampuni ya kuuza magari bali ni mtandao unatumiwa na makampuni kutangaza magari yanayouzwa. Mimi na Jamaa zangu wa karibu wawili tumeagiza na tumetumepata magari yetu. Hakikisha kuwa hautumi pesa kwenye Kampuni moja kwa moja, tumia PAY TRADE, gari utalipata. Kama utatuma pesa moja kwa moja kuna uwezekano wa kuingia kwenye mikono ya matapeli.

Nashukuru sana, mkuu! I wanted to hear ushuhuda kama huo, especially hiyo part ua Pay trade!
 
Binafsi nimeagiza gari thru tradecarview last september na gari ninayo na naitumia hata sasa, kila kitu kilienda vema. Na ninawasiliana nao kwa email almost kila week, ni waaminifu.
 
Nashukuru sana, mkuu! I wanted to hear ushuhuda kama huo, especially hiyo part ua Pay trade!

Asante kushukuru Mkuu, ukitumia Pay trade hutajuta. Ukifungu tu mtando wa trade car view unainona. Unafahamu tene mkuu Mtz wa kawaida hadi kufikia kuulizia bei ya gari ina maana umejinyima vingi, hivyo, sio vizuri pesa kama hiyo kuingia kwenye mikono ya matapeli.
 
when you use Pay trade service under tradecarview you are 100% guaranteed that you will get your car or your money refunded in case the seller fail to export the unit. What tradecarview are doing is to hold the monet until they get a copy of B/L and confirm with the shipping company that the car is on board ready for shipping to the buyer/consignee.

So mkuu I advice you to go ahead, they are really credible. Autorec ni wakweli lakini their cars are in many cases 35% more expensive than cars traded under tradecarview.
 
Mimi nimeagiza mara 3 na hawa jamaa tena bila hiyo pay trade! cha muhimu ni kuwasiliana na kampuni husika na uliza hao tradecarview watakupa list ya makampuni waliyoyafungia kwa utapeli.
 
Na mimi nina swali,

Je hizo document za kupokelea gari wanakutumia kwa njia gani? je naweza kulipia huku nilipo na nikatumiwa document huku nilipo? mimi niko nchi jirani huku, ila nataka gari nilisajilie TZ ili mke wangu atumie?
 
Mimi nimeagiza mara 3 na hawa jamaa tena bila hiyo pay trade! cha muhimu ni kuwasiliana na kampuni husika na uliza hao tradecarview watakupa list ya makampuni waliyoyafungia kwa utapeli.

Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, usihatarishe pesa yako ilhali i kuna njia salama.
 
Na mimi nina swali,

Je hizo document za kupokelea gari wanakutumia kwa njia gani? je naweza kulipia huku nilipo na nikatumiwa document huku nilipo? mimi niko nchi jirani huku, ila nataka gari nilisajilie TZ ili mke wangu atumie?

Ukisha chagua gari watakupatia maelekezo yote, watakutumia profoma invoice, pesa utatuma kwa Telegraphic Transfer (T/T) via you bank, watakutmia confirmation mara watakapopokea pesa, gari likiondoka kwa Meli wanakutumia documents na zinakufikia within one week, ukipata document unalipia TIN unakabidhi kwa Clearing Agent wako, then unasubiri kuletewa gari nyumbani.
 
Watch out n be carefully na kabla ya kutuma sai salamu maria mara 70
 
Ukisha chagua gari watakupatia maelekezo yote, watakutumia profoma invoice, pesa utatuma kwa Telegraphic Transfer (T/T) via you bank, watakutmia confirmation mara watakapopokea pesa, gari likiondoka kwa Meli wanakutumia documents na zinakufikia within one week, ukipata document unalipia TIN unakabidhi kwa Clearing Agent wako, then unasubiri kuletewa gari nyumbani.

Asante kwa maelezo, swali la nyongeza? je ni kiasi gani hawa jamaa wa CLEARING natakiwa kuwalipa? na je kuna malipo gani mengine baada ya kulipa watu wa TRA?
 
Samahani sikutishi kuna mtu alishalizwa na mpaka sasa akuna hiyo kampuni..alichofanya alituma ajamaa wakapokea na siku mbil zinazofwata ile kampuni ikawa aionekani..kifupi kuna watanzania wengi wamejiingiza kwenye huu mtandao na makampuni yao feki na hii baada ya kuona wengi wanaamini kutuma hela kupitia makampuni yalio kwenye hii website nakwambia yule kijana alikonda miezi sita kama anaumwa cancer ya kibofu ni baada ya kuoa ndio kaafya kaanaanza anza kurudi kwa taabu..sasa sembuse we ndugu yangu..muwe makini tu na hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom