Stories of Change - 2023 Competition

Pics

JF-Expert Member
May 21, 2020
240
181
Mimi ni mwanazuoni kutoka chuo Fulani, niko na maendeleo mazuri sana kielimu, ninaona nuru kila siku. Lakini haya yote yametokana na jitihada kubwa za wazazi wangu na malezi bora kutoka kwa walimu na walezi wangu tangu shule ya msingi. Nilipelekwa shule za bweni tangu nikiwa mdogo, kwani hakukuwa na shule nzuri katika eneo langu. Nimekua sio tu kielimu, bali pia kimaadili, kiakili, kimwili na kiafya.

Lakini sasa nimekuwa na huzuni sana kuona shule za bweni ninazoziamini kuwa ni bora katika kukuza mtoto kwa mazingira bora ya kielimu, kiakili na kimwili zimebadilika na zinawaletea watoto maumivu makali kutokana na vitendo vya kikatili na vya kinyama visivyokuwa na huruma.

Naomba tupige hatua nyuma na kurudi kwenye nafasi tulipotoka, ambapo kila mtoto alionekana kama mwana wa jirani yetu na tuliwajibika kumlinda bila kujali lolote. Turudi kwenye enzi hizo ambapo matroni, walimu, masista, walinzi, na madereva wa magari ya shule walifanya wajibu wao wa kuwalinda watoto bila malipo makubwa. Kumlinda mtoto ilikuwa ni jambo muhimu sana.

Nimekumbuka mazingira tuliyokuwa nayo zamani, na natamani kila mtoto anayesoma shule za bweni apate kumbukumbu nzuri, yenye furaha na yenye kumshukuru mzazi wake, walimu wake na walezi wake bila kuwalaumu au kuwafanya wazazi wahisi walikosea. Lakini haya yote hayatafikiwa mpaka kila mmoja wetu atakapo wajibika katika nafasi yake ya kumlinda mtoto. Sote tufanye wajibu wetu kuwafunza watoto wetu na wale tunaowalea kujilinda wenyewe na kuwalinda wenzao.
 
Back
Top Bottom