Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Habarini wakuu…

Wakati bado tukiwa kwenye maombolezo, nimeona ni vema nifanye utafiti kidogo wa kumulika uchumi wa Hayati Magufuli, ili tuweke record zetu sawa, maana huku mtaani na kwenye vyombo vya habari kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana.

Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia. Nataka tufike kwenye mizania ya kujua ukweli wa Magufuli, ili kama mtu unasifia ujue unasifia kitu gani na kama unaponda ujue unaponda kitu gani.

Leo ntagusia viashiria vichache ambavyo vinanguvu katika uchumi wa nchi yeyote. Na viashiria hivo vina uhusiano wa viwakilishi kwenye kanuni ya kutafuta zao la nchi yaani GDP.

(GDP = Consumption + Investment + Government Spending + Net export)

Viashiria ambavyo ntaviangalia ni hivi vifuatavyo

1) Credit growth (Ukuaji wa mikopo inayotolewa na benki za kibiashara) – Hiki kiashiria kinawakilisha performance ya sekta binafsi kwenye uwekezaji, ukuaji wa mzunguko wa pesa, private sector confidence, performance ya mabenki ya kibiashara, na pia ni kiashiria cha consumption. Unapokuwa na declining trend, kwenye credit growth maana yake hayo mambo yote niliyoyataja lazima yawe negatively affected.

Ni nini kina determine credit growth? (Ama ni nini kisababishi cha ukuaji wa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kwa sekta binafsi?) – Nadhani hichi ni kitendawili ambacho Hayati Magufuli na wanaomzunguka wameshindwa kukijibu kwa miaka karibu sita aliyokuwa madarakani.

Asilimia karibu 65% mpaka 75% ya uchumi wa Tanzania upo determined na sekta binafsi, na hiyo inayobaki 25% mpaka 35% ndo sekta ambayo ni government nikimaanisha ile sekta inayohusu ukusanyaji wa mapato na bejeti ya nchi.

Utawala wa Magufuli, ulikuja na uwekezaji na matumizi makubwa kwenye projects kama Kununua Ndege, Ujenzi wa flyovers, Ujenzi wa Madaraja, Ujenzi wa Makao Makuu Dodoma, Ujezi wa Bwawa la Umeme, Ujenzi wa SGR na vinginevyo. Kwa ufupi naweza kukadiria kwamba, kwa miaka 6 iliyopita kuna Trillioni 40 mpaka 60 ambazo zilienda kwenye hizi projects za utawala Magufuli. Binafsi sina tatizo na hii approach ya Magufuli kwenye miundo mbinu, kwanza ntazidi kumsifu kwenye hili suala.

Tatizo kubwa ambalo nililiona na ambalo ndo kitendawili alichoshindwa kukijibu Magufuli na utawala wake ni kwamba, mipango ya kutekeleza hii miradi haikuangalia uwezo halisi wa nchi wa kutengeneza mapato ya ku finance hii miradi ambayo ilihitaj kiasi kikubwa cha pesa na rasilimali za viwandani.

Matokeo yake, serikali ya Magufuli ikajikuta ipo kwenye stress kubwa ya kupata pesa za ku finance hii miradi ya mapesa mengi. Kwa hiyo option zilikuwa ni mbili 1) Aaache kutekeleza hii miradi ya mepesa mengi au 2) Afanye kila njia kupata pesa.

Haiba ya Magufuli ilimfanya atumie njia namba mbili ‘Kutafuta pesa kwa gharama yeyote’. Nadhani hii njia ndo imefanya mpaka leo tuna vilio kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyakazi, mabenki, kwa sababu hii njia ilikuja na action zifuatazo za kutafuta pesa.

a) Kikosi kazi cha kukusanya kodi – Fairness kwenye mfumo wa kodi ilipotea, hakukua na logic tena, naweza sema kwa miaka sita iliyopita nchi ilikuwa kwenye ‘Unyang’anyi wa kodi’ na sio ‘Ukusanyaji wa kodi’. Madam President ameongea vema sana jana kuhusu hichi kitu. Hichi ndio kikubwa ambacho kimeua confidence ya sekta binafsi, matokeo yake ikaathiri mzunguko wa pesa kwenye uchumi, kwasababu kumbuka sekta binafsi ndio haswa wateja wa mabenki ya kibiashara. Kwa kuthibitisha hilo angalia trend ya utoaji mikopo kuanzia mwaka 2010 enzi ya kikwete mpaka 2020. Enzi ya Kikwete sekta binafsi ilikuwa inakuwa kwa kasi sana n ahata unaweza kuona trend ya utoaji wa mikopo ambayo ilikuwa ni kwa wastani wa asilimia Zaidi ya 13% wakati ukuaji wa mikopo kwenye utawala wa Magufuli ni wastani wa asilimia 5.6% kwa miaka mitano iliyopita. So unaweza kuona ni kwa namna gani sera ya Magufuli kwenye kodi ilivoua sekta binafsi na ukuaji wa mikopo.

