Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hawezi kuwa Rais kwasababu hizi

Philipo Mwakibinga

Senior Member
May 13, 2013
111
175
Hii ni kwasababu kwanza bado hajajua achague kipi kati ya kuendelea kuwa Mwanaharakati au Kujiandaa kuwa Kiongozi. Hali hii imemfanya afanye harakati sana hata anapokuwa kiongozi. Nivyema akabaki kuwa Mwanaharakati tu kwasababu huwezi kuwa Mwanaharakati halafu kiongozi hakuna kabisa kwenye ulimwengu wa siasa.

Hana rekodi yoyote ya Uongozi Bora. Lissu amekuwa mpambanaji kwa muda wote na siyo kiongozi. Sifa ya Mpambanaji anaweza kuambania hata yasiyo ya msingi au yale yalomsingi. Lissu kwa muda mrefu kazi yake kubwa ni kuambania hata ujinga tu ilimradi yeye unamfaa. Kuna wakati alipewa nafasi ya kuwa Kiongozi wa ngazi ya Juu wa TLS chama cha Wanasheria Tanzania lakini hakuna alichofanya au kuifanyia taasisi hiyo zaidi akajaribu kukigeuza kuwa chombo cha kiharakati japo hakufanikiwa.

Alishavuliwa uenyekiti wa kanda ya Kati yenye mikoa ya Singida, Morogoro na Dodoma (CHADEMA )baada ya kanda hizo kushindwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Mwaka 2014. Mbowe alimvua Lissu mbele ya Wajumbe wengi kwasababu ya kushindwa Uongozi. Mtu aliyeshindwa kuongoza mikoa mitatu yenye wanachama laki moja jumla yake tena kwa ngazi ya Chama kidogo cha siasa siyokweli kama anaweza kuongoza Taifa kumwa lenye watu zaidi ya Milioni 50.

Chuki fitina na visasi. Lissu nimtu wa visasi na chuki. Ndiyo maana anatumia jambo lake binafsi la kuumizwa kama vita ya Watanzania wote. Lazima tufahamu kuwa siyo wote wanapenda tabia hii maana ukweli wa tukio lile yeye ni shahidi namba moja ndiyo maana hadi leo hataki Dereva wake aonekane hadharani.

Mvunjaji mkubwa wa sheria. Lissu ni muumini wa kufanya mambo bora liende tu na siyo mtu makini. Mfano mzuri ni hiki kipindi cha kampeni za uchaguzi. Kaamua kuvinja sheria makusudi tena alizozisaini yeye mwenyewe,hatimaye kawekwa kifungoni kwa siku 7. Kwa mtu makini hawezi kufanya utoto huu kwani angepaswa kujua ukubwa wa Nchi na muda wa kufanya kampeni.
Lissu aendelee kuwa Mwanaharakati na siyo kiongozi.
 
Kuichagua CCM ni kutaka mambo mabaya yaendelee;

Mambo kama ya ukatili,mauaji, kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, na kutakatisha fedha.

Kuweka watu mahabusu ambao hawana hatia nk.

Tukumbuke kuna Mungu ipo siku atatuuliza tuliwajibika vipi kuzuia hayo mambo mabaya ya CCM, mimi nitamjibu sikuichagua CCM.

CCM ni shetani tuikatae CCM na mambo yake yote.
 
Mbona sumaye aliomba akapata kura 2 bila kumsahau Cecilia Mwambe je walifanywa nini?
Na membe alipotaka kumchalange jiwe ilikuwaje?
Mbona sumaye aliomba akapata kura 2 bila kumsahau Cecilia Mwambe je walifanywa nini?
Na membe alipotaka kumchalange jiwe ilikuwaje?
Sumaye alitaka uenyekiti akapigwa ban mpaka uenyekiti wa kanda Mbowe si mchezo akaambiwa sumu haionjwi.
 
Lissu baada ya uchaguzi atakuwa hana kazi ya kufanya, siasa itapigwa marufuku mpaka uchaguzi ujao, na kesi zitakuwa zinamuandama. Mbowe atamfanyia zengwe mpaka ataonekana hafai ndani ya Chadema.

Sijui itakiwaje Mungu wangu, ewe Muumba mjalie Lissu atakapopatwa na mambo haya magumu arudi CCM ili apate msamaha wako kwa kuisaliti nchi yetu.
 
.
Lissu aendelee kuwa Mwanaharakati na siyo kiongozi.
Mwakibinga ni wewe ndio ulikua UDOM? Aisee sitaki kuamini umekua hivi? Kipindi kile tulikuona ndio future ya CHADEMA leo hii unaishia kudhihaki watu bila hoja.

Unatia huruma sana, ulikimbilia ACT ukidhani maarufu kuliko CHADEMA ukaambulia kura ngapi? Leo hii hamna anayekujua hta uteuzi hujapata. Unatia sana huruma. Tamaa ziliua ur political future.

Ulipaswa uwe unaandika mada za jinsi ya kutatua kero za vijana, au mabadiliko sera ya uwekezaji n.k ila unaishia kuwa propagandists wa kutumika tu!!

Aisee bado siamini
 
Back
Top Bottom