Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

..Muro nadhani ana tatizo na Tundu Lissu.

..statement ile ni ya Tanganyika Law Society na Tundu Lissu ni mjumbe tu.

..Jerry Muro anajitambulisha kama mtaalamu wa mawasiliano, lakini ameshindwa kuwasilisha hoja kulingana na viwango vya mwanataalum wa mawasiliano.

.."Professional communicator" hawezi kutoa taarifa huku akirusha vijembe "...TUNDU, TUNDUNI" au "AKILI NDONGO"

..muda wote wa andiko lake alikuwa amejificha, lakini mwisho ndiyo akafunua uhalisia wake kwa kumrushia kijembe Tundu Lissu.

..kwa hiyo utaona kabisa Jerry Muro yuko biased. Statement yake haikulenga kuwasaidia TLS bali kumshambulia Tundu Lissu.

..kosa lingine la Jerry Muro ni kuilaumu TLS kwa kutokugoma wakati wanachama wao maarufu walipouawa kutokana na mashambulizi ya kikatili. kwangu mimi hiyo siyo hoja. kama walikosea huko nyuma haimaanishi kwamba hawana uhalali wa kurekebisha makosa yao sasa hivi. Pia nyakati na mazingira ya matukio hutofautiana, na hivyo hati hatua wanazopendekeza TLS lazima zitatofautiana.
 
Jerry Muro ndio yule alikamatwaga kwa kula rushwa ya 10mil. au ni mwingine? Na ambaye alikuwa msemaji wa Yanga akafukuzwa!!?

Suala la Rushwa alisafishwa Kisheria hivyo hakuhusika nalo bali lilikuwa ni la ' Kichuki ' zaidi dhidi yake kutoka katika ' Mamlaka ' fulani nchini ambayo ilichukiwa Kitendo cha Muro kuwaonyesha wakichukuwa ' rushwa '. Kuhusu Yanga ambako alikuwa ni Msemaji wake wala hajafukuzwa kama ambavyo Wewe na wenzako wengine mnasema bali mkataba wake ulifikia mwisho na wakati huo huo Jerry Muro alikuwa ameshapata ' shavu ' jingine tena la maana huko SUMATRA ambako yupo hadi sasa ' akitiririka ' na ' kuserereka ' vyake tena kwa raha zake huku akila ' bata ' ambazo pengine angeendelea kuwa Yanga hadi leo angezisikia tu ' ndotoni '.

Mwisho ushauri wangu tu mzuri Kwako ili kuonyesha kwamba kweli Wewe ni Great Thinker wa JF basi siku zingine uwe unajikita katika ' mada ' husika iliyopo na siyo ' Kushadadia ' vitu vingine ambavyo vingepaswa ' vishadadiwe ' sana na akina Dada, Mama na Bibi zetu ila bahati mbaya sana ' vinashadadiwa ' na Dume zima. Unatutia mno wasiwasi Sisi ' Wadindaji ' wenzako Mkuu kama kweli Wewe ni mwenzetu.
 
Jerry umetumia maneno meengi kupinga na kumkosoa LISSU, lakini hatukuona pia ukitumia maneno meeengi kulaani shambulio kwenye ofisi za IMMA ADVOCATE..

Kwa huu uzi wako unamaanisha tukio la kulipuliwa ofisi za IMMA advocates ni sawa, lakini tamko alilolitoa LISSU ndio sio sawa. Kupitia uzi wako unataka kutuaminisha LISSU na IMMA advocates ni waasi wa TANZANIA na ndio chanzo cha umasikini Tanzania.

Kwa kukusaidia tu, IMMA advocates ni kampuni iliyosajiliwa kufanya kazi Tanzania kwa kifupi ina lesseni ya kuoperate Tanzania, pia LISSU ni Rais wa TLS aliyechaguliwa na members wa TLS na akienda kinyume atawajibishwa na TLS na sio JERRY MURO na bahati mbaya Muro sio member wa TLS na hazijui taratibu za TLS..

JERRY kama kweli ni mzalendo ungeandika uzi mrefu saaana na ikiwezekana kuuandamana peke yako kuishinikiza serikali kuwakamata, kuwafilisi wenye deep green na wanufaika wa deep green. Ni unafiki wa hali ya juu Mtanzania kuvimbisha misuli ya shingo dhidi ya LISSU eti kwa kigezo cha vita ya uchumi.
 
kila mtu anapo kuwa na mawazo yake yasijumuishwe kuwa ni mawazo ya wote... au kuya fananisha kwakuwa kila mtu kachambua kivyake... au kajieleza kivyake...

wewe ukiulizwa jina na yule hivyo hivyo... mtataja jina moja kuwa JUMA ABDUL... swali laweza kuwa moja majibu ni tofauti... na ndio maana kuna nyuzi za kilimo lakini kila mtu kaelezea yeye kwa namna yake
Sioni hoja inayopinga post zaidi ya madhambulizi ya kishabiki. Post nzuri leteni hoja zenye mashiko. Sisi tupo kwa kujifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
swali ambalo sijapata jibu ni kwa kua mtanzania wa kwanza kumiliki pingu acha na makandokando mengineyo
very true,
alikuwa nazo ukiacha nakandokando mengine. alikutwa nazo basi tu alipona kutokana na mapungufu ya wale nanihii wa serikali kule kwa pilato.
 
Kwa kumbukumbu zangu na kama sikosei,Jerry Muro hata uvamizi wa Bashite clouds aliutetea hadharani.

Si hivyo tu,hata Manji alipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya alionekana kuunga mkono kukamatwa kwake pale alipohojiwa channel 10 katika kipindi cha Mada Moto.

Huyo ndio Jerry.

U-DC unatafutwa kuputia migongo ya watu.
Tatizo anazo hoja unless ithibitike kiushahidi kuwa "polisi" walihusika.
 
Hapa ishu iko hivo, kwa wale wazee wa ufipa (chadema) hawatakuja na arguments yenye mashiko unless they will attack muro's personality! Hii ni kuonesha hawajakomaa kisiasa na wanamsujudia huyo lissu kama ndio msomi wa kwanza kutokea ndani ya CDM..that a big shame


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom