Tundu Lissu atangaza rasmi Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
ZITTO NJIAPANDA
1.Kukata rufaa: Anaweza kukata rufaa mahakamani ili aendelee na ubunge na kukamilisha ratiba ya PAC ya kusikiliza ripoti ya Tanesco (leo), BoT na TRA (kesho) na majumuisho (Ijumaa) kabla ya kwenda bungeni Jumatatu.
2. Chama kipya: Zitto anaweza kuamua kwenda moja kwa moja katika chama kipya ambacho amekuwa akitajwa kukiasisi cha ACT. Taarifa za kuaminika ni kuwa alipanga kuaga na kutoka bungeni Machi 18.
SOURCE MWNANCHI
 
"Chadema itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa mujibu wa Katiba, si mahakamani.Asiyefuata atafukuzwa uanachama." Wakili Tundu Lissu
‪#‎TunduLissu‬

11034229_10153114163364339_2906182317196896366_n.jpg
 
“Hakuna kitu kibaya kama siasa za kulipizana visasi, unaweza kukuta hata wale walioko madarakani hawana uhakika na wanaotaka kuja, kwamba hili litaendelea bila kulipizana visasi… Dhambi ya kulipiza visasi, majungu, fitna na uvivu wa kutofikiria, dhambi ya ubaguzi.. Tanzania yetu leo hii ni ipi?, hatuna itikadi, akiingia huyu ataendelea na pale mwenzake alipoishia”
Niombe watanzania kwa moyo wa unyeyekevu kutika ndani ya sakafu ya moyo wangu wachague viongozi was iona mlolongo wa sifa nyingi, ziwe nne tu ya kwanza awe mwenye uwezo,
pili mcha MUNGU,
tatu awe mkweli.. aseme ukweli na si kutumia jukwaa la siasa kinyume, na nne mwenye kuchukia ufisadi…“

JAMES MBATIA
 
Tundu lisu ni msukule tu maagizo ya kumfukuza zitto yametoka kwa mwenye chama chake mtei na vijana wake mbowe na lema
 
Katika huo uzi aliounzisha hapa wanachama mbali mbali walitaka aweke bayana matendo aliyoyafanya ambao aliyaona hayakuwa sawa, hakujibu hili wengine walimuuliza kuhusu mawasiliano yake mbali mbali na watu ndani ya MACCM na Serikali miezi michache kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2010 ikiwemo mawasiliano yake na Roastam Aziz akalikwepa swali kiaina na hata kudai namba ya simu iliyotumika katika mawasiliano pamoja na kuwa ni yake lakini aliacha kutumia namba hiyo miezi mingi. Kulikuwa na swali je namba hiyo alimruhusu mtu mwingine aitumie? Na kama alimruhusu mtu mwingine aitumie ni nani huyo!? Hakujibu swali.

Hivi kuna Ubaya gani mwanasiasa wa Upinzani kuwa na mawasiliano na wanasiasa wa chama tawala? Je unaamini ni Zitto pekee mwenye Mawasiliano na wanasiasa wa chama tawala?
 
Inaleta picha ipi pale kiongozi wa chama anapoamua kuja JF (hadharani) kuwaomba samahani wanachama wa chama chake kwa matendo yake ambayo yalipunguza/kuvuruga mshikamano ndani ya chama na kisha kukwepa kujibu maswali muhimu kuhusu baadhi ya matendo yake na baadaye kutaka uzi ule aliouanzisha ufutwe!? Kama unawasiliana na wanasiasa wa chama tawala kwanini ufanye hivyo kwa kificho? Kwanini upate kigugumizi unapoulizwa "mlikuwa mnaongea kuhusu nini" na fulani!?

Hivi kuna Ubaya gani mwanasiasa wa Upinzani kuwa na mawasiliano na wanasiasa wa chama tawala? Je unaamini ni Zitto pekee mwenye Mawasiliano na wanasiasa wa chama tawala?
 
Kila nikilitafakari suala la aliyekuwa Mbunge nguli kijana toka Kigoma naishia kukumbuka kile kisa cha kiimani cha ibilisi kutupwa toka mbinguni mpk kuzimu. Ibili huyo aliyejulikana kama Lucifer hapo kabla alikuwa ni kiongozi mashuhuri ktk jeshi la kumlaki Mungu kule Mbinguni, alikuwa ni hodari sana ktk uongozi wake.. Maandiko yanaendelea kutujuza kuwa ilifika wakati huyu bwana lucifer akavimba kichwa na kujiona yeye ndio yeye.. akawa haambiliki na ikafika wakati akaamua kumdharau hata aliye MKUU kwake ambaye ndiye alimpa nafasi hiyo adimu iliyomuweka kwenye ramani ya uhodari. Ilifika pahala ibilisi/ lucifer akaanza mkakati wa kumpindua MKUU, basi baada ya MKUU kuona ibilisi haambiliki tena akaamua kumtupa kuzimu kule ambako amepangiwa kuja kukutana na ule moto wa milele pamoja na waongofu wenzake.

Mwisho wa TAFAKARI.. **
 
Hii ndio thima ya kisa chenyewe mwanzo mwisho. Asante mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom