Tuwe Makini na Watu Tunaowasaidia, Itatugharimu!

Wabogojo

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
354
87
FYI
Nimetumiwa na rafiki yangu leo hii.

Mzee Mbene

JUMAPILI ILIYOPITA MJOMBA WANGU ALIKUWA KWENYE DALADALA AKITOKEA UBUNGO KWENDA TEGETA.BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA WENGINE WAKAWA WAMESIMAMA, KATI YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA ALIYEKUWA NA HAND BAG KAMA TUNAZOBEBEA LAPTOP HIVI, YULE MZEE ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE KUMSHIKIA BAG LAKE KWAKUWA YEYE ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA KUMSAIDIA KALE KA BAG"BAADA YA VITUO VIWILI YULE JAMAA MWENYE KA BAG; ALITEREMKA BILA MJOMBA WANGU KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE MZIGO AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.

KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU WALIOJITAMBULISHA KWAMBA WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA KITU WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU ABIRIA WOTE WATEREMKE KWENYE GARI,WALIFANYA HIVYO NA MMOJA WA WALE POLISI, ALIMFUATA MJOMBA WANGU NA KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO LANGU KWA HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!! WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE YUKO WAPI TUONESHE" AKAANGALIA KATI YA WALEA BIRIA WENZAKE HAKUMUONA.

WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA SILAHA AINA YA PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI UTAENDA KUJIELEZA HUKO. BASI LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI, WAKIWA NJIANI WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA WAMWACHIE ATOE LAKI NANE 800,000/= VINGINEVYO WATAMUUNGANISHAKATIKA KESI YA WIZI WA KUTUMIA SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA NA SIWEZI KUTOA .MPAKA SASA BADO YUPO NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA TUWE MAKINI NA MISAADA TUNAYOITOA.

MZEE ALIKUWA NA NIA NJEMA KABISA YA KUTOA MSAADA ILA MSAADA UMEMGHARIMU MAISHA.

My Take: Napenda kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na watu tusiowajua, itatugharimu ndugu zangu.
 
Asante kwa tahadhari hiyo ya ukweli ndugu ila umenichosa sana kwa kutumia herufi kubwa. Kwa nini herufi kubwa?
 
Nikweli inabidi tuwe makini sasa pamoja na kuwa watanzania ni watu wanaopenda kusaidia. Imefika wakati mambo yamebadilika si kama zamani, imani na uaminifu kwishney kabisa. Huko tunakoelekea tutashauriana tusisaidie tusiyemjua.
 
kuna siku nakumbuka miaka 4 nyuma,ilikuwa stend pale posta mpya muda wa jioni watu kurudi nyumban,wakat,kuna kijana alikuwa anasubiri usafiri,mara akatokea mama mtu mzima,akamuomba simu aweke line awapigie ndugu zake,yule kijana akampatia simu yule mama akatoa line ya jamaa na kuweka yake,baada ya kuongea yule mama akajifanya kama anarudisha line ya jamaa kumbe akufanya hivo,bus la mwenge lilivyokuja wote wakaingia,mara yule mama akaanza kulalamika kaibiwa simu,basi watu fasta wakasema mama atoe namba ya simu wapige kabla mwiz ajaizima,watu kupiga namba ikaitia kwa simu ya jamaa,wabongo bila kupata habari kamili,wakampokonya simu na kumpa yule mama,na kuanza kumshushia kipigo,yule mama akateremka fasta akapotea,jamaa adi anajieleza yule mama alikuwa ameondoka na jaa ashapigwa
 
dah mkuu hiyo kiboko, very sad. Ndio maana hata mtu akiwa na shida ya kweli hasaidiwi kisa wapumbavu wachache kama hao.
 
dunia tunayoishi sasa sio ya urafiki na undugu ni kuwa makini na kila mnayemwona. hili ndio la msingi. siku hizi hata ombaomba unaogopa kuwasaidia maana wengine wanga wana chuma ulete yani duniani sio sehemu rafiki tena.
 
dah mkuu hiyo kiboko, very sad. Ndio maana hata mtu akiwa na shida ya kweli hasaidiwi kisa wapumbavu wachache kama hao.

Kweli Mkuu.
Manake siku hizi ni bora ukajiepusha na kusaidia kuliko kufanywa Mbuzi wa Kafara..
 
Ndo maana nimeamua kuwa Bandidu sitoi lifti au msaada kwa nisiyemfahamu ata awe na matatizo gani!
Kama msaada niatautoa kanisani au msikitini
Kuna jamaa alimpa mtu lifti si jamaa akashuka na simu si unajua gari ya home vitu huwa shaghala bagala!
 
Mkuu usinikumbushe hii nilipoteza BB yangu mpya kisa kumpa jamaa lifti aise
Mpaka leo sitamani kufanya hiyo kitu aise
 
Siku hizi hakuna kuplay role of a good samaritan,,watu hawaaminiki,ila hao waliosimamisha gari na kujiita polisi ukute fake hao wapigaji tu wa mjini
 
Sasa kwa njia hii mbona watu watakuwa hawatoi misaada.
Na ile ya ombaomba wa salenda iliishiaje?
 
Hao Police nao Hawana jIPYA!! Asiwape Hata senti Tano!! Ila kama Hiyo Hadithi ni ya Ukweli basi hii nchi haina askari wapelelezi ila ina wala Rushwa tu!!
 
Back
Top Bottom