kodi.JPG

mikopo.JPG

Kwa kuangalia data za ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa miaka 10 iliyopita pamoja na ongezeko la utoaji mikopo kwa sekta binafsi kama zilivo hapo juu, tunaweza kuwa na conclusion zifuatazo kuhusu uchumi wa Magufuli dhidi ya watangulizi wake.

  • Kwa miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Kikwete, kwa ujumla aliweza kuongeza kodi kwa karibu asilimia 88% kwa kuangalia kodi iliyokusanywa 2011 na ile iliyokusanywa 2015, wakati huo huo, sekta binafsi ilikuwa ikifanya vizuri kwa kuangalia uwiano wa mikopo na zao ghafi la ndani, ilikuwa ikipanda kutoka 12.21% mwaka 2011 mpaka 14.47% mwaka 2015 alipotoka madarakani. (Key note: Utawala wa Kikwete uliweza kuongeza makusanyo ya kodi mwaka hadi mwaka, na wakati huo huo sekta binafsi ilikuwa inamea mwaka hadi mwaka – Economically hii ndio tunaiita positive
  • Kwa miaka mine ya Magufuli 2016 – 2019 (sikuweza kupata data za 2020), kwa ujumla aliweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa asilimia 56% ndani ya miaka minne 2016 -2019, wakati huo huo mikopo kwa sekta binafsi ilianza kudorora kwa kuangalia uwiano wa mikopo na GDP ambao kwa miaka hiyo minne imekuwa ikienda chini kutoka ile peak iliyofikiwa na utawala wa kikwete ya 14.47% mwaka 2015 mpaka 12.05% mwaka 2019. Hii ki uchumi tunaiita growth ambayo ni negative, yaani GDP inakuwa lakini sekta ya mikopo inadorora, na unaweza kuona ni kipindi hichi hichi nchi ilikuwa na sera za kodi za unyang’anyi.

b) Kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma – ilikuwa pia ni lazima utawala wa Magufuli ufanye hichi kitu ambacho is unfair, kwa minajili ya kulinda pesa za kufanya miradi. Kwa miaka sita iliyopita, kipato cha mfanyakazi kimeporomoka karibu kwa asilimia 18% kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na serikali kushindwa kuongeza mishahara.

c) Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.

d) Kukua kwa haraka kwa deni la serikali (madeni ya nje na ndani) – Hii ndo ilikuwa karata ya mwisho ya kupata pesa, kwa sababu njia zote tatu hapo juu ni kama hazikuzaa matunda. (Ntaelezea kwa mapana hichi kitu nyuzi zinazofuata)

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kama sera za uchumi wa Magufuli ambao ntaendelea kuuchambua, ila kwanza nataka mnielewe taratibu ili tuweze kwenda sawa.

Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi naomba mpitie baadhi ya nyuzi zangu ambazo niliwahi kuandika kipindi cha nyuma na ambazo zitahusika moja kwa moja na uchambuzi kuhusu uchumi wa Magufuli. Naahidi kuwaletea vipande vipande na hoja chache chache ili msije kuchanganyikiwa na rundo la taarifa.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------
1. Ukali wa maisha kwa watanzania - Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!

2. Kuadimika kwa saruji nchini - Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea

3. Uchumi bado upo kwenye mkwamo - ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

4. Serikali imedumaza mifuko ya hifadhi ya jamii - ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii

5. Uchumi wetu ni dhaifu - USHAHIDI: IMF hawajakosea, Uchumi wetu ni ‘DHAIFU’
 
Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.

(Bado Kuna mataga atamsifu mwendazake aisee mlaaaniwe CCM wote na mataga yenu plus mliomuimbia nyimbo za mapambio ya kumsifu maana ndio zilimletea kiburi)
 
Ila mimi nimemuelewa Magufuli kwenye baadhi ya mambo baada ya kufariki.

Kuna vitu nimekua exposed kwake kwa hivi karibuni kwa siku za mwisho mwisho za uhai wake, ndio nikaja kujua alikua na nia gani.

