Tundu Lissu aponda safari ya Lowassa ya Matumaini adai ni safari ya matumizi

Huyu jamaa atakuwa alikuwa ametokea kwenye ile hospital yake ya hapo dodoma ndiyo maana anazungumza ubwabwa tu porojo nyingi kichwani kavurugwa.
 
yaani umethibitisha kabisa wewe ni mwanachama wa ccm,kwa kawaida huwa hakuna mwenye hoja,huwa wanaropokaga tu na kushangiliana.
Kama wewe ulivyoonesha kuwa wewe ni bavicha au bawacha maana bawacha na bavicha kazi yao ni kupiga kelele na kulalamika.
 
Kwani anatumia hela za Serikali kuzunguka huko?
Saa nyingine viongozi wa chadema wanakosa hoja kabisa
 
Tatizo Tundulisu anaropoka huwa , hafikrii kabla ya kusema....
Wewe usiyeropoka tueleze! Kuna nini cha UWONGO katika mada hiyo ambacho hakiwezi kuthibitishwa leo hii? Tumia vizuri akili yako na siyo kuleta Mihemuko. Mpuuzi usiyejitambua wewe.
 
1. Yaani kuwepo Musoma tu imetosha kujua mikakati ya kambi hiyo???!
2. Uliuliza wangapi kati ya waliokuwepo??!!
3. Majibu yao uliyapimaje kupata validity na reliability??!!
4. Mtu anayependwa unawezaje ku establish sababu za mapenzi hayo??!!

Hebu fafanua mkuu yaweza kuwa una hoja

Nitakujibu Badae niko na mkuu wa nchi Mwanza kwenye ufunguzi wa umiseta Taifa.......... kwa kazi yangu ulinilazimu kufika na msm ninajua ninachokisema.
 
Ningeshangaa sana kama angeikubali Safari hiyo ya Matumaini. Nimebahatika kuwa Musoma wakati amekuja na safari yake ya matumaini ki ukweli tuwe wa kweli Lowassa ametokea kupendwa na wananchi nimeamini habari kuwa anagawa pesa watu wajitokeze ni Uongo wa mchana.

Unajua alichopewa na huyu hapa chini? Kamata mmoja wa vijana waliokusanyika kumfata Lowasa kwa makundi halafu muulize unamfahamu Lowasa? Utashangaa atakujibu "NDIO NANI?"
Huyu jamaa ni kiboko na inahisiwa anatumia nguvu fulani isiyo ya kawaida, ila mwishowe sio mwema.
View attachment 258858
 
Ningeshangaa sana kama angeikubali Safari hiyo ya Matumaini. Nimebahatika kuwa Musoma wakati amekuja na safari yake ya matumaini ki ukweli tuwe wa kweli Lowassa ametokea kupendwa na wananchi nimeamini habari kuwa anagawa pesa watu wajitokeze ni Uongo wa mchana.

Anapendwa kwa kuhonga tu!
 
Nyie wenye mlolongo wa wagombea mnaanza kuchuja lini?
Majembe hayachujwi yote yanafanya kazi.
Subiri uone.
 
Ya lowasa ni ya wanaccm yeye yanamuhusu nini? Tunasubiri watia nia wa ukawa.
 
Lowasa hapendwi! Bali huwa ana andaa mazingira ya watu kuhudhuria mikutano yake.

Mfano: Posho, magari ya kusomba watu na bodaboda wote hupewa mafuta.

Watanzania wa sasa ni wahudhuriaji wa mikutano yoyote ile hata iwe ya nani (Rejea mikutano ya ACT- hata kama hawakipendi).

Vijana walio wengi kwa sasa wako UKAWA/CDM. Mkubali au mkatae.
 
Kumpitisha lowasa na ukiangalia jinsi alivyoanza kutengeneza mtandao wa kuungwa mkono na makundi mbalimbali kwa kutumia pesa ni dhahili kbs taifa hili litakuwa limedondoka maana sasa ndio utakuwa ndio mtindo utakao kuwa ukitumika ktk taifa hili kwa kila mwenye ndoto za kuwa Rais wa nchi, hatutapata kiongozi bora , hatupata kiongozi mwenye nia thabiti wa kujalia maslahi ya wengi maskini, ni bora hata mara 100 upinzani ukachukua nchi kuliko kumwacha lowasa awe Rais wa nchi hii kwa kigezo cha kukubalika.
 
