Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

Content yake unaionaje, acha kutafuta sababu za uvivu wa kusoma.
Kwenye keyboard ya computer kila button ina kazi yake, wacha kutetea ujinga, wewe ndio mvivu wa kufahamu. Binafsi siwezi hata kupoteza muda wangu na kujiumiza macho kusoma thread ya namna hii isiyokuwa na mpangilio.
 
Zimmeman ni great thinker, ili kumuelewa great thinker, na wewe ubongo wako lazima uwe na uwezo wa kuelwwa kwa kiwango hicho.

Kwa wale mliowahi kumsikia Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya kama kula nyama ya mtu!. Nje ya Muungano hakuna kitu kinachoitwa Zanzibar, nje ya muungano kuna Zanzibar na Pemba hivyo watawabagua Wapemba kuwa hawakushiriki mapinduzi!.

Wakishawafurusha Wapemba bado kutakuwa hakuna Wanzanzibari pure!, kuna Wanzanzibari na Wazanzibara, hapo sasa watawabagua Wanzibari wenye asili ya bara na kuwafurusha ili kutengeneza pure breed ya Sultan Said Said na kurejesha tena usultani!.

Baada ya hapo vitafuatia kulipizana visasi vya chinja chinja ya mapinduzi ya January 12!, mapinduzi yale hatimaye yatalaaniwa na Zanzibar kusheherekea tena uhuru wake wa December 4 mwaka 1963!.

Lissu has a point but it doesn't make sense!. Point ya Zimmeman really makes sense!.

Pasco.
 
Kwenye keyboard ya computer kila button ina kazi yake, wacha kutetea ujinga, wewe ndio mvivu wa kufahamu. Binafsi siwezi hata kupoteza muda wangu na kujiumiza macho kusoma thread ya namna hii isiyokuwa na mpangilio.
Mkuu Matola, its the contents that mater
and not impangilio!. Sio kila mtu anaweza kuwa Mzee Mwanakijiji!. The guy ni great thinker. Hoja ya Lissu ni " Hoja ya Nguvu" lakini hoja ya Zimmeman sio hoja ya nguvu ila ina "Nguvu za Hoja"!.

Kama mtu sio great thinker hawezi kutofautisha kati ya "Hoja ya Nguvu" na "Nguvu ya Hoja"!.
 
Nasisitiza kwamba dunia inawajibika kujifunza namna ya kuishi na waislamu na kuziheshimu taratibu hizo, hakuna haja ya ushindani kwenye hili, athari za kutofanya hivi zinaeleweka vizuri sana, hata wewe yaya unazitambua acha ubabe na ubinafsi.[/QUOTE]

Mkuu Sangarara, yawezekana uko sahihi kwa maoni yako.
Wasiwasi wangu au tatizo langu liko katika hiyo sentesi yako niliyoiwekea rangi nyekundu hapo juu.

Kwa nini dunia iwajibike kujifunza namna ya kuishi na waislamu na kuziheshimu taratibu zao na si vinginevyo, kwamba waislaam wawajibike kujifunza namna ya kuishi na watu wa dini zingine?

Ndiyo maana hapo awali katika mchango wangu Na. 14, nilisema kwamba kwa nchi zenye serikali zisizo na dini, sheria zinazotawala ni za serikali ambazo zimeridhiwa na dini zote, na watu wote.

Hivyo hakuna dini inayojiona ni bora ya nyingine kiasi cha wengine walazimike kuishi kama wanavyotaka wao.
 
Kwenye keyboard ya computer kila button ina kazi yake, wacha kutetea ujinga, wewe ndio mvivu wa kufahamu. Binafsi siwezi hata kupoteza muda wangu na kujiumiza macho kusoma thread ya namna hii isiyokuwa na mpangilio.
Kama ni hivi sidhani kama kuna watoto nchi hii madaftari yao yanakaguliwa na wazazi wao.
 
