Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,116
Aida Khenan mbunge mteule wa Nkasi amesema, yeye ni mbunge pekee aliyetangazwa na katika mkoa wake amepata madiwani 10.
Lakini amesema amesikia kwenye mitandao kuhusu msimamo wa chama chake lakini yeye hajapewa taarifa rasmi eidha ya simu au barua, anadai anaamini chama chake ni taasisi kubwa hivyo anategemea atapewa taarifa rasmi.
Amesema jimboni kwake na mkoani kwake mpaka sasa kuna taharuki kubwa, wananchi wana taharuki kubwa.
Amesema mpaka sasa ametishiwa maisha na wananchi kwa kuwa wao waliamua kuvunja rekodi ya kutoa Mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza hivyo wanadai yeye akifuata msimamo wa chama atakuwa kawasaliti wananchi ambao wapo walioumia ili yeye ashinde, pia amesema kuna kesi kama 18 za watu waliokamatwa walipokuwa wanapigania yeye ashinde.
Amedai wananchi wanamwambia kuwa machozi yao hayawezi kwenda bure asipokwenda kuwatumikia bora maisha yake wananchi wayamalize hapo.
Amedai kuwa anaomba chama chake warudie upya kutazama maamuzi yao, na kama waliyatoa kwa jazba kulingana na yaliyotekea kwenye uchaguzi basi waangalie upya na waelewe kuwa yeye hana amani anatishiwa maisha na amedai hawezi kuhama Rukwa na hawezi kuhama Nkasi.
Amedai kuwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lao wamepata Mbunge mwanamke na Mbunge wa kutoka upinzani hivyo asipokwenda kuwawakilisha wananchi madhara yake ni makubwa sana kwake aidha hata kama viongozi wake hawatayaona.
Amesema alisharipoti Polisi kuhusu kutishiwa maisha na pia msimamo huo si wake peke yake bali ni wake na viongozi wa mkoa wa chama cha CHADEMA.
Amesema katika ngazi ya taifa hakuna kiongozi yeyote aliyemtafuta hata kwa simu aweze kujua amani yake au usalama wake.
Amedai kuwa alipoomba nafasi ya Ubunge aliomba peke yake na wala hawakuomba 2 wala 3 hivyo atakwenda bungeni kama yeye Aida na atakwenda kuwasilisha sauti yake yeye peke yake kwa niaba ya wananchi wa Nkasi japo atakuwa mpweke ndani ya bunge. Anasema alipokuwa mbunge wa viti maalum alijifunza kutoka kwa wabunge waliomtangulia lakini kama wabunge wa Viti Maalum watakwenda kipindi hiki atapata faraja lakini wasipokwenda itakuwa mpweke lakini faraja atapata kwa wananchi waliomchagua anaowawakilisha.
Tundu Lissu nae anena haya Tundu Lissu anena kuwa, keshokutwa watakaa kamati kuu na ndio itatoa msimamo wa jumla wa chama, msimamo ambao waliusema wiki iliopita ni msimamo wa viongozi wakuu wa chama, lakini lazima kamati kuu itoe baraka zake au ikatae kutoa baraka zake.
Tundu Lissu amedai kuwa wao hawakua na wajibu wa kuuliza yeye Aida anafikiriaje kwa kuwa wao viongozi wakuu wana majukumu mengine ndani ya chama, amedai kuwa wao walitoa msimamo wao kuwa huo haukuwa uchaguzi.
Amedai kuwa kama chama kikisema kuwa huo ndio msimamo wa chama basi itabidi atafute utaratibu mwingine wa kuwatumikia wananchi wa Nkasi kwa kuwa Tanzania hakuna mbunge binafsi bali ni wabunge wa chama hivyo wabunge ni lazima wafuate utaratibu wa chama.
Lakini amesema amesikia kwenye mitandao kuhusu msimamo wa chama chake lakini yeye hajapewa taarifa rasmi eidha ya simu au barua, anadai anaamini chama chake ni taasisi kubwa hivyo anategemea atapewa taarifa rasmi.
Amesema jimboni kwake na mkoani kwake mpaka sasa kuna taharuki kubwa, wananchi wana taharuki kubwa.
Amesema mpaka sasa ametishiwa maisha na wananchi kwa kuwa wao waliamua kuvunja rekodi ya kutoa Mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza hivyo wanadai yeye akifuata msimamo wa chama atakuwa kawasaliti wananchi ambao wapo walioumia ili yeye ashinde, pia amesema kuna kesi kama 18 za watu waliokamatwa walipokuwa wanapigania yeye ashinde.
Amedai wananchi wanamwambia kuwa machozi yao hayawezi kwenda bure asipokwenda kuwatumikia bora maisha yake wananchi wayamalize hapo.
Amedai kuwa anaomba chama chake warudie upya kutazama maamuzi yao, na kama waliyatoa kwa jazba kulingana na yaliyotekea kwenye uchaguzi basi waangalie upya na waelewe kuwa yeye hana amani anatishiwa maisha na amedai hawezi kuhama Rukwa na hawezi kuhama Nkasi.
Amedai kuwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lao wamepata Mbunge mwanamke na Mbunge wa kutoka upinzani hivyo asipokwenda kuwawakilisha wananchi madhara yake ni makubwa sana kwake aidha hata kama viongozi wake hawatayaona.
Amesema alisharipoti Polisi kuhusu kutishiwa maisha na pia msimamo huo si wake peke yake bali ni wake na viongozi wa mkoa wa chama cha CHADEMA.
Amesema katika ngazi ya taifa hakuna kiongozi yeyote aliyemtafuta hata kwa simu aweze kujua amani yake au usalama wake.
Amedai kuwa alipoomba nafasi ya Ubunge aliomba peke yake na wala hawakuomba 2 wala 3 hivyo atakwenda bungeni kama yeye Aida na atakwenda kuwasilisha sauti yake yeye peke yake kwa niaba ya wananchi wa Nkasi japo atakuwa mpweke ndani ya bunge. Anasema alipokuwa mbunge wa viti maalum alijifunza kutoka kwa wabunge waliomtangulia lakini kama wabunge wa Viti Maalum watakwenda kipindi hiki atapata faraja lakini wasipokwenda itakuwa mpweke lakini faraja atapata kwa wananchi waliomchagua anaowawakilisha.
Tundu Lissu nae anena haya