Two Tanzanians Slain in Detroit, MI

Hapana Mzee wangu, serikali ya US ni lazima itaarifiwe mapema maana kuna ulinzi wa overtime, nani ataulipia? Protocali hairuhusu ndugu yangu ninakumbuka one time Mwalimu pale NY alitaka kumtembelea mama mmoja ambaye ni kutoka familia yake, yaani nyumbani kwake kule Queeens,

Secret Service wakakataaa kuwa hapafai kiusalama na hakwenda, isingewezekana kabisaaa yeye kuanzisha safari mpya ya kuja Detroit, kwake kumtuma Mtawa, ilikuwa heshima kubwa sana, tena sana, halafu kumbuka kuwa Mtawa alitokea bongo hakuwemo kwenye safari!

I respect lawama zako, lakini not a president Mtawa was too big kuja huko, yaani kisiasa rais mwenyewe alikuwepo!
 
Mlalahoi na Mzee ES, ni kweli Abbas katumwa hapo.. lakini alitumwa kwa sababu nyingine kabisa hiyo ya kumwakilisha Rais haina ukweli wowote!!! Kama kweli, watuambie.. Rais alitoa ubani kiasi gani kuwapa pole wafiwa? au ndo kama alivyosema Mlalahoi Rais atazuka huko Mikocheni n.k kujitokeza kutoa rambirambi? Pale watu walipomhitaji Rais wao na serikali yao, iliwaacha chini!!! Watanzania wenyewe hapa US wamechanga zaidi ya Dola elfu thelathini kusaidia msiba huu! Kama serikali ilitegemea Wabongo wataadhirika.. wamekosea.. kwanini sasa tunajua Ubalozi si wetu!!
 
Kuna watu wengi ambao kwa sababu moja au nyingine ambao hawakuweza kufika kwenye msiba na hasa kwenye siku ya kutoa heshima za mwisho na ibada ya kuwaombea marehemu iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 30 Sept 2006, Ni kwa sababu hiyo basi KLH News inawaletea taarifa ya siku hiyo ya Jumamosi ilivyokuwa pamoja na salamu za rambirambi toka kwa baadhi ya Watanzania waliobahatika kufika hapo.

Sikiliza:

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Nami naungana na watanzania wote kuwapa pole familia ya Mazula. Hata hapa nyumbani watu wamepokea hizi habari kwa shida na masikitiko makubwa. Kwa kweli watu wengi wameogopa sana mambo ya US, hasa wale wenye ndugu zao huko.

Nami nasikitika kwamba ubalozi wetu haukuchangia chochote katika kusaidia familia na wanajamii ya kitanzania huko Detroit. Nakubaliana na Mzee ES kuwa pengine Rais asingeweza kufika huko, lakini mwakilishi wake alipaswa kuwa wa maana zaidi kuliko kuonesha sura. isitoshe Rais alipaswa kutuma angalau salamu kwa familia. Hii ni wazi kuwa serikali yetu na hasa balozi zetu huku nje hazipo kwa ajili ya kusaidia watanzania. Zipo kwa ajili ya kutafuta watalii na kuomba misaada. It is a big shame. Hapa angeuwa mmarekani hapa Bongo, ubalozi wa US ungeairisha kila kitu ikiwemo kutoa hata visa. Lakini sisi tunathamini vitu (misaada) na sio utu wa mtanzania.

Mungu awabariki wanajaamii wa kitanzania mliopo Detroit; mmetutia moyo-kumbe nasi tunaweza tukiamua!
 
Mwanasiasa.. uliyosema ni kweli, na wakati wa kuwaambia ukweli umefika!! Nilikuwa nawaonea huruma sana jamaa wakihangaika huku na huko kupata fedha za kuwasaidia kwenye shughuli nzima...! Nasubiri hawa vijana walazwe kwanza ndo nianze kuropoka tena.. serikali ya Tanzania imeniudhi.. na itaudhi zaidi kama Rais, Waziri Mkuu au kiongozi mkubwa wa serikali atatokea kwenye mazishi!!
 
Mzee Es said:
Hapana Mzee wangu, serikali ya US ni lazima itaarifiwe mapema maana kuna ulinzi wa overtime, nani ataulipia? Protocali hairuhusu ndugu yangu ninakumbuka one time Mwalimu pale NY alitaka kumtembelea mama mmoja ambaye ni kutoka familia yake, yaani nyumbani kwake kule Queeens,

Secret Service wakakataaa kuwa hapafai kiusalama na hakwenda, isingewezekana kabisaaa yeye kuanzisha safari mpya ya kuja Detroit, kwake kumtuma Mtawa, ilikuwa heshima kubwa sana, tena sana, halafu kumbuka kuwa Mtawa alitokea bongo hakuwemo kwenye safari!

I respect lawama zako, lakini not a president Mtawa was too big kuja huko, yaani kisiasa rais mwenyewe alikuwepo!

Hivi Bush akifiwa ghafla inakuwaje?Protokali sio kitu rigid ambacho hakibadiliki.It's very flaxible,na naamini Secret Service wangeweza kuelewa matakwa ya Rais na kuya-accommodate bearing in mind Detroit sio Basra au Kabul ambako anything can happen hata kama kuna ulinzi wa aina gani.

Mbona JK aliporejea kutoka ziarani kusini mwa Afrika alikwenda Muhimbili on sae day kumuona majeraha wa tukio la uporaji fedha za NBC pale Ubungo?Au unataka kusema PSU ni wako more flexible kuliko kuliko Secret Service?
 
Naungana wanaforum wote katika kuexpress majonzi kwenye msiba huu. Ila inaniuma sana kuona ni jinsi gani ambavyo ubalozi wetu huko US pamoja na Rais na msafara wote jinsi walivyoshiriki. To me presence ya Rais haikuwa muhimu sana, ila ni kweli alishindwa hata kutuma vijidola vichache! Unajua kwa mtizamo wangu kilichokuwa kinagomba ni pesa ili kuweza kusafirisha miili. Najaribu kuimagine kama wangechanga sehemu kidogo tu ya per diem zao ingesaidia japo kidogo. Hapo walikosa uzalendo.
 
zaidi ya yote wametutia deni la dola 50! la kumhudumia "mjumbe huyo wa Rais" ambalo kwa kadiri linavyozidi riba yake ni asilimia 100 kila siku!
 
kulaleki! yaani huyo jamaa naye alikuja mtupu hata kujikimu binafsi ilikuwa mgogoro! it is very unfair!
 
Mtz, jamaa alikuja mtupu hata dola binafsi hakuwa nayo.. ikabidi tutumie fedha kidogo za msiba kumgharimia hapa.. halafu akaondoka hata bila ya kuaga.. anapigiwa simu kumbe mtu yuko Airport!!!
 
Aisee, mbona ilikuwa viroja hivyo, hapo ndugu yangu ndio true colours za viongozi wetu zinaonekana. Tumekosa kabisa uzalendo, hizo gharama walizotumia kumleta huyo mtu si wangeleta hiyo pesa isaidie kwenye shughuli? again nasema that defies common sense. Sasa huu ubabaishaji ndio umejaa tele bongo na dio maana mambo hayaendi kabisa. Ila watu wa US mmneifurahisha sana milvyoweza kuhandle the whole issue, sidhani kama kuna lolote zito kama litawashinda. Hongereni kwa mshikamano!
 
Bwana.. WAtanzania hapa wamechanga zaidi ya dola elfu thelathini kusaidia msiba!! Itakuwa ni uongo kusema kuwa tulitaka serikali ilipie gharama zote.. lakini hata dola 500 za ubani? Ni waswahili waliosema.. "Kutoa ni moyo..." Kilichoangaliwa si kiasi gani serikali ingetoa bali je ingetoa kiasi chochote? Sijui ni mazingira gani yatawafanya watoe fedha za ubani kama siyo tukio kama hilo? Labda hadi mtoto wa kigogo mmoja wa chama au serikali yaje yamkute huku!!!
 
Mwanakijiji,
Hata mie nimepata taarifa kuwa huyo bwana Abbas mligharamia.Unaweza kutueleza ni vitu vitu mlimlipia? Hoteli au?
 
Ningeshauri tusilumbane kabla ndugu zetu hawa hawajapumzishwa; tuzuie uchungu na jazba zetu...

Mbona mahojiano na Mzee Ayubu Mfinanga katika Radio Butiama yanaonyesha kuwa jamaa wa ubalozi wamesaidia japo kwa hali kama si kwa mali?
 
Jamani acheni kulalamika, kuna wabongo wangapi wamekufa hapa marekani na serikali haijafanya lolote? Yaani why muanze kulalamika sasa hivi while Ray Kapalata aliuliwa na mbongo mwenzake na ubalozi haujafanya lolote. Why this one has to be different? U have to be consistent kwenye haya mambo.

By the way poleni wafiwa, ndugu na jamaa.
 
Selemani, hilo ndilo tatizo letu, kwa vile serikali haijawahi kufanya kitu, basi isifanye tena! Na hilo pia ni sababu zilizotolewa na ubalozi kuwa hawataki kuanzisha mazoea (precendence) ya mambo haya. Kama Mwanagenzi anavyosema hapo juu, ngoja hawa vijana wazikwe ndo tutazungumza kuhusu feelings zetu hususan Ubalozi na misaada yao kwa Watanzania. Kama ubalozi unafanya kazi kwa woga au hoja halisi tutaliona hilo kwa kina. Kwa sasa tufikirie tu hoja zetu.
 
Mzee Mwanakijiji said:
Selemani, hilo ndilo tatizo letu, kwa vile serikali haijawahi kufanya kitu, basi isifanye tena! Na hilo pia ni sababu zilizotolewa na ubalozi kuwa hawataki kuanzisha mazoea (precendence) ya mambo haya. Kama Mwanagenzi anavyosema hapo juu, ngoja hawa vijana wazikwe ndo tutazungumza kuhusu feelings zetu hususan Ubalozi na misaada yao kwa Watanzania. Kama ubalozi unafanya kazi kwa woga au hoja halisi tutaliona hilo kwa kina. Kwa sasa tufikirie tu hoja zetu.

Fortunately,nimesoma posting yako kabla sijaandika kwa sababu nilikuwa nataka kumjibu huyo jamaa in the same way as you did.Selemani,I believe you know that two wrongs don't make a right.
 
Ndugu zangu,

Pamoja na kuuunga mkono hoja mkono pointi za Mkijiji na Mlalahoi, ni kwamba hata kama si kusaidia kiserikali, wakati wa tukio kiongozi wetu wa nchi alikuwa huku, kule nyumbani ana sifa ya kuwa "mtu wa watu" pamoja na delegation yake walishindwa hata kuchanga pesa kidogo kutoka katika masurufu yao? mimi hicho ndio kinachonisikitisha! sijui wenzangu mwalionaje.
 
Mtz, lets wait a few days...halafu tutalizungumzia hili... najaribu kumpata balozi "tuchat" kidogo..
 
Mr. Clean.. katika sehemu zilizoendelea Marekani.. Detroit si mojawapo! not in a practical sense anyway... Hivi unajua siku waliyouawa vijana watu wengine wangapi waliuawa usiku huo?... 24! Na hao ni Wamarekani.. now in the greater scheme of things.. where do we fit?
R.I.P Walter and Bonita
======
Mkuu,
1. Suala hili liliishaje? Watuhumiwa walikamatwa, sababu zilijulikana zilizosababisha vifo hivi?
2. Vipi hali ya Usalama katika jiji/kitongoji/Mtaa n.k hilo la Detroit? serikali ya Marekani imechangia chochote kuhusu
usalama hapo toka walipouwa watu 26 (wakiwemo watanzania wawili ) ?
3. Je. Bado watanzania wengi wapo maeneo hayo?
-----
Natanguliza shukrani kwa majibu.
 
Back
Top Bottom