Kwenye ujenzi wa bwawa la umeme, nilikua nampinga tu Magufuli kwa kufuata mkumbo lakini baada ya kupata facts kuhusu gharama za uendeshaji wa mitambo ya gesi na mafuta kwa tanesco, nikajua kabisa Magufuli aliona mbali na alikua na nia njema kabisa kuhusu uchumi wa nchi yetu.

Sasa naamini ukiona mtu anapinga jambo flani inaweza kua halijui vizuri, ana maslahi binafsi, hajalielewa ama anafuata tu mkumbo au ameamua tu, maana watu wengine wanaweza kuamua tu kua dogma, akapewa undeniable facts na bado akaamua tu kutokuelewa.

Mfano mzuri watu dogma ni kama Magufuli mwenyewe juu ya covid 19, aliamua tu kua dogma juu ya corona na bahati mbaya udogmatic wake umegharimu maisha yake.

Ukweli ni kwamba uzalishaji wa umeme kutumia maji ni way cheaper kuliko sources nyingine zote za nishati, ni kati ya shilingi za kitanzania 60 hadi 90 kwa unit. Lakini pia maintanance ya mitambo yake ni baada ya muda mrefu sana, zaidi ya miaka 15 na hata gharama za utengenezaji wake sio kubwa.

Ukija kwenye gas, uzalishaji wa unit moja ni mara 2.5 ya uzalishaji wa maji, lakini pia mitambo ya gesi inahitaji overhaul maintenance kila baada ya miaka 2 na ni billion of money, hao ABB ya Uingereza, Siemens ya Sweden, General Electric ya Marekani, Wartisila na wengine hela wanazofyonza pale Tanesco sio za kitoto, sio za kitoto. Hawa hawataki kusikia tunakua na chanzo kingine cha umeme zaidi ya gasi ama mafuta mazito maana ulaji wao pale Tanesco utakata.

Mfano,Kihansi wanaenda kufanya overhaul maintenance baada ya miaka 20 toka kituo kianzishwe na gharama yake haitazidi 10b, lakini kule kinyerezi General Electric ya Marekani wanataka zaidi ya 80b kufanya ukarabati mkubwa kwa miaka 3 engines na wanataka walipwe kabla ya kufanya kazi. Mitambo ya gesi inataka matengenezo kila baada ya miaka 2.5 ama 3 na gharama zake si chini ya 30B.

Sasa watu kama hao watataka tuwe na vyanzo rahisi vya nishati kama maji? Obviously hawataki kabisa na watatumia propaganda zote kutuonyesha kua maji hayafai, sijui ujinga gani.
 
Aisee nimesoma uzi mwanzo mwisho.. Huyu mtu ni kama Mungu amemchukua kulinusuru Taifa
Huu Uzi ni mzuri Sana kwakuwa uko kisayansi na tutamlaani magu milele ameharibu maisha yetu mtu yule. Alale alipojiandalia.
Hongera mleta, umetuchambulia mambo ya kitaalamu kwa lugha rahisi na nyepesi kueleweka.
Aisee nimesoma uzi mwanzo mwisho.. Huyu mtu ni kama Mungu amemchukua kulinusuru Taifa
Asante sana, na hongera sana mleta mada kwa bandiko lililokwenda shule.
Unaweza kutuletea sector by sector contribution to economy ili tuweze kujua ni sector zipi ziliboom wakati wa Jakaya na sector gani ziliboom wakati wa JPM?
Hii ni sehemu ya kwanza, nta cover sekta ya biashara, uwekezaji wa nje, viwanda, na ntaelezea kwa kina kuusu madeni ya taifa..

Ila conclusion kabisa ni kwamba 'Magufuli alichofanya ni kukopa pesa nying nje na kufanya plundering ya pesa za wafanya biashara kupitia kodi za kidhalimu ili kujenga uchumi ambao ulielemea katika projects kubwa za miundo mbinu ambayo bado hatujajua itakamilika lini'
 
Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.

(Bado Kuna mataga atamsifu mwendazake aisee mlaaaniwe CCM wote na mataga yenu plus mliomuimbia nyimbo za mapambio ya kumsifu maana ndio zilimletea kiburi)
Natafuta data nikuwekee hapa.. kwa miaka mitano Magu serikali imokopa zaidi ya 12 Trillioni.. na hii ipo kwenye financials za serikali, ni liabilities ya serikali ambao wameikopa kwa mifuko ya hifadhi..
 
Habarini wanyonge…

Wakati bado tukiwa kwenye maombolezo, nimeona ni vema nifanye utafiti kidogo wa kumulika uchumi wa Hayati Magufuli, ili tuweke record zetu sawa, maana huku mtaani na kwenye vyombo vya habari kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana.

Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia. Nataka tufike kwenye mizania ya kujua ukweli wa Magufuli, ili kama mtu unasifia ujue unasifia kitu gani na kama unaponda ujue unaponda kitu gani.

Leo ntagusia viashiria vichache ambavyo vinanguvu katika uchumi wa nchi yeyote. Na viashiria hivo vina uhusiano wa viwakilishi kwenye kanuni ya kutafuta zao la nchi yaani GDP.

(GDP = Consumption + Investment + Government Spending + Net export)

Viashiria ambavyo ntaviangalia ni hivi vifuatavyo

1) Credit growth (Ukuaji wa mikopo inayotolewa na benki za kibiashara) – Hiki kiashiria kinawakilisha performance ya sekta binafsi kwenye uwekezaji, ukuaji wa mzunguko wa pesa, private sector confidence, performance ya mabenki ya kibiashara, na pia ni kiashiria cha consumption. Unapokuwa na declining trend, kwenye credit growth maana yake hayo mambo yote niliyoyataja lazima yawe negatively affected.

Ni nini kina determine credit growth? (Ama ni nini kisababishi cha ukuaji wa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kwa sekta binafsi?) – Nadhani hichi ni kitendawili ambacho Hayati Magufuli na wanaomzunguka wameshindwa kukijibu kwa miaka karibu sita aliyokuwa madarakani.

Asilimia karibu 65% mpaka 75% ya uchumi wa Tanzania upo determined na sekta binafsi, na hiyo inayobaki 25% mpaka 35% ndo sekta ambayo ni government nikimaanisha ile sekta inayohusu ukusanyaji wa mapato na bejeti ya nchi.

Utawala wa Magufuli, ulikuja na uwekezaji na matumizi makubwa kwenye projects kama Kununua Ndege, Ujenzi wa flyovers, Ujenzi wa Madaraja, Ujenzi wa Makao Makuu Dodoma, Ujezi wa Bwawa la Umeme, Ujenzi wa SGR na vinginevyo. Kwa ufupi naweza kukadiria kwamba, kwa miaka 6 iliyopita kuna Trillioni 40 mpaka 60 ambazo zilienda kwenye hizi projects za utawala Magufuli. Binafsi sina tatizo na hii approach ya Magufuli kwenye miundo mbinu, kwanza ntazidi kumsifu kwenye hili suala.

Tatizo kubwa ambalo nililiona na ambalo ndo kitendawili alichoshindwa kukijibu Magufuli na utawala wake ni kwamba, mipango ya kutekeleza hii miradi haikuangalia uwezo halisi wa nchi wa kutengeneza mapato ya ku finance hii miradi ambayo ilihitaj kiasi kikubwa cha pesa na rasilimali za viwandani.

Matokeo yake, serikali ya Magufuli ikajikuta ipo kwenye stress kubwa ya kupata pesa za ku finance hii miradi ya mapesa mengi. Kwa hiyo option zilikuwa ni mbili 1) Aaache kutekeleza hii miradi ya mepesa mengi au 2) Afanye kila njia kupata pesa.

Haiba ya Magufuli ilimfanya atumie njia namba mbili ‘Kutafuta pesa kwa gharama yeyote’. Nadhani hii njia ndo imefanya mpaka leo tuna vilio kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyakazi, mabenki, kwa sababu hii njia ilikuja na action zifuatazo za kutafuta pesa.

a) Kikosi kazi cha kukusanya kodi – Fairness kwenye mfumo wa kodi ilipotea, hakukua na logic tena, naweza sema kwa miaka sita iliyopita nchi ilikuwa kwenye ‘Unyang’anyi wa kodi’ na sio ‘Ukusanyaji wa kodi’. Madam President ameongea vema sana jana kuhusu hichi kitu. Hichi ndio kikubwa ambacho kimeua confidence ya sekta binafsi, matokeo yake ikaathiri mzunguko wa pesa kwenye uchumi, kwasababu kumbuka sekta binafsi ndio haswa wateja wa mabenki ya kibiashara. Kwa kuthibitisha hilo angalia trend ya utoaji mikopo kuanzia mwaka 2010 enzi ya kikwete mpaka 2020. Enzi ya Kikwete sekta binafsi ilikuwa inakuwa kwa kasi sana n ahata unaweza kuona trend ya utoaji wa mikopo ambayo ilikuwa ni kwa wastani wa asilimia Zaidi ya 13% wakati ukuaji wa mikopo kwenye utawala wa Magufuli ni wastani wa asilimia 5.6% kwa miaka mitano iliyopita. So unaweza kuona ni kwa namna gani sera ya Magufuli kwenye kodi ilivoua sekta binafsi na ukuaji wa mikopo.

View attachment 1741641

View attachment 1741642

Kwa kuangalia data za ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa miaka 10 iliyopita pamoja na ongezeko la utoaji mikopo kwa sekta binafsi kama zilivo hapo juu, tunaweza kuwa na conclusion zifuatazo kuhusu uchumi wa Magufuli dhidi ya watangulizi wake.

  • Kwa miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Kikwete, kwa ujumla aliweza kuongeza kodi kwa karibu asilimia 88% kwa kuangalia kodi iliyokusanywa 2011 na ile iliyokusanywa 2015, wakati huo huo, sekta binafsi ilikuwa ikifanya vizuri kwa kuangalia uwiano wa mikopo na zao ghafi la ndani, ilikuwa ikipanda kutoka 12.21% mwaka 2011 mpaka 14.47% mwaka 2015 alipotoka madarakani. (Key note: Utawala wa Kikwete uliweza kuongeza makusanyo ya kodi mwaka hadi mwaka, na wakati huo huo sekta binafsi ilikuwa inamea mwaka hadi mwaka – Economically hii ndio tunaiita positive
  • Kwa miaka mine ya Magufuli 2016 – 2019 (sikuweza kupata data za 2020), kwa ujumla aliweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa asilimia 56% ndani ya miaka minne 2016 -2019, wakati huo huo mikopo kwa sekta binafsi ilianza kudorora kwa kuangalia uwiano wa mikopo na GDP ambao kwa miaka hiyo minne imekuwa ikienda chini kutoka ile peak iliyofikiwa na utawala wa kikwete ya 14.47% mwaka 2015 mpaka 12.05% mwaka 2019. Hii ki uchumi tunaiita growth ambayo ni negative, yaani GDP inakuwa lakini sekta ya mikopo inadorora, na unaweza kuona ni kipindi hichi hichi nchi ilikuwa na sera za kodi za unyang’anyi.

b) Kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma – ilikuwa pia ni lazima utawala wa Magufuli ufanye hichi kitu ambacho is unfair, kwa minajili ya kulinda pesa za kufanya miradi. Kwa miaka sita iliyopita, kipato cha mfanyakazi kimeporomoka karibu kwa asilimia 18% kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na serikali kushindwa kuongeza mishahara.

c) Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.

d) Kukua kwa haraka kwa deni la serikali (madeni ya nje na ndani) – Hii ndo ilikuwa karata ya mwisho ya kupata pesa, kwa sababu njia zote tatu hapo juu ni kama hazikuzaa matunda.

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kama sera za uchumi wa Magufuli ambao ntaendelea kuuchambua, ila kwanza nataka mnielewe taratibu ili tuweze kwenda sawa.

Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi naomba mpitie baadhi ya nyuzi zangu ambazo niliwahi kuandika kipindi cha nyuma na ambazo zitahusika moja kwa moja na uchambuzi kuhusu uchumi wa Magufuli. Naahidi kuwaletea vipande vipande na hoja chache chache ili msije kuchanganyikiwa na rundo la taarifa.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------
1. Ukali wa maisha kwa watanzania - Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!

2. Kuadimika kwa saruji nchini - Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea

3. Uchumi bado upo kwenye mkwamo - ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

4. Serikali imedumaza mifuko ya hifadhi ya jamii - ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii

5. Uchumi wetu ni dhaifu - USHAHIDI: IMF hawajakosea, Uchumi wetu ni ‘DHAIFU’
Mkuu Naantombe uko vizuri ila Mimi Toosweet si mnyonge.
 
Ndugu mleta mada binafsi nimekuekewa kwa uchambuzi wako huu kwenye uchumi wa taifa wakati wa uongozi wa awamu ya tano.

Ni dhahiri kabisa kulikosekana maona na waonaji kwenye utawala ule na ndio maana Mambo yalienda ndivyo sivyo na matokeo yake ndio haya.

Tumshukuru Mungu utawala ule umekoma lakini tuweke matarajio chanya kwa utawala huu Hali tukiendelea kukazana kujenga uchumi kila mmoja kwa nafasi yake huku Mungu akiwa ndie mwongozaji.
 
Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.

(Bado Kuna mataga atamsifu mwendazake aisee mlaaaniwe CCM wote na mataga yenu plus mliomuimbia nyimbo za mapambio ya kumsifu maana ndio zilimletea kiburi)

Mkuu tupo CCM tuliokaa kando kupisha buldoza lipite usitulaani kiasi hichi tafadhali
 
Back
Top Bottom