Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,256
- 219,479
Hii ndio Taarifa ya leo kwenda kwa Kasheku Musukuma na wengine wote wenye akili kama Yake, Mpaka muda huu Tundu Lissu kwenye ziara yake huko kanda ya ziwa, ametembelea na kuomba dua Maalum kwenye makaburi ya Magwiji wawili wa ukanda huo, Balozi Kasanga Tumbo kama mnavyoona pichani.
Na kaburi lingine alilotembelea ni la Alphonce Mawazo, ambaye aliuawa kikatili na watu wanaofahamika kama mnavyoona pichani.
Tundu Lissu hana mpango wowote wa kutembelea kaburi la Magufuli ambaye amemtuhumu kwamba alituma watu wamuue.
Akihutubia Mkutano wa hadhara wiki iliyopita huko Chato Lissu bila kumung'unya maneno na huku akishangiliwa na wananchi alitamka wazi hadharani kwamba John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania alituma watu wamuue na akamwagiza Job Ndugai aliyekuwa Spika wa bunge ahakikishe kwamba baada ya Lissu kuuawa Uchunguzi usifanyike na azikwe haraka kwao Ikungi.
Hotuba ya kusomwa kwenye mazishi yake ilishaandaliwa na Bunge (Habari za mkutano huu wa Lissu zimo humu jf).
Kwa namna yoyote ile hakuna mtu awezaye kutembelea kaburi la mtu katiri kama huyu aliyetaka kumuua (Shetani hana rafiki).
Tukiacha watu kama Musukuma waendelee kupotosha umma ili kutafuta kiki tutakuwa wajinga sana, ni lazima wajibiwe kwa kauli ambayo itawafanya Wanyamaze milele.
Naomba Kuwasilisha