Ukweli ni kwamba lissu jana kachemsha yani hajui kama uhamsho ni magaidi? Haya mambo mi yananitia wasiwasi kabisa kwa maana ya jinsi ninavyomjua lissu alivyomsema ukweli pasipo kuogopa ila jana kaogopa screen! Nakumbuka kwenye hoja ya muungano bungeni lissu alichambua ukweli wote tena pasipo kuogopa lakini jana kaogopa kutetea wabara na wakristo waloonewa kule zenji na mpaka sasa wamefika wanasiasa 3 walojikanyaga kuhus hili akiwemo mtatiro na zitto'

Kwa hapa nchi yetu ilipofika huwa nakuwa mzito sana kuamini kila kinachoandikwa au kuongelewa na vyombo vya habari.

Tumeshuhudia michezo michafu mingi ikichezwa lengo likiwa ni kupotosha akili za watu, au kuzihamishia kwa muda katika kile mchezesha mchezo anachotaka kuaminisha (Kama michezo kama hii ilichezeshwa wakati wa uchaguzi Tabora na Arusha). Tuna hakika gani kama swala la uamsho na muungano si sehemu ya michezo hii?

Ushauri wangu, ni vizuri tuache kuwa biased na tufanye utafiti japo mdogo kuhusu upande wa pili kabla ya kuhukumu.

Hapo kwenye red, Hao wanasiasa watatu uliowataja siasa ni kazi yao ya kila siku. Wameshafanya utafiti na kujua kilicho nyuma ya pazia katika swala zima.

Kwa nini tuwapende na kuwaamini viongozi pale tu wanapozungumza yale ambayo masikio yetu yanapenda kusikia ???
 
Zimmeman ni great thinker, ili kumuelewa great thinker, na wewe ubongo wako lazima uwe na uwezo wa kuelwwa kwa kiwango hicho.

Kwa wale mliowahi kumsikia Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya kama kula nyama ya mtu!. Nje ya Muungano hakuna kitu kinachoitwa Zanzibar, nje ya muungano kuna Zanzibar na Pemba hivyo watawabagua Wapemba kuwa hawakushiriki mapinduzi!.

Wakishawafurusha Wapemba bado kutakuwa hakuna Wanzanzibari pure!, kuna Wanzanzibari na Wazanzibara, hapo sasa watawabagua Wanzibari wenye asili ya bara na kuwafurusha ili kutengeneza pure breed ya Sultan Said Said na kurejesha tena usultani!.

Baada ya hapo vitafuatia kulipizana visasi vya chinja chinja ya mapinduzi ya January 12!, mapinduzi yale hatimaye yatalaaniwa na Zanzibar kusheherekea tena uhuru wake wa December 4 mwaka 1963!.

Lissu has a point but it doesn't make sense!. Point ya Zimmeman really makes sense!.

Pasco.

na ww bado unarudia makosa ya Tundu lissu!?!
 
Tundu Lissu yupo sahihi 100%. Lissu kama mwanasiasa ameongea kile ambacho maadui zake kisiasa na wale wa CDM wanakiona kama kuruka kiunzi na kuwanyima nafasi ya kuosha vinywa na kuendeleza agenda ya kuitenga CDM na waislam. Sasa leo nimeona thread ingine inaanza kuhusisha kaulia ya 'Mpaka kieleweke' inayotumia na CDM na UAMSHO. Kwenye hili watakuwa kama wanaruka haja ndogo wanakanyaga haja kubwa, maana inakijenga CDM zaidi ya kukibomoa.

Kinachoendelea kuhusu UAMSHO ni kweli kabisa kinatokana na hasira za suppression of thoughts and ideas. Huwezi kuwapangia wananchi nini wajadili na nini wasijadili kwa sababu tu unaogopa kuwa matokeo yake yanaweza yasikupendeze wewe.
 
Huyo Lisu kuchemsha ni kawaida yake anafanya siasa kwa jazba anatafuta umaarufu kama wa Mh Zito au Mh Mbowe au Mh Dr Slaa kwa nguvu mara nyingi uropoka na kuteleza huyu jamaa hafai kuwa kiongozi mkubwa atatupeleka shimoni,wewe jiulize kuna mahusiano gani kutaka muungano ujadiliwe na kuchoma makanisa kwa nini wasichome misikiti au mali za serikali,

Hapo Tundu kachemsha sana tuongee ukweli tusiweke siasa manake kuna mijitu mingine itamtetea kwa sababu ni kiongozi wa chama chao ebu tuweke itikadi zetu kando tujadili ukweli wa jambo hili vinginevyo tukiwa tunajadili jambo kimtazamo wa kisiasa hatutafika ata kidogo,Mh Lisu katika hili kachemsha ata wachungaji na wananchi mbalimbali wamemshangaa!
 
J Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika. Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original.
Hizi vurugu nakubali kuwa zimegusa dini kweli kwa sababu ingekuwa ni msikiti umechomwa hadi sasa tungekua tunaongelea mengine, sema tu wakristu mungu kawakirimia roho ya kutokua na kisasi. Hebu fikiria tu kule Igunga yule DC alipovuliwa mtandio akasema amevuliwa HIJABU waislamu hawakutaka kuwaelewa chadema pale walipojitetea bali waliwaagiza waislamu wawanyime chadema kura. Ila natofautiana na wewe unapofananisha kikundi cha UAMSHO na vikundi vya KIGAIDI kwa sababu kikundi hiki kina USAJILI wa KISHERIA kutoka kwa SERIKALI tangu mwaka 2001. Labda tuilaumu serikali kwa kukipa usajili bila kuangalia mipaka na outcomes zake.
 
Jana usiku nimemsikiliza kwa makini mheshimiwa Tundu Lissu kwenye kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu mada iliyosema, Je kundi la Uamsho lipo juu ya sheria? Argument ya Lissu ilikuwa kwamba fujo zote za Uamsho kuchoma moto makanisa kule Zanzibar, zisitazamwe kidini bali ziaminike zaidi kuwa ni frustrations za kisiasa hasa hasa kuhusu Muungano kwamba serikali imewaminya watu kuzungumzia uwepo au kutokuwepo kwa Muungano, bali imewapa option ya kutoa maoni ya kuuboresha. Akakoleza chumvi zaidi bwana Lissu pale alipotoa mifano ya Kanisa la kwanza East Africa kujengwa Zanzibar, na kwamba kule Egypt Ukristo umekuwepo more than 2, 000 years (Coptic Church), na uko kote (Zanzibar na Egypt) Waislamu walio wengi wameishi pamoja kwa amani na Wakristo walio wachache. Kwa hiyo udini wa Waislamu kuwachukia Wakristo kutokana na imani yao hauwezi kuwa hoja halisi iliyosababisha mali za Wakristo kuharibiwa hivi karibuni na Waislamu huko Egypt na Zanzibar bali siasa ndo mshtakiwa wa kwanza. Kwa haraka haraka unaweza ukaaminishwa na hoja hii ya Lissu pamoja na ushawishi wake wa hoja hiyo. Pamoja na kwamba mimi binafsi namkubali Lissu lakini hapa kaonyesha udhaifu mkubwa. Ni kama vile bwana Lissu kapitiwa hivi na mambo yanayoendelea ulimwenguni kuhusiana na vikundi vya aina ya Uamsho kwenye nchi zingine. Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika. Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original. Vikundi vyote vya kigaidi hasa vile vinavyotumia uislam huwa vina jambo moja linaloviunganisha. Vyote ni fundamentalist kwenye theolojia yake na vinasukumwa na nia (kwao ni nia njema) ya kutaka kutakasa dini yao kutokana na hatari wanayohihisi kwamba nguvu za kisecular na kikiristo zinaikaba na wanataka kurudisha enzi zile za Uislam safi (sharia itawale serikali, “uchafu” wote kama bar, guest houses, na kadhalika usafishwe ili kurudisha imani halisi na iliyo safi). Al Qaeda kiliundwa baada ya Wamarekani kuweka bases zake za kijeshi Saudi Arabia ili kuipiga Iraq miaka ya 90, maana Osama bin Laden aliona ni aibu kwa nchi yake yenye makazi mawili matakatifu ya Allah (Mecca na Medina) kuweka bases za kijeshi, ishara ya kutawaliwa na Kafir mkuu, Marekani. Na kumbuka katika Uislamu siasa na dini haviwezi kutenganishwa, Lissu yampasa ajielimishe vizuri na theology ya Kiislamu. Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria. Uamsho ya Zanzibar ina vichembe hivyo hivyo vya kuhisi Zanzibar inaanza kukengeuka kutoka kwenye Uislam sahihi. Muungano unachukuliwa kama culprit wa kwanza aliyesababisha Zanzibar kujaa baa, vijiwe vya kiti moto, Makanisa ya Kikristo kila shehia ya Zanzibar, watoto wa kike wa kizanzibari kuanza kuvaa kama wabara, na megineyo mengi. Wale wote wanaotumia hoja ya kanisa la kwanza EA kujengwa Zanzibar, wanasahau kwamba enzi zile kanisa lilelilionekana kama siyo threat kwa utamaduni wa kiislamu, after all waliosali mule ni wazungu wawili watatu pamoja na weusi wachache. Kanisa lenyewe moja. Zanzibar ya sasa imebadilika sana siku za hivi karibuni. Makanisa yameongezeka sana na hili linawatisha Wazanzibari. Maredio mengi ya FM yameanzishwa na muziki wa bongo fleva unapigwa sana ikiwemo chombeza chombeza sex stories kwenye hizo redio. Hili linawakera sana mafundamentalists na wanaona pa kuanzia ni Muungano kuuvunja ili wapate control kamili ya kuendesha serikali kwa kanuni zisizofungamana kwa namna yoyote na katiba ya kisecular ya serikali ya Tanganyika. Lissu anaweza akawa na nia nzuri ya kutofungamanisha mainstream Islam na vurugu zinazojithibisha kidini. Lakini ukweli upo pale pale kwamba Uamsho na vikundi vinginevyo vilivyopo huko Zanzibar vipo motivated zaidi na dini. Tafsiri yao ya fundamentalist Islam ya kutotenganisha dini na serikali inaweza isiwe muafaka kwa wakati huu lakini hilo ndilo linalowasukuma. Kwao Uislam Zanzibar umeingiliwa na yapaswa kuusafisha. Kuvunja Muungano ni hatua ya kwanza, na kama wakifanikiwa hatua zingine zitafata.

Uelewa una angle na level tofatuti na hii inashamirishwa zaidi na "information gap" uelewa wa lissu na mleta mada unatofautiana.
 
Tundu Lissu yupo sahihi 100%. Lissu kama mwanasiasa ameongea kile ambacho maadui zake kisiasa na wale wa CDM wanakiona kama kuruka kiunzi na kuwanyima nafasi ya kuosha vinywa na kuendeleza agenda ya kuitenga CDM na waislam. Sasa leo nimeona thread ingine inaanza kuhusisha kaulia ya 'Mpaka kieleweke' inayotumia na CDM na UAMSHO. Kwenye hili watakuwa kama wanaruka haja ndogo wanakanyaga haja kubwa, maana inakijenga CDM zaidi ya kukibomoa.

Kinachoendelea kuhusu UAMSHO ni kweli kabisa kinatokana na hasira za suppression of thoughts and ideas. Huwezi kuwapangia wananchi nini wajadili na nini wasijadili kwa sababu tu unaogopa kuwa matokeo yake yanaweza yasikupendeze wewe.

