Tutafika njiapanda ya akhera tukiwa hoi mno

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,635
697,929
Taifa lenye wakazi waliochanganyikiwa kuliko wagonjwa walioko Lutindi Korogwe Tanga na Mirembe Dodoma.. Na hawa wote kama si viongozi wa kisasa basi ni watu fulani wenye kaumaarufu fulani..
Sasa kama hawa ndio vioo vya Jamii basi wengine wote wana makengeza

Ripoti mbalimbali

Wale wote waliokuwa wanawasifia na kuwaanika wake zao mitandaoni naona sasa wamepata somo murua kwa njia ngumu na iliyojaa maumivu mengi kwamba mke si bidhaa ya kuanika mitandaoni.. Bado mmoja ..huyu hajakoma! Wale wanaowafunika wake zao gubigubi wana sababu kubwa sana! Wahuni sio watu

Mtu mmoja na mvi zake nyingi tu aliyewahi kukasimiwa madaraka makubwa nchini kaamua kujiandalia hatima yake kwa kujichimbia kaburi na kujinunulia jeneza imara la bei ghali.. Kweli umri sio hekima.

Jide aliwahi kujichagulia/kujinunulia jeneza na akasema kwenye msiba wake waombolezaji watakuja kwa mwaliko maalum wa card.. Mpaka leo yuko na hatima ya umaarufu ishampa kisogo! Nani ana hakika atakufa kifo cha mwili wake kuonekana! Kaburi halilali wazi

Wakosoaji muwe makini sana.. Mna rivals.. Mkikosoa wanasifu na kuabudu.. Mkikosoa tena mnaweza kuolewa hata kama hamna sehemu za ndoa.. Wanajua una marinda hayo ndio wanayafanyia kufuru..!!! Mkikosoa wasipoabudu wanakugeuza kibudu kwa namna ile wataona inawafaa. Sometimes watakuanza na mshono! Utashonwa kisawasawa, kisha watafumua marinda halafu wanakupymzisha milele!
Chizi mmoja juzi kasema eti 2020 alipewa sumu kwenye chakula lakini ikaja kugundulika siku nne baadae ila hakufa

Mengine tusiyaandike hata kwa codes.. Maana wale wana hawana simile.. Nijuavyo mimi kule SIMBA timu kubwa na maarufu Afrika na duniani kote kuna kundi maarufu la FRIENDS OF SIMBA Yaani hawa ni marafiki wa taasisi na si marafiki wa MO wala si chawa.

Kuna kituko kingine nimekishuhudia kwenye mwendelezo wa kuendelea kuinyongelea mbali taasisi kongwe inayoelekea ukingoni

Eti sasa kuna Samy queens Ukiachana na zile zingine za chawa wa Samy na friends of Samy!

Salamu kutoka akhera madukani...!*
 
Mbaya sana leo ni siku yao kuu huko Mwezini
IMG-20240308-WA0048.jpg
 
Duh, mkuu naona umemwaga risasi za rasharasha na zimewapata kisawasawa walengwa, tatizo hao walengwa wamedata, ni machizi sugu hayaelewi kitu. Nafikiri huyo chizi ulimuona alivyokuwa anajifaragua kwenye kile kipindi cha ile media. Yule ndio chizi og haelewi kitu kadata
 
Sir nature anasema "Kuku ni Kuku ila Jogoo Jina"

Hoja mjarabu Bado itaendelea kuwafanya kukesha hata kabla ya PASAKA.

Watetea ni wengi,ila term hii hawatagi.

VUMBI KUONEKANA ANGANI WAKATI NI USIKU WA GIZA TOTORO.
VUMBI KUONEKANA ANGANI WAKATI NI USIKU WA GIZA TOTORO.
 
Back
Top Bottom