Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,964
- 6,911
Jengo la kale Bagamoyo nusura limmalize Mchina
2008-10-17 22:22:34
Na Daniel Mkate, Bagamoyo
Mchina mmoja ambaye alikuwa msimamizi wa kampuni ya ujenzi ya CHICO inayobomoa jengo la kale lililokuwa Ofisi za Posta ya wakoloni kwa ajili ya ujenzi wa hoteli ya Sunrise, amenusurika kufa baada ya jengo hilo kuporomoka na kujeruhi watu watano.
Tukio hilo limetokea jana mishale ya saa 3.30 asubuhi, wakati mchina huyo, Bw. Tai Yang, akiwa anawasimamia mafundi waliokuwa wakiporomosha kuta za jengo hilo la kale.
Wakati wakiwa kazini, ndipo kuta za jengo hilo `zee`zikaporomoka hadi chini na kuwafunika wajenzi hao.
Majeruhi hao waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, wametajwa kuwa ni Cloud Nyenja, 25 mwenyeji wa Bagamoyo, Abdul Maulizo, 24 mkazi wa Dar es Salaam na Abdulrhaman Hamad, 24, mkazi wa Zanzibar.
Akizungumzia tukio hilo, fundi Nyenja amesema shughuli ya kubomoa kuta za jengo hilo walizianza hivi karibuni huku wakisimamiwa na Tai Yang, bila ya kuwa na hofu yoyote kuwa linaweza kuporomoka.
``Hatukutarajia kama lile jengo lingeweza kuporomoka, ingawa ni la siku nyingi... lakini tunamshukuru Mungu kwa kunusurika na kifo,`` amesema Bw. Nyenja.
Hata hivyo, Mchina huyo ambaye pia ni msimamizi wa ujenzi wa jengo jipya litakalojengwa, licha kuumia sana sehemu ya kichwa na miguuni, aligoma kuzungumza kabisa kuhusu jinsi jengo hilo zee lilivyopomoka.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Bagamoyo, Dk. Kussenah Lob, amethibitisha kuwapokea majeruhi hao na kueleza kuwa wanaendelea vizuri baada ya kuwapatia matibabu.
``Wanaendelea vizuri wote, kwani madaktari wamejaribu kuwashughulikia ipasavyo... tunashukuru Mungu hakuna aliyepoteza maisha,`` amesema Dk. Lob.
Aidha, Dk. Lob amesema kabla ya jengo halijaporomoka, waliwashauri wajenzi kutojisahau kwani kuna uwezekano wa kuweza kutokea madhara makubwa.
``Kauli yetu imethibitika leo (jana), kwani yale tuliyowaambia kupitia kwa msimamizi wao (Yang) yametokea, lakini tunashukuru hawakuweza kupoteza maisha,`` amesema.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa magofu ya kale mjini Bagamoyo kuporomoka, na hivyo kuwatia wasiwasi wenyeji pamoja na wageni wanaotembelea magofu hayo.
Tutabaki na nini? Hivi hao watalii tunaotegemea kukaa kwenye hiyo Hoteli Sunrise watatoka wapi baada ya sisi kubomoa majengo yote ya kale?
Mji wa Dar es Salaam unasikitisha kwa kasi ya kubomea majengo ya zamani na kujenga maghorofa bila kuangalia infrastructure iliyokuwepo!
Lesser Flamingoes tunawapigia hesabu ya kuwamaliza kwa ajili ya virupia kutoka kiwanda tutakachojenga Lake Natron.
Serengeti tunajenga mahoteli na kiwanja cha ndege kuhudumia watalii watakaokuja kuangalia wanyama ambao hayo maendeleo ndiyo kiama chao!
Kweli tunajiuliza hao watoto na wajukuu wetu tutawaachia nini?
Mungu inusuru nchi yetu.