Ningeshangaa sana kama angeikubali Safari hiyo ya Matumaini. Nimebahatika kuwa Musoma wakati amekuja na safari yake ya matumaini ki ukweli tuwe wa kweli Lowassa ametokea kupendwa na wananchi nimeamini habari kuwa anagawa pesa watu wajitokeze ni Uongo wa mchana.

Watu wanapenda hela ya Lowasa wala hawana mpango naye.
 
Wafuasi wao hawaoni hilo. . . . . Hawahoji lolote. . . . Na ukihoji utatukanwa. . . . .

Hakuna Mtu Asie Safili Kabisa Hoja Ni Anasafili Anaenda Wapi! Na Kufanya Nini! Sio Mtu Unaenda Jamaica Kufuata Bembea Tu, Au Unaenda Amelica Kupiga Picha Na Boys 2men, Unaenda Amelica Kubadilishana Madini Na Mmbunet, Na Mkumbuke Sasa Hivi Tuko Kusaka Uhulu, Na Waendesha Mashtaka Yoyote Ya Uvunjifu Wa Amani Wako Ulaya Lazima Mzee Ajipange Jins Ya Kuwapeleka Wakina Pinda The Icc Kwa Kauli Zao Za Wapigwe Tu.
 
Lissu-28April2015.jpg

MWANASIASA Machachari na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni,Tundu Lissu, ameponda Safari ya Matumaini ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, akidai si ya Matumaini, ni ya Matumizi.

Lissu alisema hayo jana katika Mkutano wa Hadhara alioufanya mkoani Dodoma katika Viwanja vya Barafu, ambapo pia alidai Watawala hao hawana uwezo tena wa kutawala kama kwanza.

Akiainisha Ishara za Watawala kushindwa kuongoza mbele ya Umati wa Wakazi wa Dodoma, Lissu alisema kuwa ni pamoja na Migogoro na Migomo kila Kona, ambapo Wafanyabiashara, Madereva, Wanavyuo, Walimu, Wakulima na Wauguzi na Madaktari, safari hii waliiasi Serikali ya CCM.

Lissu ambaye alikuwa akihamasisha kujiandikisha katika Daftari la Kuduma la Kura, aliwakumbusha Wananchi akisema, mmewasikia wasaka Urais wa CCM wanaotoka Chama kimoja wanavyotofautiana kwa Kauli Mbiu, kila mmoja ana yake! Mkiona hayo, Ukombozi umefika.

“Lowassa amesema, ana Safari ya Matumaini; Safari hiyo si safari ya Matumaini ila ni Safari ya Matumizi, …Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba, amesema, tutavushwa Ng’ambo, wengine acheni jamani…Watu wanasema, ‘Ukimwamsha aliyelala Utalala Mwenyewe”.alisema Lissu na wananchi wakshaangilia na kucheka.

Lissu alijinasifu akisema, Dhambi kubwa kuliko zote ambayo Watawala wa nchi hii wamewafanyia Watanzania, ni kuifanya nchi yetu kuwa Nchi ya watu Ombaomba, na ndiyo maana nimemsikia Mgombea Urais wa CCM, Makongoro Nyerere, akijinadi ‘tusiwape nchi hii Vibaka’.

Alisema, “Rais Jakaya Kikwete, anaomba, Mawaziri wake wanaomba, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi Wanaomba, Wakuu wa Mikoa wanaomba, Wakuu wa Wilaya wanaomba, na Polisi nao wanaomba!! Jambo hili ni aibu kwa Taifa.

Lissu alidai; Taifa hili limechafuka sana kwa Uovu ukiwemo, Wizi, Rushwa, Ufisadi na Mauaji ya Kutisha yanayomwaga Damu za Watanzania, hivyo linatakiwa kusafishwa… na njia pekee ni kujiandisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura, ili 25/10/2015, mtumie haki yenu.

Hata hivyo, Lissu alijigamba kwamba, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamejipanga vizuri kuchukua Dola, na ndiyo maana walitoka nje wakipinga Katiba na inayopendekezwa na kura ya maoni, kwamba isingewezekana Aprili 30, sasa nani Mkweli?.alihoji.

Posted by
Chadema Blogtz

Mbona sasa safari ya Matumizi imehamia CDM? Ikiwa CCM ni ya Matumizi, ikiwa CDM ni ya matumaini. Mwaka huu watanzania akilizenu zitachezewa mpaka basi...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom