Tuombe Mwaka 2024 Uwe ni Mwaka wa Mageuzi ya Kweli ya Kidemokrasia ya Kweli Tanzania. Tume Huru, Uchaguzi Huru na wa Haki! Happy New Year!

Watanzania ni watu pisi sana, hatuna watu wa machafuko type.

Jeshi la Tanzania ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania, TPDF or JWTZ, hivyo sio Jeshi la kufanya mapinduzi

Naomba tuu niheshimu mawazo yako.
P
Hao JWTZ wakati wanataka kumpindua Nyerere miaka ya 80 hawakuwa jeshi la wananchi?

Usichanganye watu peace na waoga, fahamu uoga sio jambo la kudumu. Uoga utafika mwisho tu hasa ukizangatia mabadiliko ya kizazi.
 
CCM hawawezi kukubali hilo. Kwa sasa wanatafuta kukubalika kwa wahisani wetu, ndio maaana unaona hizo sijuiR, na maigizo mengine.
 
Leo 31/12/2023 tunauaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2024, hivyo naomba nianze makala yangu hii ya kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya 2024 kwa rai moja tuu, "Mwaka 2024 ni Mwaka wa Mageuzi ya Kidemokrasia Tanzania" kwa kimombo "A Democratic Turning Point"

Ni mwaka ambao, tunabadili sheria yetu ya uchaguzi iwe sheria bora zaidi, tunabadili Tume yetu ya uchaguzi, kuunda Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, na tunapaswa kufanya mabadiliko madogo ya katiba ya JMT ili kuuondoa ubatili fulani ndani ya katiba yetu.

Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika sana na kulialia lia mwingi!, lakini tukija kwenye matendo, actions na kuchukua hatua, kusema ukweli kabisa, sisi ni wazito wa kufanya vitendo na kuchukua hatua, lakini kwenye awamu hii ya 6 ya Rais Samia, aliunda kikosi kazi, kikatoa mapendekezo, miswada ya sheria imeisha tungwa, na kusomwa Bungeni kwa mara ya kwanza, sasa inajadiliwa na wadau na kutungwa kuwa sheria, ila lile kubwa kuliko la ubatili wa katiba yetu, lenyewe bado halipo, na hilo sasa ndilo mimi nasimama nalo mwaka 2024.

Wengi huuanza mwaka mpya kwa kuweka malengo ya mwaka, “new year’s resolutions” kwamba mwaka huu nitafanya hili na lile, ila katika kupanga hayo malengo, sii wengi hufanya mapitio ya mwaka ulioisha, walipanga kufanya nini, wametekeleza nini, wamefanikiwa nini na wamekwama nini, ili baadhi ya yale malengo ya mwaka uliopita, ambayo hayakufanikiwa, yabebebwe katika mwaka unaofuata, au kama hayabebeki yafutwe, na sio kila mwaka unakuja na malengo mapya, mwisho wa mwaka hufanyi tathmini wala mapitio ya mwaka ulioisha, kisha unakuja na mengine mapya!, mwisho wa siku, unakuwa huwezi kupima mafanikio yako!.

Katiba ya nchi ndio Biblia ndio Msahafu wa uendeshaji wa nchi yetu. Kama ilivyo Ikulu ni mahali patakatifu, katiba ni kitabu kitakatifu kwa nchi yetu kama vilivyo vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu kwa Wakrusto na Quran Tukufu kwa Waislamu. Hii ndio sheria mama ya uendeshaji wa nchi yetu.

Tofauti pekee kati ya Biblia, Msahafu na Katiba, ni Msahafu haubadiliki, katiba inaweza kubadilishwa, ila mabadiliko yoyote ya katiba, lazima yawe ni mabadiliko halali ya haki.

Katiba ndio sheria kuu kuliko zote za nchi, viongozi wetu wakiisha chaguliwa, tunawaapisha kwa mujibu wa katiba, wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, na ikitokea hata rais wa JMT akikiuka katiba, anaondolewa madarakani!.

Sheria yoyote ikitungwa, ikiwa ni kinyume cha katiba, sheria hiyo inahesabika ni batili “null and void”. Anayebatilisha sheria batili sio Mahakama Kuu, ni katiba yenyewe, kazi ya Mahakama Kuu ni kuthibitisha tuu huo ubatili na tangu unapothibitika, ubatili huo unakuwa umebatilika!.

Tanzania kuna kuna sheria ya uchaguzi ambayo ni batili, kwa kwenda kinyume cha katiba ya JMT, kisha ubatili huo, ukaja kuchomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, licha ya Mahakama Kuu kuitangaza sheria hiyo ni batili, na uchomekeaji ubatili huo kwenye katiba pia ni batili, kifungu hicho bado kipo na sheria hiyo bado ipo, mabadiliko ya sheria ya uchaguzi tunayokwenda kuyafanya hayagusi mabadiliko ya katiba, hivyo ubatili huo bado upo.

Sisi Watanzania tuna fani mbalimbali, kuna wenzetu kazi yao ni kufikiri na kupanga mikakati, hawa wanaitwa think tanks, kuna wenzetu ni viongozi, kazi yao ni kutuongoza, kuna wenzetu ni watendakazi, kazi yao ni kutenda kazi kwa kutumia nguvu zao, kuna wengine tukiwemo sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, wa kiasili, yaani “traditional media” kazi zetu kuu ni tatu, kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, hatuna kutenda!. Na tumegawanyika makundi mawili, waandishi wa habari watangazaji na vyombo vya utangazaji (broadcast media) ambao kazi yao ni kutangaza na kuongea tuu, hakuna kutenda lolote!, na waandishi wa habari wa magazeti (print media) ambao kazi yao ni kuandika tuu hakuna kutenda lolote!.

Lakini ujio wa mapinduzi ya kidigitali kwenye dunia yetu na ujio wa mitandao ya kijamii, haya makundi mawili ya vyombo vya habari, yaani broadcast media na print media, yameunganishwa na mtandao wa jamii, hivyo kule kwenye mtandao, hakuna print peke yake wala broadcast peke yake. Vyombo vya utangazaji vina kurasa zake za mitandao ya kijamii navyo sasa vinaandika, mtu unaweza kusoma, vyombo vya print, kama magazeti, navyo kwenye kurasa zake, vinatangaza, na kuweka magazeti mtandao, hivyo siku hizi, kupata habari, kuangalia TV au kusoma gazeti, sio lazima ukae nyumbani uwashe TV uangalie habari, ukijisajili tuu na mtandao fulani, wanaita ku subscribe, unaletewa tuu habari, kila inapotokea, hivyo mtu hana tena haja kusubiria taarifa ya habari saa mbili usiku, kila tukio linapotokea linatangazwa live, hivyo kufikia ule muda wa habari, kila kilichotokea, watu wanakijua, magazeti ya kesho yake, sisi tunayasoma leo, maana kwenye kurasa zao za mitandao, kila habari, inachapishwa pale pale inapotokea.

Ujio huu wa mitandao ya jamii, umemfanya sasa kila mtu kuwa ni mwandishi wa habari, kila mtu sasa ni mtangazaji, hali inayopelekea hata sisi ambao ni watangazaji wa kweli wa kusomea hii kazi, kujikuta hatufui dafu mbele ya watangazaji vijana wa kisasa kwenye mitandao ya jamii, hivyo ukiwauliza vijana wa kisasa, unamjua Pasco Mayalla?, atakuuliza, Pascal Mayalla ndio nani?, utamwambia ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto, atakuuliza kiti moto ndio nini?, naomba link yake ni kitazame nikivutiwa, nita subscribe, unajikuta huna cha kumwambia!, hivyo sisi waandishi wakongwe wa ki analojia, ili tuendelee kuwepo ni lazima tubadilike na kwenda kidigitali vinginevyo tunafutika jumla!, hivyo mwaka 2024 Pasco Mayalla nae anakuja kidigitali zaidi!, anakuja na kipindi chake kipya kiitwacho KMT.