Acha kuunga tu hoja bila kuitafakari unaunga tu hoja kwa sababu imesemwa na Lisu,kiongozi ndani ya chama chako , huo ni upofu wa mawazo fikra mgando,hujiulizi why wachome makanisa tu iweje wasichome misikiti, mali za serikali au wasichome vyote kwa pamoja? Acha upimbi amka tumia akili yako kuchanganua jambo angesema Mh Nape ungempinga ila tu kwa sababu kasema Mh Lisu unaunga tu mkono bila kuchanganua!
 
Kamwe Zanzibar hawataweza kujitenga na Bara labda Wamarekani walale.Wameshasoma mchezo mzima wanajua ni alshabab wengine watatoka kule.Ndo maana wakawahi mapema kwenda kule baada ya tukio lile kutokea
 
Ndugu mwandishi nitakuambia kitu,hawa magwanda wanatoa kalui kama hizo ili kujikomba kwa wazanzibari ili chama chao kipokelewe na wazanzibari,pia hawa viongozi wa cdm naona wanachizi,angalia kauli ya zito kuhusu vurugu hzo,then tundu lisu,yote ye yote waraka wa mbowe kwa kikwete yani pumba tupu.
 
Lissu yuko sahihi. Tatizo Zanzibar ni Muungano, na kwa muda mrefu serikali imekaa kimya badala ya kutatua kero za muungano. Watu waliochoma kanisa sio tu wamechoma kwa sababu za dini, ila wanaona kanisa kama 'symbol' ya muungano ambao kwao ni kero. Kama serikali ingekuwa makini na kushughulikia matatizo ya muungano hawa wachoma kanisa wangekosa 'kisingizio' cha kufanya walichofanya. Kwa sasa inakuwa vigumu kutenganisha mambo lakini kama tunataka kudeal na mzizi wa tatizo basi muungano lazimwa uangaliwe upya.
 
Huyo Lisu kuchemsha ni kawaida yake anafanya siasa kwa jazba anatafuta umaarufu kama wa Mh Zito au Mh Mbowe au Mh Dr Slaa kwa nguvu mara nyingi uropoka na kuteleza huyu jamaa hafai kuwa kiongozi mkubwa atatupeleka shimoni,wewe jiulize kuna mahusiano gani kutaka muungano ujadiliwe na kuchoma makanisa kwa nini wasichome misikiti au mali za serikali,hapo Tundu kachemsha sana tuongee ukweli tusiweke siasa manake kuna mijitu mingine itamtetea kwa sababu ni kiongozi wa chama chao ebu tuweke itikadi zetu kando tujadili ukweli wa jambo hili vinginevyo tukiwa tunajadili jambo kimtazamo wa kisiasa hatutafika ata kidogo,Mh Lisu katika hili kachemsha ata wachungaji na wananchi mbalimbali wamemshangaa!

sijaona mchango wako!
kuna propaganda nyingi sana zimepandikizwa kwenye hiki kikundi cha uamsho, wazanzibar sasa hivi wameshagundua kuwa wanasiasa wanawadanganya na sasa hivi wameamua kuwa wao kama wazanzibar (nawaunga mkono), nakumbuka mwaka jana wawakilishi wote wa zanzibar bungeni kutoka CUF na CCM walimponda sana lisu baada ya ile hotuba yake ya kuuponda ule mswaada na kuuhoji muungano, na wakati huo huo huko zanzibar kulikuwa na moto wakuukataa ule mswaada wa katiba wa mwanzo.. mpaka nikajiuliza hivi wazanzibar wanawasikia wabunge wao?
CUF na CCM wameshapoteza credibility kwa wazanzibar na msishangae kusikia mapinduzi ya pili ya zanzibar
 
Mkuu ni lazima tuishi maisha ya kuvumiliana na kujaliana kama tunadhamira ya kweli ya kuishi kwa amani na utulivu kwenye jamii zetu, wakirsto wanaelekezwa kwamba kama kula kwao nyama kuna mkwaza mtu mwingine basi na waache kuila hiyo nyama, wanaekekezwa kuwapenda jirani zao kama wanavyojipenda wao, na wanashauriwa kutokuwaudhi watu wengine, hii ni katika kuhakikisha kwamba jamii za kikirsto zinaishi kokote pale duniani bila kukorofishana na jamii zenye imani tofauti.

S

Nikiwa mdogo nyumbani, ilikuwa ni marufuku kula kuku ambaye hajachinjwa na muislamu, kwa sababu waislamu huchukulia kuku ambaye hajachinjwa na muislamu ni nyamafu na hastahiri kuliwa, sasa kama kweli mmeamua kuishi kidugu kumuachia muislamu achinje kuku kuna matatizo gani.
Nasisitiza kwamba dunia inawajibika kujifunza namna ya kuishi na waislamu na kuziheshimu taratibu hizo, hakuna haja ya ushindani kwenye hili, athari za kutofanya hivi zinaeleweka vizuri sana, hata wewe yaya unazitambua acha ubabe na ubinafsi.

Sikubaliani na hoja yako hata kidogo. Ili watu waweze kuishi katika jamii moja jambo la msingi sio kufuata matakwa au imani ya mtu mwingine ili uweze kukaa naye kwa amani. ukishafanya hivyo tayari umekuwa "MTUMWA"
Jambo la kuzingatia ni kuheshimu uhuru wa mtu mwingine. Mwana falsafa mmoja alisema kuwa "katika msongamano wa watu mwisho wa uhuru wako ni pale linapoanzia bega la mwenzako" Tafsiri yake ni kuwa katika jamii inayoheshimu uhuru wa watu uhuru wako wa kufanya mambo ni kwa kiwango kile tu ambacho hutamuathiri jirani yako.
Kwa hiyo basi tukisema kuwa ili tuishi nao ni lazima tukubaliane na matakwa yao ni dhahiri kuwa tutakuwa watumwa wao. wewe unasema kuwa kwenu mmekubaliana kuku lazima achinjwe kiislamu ili kuwaridhisha, ni sawa ila ukumbuke halitaishia hapo.
- kesho watasema lazima mavazi uvae kwa mujibu wa dini ya kiislamu utakubali?
-Halafu mkikubali watakuja na hili; bar, guest house nk zivunjwe kwa kuwa haziendani na imani yao. tukikubali watasema sheria za nchi hazifai bali sharia za kiislam ndio zifuatwe na watu wote hili ni pamoja na kufanya mashauri yote (ya waislamu na wasio waislamu) kwenye mahakama ya kadhi ili tuweze kukaa nao kwa amani
Mwisho watasema hata raisi lazima awe shehe maana kwa mujibu imani yao hawawezi kutawaliwa na kafri.

Mimi nafikiri uhuru wa kiraia ni muhimu zaidi, kila mtu afanye mambo yake ili mradi asifunje sheria ya nchi ambayo inatuunganisha wote na sheria hii ilinde haki na uhuru wa kila mmoja bila kujali imani.
 
Hivi Ugaidi maana yake nini??

Who coined the word 'ugaidi'??

Hivi kweli muungano wetu ni 'SACRED' au ni dogmatism za wanasiasa wanaofaidika kisiasa na ki maslahi na Muungano huu??

Kwa nini suala hili lilipelekwa kwa hati ya dharula bungeni tena jumapili na j3 ikatangazwa Muungano??

Kwa nini Serikali iwaamulie wananchi suala la kujadili na namna gani ya kujadili, hivi sisi wanadamu ni mahayawani na hatuna haki ya kukubali au kukataa??

Kwa nini Mwanasheria kutoka kituo cha Sheria na haki za binadamu alikuwa na kigugumizi sana ili hali akikili kuwa hata katika zile aina mbili za miunngano tunazojifunza darasani yani fed na uni muungano huu haupo hata kati ya hizo mbili??

