Tupashane Habari za Sikukuu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Niko Maeneo ya Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na kuwa hapa jioni hii siku yangu ya leo imekuwa salama tu sijapata tatizo lolote lakini kuna mambo kadhaa nimeyaona huko mitaani toka jana usiku , sina budi kuwashirikisha wadau wengine kama wana simulizi wa kutupa kutoka maeneo yao karibuni sana .

Kwanza jana usiku kuanzia saa 3 hivi nilisikia milio ya risasi kama 4 hivi maeneo ya ubungo River Side lakini baadaye hali hiyo ilitulia sijajua kama ni mtu na mkewe walikuwa wanapimana shabaha manake kila unayemuuliza anaonyesha kidole nyumba ile na kutulia kama maji kwenye mtungi .
Leo asubuhi sehemu nyingi sana zilifunga biashara zao haswa zile za mawasiliano kwa njia ya mtandao internet café kuanzia kimara , magomeni , buguruni , ilala , sinza hata hapa Mlimani , Mwenge kati kati ya jiji na sehemu zingine nyingi naona Watanzania bado hawajajua umuhimu wa mawasiliano kwa jamii zinazowazunguka na hata hawajui jinsi zinavyosaidia kuweka maisha ya wenzao katika hali nzuri pindi wanapofungua sehemu zao za mawasiliano .

Kwa upande wa barabara kwa kweli leo sijaona foleni sehemu yoyote kuanzia asubuhi nilipopia ubungo kuelekea buguruni mpaka uwanja wa ndege , kurudi kupitia buguruni mpaka magomeni , morogoro mpaka mwenge na mwisho hapa UDSM sijaona foleni yoyote hata wale ambao wako maeneo ya mbezi beach na mbezi shamba leo hawana wasiwasi wowote wa foleni muda wa jioni kwa sababu magari sio mengi .

Lakini kitu kilichonitisha kulivyo vyote ni hali ya ulevi wa pombe na aina nyingine ya anasa miongoni mwa vijana , mtaani kwetu kuna watoto niliwaona leo asubuhi kuanzia saa 1 hivi bar wameanza kunywa baadaye wakaungwa mkono na wazazi wao kwenye bar hizo kwa ajili ya kuendelea na ulevi , hawa ni watoto wadogo ambao tunategemea mbeleni waje kuwa wafanyakazi bora na viongozi bora wa nchi hii wako na wazazi wao wanalewa kuanzia asubuhi saa 1 .

Baadaye watoto hawa wanaweza kuamua sasa kwenda kutafuta watoto wenzao kwenda kujiburudisha zaidi kama ni watoto wakike unakuta ana vibuzi vyake huko mitaani basi akishalewa kibuzi chake kina mngoja mitaani kwake burudani zingine zinaendelea nani atamzuia wazazi wamelewa nao wanaenda bujiburudisha kivyao tena wazazi wengine wanaenda kwenye nyumba ndogo zao iwe wa kike au wakiume ?

Lililonisikitisha zaidi ni kuona miti ya Krisimasi ikikanyagwa na magari maeneo mengi ya kuuza miti hiyo ile ambayo inatolewa mikoani watu wamekataa kabisa kuinunua badala yake wanahamia kununua miti iliyoagizwa kutoka nje yenye vita vya kuwaka waka hali hii kwa kweli imenisikitisha sana , Pamoja na kuwa na wataalamu ,viwanda na aina nyingine ya malighafi vitu vidogo kama hivi vinatushinda mpaka viagizwe kutoka nje na wazalendo wananunua hivi vifaa kwa mamia

Naomba niishie hapa , napenda kukutakia tena wakati mwema wa sikukuu za xmass na mwaka mpya .

Endelea kuwa mwaminifu Katika uwajibikaji na ukubali kuwajibika bila kulazimishwa .
 
Back
Top Bottom