Hivyo kwa vile mimi kazi yangu ni kuandika tuu na kutangaza tuu, nikikaa chini na kuutafakari mwaka 2023, nimeandika mangapi na kutangaza mangapi, kuhusu katiba na yapi yamefanyiwa kazi, nimejikuta nimekata shauri kwa mwaka huu 2024, ili kulisaidia taifa na kuisaidia jamii, na kulisaidia taifa, nisiishie kuandika tuu, na kutangaza tuu, ninapaswa nifanye kitu cha ziada kwa kwenda mbele zaidi kwa kufanya jambo la ziada zaidi ya kuandika tuu na kutangaza tuu.

Kitu ninachokwenda kukifanya kwa ziada ni uelimishaji umma kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu, kupitia makala hizi ambazo sasa zinakwenda sambamba na kipindi cha TV kiitwacho KMT.

Hili nitalifanya kwa moyo wangu wote kwa mwamko wa yale maneno ya rais kijana wa Marekani, John F. Kennedy aliyowaeleza Wamarekani, “usijiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia nini Marekani?”. Hivyo tunapoukaribisha mwaka mpya, wa 2024, kama kila mmoja wetu atajitafakari kwa kujiuliza “jee ameifanyia nini Tanzania” akijikuta hajaifanyia kitu chochote cha maana huko nyuma, basi mwaka huu wa 2024, abadilike kwa kupanga malengo yenye mipango mkakati kwa kujiuliza, “jee ataifanyia nini Tanzania?”, Inawezekana kama kila mtu atatimiza wajibu wake kikamilifu.

Mwaka huu wa 2024 ni mwaka wa mabadiliko, japo hili la mabadiliko ya katiba halipo, Rais Samia ni rais msikivu, serikali yake ni serikali sikivu, nawaomba muungane nami katika hii safari mpya ya elimu ya Katiba, sheria na haki, “it can be done, play your part” .
Kwa heri 2023, karibu 2024
Happy New Year!,
Heri ya Mwaka Mpya!.
Paskali.
Mkuu unaota NDOTO ya mchana CCM imetest MITAMBO yake ya WIZI wa KURA katika Chaguzi za hivi majuzi ni IMEFANIKIWA
 
Pasco tatizo lako jambo dogo rahisi huwa unaliandika Kwa urefu bila sababu ya Msingi.

CCM wanaposema kuwa hitaji la watanzania siyo Katiba Mpya Bali barabara, maji, ajira na mengineyo huwa unawaelewaje???
Ndugu yangu Allen Kilewella, hapo kwa Pascal Mayalla, unampigia mbuzi gitaa.

Ni Tanzania unapowapata watu waliopafata F masomo yote form four hivi leo ni PhD holders.
Na kwa sasa hawa ndio viongozi wakuu wa kitaifa wanaoitafuna nchi kwa urefu wa kamba zao!

Masikini waliopata distinction katika masomo yote form four, wengi wao ni malofa wa kutupwa.
Ndio hao hao wanaozurura na vyetu vyao mitaani na mwisho huishia kuendesha bajaj na boda!
 
Ndugu yangu Allen Kilewella, hapo kwa Pascal Mayalla, unampigia mbuzi gitaa.

Ni Tanzania unapowapata watu waliopafata F masomo yote form four hivi leo ni PhD holders.
Na kwa sasa hawa ndio viongozi wakuu wa kitaifa wanaoitafuna nchi kwa urefu wa kamba zao!

Masikini waliopata distinction katika masomo yote form four, wengi wao ni malofa wa kutupwa.
Ndio hao hao wanaozurura na vyetu vyao mitaani na mwisho huishia kuendesha bajaj na boda!
Kuna kijana nilimuiliza yaani umesoma miaka 15 ili uje kuwa mwendesha Babaji??

Mwingine anachoma mahindi anajisifu "alivyojigeuza" badala ya kutafuta ajira akaamua kuwa Mchoma mahindi.

Na ni watanzania akili na matendo yetu ndiyo yanayotufikisha Kila mara kwenye ile falsafa ya "heri nusu mkate kuliko kukosa kabisa".

Maandiko yanaonesha Adam na Hawa walikuta watu wengine duniani waliokuwepo kabla yao. Jee na watu hao pia waliumbwa na Mungu. Watu hao siyo sisi kweli??
 
Tume huru itatoka wapi ikiwa Katiba iliyopo hairuhusu kabisa suala la kuwepo kwa Tume Huru?

Demokrasia itatoka wapi ikiwa Katiba iliyopo inatambua uwepo wa Utawala wa Kijamaa/ kikomunisti hapa nchini?

Kumbuka: Ujamaa/ukomunisti hasa ni udikteta, au uimla. Demokrasia na Ujamaa/ ukomunisti havikai pamoja na wala haviwezi kuishi katika nyumba moja, ni mwiko kabisa.

Aidha, Mtoto wa nyoka ni nyoka, kamwe nyoka hawezi kuzaa sungura.
Ngoja tuone
 
Ndugu yangu Allen Kilewella, hapo kwa Pascal Mayalla, unampigia mbuzi gitaa.

Ni Tanzania unapowapata watu waliopafata F masomo yote form four hivi leo ni PhD holders.
Na kwa sasa hawa ndio viongozi wakuu wa kitaifa wanaoitafuna nchi kwa urefu wa kamba zao!

Masikini waliopata distinction katika masomo yote form four, wengi wao ni malofa wa kutupwa.
Ndio hao hao wanaozurura na vyetu vyao mitaani na mwisho huishia kuendesha bajaj na boda!
Hahaha Allen anajisumbua tu
 
Ndugu yangu Allen Kilewella, hapo kwa Pascal Mayalla, unampigia mbuzi gitaa
mkuu Mag3 .., duh!
Ni Tanzania unapowapata watu waliopafata F masomo yote form four hivi leo ni PhD holders.
duh…!
Na kwa sasa hawa ndio viongozi wakuu wa kitaifa wanaoitafuna nchi kwa urefu wa kamba zao!
unamanisha hata nanilii alipiga mafagio?!.
Masikini waliopata distinction katika masomo yote form four, wengi wao ni malofa wa kutupwa.
Ndio hao hao wanaozurura na vyetu vyao mitaani na mwisho huishia kuendesha bajaj na boda!
dih…!
p
 
wamejenga Animal Farm mpya.
Animal farm!

Wale nguruwe waliweza kutamba sababu majority walikuwa kondoo wasiokuwa na uwezo wa kushughulisha ubongo wao.

Kuna mfanano wa kutisha na taifa letu; labda twaweza pia kujiuliza, tukifanikiwa kuwatoa hawa nguruwe tutapata unafuu?

Mabadiliko tunayolenga sharti yawe yenye maslahi na faida kwa mwananchi, na yasiongozwe na hawa wabinafsi wanaojiita wanasiasa.
 
Animal farm!

Wale nguruwe waliweza kutamba sababu majority walikuwa kondoo wasiokuwa na uwezo wa kushughulisha ubongo wao.

Kuna mfanano wa kutisha na taifa letu; labda twaweza pia kujiuliza, tukifanikiwa kuwatoa hawa nguruwe tutapata unafuu?

Mabadiliko tunayolenga sharti yawe yenye maslahi na faida kwa mwananchi, na yasiongozwe na hawa wabinafsi wanaojiita wanasiasa.
Tuliwaondoa watawala weupe kwa pamoja tukijua tutajenga taifa la asali na maziwa pasipo kujua kati yetu tunaowaamini ni waroho na wabinafsi kuliko wakoloni tuliowaondoa.
 
Back
Top Bottom