Hoja tuangalie sababu ya kwa nini Nyerere na Karume waliridhia kama bado ziko valid hadi sasa ni mufilisi kwani hakuna anayefahamu ni sababu zipi zilipelekea muungano kuwepo!

Nadhani kwa kuwa sisi ni wanafiki sana basi tuendelee na unafiki wetu na tujadili kuuboresha Muungano!


Kama muungano huu ungekuwa ulitokana na misingi imara,na serikali ingekuwa makini kuboresha na kurekebisha kasoro za muungano wananchi wa tanzania pengine wasingekuwa na mengi ya kuhoji juu ya muungano.Muungano huu ni bubu,maswali mengi hayana majibu.na serikali ya magamba badala ya kutafuta majibu na kutatua matatizo ya muungano kwa meza ya majadiliano,wameazimia kudumisha muungano kwa kuwafunga mdomo wananchi,hawaelewi kwamba kujaribu kuwafunga mdomo wananchi ni kuwaambia,huu muungano hauwahusu,unatuhusu sisi wenye kunufainika nao,hivyo fungeni midomo yenu maana utakuwepo tu mtake msitake.Hongera Lissu kwa kuepuka mtego wa magamba wa kuonekana una chuki na uislamu maana ule wimbo wao wa ukristo wa chadema wangeanza kuuimba tena kwa kutumia maneno yako.magamba kwishnei
 
lisuu ypo sahihi kabisa na wasipo wapo zanzibar yao ipo siku uamsho litakuwa kundi la kigaidi,tatizo serikali ya ccm haiwezi kuona jambo bila ya mashinikizo,suluhisho hapo ni muungano tu kuvunjwa.
 
Acha kuunga tu hoja bila kuitafakari unaunga tu hoja kwa sababu imesemwa na Lisu,kiongozi ndani ya chama chako , huo ni upofu wa mawazo fikra mgando,hujiulizi why wachome makanisa tu iweje wasichome misikiti, mali za serikali au wasichome vyote kwa pamoja? Acha upimbi amka tumia akili yako kuchanganua jambo angesema Mh Nape ungempinga ila tu kwa sababu kasema Mh Lisu unaunga tu mkono bila kuchanganua!

Rafiki yangu panadol hunijui sikujui, JF huwa tunaongea kwa hoja ukitaka kuanza kuipima akili yangu, utashangaa kujikuta kuwa akili zako zote ulizo nazo ni sawa na 0.005% ya akili zangu. Naomba usinihusishe na Chama cha siasa mimi sina kadi ya CDM hivyo huwezi kusema ni chama changu, chama mimi ni 'Tanzania iliyo isiyokuwa na rushwa' maana ndiyo adui namba moja wa maendeleo. CDM ni chama ambacho kilichoweza kunishawishi kuwa kinaweza kabisa kuungana na chama changu (ie Tanzania isiyo na rushwa na inayoangalia wananchi kwanza kabla ya viongozi).

Kama wewe unaona kuchomwa makanisa ni kigezo ambacho kinaweza kumfanya Lissu awalaani waislam utakuwa umekosea sana, maana uislam haufundishi uharibifu wa mali zisizo za waislam. Wewe una uhakika gani kuwa waliochoma ni waislam?, je kesho na kesho kutwa polisi wakimkata mtu asiyekuwa muislam kuwa amechoma kanisa hilo utakubali au utakataa?. Siungi mkono uharibifu wa mali mali ziwe za kanisa au za synagogue au za msikiti. Jumping into conclusion inaonesha dhahiri kuwa wewe una 'Prejudices' na uislam na waislam na ungependa sana kila mtu aongee unavyofikiria wewe ndiyo awe sahihi, hiyo ni 'myopia' ya hali ya juu sana.

Changia hoja acha personal attacks!
 
Back
Top Bottom