Turufu yetu ya mwisho kujitoa mkataba wa DP World ni kuwakata waliohusika kujadili na kusaini kwa tuhuma za rushwa

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Kama mkataba ni mbaya na ni wa milele,

Turufu yetu ya kwanza kujitoa ilikuwa kupingwa na bunge ingekuwa wazi kwamba mchakato wa kisheria haukamiliki kwa mtu mmoja kutia saini.

Hiyo wabunge wetu wanajigamba kuwa magwiji wa sheria hawakuona.

Sasa ni kuunda timu ya kuchunguza ambayo itaibuka na tuhuma za rushwa kwa watu waliohusika kusaini na hiyo itatupa nguvu ya kuukataa na hawa jamaa wakitupeleka mahakama yoyote kimataifa hoja zao hazitakuwa na mashiko.

Cha msingi tusisikilize wanasheria wetu, wengi ni mbumbu wamezoea kesi za kutolea watu dhamana segerea ila hapa tunahitaji watu wa kutuambia ni jambo gani ambalo likibainika lilifanyika mkataba unakuwa umeisha nguvu.

Moja ni kuonyesha kuna mchezo mchafu ulifanyika na tujue taratibu za kimataifa zinataka unapobaini hilo unatakiwa kufanya nini na sisi tutimize matakwa hayo karatasi tulilosaini liendelee kuwa karatasi
 
Kweli kuchomoka hapa. Lazima Arguments za Rushwa ziwe raised against DP World. Tuwa toe kafara Wabunge 30 wote walio enda Dubai. Na ni marufuku kwao kupanua madomo yao kutuelezea Bandari. SPIKA. AG. Watendaji wa juu Ikulu, na Waziri , Naibu Waziri na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi. Wakamatwe. Account zao zote na za DP zichunguzwe.
 
Mkataba huu unavyotetewa na wakubwa upande wa serikali unatia shaka. Wengi ni wanasheria wabobezi kabisa. Haiwezekani wakatetea makosa ya wazi kiasi hiki . Ipo sababu.... Meli inasogezwa maji makuu penye mkondo hatari ! Sijui ikizama nani atafaidi.. .mshaurini mkuu vema . Acheni kumdanganya . Nimetafakari ubongo ukagoma... Sielewi kwa nini . Hata kama ni hongo, siamini kwani wengi wameshiba, sio watu wa shida kiasi hicho... No !!!!
 
Kweli kuchomoka hapa. Lazima Arguments za Rushwa ziwe raised against DP World. Tuwa toe kafara Wabunge 30 wote walio enda Dubai. Na ni marufuku kwao kupanua madomo yao kutuelezea Bandari. SPIKA. AG. Watendaji wa juu Ikulu, na Waziri , Naibu Waziri na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi. Wakamatwe. Account zao zote na za DP zichunguzwe.

Mkuu nani wa kufanya hayo? Mchakato mzima umeasisiwa na una baraka zote za mamlaka kuu… jipe tu matumaini, wanasubiri tunyamaze ila hakuna kitu kitabadilika wala hakuna mtu atawajibika…nipo hapa utaniambia!
 
Back
Top Bottom